Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,314
- 33,108
Monday, 01 November 2010 16:14
Salim Said
MATOKEO ya awali katika nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanaonyesha kuwa, mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete anaongoza kwa asilimia 64 ya kura zilizotangazwa dhidi ya asilimia 25 za Dk Willibrod Slaa wa Chadema.
Kikwete ameshinda katika majimbo ya Babati Mjini mkoani Manyara, Korogwe Mjini Tanga, Nkenge Kagera, Singida Mjini, Mafia Pwani na Tarime mkoani Mara huku Dk Slaa akishinda katika baadhi ya majimbo ya Kanda ya Ziwa.
Mgombea wa CUF profesa Ibrahim Lipumba anashikilia nafasi ya tatu kwa kupata asilimia nane na Peter Mziray akiambulia asilimia moja.
Wagombea wengine wote waliobaki wanashikilia nafasi ya mwisho kwa kupata asilimia 0.0 ya kura zilizohesabiwa na kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Hata hivyo kazi ya kukusanya, kujumlisha na kutangaza matokeo inaendelea.
Tafadhali endelea kufuatilia hapa.
chanzo: Gazeti la Mwananchi