JK aonewe huruma!

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,784
12,226
Ni ukweli usiopingika kuwa JK alipoanza muhula wake wa kwanza mwaka 2005 wa kuiongoza nchi hii alichagua watu ambao ni cream ya juu kabisa kutoka chama chake cha CCM ili kuunda baraza lake la mawaziri wakiongozwa na Mhe. Edward Lowassa kama Waziri Mkuu.

Baada ya takribani miaka miwili mitatu hivi Waziri wake Mkuu akaingia katika kashfa kubwa ya Richmond hivyo akalazimishwa na Bunge kujiuzuru na kusababisha JK abadilishe baraza lake la mawaziri na kumteua mtoto wa mkulima Mhe. Kayanza Peter Pinda kuwa Waziri Mkuu na mawaziri ambao ni cream iliyobakia ya CCM ndani ya Bunge!

Baada ya kuanza awamu yake ya pili JK aliteua baraza jipya la mawaziri likiongozwa na Mhe. Pinda ikiwa ni cream mpya ya awamu ya pili toka CCM. Hata hivyo JK alilazimika kubadili baraza lake la mawaziri baada ya kashfa mbalimbali walizopata mawaziri wake katika sekta ya fedha, maliasili na madini!

Hivi sasa kutokana na usimamizi mbovu wa operation Tokomeza mawaziri wanne wameng'olewa! Aidha kuna mawaziri kadhaa ambao wametajwa na CCM kuwa ni mizigo wakiwemo Hawa Ghasia, Selina Kombani, Christopher Chiza na Dr. Shukuru Kawambwa. Pia wamo mawaziri waliotajwa na upinzani kuwa wao si mizigo tu bali ni mabomu! Hawa ni pamoja na Ole Madeye, Mkuchika na Mulugo! Vilevile baadhi ya wabunge kutoka pande zote za chama tawala na upinzani wanadhani kuwa hata Mhe. Pinda ni bomu!

JK analazimika kusuka upya baraza lake la mawaziri! Cream ndani ya CCM imekwisha!

Sasa JK afanye miujiza gani kupata watu mahiri wa kutuvusha salama katika awamu hii?!

Wana JF tujadili na kumshauri Rais wetu ili aweze kuteua watu makini na mahiri katika utendaji ili tuondokane na hili janga la umaskini!! Ikumbukwe kuwa JK amekwishamaliza nafasi zake 10 za kuteua wabunge!
 
Akafie kwao msoga,tumemchoka,alipokuwa anatengeneza mfumo wa kifisadi kwenda magogoni alidhani ni mat.a.ko kwamba kila mtu anayo! Tumchoka huyu mzi....go no moja
 
JK anapaswa kumrejesha Mhe Lowassa kwenye nafasi ya PM...kwa kufanya hivyo atakuwa ameokoa gharama ya kuwa na mlolongo mrefu wa ma-PM waliopita, pili atapata mtu anaeheshimika na mtendaji...at least kuna ambao wanamgwaya...Faida nyingine kichama itakuwa amevunja mpasuko ambao unaoneka ni inevitable kwa sasa...
 
Mkuu viongozi wanatengenezwa ama waandaliwa. CCM pamoja na serikali haijawahi kuwa mpango wa kuwaandaa viongozi wa vizazi vijavyo baada ya kizazi kilichopo. dhana hii ndio inawatesa CCM kwa sasa na ndio maana utakuta mtu anakuwa mbunge kwa miaka 20 kwenye jimbo moja halina maendeleo na bado chama kina mpitisha kugombe tena kwenye uchaguzi unafuata. Hivyo basi inapotokea changamoto kama iliyopo sasa the best choices either zimekwisha, ama zimetumika na sasa haziwezi kufanya kazi kwenye mazingira yaliyopo ama haziendani na wakati. Hiki sio tu kwenye Bunge hata kwa watendaji wa Serikalini. Mfano mmoja MD wa SIDO ame staff tangu June hakukua na jinsi ya kupata mrithi wake haji Juzi. JK alifahamu security officers wake wakuu (IGP, DCI,etc) wanastaaf mwaka huu lakini hakuna aliekua ameandaliwa hivyo wanaongezewa miaka ya kufanya kazi. Je kwa style hii tutafika?
 
Ni vema tukafanya uamuzi wa busara katika katiba mpya kuwa watendaji wote wa serikali wakiwemo mawaziri wasiwe wabunge! Kwa kufanya hivyo kutamwezesha rais awe na wigo mpana wa kuteua wasaidizi wake!
 
Ni ukweli usiopingika kuwa JK alipoanza muhula wake wa kwanza mwaka 2005 wa kuiongoza nchi hii alichagua watu ambao ni cream ya juu kabisa kutoka chama chake cha CCM ili kuunda baraza lake la mawaziri wakiongozwa na Mhe. Edward Lowassa kama Waziri Mkuu.

Baada ya takribani miaka miwili mitatu hivi Waziri wake Mkuu akaingia katika kashfa kubwa ya Richmond hivyo akalazimishwa na Bunge kujiuzuru na kusababisha JK abadilishe baraza lake la mawaziri na kumteua mtoto wa mkulima Mhe. Kayanza Peter Pinda kuwa Waziri Mkuu na mawaziri ambao ni cream iliyobakia ya CCM ndani ya Bunge!

Baada ya kuanza awamu yake ya pili JK aliteua baraza jipya la mawaziri likiongozwa na Mhe. Pinda ikiwa ni cream mpya ya awamu ya pili toka CCM. Hata hivyo JK alilazimika kubadili baraza

lake la mawaziri baada ya kashfa mbalimbali walizopata mawaziri wake katika sekta ya fedha,
maliasili na madini!

Hivi sasa kutokana na usimamizi mbovu wa operation Tokomeza mawaziri wanne wameng'olewa! Aidha kuna mawaziri kadhaa ambao wametajwa na CCM kuwa ni mizigo wakiwemo Hawa Ghasia, Selina Kombani, Christopher Chiza na Dr. Shukuru Kawambwa. Pia wamo mawaziri waliotajwa na upinzani kuwa wao si mizigo tu bali ni mabomu! Hawa ni pamoja na Ole Madeye, Mkuchika na Mulugo! Vilevile baadhi ya wabunge kutoka pande zote za chama tawala na upinzani wanadhani kuwa hata Mhe. Pinda ni bomu!

JK analazimika kusuka upya baraza lake la mawaziri! Cream ndani ya CCM imekwisha!

Sasa JK afanye miujiza gani kupata watu mahiri wa kutuvusha salama katika awamu hii?!

Wana JF tujadili na kumshauri Rais wetu ili aweze kuteua watu makini na mahiri katika utendaji ili tuondokane na hili janga la umaskini!! Ikumbukwe kuwa JK amekwishamaliza nafasi zake 10 za kuteua wabunge!
Ampe Zito
 
Ni vema tukafanya uamuzi wa busara katika katiba mpya kuwa watendaji wote wa serikali wakiwemo mawaziri wasiwe wabunge! Kwa kufanya hivyo kutamwezesha rais awe na wigo mpana wa kuteua wasaidizi wake!

Hili ni pendekezo la busara sana katika katiba mpya lakini cha kushangaza ni kwamba wabunge wa ccm wanalipinga kwa uroho wao wa madaraka; kwavile ccm wamechakachua sheria ya uundwaji wa bunge la katiba wanaweza kutumia wingi wa wajumbe wao kupinga mapendekezo ya wananchi walio wengi kama hili la wabunge wasiwe mawaziri na uwepo wa serikali tatu!! Tungoje vituko vya magamba kwenye bunge la katiba.
 
Tumeshamchoka huyo,akitaka ateue hata wanafamilia wake!

Hivi akikuteua wewe au mimi halafu kwa bahati mbaya ikabidi tuwajibike kama ilivyotokea juzi, makosa bado yanaendelea kuwa yake JK tu? Nini maana ya kiapo unapoteuliwa kuwa waziri/kiongozi? Huwa unaapa kwa JK au kwa Mungu na watanzania wakiwa mashahidi?
 
Hili ni pendekezo la busara sana katika katiba mpya lakini cha kushangaza ni kwamba wabunge wa ccm wanalipinga kwa uroho wao wa madaraka; kwavile ccm wamechakachua sheria ya uundwaji wa bunge la katiba wanaweza kutumia wingi wa wajumbe wao kupinga mapendekezo ya wananchi walio wengi kama hili la wabunge wasiwe mawaziri na uwepo wa serikali tatu!! Tungoje vituko vya magamba kwenye bunge la katiba.
Watanzania tunatakiwa kuvaa ujasiri wa kuchagua watu makini na wasio waoga kuelezea matakwa yetu watakaoingizwa katika bunge la katiba!
 
PM awe Filikunjombe! Hivi mbunge wako Aliko Kibona anafaa kuwa hata naibu w?
 
Hata yeye mwenyewe Jk nahisi anajuta kwa Kuwait kwenye chama chenye watendaji wabovu, mikutano yore ya nje na mikubwa ya ndani lazima ashiriki yeye akiteua mawaziri kumwakilisha hata hutuba tu walizoandaliwa hawawezi kuzisoma vilevile hata hao wanaobaki akiwa nje ni madudu Mara tutatoa taraka.
 
Watanzania tunatakiwa kuvaa ujasiri wa kuchagua watu makini na wasio waoga kuelezea matakwa yetu watakaoingizwa katika bunge la katiba!

Inaelekea hujaisoma sheria inayohusu nani ataingia kwenye bunge la katiba!! Licha ya wabunge wote na wajumbe wa baraza la wawakilishi kuwa wajumbe wengine wanaobaki wote wanateuliwa na RAIS ingawa wanapendekezwa na taasisi mbali mbali!!! Hapa ndipo magamba walipolipiga bao Taifa la wadanganyika!!
 
Waziri mkuu awe mwakyembe

Licha ya huyo Mwakyembe hata kama waziri mkuu atakuwa mwakychungwa mambo yatakuwa ni yale yale tu kwasababu kwa mfumo huu tulionao waziri mkuu hana powers zozote anaehodhi madaraka yote ni RAIS!! Pinda is just a victim of circumstsnces kwasababu hao mawaziri hana mamlaka nao they are all accountable kwa Kikwete na sio mawaziri tu bali hata makatibu wakuu na appointees wa RAIS wote na ndio maana kama mtakumbuka wakati wa sakata la Jairo, Pinda hakuweza kumchukulia hatua za kinidhamu mpaka Kikwete aliporudi!! The problem lies with the system.
 
Back
Top Bottom