JK aongeza muda wa kuwasilisha majina ya wajumbe Tume ya katiba... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK aongeza muda wa kuwasilisha majina ya wajumbe Tume ya katiba...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bibikuku, Mar 17, 2012.

 1. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Awali mwisho wa wadau wote kuwasilisha majina ilikuwa Jana Machi 16 ambapo majina yalitakiwa kuwa yamefika kwa Katibu mkuu Kiongozi.

  Hata hivyo JK amesogeza mbele muda huo na kudai kuwa huenda kuna wengine wamechelewa njiani. Sasa mwisho wa kuwasilisha majina ya watu wanaoombwa kuteuliwa katika Tume ya Katiba ni Machi 23 mwaka huu. Rais anatarajia kuitangaza tume hiyo ya katiba mwezi Aprili mwaka huu.

  Source: IKULU

  WAZO BINAFSI: Hivi JF hatuoni umuhimu wa kuteua wawakilishi wetu japo wawili tumpelekee Rais jmajina kweli??

   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hapa suala si kuextend muda wa kuwasilisha hayo majina, hoja kuu ni kwamba Watanzania wanataka watu makini na wenye moyo wa uzalendo na Taifa letu ndio walisimamie hili suala la kukusanya maoni ya Wananchi ya namna wanavyotaka Katiba ya nchi yetu iweje ili kuleta mwanga wa kijani kwa ajili ya mustakabali na ustawi wa nchi yetu.Mimi naamini kabisa katiba bora ya nchi hutoka kwa wananchi wenyewe na wala si watawala au wanasiasa. Mungu Ibariki Tanzania.
   
 3. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hivi kweli Rais kama taasisi ameshindwa kuitumia taasisi hiyo kupata watu muafaka hadi aletewe na wananchi??
   
 4. Companero

  Companero Platinum Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  1. Mchambuzi
  2. Mwanakijiji
  3. Gaijin
   
 5. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana nawe, lakini namba mbili kwanini asiingie Rejao?
   
 6. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Zingatieni Gender jamani, nichagueni na mimi
   
 7. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  mizizi nadhani hilo limezingatiwa, nahisi Gaijin ni mdada, ataniwia radhi kama nitakuwa nimekosea lakini nahisi kitu kama hicho
   
 8. Companero

  Companero Platinum Member

  #8
  Mar 17, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Rejao ameshawakilishwa vya kutosha
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kukubali kuingia kwenye hiyo tume kuna presume kuwa mtu anaikubali. Mimi binafsi sikubali kwani imenyang'anya madaraka ya wananchi na kuyapeleka kwa RAis.
   
 10. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Kutaka watu waombe kuwa wajumbe wa Tume wakati rais bado Ndio mwenye mamlaka ya mwisho kwenye uteuzi ni kiini macho.

  Madhumuni ya zoezi hili ni kutaka kuonesha watu kuwa wananchi walishiriki wakati ukweli ni kuwa ushiriki wa wananchi ni mdogo sana.

  Nakupongeza kwa msimamo huo, watanzania wengi tungekuwa na mtazamamo wa namna hii tungekuwa mbali sana.
   
 11. NGOGO CHINAVACH

  NGOGO CHINAVACH Verified User

  #11
  Mar 17, 2012
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 798
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  Sasa wananch wanapropose,halafu nani anamaamuzi ya mwisho?ukipata jibu hapo utaona bado mtanzania hajashirikishwa vya kutosha
   
 12. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Akikataa Jina halazimiki kutoa sababu ya kulikataa jina hilo, na hawezi kuwa challenged kwa kufanya hivyo, ni upuuzi wa Hali ya juu.
   
 13. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  na sisi akina mama jamani ndi
  o tumebeba mimba na kumzaa Rais tunahitaji kuwakilishwa. nichagueni mimi
   
 14. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mimi ninaswali, Ni vipi tunayawakilisha majina ya hawa watu kwa Mhe rais?
   
 15. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  MM, unadhani njia gani ingekuwa bora zaidi kukusanya haya maoni mbali na kutumia tume??
   
 16. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kuna anwani wametoa na fax na email address, pia kwa mkono inaruhusiwa we fikisha pale geti la Ikulu uwe umei-address kwa Katibu mkuu Kiongozi
   
 17. Companero

  Companero Platinum Member

  #17
  Mar 18, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  haisaidii, ni sawa na kusema unapinga katiba iliyopo ila bado unaitumia; utapinga tume ila itaundwa na katiba itatungwa na utainukuu na kuitumia kama mtanzania,hivyo ndivyo siasa ilivyo - mambo ni kwa maridhiano (compromise)
   
 18. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  HAKIKISHA WATU HAWA HAWAKUSOMA KATIKA VYUO VIFUATAVYO:
  1-CCM-Kivukoni
  2-CCM-Hombolo
  3- CCM-Handeni

  Kama tume ya katiba ikimuweka mtu mmoja aliyesoma katika vyuo hivyo, basi ni sawa na kutia mchicha katika glass ya mtindi.
   
Loading...