Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,798
- 34,170
HATIMAYE ndoto ya Jakaya Mrisho Kikwete kuchaguliwa na Watanzania kuongoza Tanzania kwa muhula wa pili wa miaka mitano imetimia.Kwa mujibu wa Katiba, rais anatakiwa kukaa madarakani sio zaidi ya mihula miwili ya miaka mitano mitano. Kikwete amemaliza mhula mmoja na iwapo angeanguka kwenye uchaguzi huu angekuwa rais wa kwanza kushindwa kutetea kiti chake tangu Katiba ilipoweka ukomo huo mwaka 1992.
Kikwete, ambaye amekulia ndani ya CCM akishika nafasi mbalimbali kabla ya kuwa mbunge na baadaye waziri, aliibuka na ushindi wa kura milioni 5.3 akifuatiwa na mgombea wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, aliyepata kura milioni 2.3 baada ya asilimia 42 ya watu waliojiandikisha kupiga kura kujitokeza Oktoba 31.
Wagombea wengine wa urais ni Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, Hashim Rungwe wa NCCR, Fahmi Dovutwa wa UPDP, Peter Mziray wa APPT Maendeleo na Mutamwega Mugahywa wa TLP.
Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, ataapishwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kukabidhiwa dhamana ya kuliongoza taifa kwa miaka mingine mitano akiwa na Bunge lenye mtazamo na sura mpya, hasa za upinzani.
Kihistoria rais mteule Kikwete alizaliwa mwaka 1950 kwenye Kijiji cha Msoga wilayani Bagamoyo, Pwani ambako alitumia sehemu kubwa ya maisha yake ya utotoni. Ni mtoto wa sita kwenye familia ya watoto tisa ya Khalfani Mrisho Kikwete na mama yake Asha Kayaka.
Alisoma darasa la kwanza hadi la nne (mwaka 1958-1961) kwenye Shule ya Msingi Lugoba na baadaye kuendelea na masomo Shule ya Kati Lugoba ambako alisoma darasa la tano hadi la nane (mwaka 1962-1965).
Mwaka 1966-1969 alisoma Shule
ya Sekondari Kibaha, kidato cha kwanza mpaka cha nne, mwaka
1971-1972 alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Tanga.
Alianza siasa ndani ya Tanu alipokuwa sekondari na alishika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho ambacho mwaka 1977 kiliungana na chama tawala cha visiwa vya Zanzibar, ASP kuunda CCM.
Alisoma Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) na kutunukiwa Shahada ya Uchumi mwaka 1975. Pia, alipitia mafunzo ya kijeshi kwenye Chuo cha Maafisa wa Jeshi cha Monduli mkoani Arusha kati ya mwaka 1984 hadi 1986.
Akiwa chuoni hapo, Kikwete alionyesha uwezo mkubwa katika siasa hata kuteuliwa kuwa mkufunzi mkuu wa makamisaa wa siasa katika chuo hicho, lakini alijiuzulu jeshi mwaka 1992 wakati nchi ilipoingia kwenye siasa za vyama vingi, hivyo kuamua kuondoa siasa kwenye taasisi za serikali.
Ndani ya CCM, Kikwete alianza kushika nafasi za juu tangu mwaka 1982 alipochaguliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, nafasi ambayo amekuwa akiitetea kila baada ya miaka mitano.
Mwaka 1988, rais wa serikali ya awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, alimteua Kikwete kuwa mbunge na kumpa nafasi ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini. Mwaka 1990, Kikwete aliteuliwa kuwa waziri kamili wa Nishati na Madini baada ya kuingia bungeni kwa kushinda uchaguzi kwenye Jimbo la Bagamoyo na mwaka 1994 aliteuliwa kuwa Waziri wa Fedha.
Uteuzi huo ulimfanya kuwa waziri wa kwanza kushika nafasi hiyo (Waziri wa Fedha) akiwa na umri mdogo kuliko wote katika historia ya Tanzania.
Katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995, Kikwete alijitokeza na kuwa miongoni mwa waliowania kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM, lakini alipigwa kumbo na Benjamin Mkapa katika awamu ya pili na hivyo kulazimika kusubiri kwa miaka kumi kuingia Ikulu.
Hata hivyo, alipounda serikali yake ya awamu ya tatu, Mkapa alimteua Kikwete kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, alifanya kazi hiyo kwa miaka kumi hadi mwaka 2005 alipoingia kwenye kinyang'anyiro cha urais ndani ya CCM.
Na nyota yake iling'ara kwa CCM kumpitisha kugombea urais ambao aliupata kwa ushindi mkubwa wa asilimia 81.
Pamoja na ushindani mkubwa aliopata kutoka kwa mgombea wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, Kikwete amefanikiwa kutimiza ndoto yake ya kuongoza kwa vipindi viwili.
chanzo: Gazeti la Mwananchi