JK angeongoza kabla ya Mkapa tungekuwa wapi??

Mpelijr

Member
May 17, 2010
89
11
Nilikuwa natafakari last time...jk angeweza kuwa raisi mwaka 1995 kama mwl. asingewazuia na kuwaambia kikwete na kundi lake kuwa bado hawajakomaa kua viongozi wa nchi...lakini je mustakabali wa nchi yetu ungekuwaje kama jk angeupata uraisi kabla ya mkapa?
 
Bora Mkapa angekuja baada ya huyu mkwere na bongo ingekwenda mbele kuliko tunavyozidi kurudi nyuma ndo tunazidi kwenda miaka ya tisini mwanzoni!
 
Ingekuwa afadhali kwani mkapa angesafisha huu utumbo wake katika hiki kipindi cha miaka mitano. Sipati picha kama EL akichukua 2015 tumekwishaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Kikwete angeliukwaa urais 1995 kiwango cha ufisadi Tanzania kingelikuwa chini. Iliitaji ujeuri wa mtu kama BWM kubomoa kila jema aliloacha Baba wa taifa. JK hasingelikuwa na ubavu huo. Dhambi kubwa aliyofanya BWM ni kutupilia mbali dhana ya kuwa cheo kilikuwa ni dhamana na kwamba mtu alikuwa aruhusiwi kutumia cheo chake kwa manufaa yake, na badala yake akaanzisha dhana mpya kwamba mtu anakula kulingana na urefu wa kamba yake. Ni dhana hiyo iliyohalalisha wakubwa kujiuzia mashirika na majumba ya umma kwa bei poa, ni dhana hiyo inayowawezesha kuchota fedha za umma wapendavyo, ni dhana hiyo iliyowawezesha kujipangia mishahara na marupurupu ya kutisha n.k. Kwa upande mwingine BWM angeliukosa urais 1995 ndiyo ilikuwa basi, kwani bila ya kubebwa na Baba wa Taifa hasingelifika kokote.
 
WIZI WA EPA UNGEGUNDULIKA MAPEMA
MIKATABA YA MADINI INGENUFAISHA TAIFA
TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA YASINGEUZWA KWA BEI YA KUTUPA E.g NBC
NDEGE YA RAISI NA RADA VISINGENUNULIWA na WABINAFSI WACHACHE KUPATA 20PC ZAO.
RASILIMALIMALI KIBAO ZA NCHI HII ZISINGEUZWA
UJAMBAZI USINGEKUEWEPO KTK KIWANGO ULICHOFIKA WAKATI WA MKAPA
MAUWAJI YA RAIA YANAYOFANYWA NA SERIKALI KWA AMRI YA MAPADRI WA KATOLIKI YASINGEKUWEPO, REF mWEMBECHAI NA PEMBA
UHURU WA VYOMBO VYA HABARI UNGESHAMIRI NA JF INGEASISIWA MAPEMA ZAIDI
TANZANIA ISINGETOA WAKIMBIZI KUJIHIFADHI NCHI JIRANI N.K
 
wizi wa epa ungegundulika mapema
mikataba ya madini ingenufaisha taifa
taasisi na mashirika ya umma yasingeuzwa kwa bei ya kutupa e.g nbc
ndege ya raisi na rada visingenunuliwa na wabinafsi wachache kupata 20pc zao.
rasilimalimali kibao za nchi hii zisingeuzwa
ujambazi usingekuewepo ktk kiwango ulichofika wakati wa mkapa
mauwaji ya raia yanayofanywa na serikali kwa amri ya mapadri wa katoliki yasingekuwepo, ref mwembechai na pemba
uhuru wa vyombo vya habari ungeshamiri na jf ingeasisiwa mapema zaidi
tanzania isingetoa wakimbizi kujihifadhi nchi jirani n.k

crap
 
ingekuwa mbaya sana, Mkapa aliikuta nchi ikiwa mbaya sana kiuchumi, sasa huyu angepata sahani hilo tupo angelibomoa, yaani angeuza kwa fujo maliasili, sipati picha, huyu tulimchangua tu kwa sura na si utendaji. NAJUTA KUMPA KURA YANGU MWAKA 2005
 
Should have never been a president at any time in our history;time is not an issue, it is a person, so JK wa 1995 wont be different from the one we have now, same woe same woe
 
Tungekuwa na maumivu ya hali ya juu na CCM ingepata stroke ya kuchomolewa madarakani!!
 
Kwanza serikali ingekuwa imeshafilisika. Kumbuka Mkapa alikuta treasury ikiwa tupu na akaanzisha zoezi la kukusanya kodi, TRA. Mkwere asingekuwa na hiyo akili, angejaribu kuendeleza yale yale aliyoyafanya Mwinyi na tungekuwa tumeshafanana kama Bangladesh vile, kama siyo Somalia.
 
Correction, Bangladesh ni hile ya zamani. Kwa sasa wanafanya vizuri kiuchumi.
 
Should have never been a president at any time in our history;time is not an issue, it is a person, so JK wa 1995 wont be different from the one we have now, same woe same woe
that is the exact thought that came to my mind..its the person and i wondered ...where could we be?
 
ingekuwa mbaya sana, Mkapa aliikuta nchi ikiwa mbaya sana kiuchumi, sasa huyu angepata sahani hilo tupo angelibomoa, yaani angeuza kwa fujo maliasili, sipati picha, huyu tulimchangua tu kwa sura na si utendaji. NAJUTA KUMPA KURA YANGU MWAKA 2005
Siyo wewe tu ndugu yangu....ni wewe na watanzania wapatao milioni 20.....tulidanganywa na propaganda ya raisi kijana na siyo raisi mtendaji!!!!
 
Back
Top Bottom