Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,795
- 12,239
Ni ukweli usiopingika kuwa JK alipoanza muhula wake wa kwanza mwaka 2005 wa kuiongoza nchi hii alichagua watu ambao ni cream ya juu kabisa kutoka chama chake cha CCM ili kuunda baraza lake la mawaziri wakiongozwa na Mhe. Edward Lowassa kama Waziri Mkuu.
Baada ya takribani miaka miwili mitatu hivi Waziri wake Mkuu akaingia katika kashfa kubwa ya Richmond hivyo akalazimishwa na Bunge kujiuzuru na kusababisha JK abadilishe baraza lake la mawaziri na kumteua mtoto wa mkulima Mhe. Kayanza Peter Pinda kuwa Waziri Mkuu na mawaziri ambao ni cream iliyobakia ya CCM ndani ya Bunge!
Baada ya kuanza awamu yake ya pili JK aliteua baraza jipya la mawaziri likiongozwa na Mhe. Pinda ikiwa ni cream mpya ya awamu ya pili toka CCM. Hata hivyo JK alilazimika kubadili baraza lake la mawaziri baada ya kashfa mbalimbali walizopata mawaziri wake katika sekta ya fedha, maliasili na madini!
Hivi sasa kutokana na usimamizi mbovu wa operation Tokomeza mawaziri wanne wameng'olewa! Aidha kuna mawaziri kadhaa ambao wametajwa na CCM kuwa ni mizigo wakiwemo Hawa Ghasia, Selina Kombani, Christopher Chiza na Dr. Shukuru Kawambwa. Pia wamo mawaziri waliotajwa na upinzani kuwa wao si mizigo tu bali ni mabomu! Hawa ni pamoja na Ole Madeye, Mkuchika na Mulugo! Vilevile baadhi ya wabunge kutoka pande zote za chama tawala na upinzani wanadhani kuwa hata Mhe. Pinda ni bomu!
JK analazimika kusuka upya baraza lake la mawaziri! Cream ndani ya CCM imekwisha!
Sasa JK afanye miujiza gani kupata watu mahiri wa kutuvusha salama katika awamu hii?!
Wana JF tujadili na kumshauri Rais wetu ili aweze kuteua watu makini na mahiri katika utendaji ili tuondokane na hili janga la umaskini!! Ikumbukwe kuwa JK amekwishamaliza nafasi zake 10 za kuteua wabunge!