JK aomba kura kwa kukaa chini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK aomba kura kwa kukaa chini

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kwamwewe, Sep 25, 2010.

 1. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2010
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,315
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  JK aomba kura kwa kukaa chini  [​IMG]Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Jakaya Kikwete ,akiwa ameketi chini ardhini ili kumsikiliza Mama Sara Mageni mkazi wa Wilaya ya Makete, wakati mgombea huyo alipowasili kuhutubia mkutano wa kampeni. Sara alikuwa akitoa shukrani zake kwa Rais Kikwete baada ya kumnunulia Bajaj ili kurahisisha shughuli zake, alipotembelea wilaya hiyo mwaka jana
  Fidelis Butahe, Iringa
  MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete alitumia staili ya aina yake kuomba kura wakati alipolazimika kuketi ardhini ili kumsikiliza mwananchi wakati akiwa kwenye moja ya mikutano ya kampeni za kuomba kura kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31.

  Mbali na tukio hilo, kabla ya kupanda jukwaani mjini

  Ludewa wilayani Mbalali, Kikwete alikuwa akizungumza na simu na baada ya kumaliza aliwaambia wananchi kuwa alikuwa akizungumza na balozi wa Marekani nchini Tanzania na kwamba balozi huyo amemueleza kuwa Rais Barack Obama ameahidi kuwa serikali yake itaendelea kutoa misaada kwa Tanzania.

  Watu wengi hawakuamini macho yao wakati Kikwete alipoanza kukaa chini kwa ajili ya kumsikiliza mwananchi huyo, Sara Mageni kwenye mkutano wake uliofanyika kwenye Uwanja wa Mabehewa wilayani Makete ambako wakati huu wa majira ya kipupwe vumbi limeshamiri.

  Sara, ambaye ni mlemavu wa miguu, alikuwa akitoa shukrani zake kwa Kikwete ambaye alimnunulia pikipiki ya matairi matatu aina ya Bajaj ili kurahisisha shughuli zake wakati mwenyekiti huyo wa CCM alipotembelea wilaya hiyo mwaka jana.

  Akiwa katika uchangamfu wake wa kawaida na mavazi yake ya CCM, Kikwete aliketi chini kwenye vumbi na nyasi na kumsikiliza Sara na alimuuliza ni hali gani anayokabiliana nayo kwa wakati huo.

  Akiwa wilaya ya Makete, Kikwete amewahakikishia watu wenye ulemavu kuwa mwaka 2010-2015, serikali yake itaendelea kulinda haki za walemavu.

  "Serikali ya CCM inalinda haki za walemavu kutokana na kuridhia haki za kimataifa za walemavu, pia tutajenga kwa kiwango cha lami barabara ya Njombe-Makete yenye urefu wa kilomita 109," alisema Kikwete.

  Aliongeza kusema: "Kukamilika kwa barabara hii kutasaidia wakulima kusafirisha zao la pareto."

  Kikwete, ambaye anawania kurejea Ikulu kumalizia ngwe ya pili, alisema zao hilo limepata mnunuzi kutoka Marekani hivyo wananchi wa Makete wanatakiwa kutumia fursa hiyo kuimarisha pareto pamoja na kulifufua shamba la Kituro ambalo lilikuwa maarufu kwa ufugaji wa kondoo wa sufi.

  Katika mkutano huo, Kikwete alimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Makete, Binilith Mahenge pamoja na wagombea udiwani.

  Akizungumzia ujumbe aliopewa kwenye simu na balozi wa Marekani nchini, Kikwete alisema kuwa amehakikishiwa misaada kuendelea kumiminika Tanzania kutoka taifa hilo kubwa duniani

  "Nilikuwa nazungumza na balozi wa Marekani nchini na amenieleza kuwa rais wa nchi hiyo, Barack Obama akiwa katika mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa alitolea mfano kuwa Tanzania ni nchi inayofuata utawala bora hivyo wataendelea kutusaidia," alisema Kikwete,

  "Maneno haya yanasemwa na Wamarekani sio mimi... watu wanasema tu Marekani, Marekani lakini huo ndio ukweli wenyewe; huo ndio ujumbe niliopata; wameonyesha kutusaidia na watatusaidia,".

  Akiwa Igwachanya, mgombea huyo wa CCM aliahidi kuwa serikali ijayo itaendea kuhamasisha uanzishwaji wa Vyama vya Kuweka na Kukopa (Saccos) ili kuwainua kiuchumi wananchi na kuondokana na umasikini.

  Alisema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, serikali yake ilihamasisha uanzishwaji wa Saccos hali iliyowawezesha wananchi wengi kupata mikopo na kujiendeleza.

  "Saccos ndio njia zitazowawezesha wananchi wenye kipato cha chini kukopa na kujiendeleza kiuchumi, hivyo tutaenda kuhamamisha uanzishwaji wa Saccos ili wananchi wengi zaidi waweze kujiendeleza," alisema Kikwete.

  "Bila kufanya hivyo, itakuwa vigumu kuwainua wananchi wa chini. Tajiri kama (mwenyekiti wa CCM mkoani Iringa) Deo Sanga akienda benki kukopa Sh400 milioni baada ya saa moja atapatiwa, lakini wewe mwananchi masikini ukitaka hata mkopo wa Sh2,000 itachukua hata miaka 10 na usipate. Hivyo njia ya kuwaokoa ni uanzishwaji wa Saccos," alisema Kikwete.

  Aidha, mgombea huyo wa urais alisema serikali yake ijayo itaanzisha shirika la mazao mchanganyiko, ambalo litawaongezea soko la uhakika wakulima wa mazao mbalimbali.

  "Tulianzisha SGR kwa ajili ya zao la mahindi, lakini sasa tutaanzisha shirika la mazao mchanganyiko ambalo wakulima wa ufuta, maharage, kunde na mengineo wataweza kuuza mazao yao kwa uhakika," alisema Kikwete.
   
 2. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Hakuwa anaomba kura alikuwa anguke hivyo kaamua kujifanya anakaa chini.

  Afya mgogoro.
   
 3. a

  akilinyingi Member

  #3
  Sep 25, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani hebu muacheni baba wa watu maneno maneno tu, afya mgogoro ni nani mwenye uhakika na afya yake acheeeeeeeeeeeeeeni hizo
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  kampeni za nyasi kwa nyasi
   
Loading...