JK ashusha panga: Filikunjombe, Lembeli, Mkono, Bashe, Kingwangalla, Premji, Diallo watoswa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK ashusha panga: Filikunjombe, Lembeli, Mkono, Bashe, Kingwangalla, Premji, Diallo watoswa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ludewa, Sep 26, 2012.

 1. L

  Ludewa JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM - NEC kimemalizika hivi punde huko Dodoma, huku wale wabunge wa CCM waliosaini fomu ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, majina yao yakiwa yamekatwa. wabunge waliokatwa majina yao kwa kosa la kumwadhibisha waziri mkuu ni Mhe. Deo Filikunjombe, ambaye aliomba nafasi ya UNEC wilaya ya Ludewa na mhe. Nimrodi Mkono aliyeomba Unec na Uenyekiti wa Wazazi Taifa.

  My take: Mie nilidhani Filikunjombe na Mkono na wabunge wengine waliosaini ile fomu waliisaidia serikali ya CCM, loh kumbe kitendo kile kiliwaudhi wakubwa! ama kweli ccm ina wenyewe, akina Pindi Chana.

  Zaidi:
   
 2. J

  JF-MBUNGE JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  CCM kama wee sio mshirika wa mafisadi huna chako
   
 3. mwaxxxx

  mwaxxxx JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 846
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  zidumu fikra za mwenyekiti ........magambazzzzz
   
 4. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,597
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo ule mkwala wa Nimrod Nkono kwamba asipopitishwa patachimbika haujasaidia kitu? kudadadeki CCM, cjui ina gamba la mti gani wallah!
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tunashukuru kwa taarifa, ni habari njema maana ndiyo tuliyotegemea. Nasema habari njema kwa maana ya wanamageuzi ya kweli wanapokatwa majina yao watanzani tuko nyuma yao, na hakika uwanja ni mpana tu, na CCM watajutia nafasi za watu hao waliowakata katika jamii wanazowakilisha. Sikio la kufa halisikii dawa, ndio maana tunaona miti mingi inazidi kuteleza ambayo nyani amezoea kujishikila.

  Waliokatwa majina yao hoja za msingi zinaeleweka kwa sababu ya kutolinda masilahi ya wasaliti wa taifa letu. Uwanja ni mpana na wazi, chagueni timu nzuri ambayo mtaongeza kasi ya mchezo kuchukua kombe.
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mkwara wa Nimrod Mkono kwamba patachimbika si mjengoni Dodoma, subirini yatakayojilia na hatima za vuguvugu la mageuzi.
   
 7. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Msemaji wa haya ni Nape Nauye! Msipende kupewa taarifa potofu wakati kuna taarifa sahihi!
   
 8. ndiyomkuusana

  ndiyomkuusana JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 627
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Imeandikwa na Happiness Mtweve | Tanzania Daima | 26, Sept 2012

  HATIMAYE Panga la Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, limewashukia vigogo wa chama hicho na kuwatupa nje ya kinyang'anyiro cha kuwania nafasi za uongozi wa jumuiya za chama na ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

  Wakati panga hilo likiwashukia baadhi ya vigogo, Rais Kikwete ametoa kauli nzito ya kutaka wagombea waliopata kutoa kauli za vitisho dhidi ya chama hicho kufanya kile walichokusudia kukifanya.

  Kikwete katika kauli yake hiyo alionekana waziwazi kukerwa na kauli za ‘patachimbika' au zile za kutishia kujitoa na kujiunga na vyama vya upinzani.

  Akizungumza kwa ukali, Kikwete ambaye juzi alitamba akisema CCM haitakufa kama inavyotabiriwa na baadhi ya watu, alihitimisha kauli yake kwa kusema watu wenye kauli za namna hiyo walikuwa hawafai kuendelea kuwa wanachama wa chama hicho.

  Zaidi, angalia 1st post...
   
 9. J

  JF-MBUNGE JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  nahesabu siku za Mwakyembeee...,SIttaa...,sijui mgufuli.., hawa utawala ujao wanapumzishwa kwa umri am telling uuu. Na hv hawawezi piga ma deal ya nguvu ahahha watamaliza vyeo vyao na mshahara na marupupu chezeaa wasanii weyeee.

  Mzalendo wa kweli hatakiwi CCM...,lbd mzalendo maneno na mzalendo wa kuegemea kundi mojawapo la watafuna nchi.

  CCM inawenyewe kila siku mnaambiwa na wenyewe ndioo....sisiii...wanaitiaga kwa nguvu kweli kumbe chaguzi zinazokuja wanapunguzwaa na kuwa sio yao tena lol.....
   
 10. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #10
  Sep 26, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,246
  Likes Received: 3,812
  Trophy Points: 280
  Alama za nyakati hazizuiwi kwa matambiko wala mahoka, hilo ni pigo moja muhimu sana kwa ccm katika nyanja kuu mbili, siasa za uzee za kistarabu wamezitupa rasmi kwa kumtoa Mkono, na pili ni siasa za vijana zilizoanza kuleta sura muhimu isiyo ya kisultani baada ya kung'aa kwa nyota ya kisiasa ya Filikunjombe, sasa ni dhahi chama cha vijana kimeshikwa na Ridhiwani, Januari, na wengine wengi waikubalio IMLA
   
 11. p

  politiki JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  JK watanzania wangekupima kwa vigezo unavyowapima navyo wenzako wewe ungebakia kweli?

  Hakuna kiongozi anayeongoza nchi kwa vitisho kama wewe kumbuka kauli zako wakati wa mgomo wa wafanyakazi!!

  Unakumbuka kauli zako wakati wa mgomo wa madaktari?

  Kuzushiana mambo hakuna mtu mzushi kama wewe JK, unakumbuka ulivyowazushia wenzako wakina Salim A Salim kuwa ni waarabu na uchafu mwingi uliowatupia wenzako ikiwemo kashfa za kutunga?

  Suala la rushwa:
  Serikali yako imejaa viongozi wala rushwa watupu ukiwemo wewe mwenyewe, wakati ulipokuwa waziri wa madini uligawa migodi kama njugu na pia ikiwemo suti uliyonunuliwa na yule mwarabu huko London.
   
 12. J

  JF-MBUNGE JF-Expert Member

  #12
  Sep 26, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nakwambia Yeriko shv kijana ukiwa mtetezi wa nchi yako kwa dhati kbs hauchukui muda CCM unafanyiwa zengwee kisa ni kulinda vijana wa kisultani. Kazi ipo na sita nae nashangaa anapiga makelel anasambabisha kina lembeli wanatolewa kafara wkt uspika tu alishindwa kuwazidi kete wapinzani wake na bado alikuwa hot je shv alivyochafuliwa kote CCM na CDM atauweza urais ...nae amalizie za mwisho mwisho na kina nape na mwakyembe wake
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,532
  Trophy Points: 280
  Uchaguzi wa ndani wa CCM ni "sadakalawe", mwenye kupata apate, mwenye kukosa akose!. Fainali ni 2015!.
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Sep 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  [​IMG]
  [​IMG]


  Hii ndiyo CCM na mwenyekiti wake ni burudani tupu, hapo nchi itajengeka kwa mtindo huu?
   
 15. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #15
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  politiki;

  Umesema ukweli mtupu ndugu yangu maana kama kweli mbingu ipo Jk ataumbuka sana siku hiyo!

  Lakini mkuu usisahau kwamba katika nchi hii CCM wana sera ya kuwafunga wezi wadogo na kuyafanya majambazi sugu kuwa watoa hukumu kwa wadokozi na raia wema huku yakishika nafasi za uwaziri, urais, makamu wa rais ubunge udiwani na vyeo vingi vya kichamachama ili mradi kutumia hicho chama kama kichaka; so usishangae kuona Kamuhanda ni kamanda wa polisi anaruhusu mauaji ya mtu asiye na hatia jiulize kama angekua ndio Jambazi ingeekuaje?

  Hivyo amini tunaongozwa na majambazi na magenge ya wauaji yaliyopachikwa vyeo bandia vya kuongoza nchi hii
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #16
  Sep 26, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  najiuliza hivi Diallo kakosa nini mbona wamemtupa nje

  halafu hii kauli ya " msipo nichagua/niteua naenda upinzani " mbona nasikia hata yeye aliitumia kumbe alikuwa anatishia tu
   
 17. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #17
  Sep 26, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,799
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Alikuwa anatishia nyau yule mzee apumzike siasa amechoka mwili na akili!!
   
 18. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #18
  Sep 26, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,799
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  ina gamba la kobe!!
   
 19. J

  JF-MBUNGE JF-Expert Member

  #19
  Sep 26, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Yaani unauliza fisadi Diallo kakosa nini haujui vyombo vyake vya habari vinavyyooichafua CCM na kuipambaCDM mwanza...kwanza nae hana jipya huyo mafisadi alipokuwa waziri alituibia sn pale wizarani
   
 20. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #20
  Sep 26, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  anaye jua tafasiri ya maneno haya atupe hapa maana nadhani huu ni unabii kwao

  '' MENE MENE TEKERI PERESI ''
   
Loading...