Elections 2010 Jk aogopa tucta kumobilise wafanyakazi, shimiwi yapigwa stop

Shoo Gap

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
246
71
Shirikisho la michezo ya Idara za serikali, wizara na ofisi za wakuu wa mikoa(SHIMIWI) limetangaza kusitishwa kwa michezo hiyo iliyokuwa ifanyike Tanga 17th September -2nd October.

Wadadisi wa mambo wanasema maandalizi yote yalishakamilika na fedha zilishatengwa, lakini jana ghafla yametangazwa kusitishwa, hivyo hakutakuwepo na mashindano hayo mwaka huu. "Wanaogopa mkusanyiko mkubwa kama huu wa wafanyakazi toka idara zote za serikali na mikoa yote huenda ukatumiwa na TUCTA kuendelea kumwaga 'sumu' kwa wafanyakazi, ili wasimpe kura aliyezikataa" alisikika mfanyakazi mmoja akisema.

Serikali itakuwa imepata hasara kubwa kwa kusitisha mashindano haya kwani, idara karibu zote walishafanya booking za hoteli na kulipia advance, baadhi ya idara zilishafanya manunuzi ya vifaa vya michezo, na gharama kubwa ilishatumika kufanya maandalizi kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja.

HII SIO DALILI NZURI HATA KIDOGO.
 
Pengine serikali inajaribu kupunguza matumizi makubwa ya uendeshaji wa serikali yake. Ulilifikiria hilo?
 
You must be joking -- Kupunguza matumizi ya uendeshaji wa serikali ? Lets be serious for once.
 
Pengine serikali inajaribu kupunguza matumizi makubwa ya uendeshaji wa serikali yake. Ulilifikiria hilo?

Leo ndo wanashtuka kubana matumizi? Wangeanza kwa kuacha kununua mashangingi, safari za anasa nje ya nchi n.k.
 
Uwoga hauwaishi, kila kitu wanaogopa. Kutajwa wezi wanaogopa, mdahalo wanaogopa, mashindano wanaogopa sasa tuwaeleweje?
 
Sidhani kama ni hatua ya kubana matumizi, nafananisha hii na ile ya kuzuia wasomi wa vyuo vikuu kurudi kabla ya uchaguzi.... typical signs of a coward

Ukiwa mwovu, hata ukiona watu wanacheka unahisi wanakucheka wewe...

very low indeed
 
Pengine serikali inajaribu kupunguza matumizi makubwa ya uendeshaji wa serikali yake. Ulilifikiria hilo?

You are kiddin me may be sijaielewa hii statement yako vizuri hebu irudie kuiandika upya unapswa kuiedit
 
Uwoga hauwaishi, kila kitu wanaogopa. Kutajwa wezi wanaogopa, mdahalo wanaogopa, mashindano wanaogopa sasa tuwaeleweje?
hakuna namna ya kuwaelewa si watu hao, ni waoga, wachoyo, wanafiki na hawapendi watu wajue maovu

divide and rule is their rule of the game
 
hakuna namna ya kuwaelewa si watu hao, ni waoga, wachoyo, wanafiki na hawapendi watu wajue maovu

divide and rule is their rule of the game

Hasa kwa wakati huu maana wanahangahika in every corner kama panya anayetafuta msosi chochote kile ambacho kinakutanisha kikundi cha watu sasa hivi ni mwiba kwao kwa maana kwa kuwa matendo yao si mazuri basi kila saa wako alert
 
Kila uovu huwa una mwisho. Leo hi KANU kiko wapi? Makaburu Afrika Kusini wako wapi? Zambia, Malawi, vyama kongwe viko wapi? TIME WILL TELL!
 
Leo ndo wanashtuka kubana matumizi? Wangeanza kwa kuacha kununua mashangingi, safari za anasa nje ya nchi n.k.

Wanunue pikipiki kwa wananchi, wawanunulie wanavijiji vitrekta vibovu from China, wawanunulie wanawake kanga, akina dokii nao wapate posho zao unadhani wanazitoa wapi pesa zote hizo? Bado kuwa lipa watu pesa za kwenda kuhudhuria mikutano
 
This is a serious issue.
Ila kwa sababu idara tajwa ziko chini ya serikali, sidhani kama kuna maswali yataulizwa hapo.
Labda moja ya vyama vya upinzani walifuatilie hili jambo na kupata maoni ya wahusika.

Na ni hii hii serikali ya chama kinachotoa ahadi za kukuza michezo Tanzania?
 
Kama ni kunaba matumizi wasingefanya maanadalizi yote alafu lastmin unacancel kila kitu tayari wameshaingiza hasara. hawana lolote ni kukwepa TUCTA TU wanajifanya kuwapa nafasi wafanyakazi kutoa huduma leo ndio wamejua kuwa wanahitaji kutoa huduma??

WAFANYAKAZI MSIMAMO WETU ULE ULE HATUWAPI KURA MAANA ITAKUWA TUNAJIPENDEKEZA KWAO, TENA NI KASHFA KUBWA MTU AMETUKANA MBELE YA ULIMWENGU MZIMA HALAFU TUNAMPA KURA LOL! TBC INAONEKANA SEHEMU NYINGI DUNIANI TENA KWA MBWEMBWE NYINGI NA VIFIJO VYA WALE WAZEE WALIOKUWA WANAMPIGIA MAKOFI AKATUKANA LEO HII TUMPE KURA HAIWEZEKANI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
hii ni sawa na kuziba pancha wakati ukijua tairi ni bovu madhara yake ni makubwa sana...yetu macho
 
Kama ni kunaba matumizi wasingefanya maanadalizi yote alafu lastmin unacancel kila kitu tayari wameshaingiza hasara. hawana lolote ni kukwepa TUCTA TU wanajifanya kuwapa nafasi wafanyakazi kutoa huduma leo ndio wamejua kuwa wanahitaji kutoa huduma??

WAFANYAKAZI MSIMAMO WETU ULE ULE HATUWAPI KURA MAANA ITAKUWA TUNAJIPENDEKEZA KWAO, TENA NI KASHFA KUBWA MTU AMETUKANA MBELE YA ULIMWENGU MZIMA HALAFU TUNAMPA KURA LOL! TBC INAONEKANA SEHEMU NYINGI DUNIANI TENA KWA MBWEMBWE NYINGI NA VIFIJO VYA WALE WAZEE WALIOKUWA WANAMPIGIA MAKOFI AKATUKANA LEO HII TUMPE KURA HAIWEZEKANI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Jk alinitukana pale Diamond Jubilee akaniambia hataki kura yangu hata nikigoma miaka minane leo nimpe ninakichaa, hata nikiwa naelekea kaburini kura yangu msimpe JK bora nimpe mgombea wa TLP kama Slaa hatakuwepo.
 
Back
Top Bottom