JK apende asipende CCM ipende isipende katiba itaandikwa siyo ombi.

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Wakili wa Kujitegemea na mwanachama wa Chadema, Mabere Marando, alisema suala la katiba mpya kwa sasa halina mjadala tena.

“Katiba mpya, tupende tusipene, Kikwete apende asipende, CCM ipende isipende, lazima iandikwe upya hilo si suala la mjadala tena,” alisisitiza Marando a kuongeza:

“Hoja iliyopo ni je viongozi walio madarakani wanasoma alama za nyakati au wapo tu kama kisiki wanasubiri wafagiwe na upepo”.

Marando pia aliponda hali ya kupingana iliyojitokeza kwa mawaziri, baraza la vijana wa CCM kupingana na wazee kuwa ni ishara kuwa chama hicho kinaelekea kufa.

“Chama chochote cha siasa kinazaliwa, kinakua, kinazeeka na kinakufa, CCM sasa inakufa. Hebu kisaidieni kife bila ya sisi kupata madhara,” alisema Marando ambaye ni mmoja wa waasisi wa mageuzi nchini.

Na mimi naongeza wanaJF wote wanaopinga kuandikwa kwa katiba kwa sababu yoyote ile wapende wasipende itaandikwa tu.
 
Ni kama mtu ukiwa na haja ya kuijsaidia ni lazima utaenda sehemu husika tu. Kwa saizi katiba imekuwa kama haja kwa mwanadamu, msalani ni lazima. Yapo mengi yanapelekea hali hiyo labda viongozi wetu kwa upofu walionao wa kutosoma alama za nyakati.
 
Bado kuna watu wachache wasioona mbele kama kina Tambwe wanafikiri wanaweza kuzuia mabadiliko.
 
JK ndio muasisi wa wa kuandikiwa katiba mpya..unachoongea ni nini sasa? au unataka umaarufu tu?

Kwakuwa JK amependa tuwe na katiba mpya, wakati wa mkapa watu walikuwa wanadai katiba mpya lakini hawakusikilizwa

Amewasikiliza mnatafuta umaarufu na ligi lol.
 
Kuna kupenda kwa hiari na kupenda kwa kulazimishwa sasa yeye apende asipende katiba itaandikwa si kwa hiari kwa lazima.
 
Katiba mpya tutapata na hata CCM wafanye mikakati yoyote ile ... this time tunakwenda moja kwa moja. Hatuhitaji ruhusa kwa CCM chochote kile na lazima waelimishwe hili...tukimaliza tunapitia Dowans, Uchaguzi na Ugaidi Wote.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom