JK anoa panga CCM; WABUNGE WALIOWEKA SAINI KUMNG’OA PINDA KUKATWA NEC

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
h.sep7.gif


• WABUNGE WALIOWEKA SAINI KUMNG’OA PINDA KUKATWA NEC

na Mwandishi wetu


PANGA la vikao vya juu vya mchujo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), limenolewa.


Vikao hivyo vya mwisho vya mchujo ambavyo vitaendeshwa na Mwenyekiti wake taifa, Rais Jakaya Kikwete, vinatarajia kuanza rasmi Septemba 21 na 26.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa wakati vikao hivyo vikianza, CCM imepanga mkakati mzito kukata majina ya baadhi ya wagombea uongozi ambao pia ni wabunge ndani ya Bunge la Muungano.


Kundi lingine la walengwa wa mkakati ule ni la viongozi wa CCM hasa wenyeviti wa mikoa na wilaya waliokuwa wakiendeleza makundi na malumbano na kusababisha kuporomoka kwa hadhi ya chama hicho.


Habari zaidi kutoka ndani ya CCM, zinasema kuwa NEC imepanga kufanya maamuzi magumu ya kuwakata baadhi ya wagombea waliokuwa wakiandamwa na tuhuma za ufisadi hata kama watakuwa wamepita bila kupingwa au kupitishwa na vikao vya chini.


Tayari Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, mmoja kati ya makada wanaoandamwa kwa tuhuma za ufisadi, amepita bila kupingwa wakati majeruhi mwingine wa ufisadi, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, amepitishwa na vikao vya chini, sasa wanasubiri idhini ya NEC.


Duru za siasa kutoka ndani ya CCM, zinasema kuwa wabunge wanaolengwa kwenye panga hilo ni wale waliokuwa kimbelembele kuikosoa serikali bungeni na kufikia hatua ya kusaini majina yao kwenye fomu zilizokuwa zikipitishwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ili kupata saini 70 za kumng’oa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.


Tayari athari za saini za kutaka kumng’oa Waziri Pinda zimeshaonekana kwa Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono ambaye hivi karibuni alienguliwa katika kikao cha mchujo wilayani na yeye kutahadharisha kama jina lake halitapitishwa NEC, ndani ya CCM patachimbika.


Mkono ambaye ni wakili maarufu nchini, aliwania nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazee taifa. Wengine waliowania nafasi hiyo ni Mbunge wa Bukoba Vijijini, Joson Rweikiza, Matha Mlata na Salum Chicago.


Waliopendekezwa na vikao vya chini kuwania kiti hicho ni Abdallah Bulembo, Matha Mlata na Halima Mamuya.


Kwa upande wa Umoja wa Wanawake, waliopendekezwa ni pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sofia Simba, Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango na Mayrose Kavura Majinge.


Mbunge mwingine aliyekwishaenguliwa na vikao vya chini ni Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, ambaye alikuwa akichuana vikali na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.


“Tunaambiwa wabunge wengi walioomba NEC watakatwa hasa wale waliotaka kumng’oa Pinda na sababu ya pili ni kwamba wabunge wana nafasi kumi za NEC ndani ya Bunge, hivyo hawana sababu ya kuwania NEC nje ya Bunge,” alisema mtoa habari wetu.


Mkono, Nagu na wengine waliopendekezwa kuachwa na vikao vya chini, sasa wanategemea kudra za NEC.


Mkoani Shinyanga, taarifa zinasema kuwa mgawanyiko umetokea baada ya kuwapo taarifa kwamba kuna mpango wa kulikata jina la mwenyekiti wa sasa wa CCM mkoa huo, Khamis Mgeja.


Habari zinasema kuwa mkakati huo unapangwa na vigogo wa CCM kutoka ofisi ndogo ya makao makuu, Lumumba, jijini Dar es Salaam na kumhusisha mtoto wa kigogo.


Hatua hiyo imedaiwa kuwa ni moja ya mikakati ya viongozi hao kupanga safu ya uongozi mwaka 2015 ambapo Mgeja anatajwa kuwa mmoja wa watu anaopingana nao hivyo kuwa kikwazo katika kufanikisha mipango yao.


Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya wana CCM mjini hapa, inadaiwa kwamba vigogo hao hivi sasa wanajitahidi kuwashawishi wajumbe wa vikao vya juu ili kuhakikisha jina la Mgeja linakatwa na linabakizwa la mtu ambaye ni chaguo lao.


Yapo madai kwamba mkakati wa vigogo hao unaungwa mkono na baadhi ya wabunge wa CCM mkoani Shinyanga ambao hawamuungi mkono Mgeja.


Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wamewaeleza waandishi wa habari mjini Shinyanga kwamba tayari kuna vikao vingi vya usiku vinavyofanywa na mawakala wa vigogo hao kwa lengo la kuhakikisha Mgeja hachaguliwi hata kama NEC itakuwa imerejesha jina lake.


Katika hali isiyokuwa ya kawaida mmoja wa wagombea ambaye alipata fununu za jina lake kupendekezwa kuwa miongoni mwa wagombea nafasi ya uenyekiti wa mkoa, aliamua kufanya sherehe kubwa katika moja ya baa eneo la Lubaga ambako alisikika akitamba kwamba yeye ni chaguo la Rais Jakaya Kikwete.


 
Hakuna Demokrasia ndani ya CCM; Sasa Mkono ni FISADI kwanini na wengine Wamepita? CHENGE n.w

Msicheze na ZITTO KABWE ndio aliyeanzisha... wa CCM ni scape goat... Kikwete kafurahi kapata wa kutupa nje ya NEC


 
Hivi Filikunjombe naye anagombea NEC? Huu ni mtihani mwingine kwa CCM yaani mtu apite bila kupingwa halafu jina lake lisirudishwe? Naona CCM wanataka kusababisha vita y majimaji!
 
Huyo mtoto wa kigogo hakuna mwengine isipokua Prince Ridhwan mna yeye na Nape Nauye wameigeuza CCM kama mali yao ila kila lenye mwanzo halikosi kua na mwisho...CCM Oyeeeeeeeeeeeeee
 
Kwa maelezo haya nashawishika kutambua kua katika usukaji wa jopo la mawaziri lililowaondoa kina Ngeleja and Co halikuwafurahisha.

Na pia nashawishika waliteuliwa kiushkaji/undugu au ujamaa wa karibu na si utendaji. Ili kumuokoa W/Mkuu ilimbidi kuunda upya jopo la Mawaziri ili kukata maneno ya Watanzania.

Kisasi ndio historia ya huyu jamaa kama mnakumbuka mwanamziki maarufu anaeozea jera kuna tetesi kisa kilianzia wakati hajawa Mkuu, alipopata rungu tu kasuka kilichompotezea jera.

Auae kwa panga nae atapitia hapohapo!
 
Kama hili likibainika kufanywa kwa madhumuni ya kuwaengua waliopinga malfunctioning ya serikali, basi nashawishika kusema hapo ndiyo CCM itazidi kujichimbia kaburi. Wengi wetu tumebakiwa na chembechembe za kuiamini CCM na serikali yake sababu tu ya hawa wachache sana wasiokubaliana na maovu/hujuma ndani ya chama na serikali. Pia wakilitekeleza hill, basi tutadhihirisha ya kuwa CCM na serikali yake haitusimamii hyena wannchi, bali ipod kwa ajili ya mutants ufisadi na kulinda ufisadi kwa nguvu zote.
 
ni funika kombe mwanaharamu apite tu hii.
hata riziwana na maza wake wawepo kwenye kundi la mafisadi pia.
 
Mpaka nimecheka aisee. Wenye tuhuma za mafisadi out, Wenye kiherehere kutetea maslahi ya wananchi out. Wanabaki wale wakimya wanaotetea maslahi ya Kiwete na familia yake. Very good move towards the grave. 2015 tutakuja kuweka shada la maua kwenye kaburi la CCM
 
Kaburi la ccm lipo karibu kumalizika 2015 ndo tamati yao hawa wahuni
 
Ccm watakuwa wanapoteza mda bse kwa siasa za sasa watakaotemwa wana pa kwenda
 
Back
Top Bottom