JK apata mshituko juu ya ongezeko la bei ya vyakula; aagiza serikali kuingilia kati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK apata mshituko juu ya ongezeko la bei ya vyakula; aagiza serikali kuingilia kati

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mchakachuaji192, Mar 30, 2011.

 1. mchakachuaji192

  mchakachuaji192 JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, ameshtushwa kupanda kwa bei ya vyakula na gharama za maisha mijini.Kutokana na hali hiyo, Rais Kikwete ameagiza chakula cha akiba cha taifa kuingizwa katika masoko ya mijini hasa jiji la Dar es Salaam mara moja ili kupunguza bei ya chakula katika masoko ya miji na kupunguza makali na gharama ya maisha kwa wananchi.

  Rais Kikwete ameagiza kuwa kazi hiyo ya kuingilia soko na kupunguza bei ya chakula kwa wananchi iwe kazi ya nyongeza na ya kudumu ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika pamoja na Wakala wa Akiba ya Chakula ya Taifa (NFRA).

  Amesema kuwa miji ya Tanzania ina masikini wengi na malalamiko makubwa ya masikini hao ni bei kubwa ya chakula na kuwa ni wajibu wa Serikali kuchukua hatua za makusudi kuwapunguzia wananchi gharama hizo za maisha kwa kuingiza chakula cha bei nafuu katika masoko ya mijini.

  Rais alitoa maagizo hayo wakati alipotembelea maghala ya NFRA mjini Dar es Salaam kama mwendelezo wa ziara zake na Wizara mbalimbali na taasisi za wizara hizo.

  Rais Kikwete amesema kuwa kama hatua za kuingilia soko zingechukuliwa tangu Oktoba mwaka jana wakati bei ya mahindi ilipokuwa sh. 300 kwa kilo mjini Dar es Salaam, bei hiyo isingepanda na kufikia sh. 430 kwa bei ya sasa.

  “Hii ndiyo kazi yetu kuanzia sasa yaani kuhakikisha kuwa tunaingilia soko, kuingiza chakula cha kutosha na hasa mahindi kwa sababu hiki ndicho chakula kikuu cha Watanzania na kuhakikisha kuwa tunaishusha bei hiyo ya mahindi hadi sh. 300 katika kipindi kifupi iwezekanavyo,” Rais amewaambia maofisa wa Wizara na Wakala huo.

  Amesema kuwa lazima viongozi waelewe kuwa hata mijini kuna upungufu wa chakula.

  “Tafsiri ya njaa ni kama mji haupati chakula cha kutosha basi kuna njaa, Hivyo tujipe mamlaka ya kuingiza haraka soko ili kuwalinda wananchi kwa sababu hatuwezi kuwaacha wananchi mikononi mwa wafanyabiashara binafsi wa chakula ambacho kichocheo chao kikubwa ni faida,” amesema Rais Kikwete.

  Amesema hiyo sasa ni kazi yao ya kila siku yaani kufuatilia masoko na kuhakikisha kuwa kinakuwepo chakula cha kutosha kupunguza bei.
  Amewaagiza viongozi kucheza na soko la Dar es Salaam ili kuhakikisha kuwa bei zinakwenda chini haraka iwezekanavyo.

  Amesema kuwa siyo busara kwa mahindi kubakia maghalani kusubiri njaa wakati bei za vyakula zinapanda sana. Nyie mna wajibu wa kulilisha taifa hili.

  Source: Dar leo
  My take ina maana yeye anakaa tu magogoni bila kujua changamoto zinazowakabili wananchi wake? huyu baba Rizione One day yes
   
 2. h

  housta Senior Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hapo ndipo tunapoona upeo wake mdogo wa kufikiri.Yeye anadhani tu kuingiza chakula cha akiba ndio kutapunguza mfumuko wa bei.Kuna factors nyingi sana zinachangia,mfano bei ya mafuta.Mfumuko wa bei unachangiwa zaidi na bei ya mafuta.Akiweza kudhibiti bei ya mafuta,mfumuko na utapungua.Lakini kwa sababu hana hata idea hizi,basi tujue tu inakula kwetu kwa sana tu mpaka 2015.Inatia huruma kuwa na kiongozi ambaye ana mawazo duni kama huyu wa sasa.
   
 3. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Mbona CHADEMA walipoandamana juu ya ugumu wa maisha na gharama za maisha kupanda akasema wanataka kupindua nchi?? Leo tena anaomba watu washushe bei?? Nani hapo anataka kupindua nchi sasa??
   
 4. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Huyu mchumi wa ajabu sana.......hayo mahindi atakayoyaachia yataishia kwa BAKHRESSA....nadhani hajui hata maana ya hiyo SGR....ni kwa ajili ya kukimu wakati wa NJAA ambao unakuja....yeye alitakiwa kufanya haya:
  1. Kushusha VAT ya mafuta toka 18% mpaka 10%
  2. Kuondoa VAT kwenye LUKU
  3. Kufuta kodi zote katika sukari inayozalishwa nchini
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hIZI MOVES ZITALIPUNGUZIA TAIFA MAPATO
   
 6. mchakachuaji192

  mchakachuaji192 JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Huyu jamaa waliopendekeza awe kiongozi wa nchi sijui waliona nini maana hata wizara alizokuwepo kabla ya hapo ameacha maneno mengi sana
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu unamaniiisha hana washauri wa hivi! I mean hata wachumi wakumshauri haya!?
   
 8. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mbona Idd Amin Dada alipoambiwa serikari imeishiwa fedha akaamuru zichapwe pesa za kutosha ili kukidhi mahitaji! Kuna tofauti gani na hii?
   
 9. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hivi huyu JK anaishi dunia gani. Kila kitu kwake ni kipya na anabaki kushangaa pasipo majibu. Hakuna tatizo hata moja ambalo ameweza kusimama na kutoa ufumbuzi wake. Anapozungumzia kupanda kwa bei ya vyakula halafu anasema fungueni maghala ambayo yamejaa mahindi pekee anamaanisha nini. Hivi anafikiri kwa kujaza mahindi kwenye soko ndiyo bei ya vyakula itapungua? Waliacha wajanja wachache wakaficha sukari kwa lengo la kupandisha bei lakini Serikali ilishindwa kufanya lolote. Sukari iliyokuwa inauzwa kati ya sh. 1400-1500 sasa inauzwa kwa sh. 1700-2000 kwa kilo. Mafuta ya kupikia lt 5 yalikuwa yanauzwa kati ya sh 14,000-16,000 kwa sasa mafuta hayo yanauzwa kati ya sh. 19,000-20,000. Kwa hali hii Mtanzania atawezaje kuyamudu maisha ilhal ongezeko hilo ni kwa kila kitu hadi nauli za daladala. Watu wakihoji Rais anasema wanataka kuangusha Serikali, anapoulizwa anabaki kushangaa na kipato cha Mtanzania kinazidi kuporomoka,

  Tufanye nini katika hali kama hii ama ndiyo kiama kwa wanyonge kinatimia?
   
 10. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Hapana...unaposhusha kodi bei hupungua na watu hufanya manunuzi zaidi....kutokana na unafuu wa bei...watu watanunua zaidi(in terms of volumes) na wigo wa kodi kupanda....simple economics...kwa vile VAT sio production cost
   
 11. W

  WildCard JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mchakachuaji,
  Rais wetu mgonjwa halafu unaweka heading hiyo. Umetushtua kidogo. Maagizo/ Ushauri wake huo una walakini. Haoni kutokuwa na kodi kwenye mafuta ya taa kunavyochangia uchakachuaji kwenye mafuta mengine?
   
 12. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mbona Idd Amin Dada alipoambiwa na gavana wake wa fedha kuwa nchi haina pesa aliamuru zichapishwe pesa za kutosha ili kukidhi mahitaji! Kuna tofauti gani na hii?
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mbadala wa mapato haya?
   
 14. msafiri.razaro

  msafiri.razaro JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 616
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Usalama wa Taifa walipaswa kuna na wataalamu wa kuthibiti mfumuko wa bei, kwani umfumuko wa bei unachangia kukosekana na usalama. Hii ni Hatari ya kuwa na Cocktail ya waagizaji wa bidhaa Nchini (importers), wanauwezo wa kukaa meza moja na kupanga kupandisha bei za bidhaa, lakini kama kungelikuwa na kitengo cha kudhibiti mfumuko wa bei hali isingekuwa hivi ilivyo. Kulitakiwa kuwe na mfumo wa kibiashara unaothibiwa usalama wa nchi, yaani kutafuta, kununua, kuingiza bidhaa muhimu kama mafuta, nafaka, sukari n.k na kuziuza kwa bei poa ilikulazimisha kushusha bei. Kwa mfano TPDC, na Mashirika ya Umma, yakiongozwa na Usalama wa taifa kwa kificho au wazi wakatumia pesa za serikali kuagiza bidhaa na kuuza kwa bei poa wafanyabiashara nao watashusha. Sio sahihi kwa serikali kujitoa kufanyabiashara, asali zake ni hizi...
   
 15. m

  msosholisti Member

  #15
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe unapenda sana chai.
  jiulize umeifanyia nini serikali na siyo ikufanyie nini?
   
 16. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Kupunguza matumizi ya serikali yasiyo ya lazima.....kama mtu mmoja kutumia gari lenye seats 8 peke yake linalokula 200 litres per week....na wako kama 4,000 watu hawa...kupunguza safari zisizo za lazima wala tija
   
 17. m

  msosholisti Member

  #17
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Upo sahihi kabisa. sio km hawa wachangiaji wa cdm. bure kabisaaa.
   
 18. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  na atashindwa kuilipa dowans?
   
 19. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #19
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Sote tunapenda chai mimi na wewe na hatuwezi kununua sukari kwa 2,000.....mimi nalipa kodi nyingi sana serikalini...ndicho ninachokifanyia serikali
   
 20. W

  WildCard JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hivi ule mradi wa kukataa mashangingi wa WM Pinda umeishia wapi?
   
Loading...