JK angepewa Nchi mwaka 1995 tungekuwa wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK angepewa Nchi mwaka 1995 tungekuwa wapi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by akilimtindi, Jan 4, 2009.

 1. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2009
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wakuu samahanini sijatokea kwa siku kadhaa lakini naomba nitokee kwa haka ka-swali kangu, nimekauliza kwa kuwa kuna watu wengi humu naona sasa wanamtetea JK kwamba ni safi sana sasa.

  Mimi naona Mkapa alijitahidi sana alipopokea nchi maana ilimbidi kwanza kuweka utaratibu kwenye mstari maana kodi ilikuwa ni zero na serikali ilishaishiwa kabisa, ingawa tunakubali pia kwamba upinzani kisiasa haukuwa mkubwa kwahiyo CCM haikutumia mamilioni kupiga kampeni. Ilitumika tu fimbo ya mchonga. Kwahiyo Mkapa alipopokea ilimbidi kutafuta mbegu akapanda, kisha akapalilia halafu mahindi yalipokuwa tayari akakata kidogo akachoma, akamkwanyulia shemejiye Yona kidogo wakaendelea hivyo hivyo.

  Lakini hii ya Mkwere mimi naona sio ulafi ila uzumbuku, alisema vizuri sana alipopewa nchi mwaka 2005 kwamba Mzee Ben ameacha mambo safi. Iweje mara hili mara lile? Akampa swahiba wakashirikiana kuvuna mahindi yote wakachezea chezea wakala yote bila hata kuacha mbegu. Sasa tuwaeleweje wala mbegu? Alipoachiwa nchi alisema msingi ulikuwa tayari yeye sasa ni kujenga tu, juzi after miaka 3 anasema alikuwa anaweka misingi mizuri sasa muda si mrefu ataanza kujenga.

  Naamini mwaka 2010 atasema ameshaweka misingi, sasa tumpe miaka mingine 5 apandishe mjengo. Na mimi naamini watanzania watampa. Je tuko tayari kufanya tathmini 2015?
   
 2. Companero

  Companero Platinum Member

  #2
  Jan 5, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Uozo mwingi unaoisumbua Serikali ya JK imeurithi kutoka kwenye Serikali ya Ben.

  -Sheria mbovu za kodi za madini zilitungwa kizembe wakati wa Ben
  -Sheria za Ardhi zilitungwa na kurekebishwa kiholela wakati wa Ben

  -Mikataba mibovu ya IPTL ilisainiwa wakati wa Ben
  -Mikataba mibovu ya CW ilituadhiri wakati wa Ben

  -Kiwira, Meremeta, Tangold,...,...Ben
  -M Bank, BOT EPA, PEDP,...,...Ben
   
 3. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2009
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
   
 4. A

  Adili JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 2,017
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Tungekuwa Kenya!
   
 5. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Na pia inamgusa JK akiwa kama cabinet member na pia waziri! When you point one finger, three point back to you.

  Let us talk about:
  EPA - it is uchaguzi 2005 so it falls in JK's and his cronies' lap, Richmond, Ndege ya jeshi iliyodondoka ikisafirisha wageni wasioleleweka wa rais (wazungu waandishi), Sullivan summit and the millions of dollar spent for nothing, safari zisizoisha za JK. Yaani hizi nimezitaja bila hata kutumia dk 2 kufikiria, je tukianza analysis, unafikiri list in 3 years itazidi ile ya Ben in 10 years.
  We acha tu.....
  Mimi binafsi nadhani tunahitaji kuwa fair na JK, he just wanted to be president for the marupurupu and also to hear his name with the title Mr President. But he never was prepared to govern. IN this sense, I see some very strong similarities with W. Bush. Maybe that's why they are friends! :)
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kumbuka JKN aalikuwa hai bado kipindi hicho!!!!!
   
 7. Modereta

  Modereta Senior Member

  #7
  Jan 5, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kiti moto anaekijua ni yule aliyekikalia. Tuache munkari tuwe analytical na tutoa mawazo kipi kifanyike ili tuendele, pengine bila hata hawa wanasiasa. Wakati mwingine nakumbuka kule uchagani pale wanakijiji kila jumamosi walijitolea kutengeneza barabara zao bila kungoja mbunge au waziri kuja wahamasisha. Yako maendeleo mengi yanaweza kuletwa bila ya hawa wanasiasa. Mbona vikao vya harusi vyenye bajeti ya papo kwa papo ya millioni 5-15 vinafanyika kwa bidii bila wanasiasa??????????????
  Tufanye yetu halafu tuwakosowe huku tumeshiba ugali tuliolima wenyewe.
   
 8. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Point taken, mkuu, but still the buts and ifs only count to a certain extent. We don't know what would have happened if JKN would be still alive, now would we? We are also in danger of elevating JKN to sainthood, as if we needed and still need some invisible hand of justice and goodness to guide us. JKN did have weight but about his influence, we can never know whether it would be still strong or wanning.
  However if we look at the fact, BWK took over the country in a very bad economic shape in 1995 and in 2005, handed it over with double digit economic growth. In 3 years of JK, economic growth has declined, the ruling party is in fractures and FDI is plunging. And if you ask any ordinary Tanzania, "Are you better off, than in 2005?" a vast majority will say "NO" whether this is true or perceived, but this is the bottomline that I believe we need to look at.
  Again, I still feel that we are unfair with JK because he never thought he needed to govern. He was always comfortable handing over the nitty gritty part of his (campaign, ministerial post, presidency) to his sidekicks like Membe, EL and RA.
   
 9. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2009
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Enzi za ben kazi ilikuwa inathamani, sasa hivi ni ujanjaujanja tu hamna lolote linalofanyika,hata sarafu ilikuwa inathamani,kigamboni ilikuwa bado haijauzwa, sasa hivi ni upuuzi mtupu!
   
 10. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mkuu, nakubali hoja yako, lakini unayoyasema yanawezekana mpaka level fulani tu, beyond a certain level, ni lazima mwanasiasa au political administrator anahitajika. Hatuwezi kuendelea bila viongozi bora, hatatukitaka hayo maendeleo kwa kasi mpya na ari mpya, kwikwikwii!
  but seriously, muda umefika wa kuchagua viongozi bora. Period.
   
 11. M

  Middle JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2009
  Joined: Feb 7, 2007
  Messages: 243
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sasa tumpe nani 2010?
   
 12. Modereta

  Modereta Senior Member

  #12
  Jan 5, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe kuwa yako tunayoweza fanya wenyewe mpaka mahali fulani, halafu tuhitaji wanasiasa. Ila sasa wakati mwingine tunalalamikia hata yale madogo tu.
  Pia kweli bila viongozi wazuri tutaendelea kupiga kelele tu, hivyo tunapofika kwenye uchaguzi, mapema wale mabomu waonolewe ili tusijikute tuna gunia la viazi vibovu vyote halafu tunaambiwa tuchagua kizuri humo. Matokeo unachagua kujaza nafasi na sio kupata mtu mwenye uwezo wa sehemu hiyo
   
 13. Companero

  Companero Platinum Member

  #13
  Jan 5, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  'Zimwi likujualo halikuli likakwisha': Hivi tunalinganisha mazimwi hapa? Je, hili ni swali la 'lesser evil', yaani 'asiye mbaya kuliko mwenzake'? Au ni suala la 'birds of a same feather flock together', yaani 'ndege wenye nyoya linalofanana hukusanyika pamoja'?

  Tuliliwa tule wakati wa Mbabe. Tunaliwa tule wakati wa Muungwana.Tisa kumi wajinga ndio waliwao anasisitiza Ikwabe Itembe.
   
 14. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Angepewa utawala mwaka 1995 , nchi hii ingetapakaa damu ya wenyewe kwa wenyewe!! Wakristo vs Waislam kwani angeanzisha kwa nguvu Mahakama ya Kadhi na kuiingiza Tanzania OIC kama anavyotarajia kufanya hivi sasa.
   
 15. M

  Majisafisalama Member

  #15
  Jan 5, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunabwata weee mchana kutwa, usiku ukifika twaingia vyumbani mwetu hadi kunakucha, salaama na amani. Hamshukuru nyie!!!! 'something is done'. asubuhi kelele tena, JK hivi Ben vile, EPA, BUZWAGI kadha wa kadha. TUFANYE KAZI KWA BIDII...Hakimu, polisi, magereza, mwanahabari, raisi tena wote hata kama ni wataasisi au wa wanafunzi, mwalimu, daktari, machinga piga kazi, wanasiasa nao wakipiga kazi sawasawa bila shaka wapiga kura nao watachapa kazi. Idadi yetu kwenye jukwaa hili ni kubwa kuliko maeneo mengine ya JF, hii inaonesha jinsi tulivyo mahiri kupepeta domo, SAMAHANI. Hata kama tukiachiwa mbegu tupande wenyewe kama tayari zina wadudu ndani, kitastawi kitu kweli?????? 'COMPLETE THE CIRCLE', usiuze maembe bali juice, what about us? Add value bwana.
   
 16. M

  Majisafisalama Member

  #16
  Jan 5, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unanichanganya, hapa sielewi mdini ni yupi? anayerejesha kilichokuwepo au anayepinga kisiwepo? help please.
   
 17. Lyampinga

  Lyampinga Senior Member

  #17
  Jan 5, 2009
  Joined: Apr 13, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  JK is the worst leader, i have ever come across. Ushikaji ushikaji mwingi, marafiki kawajaza kwenye kila idara
   
 18. D

  Deo JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  JK angechukua nchi 1995 hali ingekuwa mbaya zaidi.
  BM anajua kuongoza na bei ya vitu ilishuka na kuwa chini wakati wake. Lakini bwana ni mlezi wa ufisadi. Kwa Jk labda watu wanaogopa au hawajui! Lakini vipi Richard Monduli na sasa Grey Mgonja ameachiwa kwa ile sheria ya mwaka huu.
  Labda tumulize yule mzee wa channel 10 Kama tutafika 2015? Labda atatupa jibu
   
 19. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  My dear friend, Companero, tumeanza kuliwa since JKN!! We have to change or mind set! But your question is valid, we are talking of the lesser evil not good governance! But at the end of the day it is the same party... so it's same sh** different toilet... if you get my gist.
  Asante, mkuu!
   
 20. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Mwinyi then JK, ingekuwa hatari kwelikweli. May be TZ ingegeuka Somalia.

  Tatizo BWM alimuogopa Salim, nafikiri ndiye kiongozi pekee kwa wakati huu mwenye qualities za kutuongoza. Naona mambo ya mafisadi yanavyoendelea chini ya JK, kama ingekuwa Salim nafikiri asingepona mtu. Anyway maji yalishamwagika........... Tuombe CCM watufanyie huruma 2010.
   
Loading...