JK apingwa kortini kugombea urais 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK apingwa kortini kugombea urais 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mag3, Aug 4, 2010.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Na Makumba Mwemezi - Majira

  RAIS Jakaya Kikwete amewekewa pingamizi kortini kugombea urais mwaka huu kwa madai ya matumizi mabaya ya madaraka na ufujaji wa fedha za umma katika safari zake za nje.

  Hayo yameelezwa na Mwalimu Mstaafu na Mkazi wa Dar es Salaam, Bw. Paul Mhozya ambaye amefungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam kupinga mgombea huyo katika uchaguzi wa Oktoba 31, mwaka huu.

  Akizungumza na Majira jana, Bw. Mhozya alisema amefungua pingamizi hilo chini ya hati ya dharura akiitaka mahakama kulisikiliza mapema kabla kampeni kuanza, hivyo akaishauri CCM kuteua mgombea mbadala mapema, badala ya kusubiri uamuzi wa mahakama.


  Katika hati ya mashtaka yenye sababu kumi za kuiomba mahakama imuengue Rais Kikwete kwenye kinyang'anyiro cha urais Bw. Mhozya anasema, rais ametumia nafasi aliyopewa kwa mambo binafsi, amekiuka katiba na kuvunja haki za binaadamu pamoja na matumizi holele ya fedha za watanzania kwa mambo yake mwenyewe.

  Gazeti la The Citizen toleo la jana lilimkariri Bw. Mhozya kuwa aliwahi kufungua kesi ya kikatiba kama hiyo mwaka 1993 dhidi ya Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi kuwa alivunja katiba kwa kuruhusu Zanzibar kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu (OIC), lakini ikatupwa na Jaji Barnabas Samatta kuwa mamlaka ya kumwondoa rais madarakani yalikuwa mikononi mwa bunge peke yake, chini ya kifungu cha 46A cha katiba.

  Bw. Mhozya alisema amefikia uamuzi wa kufungua kesi hiyo kutokana na ujeuri uliooneshwa na Rais Kikwete katika miaka mitano ya uongozi wake, hivyo ni vema akazuiwa kuurudia kwa kumzuia asirudi madarakani.

  Alisema anayo orodha ndefu ya mambo mabaya aliyofanya Rais Kikwete wakati wa uongozi wake, ambayo anatarajia kuyatumia kama ushahidi na uthibitisho wa malalamiko aliyopeleka mahakamani, ambayo anaamini yatakubaliwa na kumwondoa kwenye kinyang'anyiro.

  "Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi (NEC), Jaji Lewis Makame alikwishasema kuwa tume iko tayari kupokea pingamizi dhidi ya mgombea yoyote kwa maslahi ya umma na kuwa itachukua hatua stahili, ninasubiri kauli ya mahakama na ninaamini itasikiliza hoja zangu na kuzifanyia kazi," alisema.

  Alisema kuwa yeye kama Mtanzania anayo mamlaka chini ya ibara ya 30 (3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufungua kesi dhidi ya uvunjaji wa ibara yoyote ndani ya katiba hasa zinazohusu haki za binaadamu.

  Ibara ya 30 (3) inasema "Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Sehemu hii ya Sura hii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au wajibu kwake limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza kufungua shauri katika Mahakama Kuu"

  Bw. Mhozya anasema pamoja na kuwa Rais ana kinga kisheria lakini Kikwete hana kinga ya kuwekewa pingamizi kama mgombea kwa sasa, ndio maana akaamua kufungua kesi hii wakati huu badala ya kusubiri atakaposhinda na kuwa rais, kwani atakuwa na uwezo wa kutumia kinga yake.

  Alisema katika kipindi cha uongozi wake rais amefanya safari za ughaibuni zisizo za lazima nyingi kwa fedha za umma, jambo ambalo limesababisha wananch wengi kuishi maisha ya taabu na umaskini mkubwa, huku akidai kuwa urais ni suala binafsi, akisema kuwa ndio maana alimteua mwanawe kumtafutia wadhamini.

  Alisema sheria inaitaka NEC kutoa muda wa ziada kwa chama ambacho mgombea wake amekufa au ameshindwa kuendelea kukiwakilisha, ili chama hicho kiweze kuteua mgombea mwingine, hivyo anaamini kuwa baada ya pingamizi hilo kukubaliwa mahakamani, NEC itawaamuru CCM kufanya hivyo kwa kuwaongezea muda.

  "Sasa kwa vile sheria inasema NEC itawaongezea muda wa kuteua mgombea mwingine, mimi nashauri wakateua kabisa mgombea mwingine na kumshauri niliyemwekea pingamizi kujitoa, hii itaepusha kupoteza muda pindi pingamizi likikubaliwa, hakuna jinsi," alisema Bw. Mhozya.


  Alisema yeye anahofia zaidi mustakabali wa nchi na vizazi vijavyo kuliko anavyohofia maisha yake, hivyo pamoja na vitisho anavyopata bado hataogopa kusimamia ukweli na kuwafichua waovu kama anavyofanya.

  "Nimetoka mahakamani leo (jana), nilikwenda kuwaona makarani wa wanipatie 'samansi'(hati ya kuhudhuria mahakamani iliyo na tarehe ya kusikilizwa kesi) lakini walisema bado haijatoka naamini itatoka hivi karibuni ili tukasikilizwe. Matatizo yapo na nilikwisha yazoea," alisema Bw. Mhozya.
   
 2. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Bravo bwana Mhozya, nafikiri katika Watanzania 30m wenye upeo wewe umeliona hili, asante sana
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Part of mafioso plot ?? (Referring yule kigagula aliesema hakutakuwa na uchaguzi mwaka huu)
   
 4. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  sio hilo tu ..pia ashitakiwe kwa kuwaficha wezi wa mabilioni ya EPA, sheria gani inayoruhusu mwizi arudishe tu pesa alizoiba then basi.?

  what abt meremeta...? what abt richmond ...?the list is endless...!

  SAY NO TO KIWETE...! ENUF IS ENUF..!
   
 5. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,507
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Wrong stepping. Kazi ya kumuengua mgombea ni ya Tume ya Uchaguzi na si mahakama.
   
 6. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,050
  Likes Received: 3,957
  Trophy Points: 280
  safiii
   
 7. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kumbe sio Mtikila peke yake anayeyaona haya na kuyasema hadharani hata kama kwa kufanya hivyo kutahatarisha pumzi yake?
  Congrats.
   
 8. r

  rimbocho Member

  #8
  Aug 4, 2010
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana mzee kwa kutukomboa sisi tusiojua namana ya kutumia haki zetu kwa kutokujua hata katiba inafananaje, wala sheria za nchi hii zinasemaje juu ya haki za raia. Kama kweli uraisi si jambo binafsi, iweje kikwete aseme et alimtuma mtoto wake kumtafutia wadhamini kwa sababu eti ni jambo la kifamilia. Bravo Mhozya tupo tunakuunga mkono. Ule utabiri wa nabii Isaya kuhusu Taifa la Tanzania unaweza kutimia mwaka huu. Nabii Isaya anasema Mungu hapendezwi na tabia ya viongozi wachache kutumia madaraka yao kujinufaisha wao na familia zao wakati wananchi waliowengi wanateseka na umasikini uliokithiri, wajane wananyang'anywa haki zao, yatima wanateseka hakuna wakuwaangalia.
  :hippie:
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,174
  Trophy Points: 280
  Tatizo hapa hamna kesi, hatujaonyeshwa sharti lililovunjwa na huyu bwana akiambiwa ahakikishie mahakama ni jinsi gani safari za JK zinafuja mali ya umma ni vigumu sana kuonyesha, hasa kwa sababu ni vigumu kuchanganua kwa uhalisi safari za raisi zinafanya kazi gani hata zile tangible tu, ukiachilia mbali zile intangible ambazo ndiyo kabisa kuzi quantify ni vigumu.

  System yenyewe haina transparency, evidence yote iko classified hata ile isiyostahili, rais yuko juu ya sheria halafu yeye ndiye anayechagua majaji wote na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi. Unategemea nini ?

  Kesi inaweza kuburudisha watu, kuonyesha watu walivyochoka na kutoa msukumo wa kumpinga JK, lakini haina legal merit.

  Legal merit, which is quite different from merit period. The law is an a.s.s.

  It is not what happenned, it is what you can prove happenned.
   
 10. s

  sha Senior Member

  #10
  Aug 4, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35  NDG Kiranga ujue sheria haipo juu ya MUNGU, huo ndio mwanzo tu wa mpango wa Mungu kuikomboa nchi hii kutoka kwa utawala huu, MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 11. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu hilo linajulikana tunasubili tu mahakama itamke kwamba nayo hii ni kesi ya kisiasa, tumeiozea!
  Lakini Bravo kwa huyu mzee, umefanya vyema.. kwani kwa sasa Tanzania ilikuwa imefikia hatua ya kwenda kisangoma sangoma hasa baada ya shekh Yahaya kuwatishia nyau waliokuwa na nia ya kumpinga JK kwamba watakufa! na kweli wote wakaogopa! Kwa mzee kama huyu kuamua kabisa kumfungilia kesi halali.. ni hatua njema kabisa ambayo japo haita fika mbali lakini itasikika na itaendelea fungua masikio ya walio wengi.
   
 12. K

  Kenge (Eng) JF-Expert Member

  #12
  Aug 4, 2010
  Joined: Dec 7, 2006
  Messages: 502
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Sawa namtakia kila la kheri ila niseme ataweka historia. Kwa UFUPI anapoteza muda hakuna kitu hapa. Najua sitaeleweka ila ndio hivyo.
   
 13. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Kiranga umesema yanayonikera kila siku, huwezi kuwa na NEC yenye meno inayotokana na rais mwenyewe kuteua, kama Takukuru ilivyo! mfumo wa mahakama ulivyo nk. Hawa jamaa inabidi sasa wawe wanaapishwa bungeni wala siyo rais jamani.

  Anyway, kesi ni nzuri ila mwisho wa siku haitakuwa na maana.
   
 14. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kazi ni ngumu kuanzisha. Lakini kwa kuwa jamaa keshaanza, nakwambia watajitokeza wengi tu kumuunga mkono na kumsaidia katika mambo ya kisheria na kuweka bayana vifungu vya katiba vilivyovunjwa na Rais alipokuwa madarakani. Tutasikia mengi mwaka huu. Hapo ndo utabiri wa Sheik Yahya utakapotimia, kwamba itaundwa serikali ya mseto, na uchaguzi utaahirishwa. Tusubiri tuone.
   
 15. Smiles

  Smiles JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 1,231
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mmh.....
   
 16. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Unasema hamna kesi wakati kesi imekwisha kuwa filed una maana gani? Si usubiri kwanza mentioning and hearing ndipo uweze kubashiri hukumu yake!!
   
 17. A

  Anold JF-Expert Member

  #17
  Aug 4, 2010
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,378
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Hakuna haja ya kumharibia Rais wetu, Huko nje nasikia amepata kufahamiana na watu wengi sasa nchi yetu inafahamika sana Marekani, hata Obama ameshatujua Tanzania hivyo ataudhamini Tukienda Kukopa, Hakuna wa kutunyima maana tumeshajitangaza vyakutosha kuwa sisi ni aroro apweche. Sasa kama asingeenda hizo safari tungepata wapi wa kutukopesha? Hata hivyo vyandarua vilivyozua kashfa huko Temeke ni matokeo ya Hizo safari hata Bill klinton kaja mpaka Ntwara kuangalia kama matumizi ya fedha zake yameenda sawia au la japo niliona kile kituo cha afya kama changa la macho vile!!!!!!:bowl::bowl::bowl::bowl::bowl::bowl::bowl::bowl::tape:
   
 18. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #18
  Aug 4, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,555
  Likes Received: 4,682
  Trophy Points: 280
  Chukua tano mwalimu, na uongeze kipengele cha afya , JK afya yake ni mgogoro kwani anazimika zimika majukwaani, ushahidi upo.Endeleza mapambano mkuuu,mpaka kieleweke
   
 19. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #19
  Aug 4, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Haya tujiandae kusikia vioja vingi mwaka huu wa uchaguzi...............
   
 20. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #20
  Aug 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  tusitegemee matokeo chanya kwenye kesi hii ............lakini nampa hongera kwa kutubutu na kujaribu kuchukua hatua. wengi wa watanzania tunatabia ya kutochukua hatua hata pale inapowezekana
   
Loading...