JK anatoa maagizo kama Rais au kama mgombea kupitia CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK anatoa maagizo kama Rais au kama mgombea kupitia CCM?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ngolinda, Aug 31, 2010.

 1. Ngolinda

  Ngolinda Senior Member

  #1
  Aug 31, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika pitapita zangu kwenye blogs..nilikutana na swali au maoni yaloandikwa na mmoja wa wadau na yanasomeka hivi:

  "Ninagusia suala moja tu, 'agizo' la Raisi kwa Wakala. Nawaza na kujiuliza ikiwa agizo hili la Raisi latolewa kama Raisi katika shughuli zake za Kiserikali au kama Mgombea wa Uraisi kupitia CCM katika kampeni?

  Sina ufahamu wa miiko ya Katiba na Sheria ya Uchaguzi, hivyo mniwie radhi kwa kuwaza hivi, pengine ikipelekwa kesi mahakamani au ukapotolewa ufafanuzi, nitapata uelewa wa kunisaidia kutofautisha kauli za Raisi wa nchi kwa sasa dhidi ya kauli za Mgombea wa Uraisi kupitia CCM ambaye ni Raisi wa nchi kwa sasa.

  Nasema hivi kufuatia kauli ya CHADEMA kuishitaki CCM/Raisi Kikwete kwa anaosema na kuagiza ndani ya kipindi hiki cha kampeni, inakuwa kama "unfair advantage" kwa kuwa yeye ni Raisi kisha anagombea Uraisi.

  Yaani ni sawa na kusema kwamba, kwa vile yeye kwa sasa ni Raisi na vile vile yeye ni mgombea Uraisi, basi anatumia kofia mbili kama msumeno kukata kuwili, yaani kutoa agizo kama Raisi na kisha kufanya kampeni kama Raisi mtarajiwa. Unakosekana mpaka (a clear demarcation) wa hili ni agizo haliingiliani na sera. Je, ilipaswa auze sera za CCM Tunduma kisha aondoke, na apange safari nyingine upya, au akiwa katika ofisi yake ya Kitawala, atoe agizo kama Raisi kuhusu Wakala wa ununuzi Tunduma? (waweza kubadili pia kuwa alipaswa atoe agizo kama Raisi na kisha afunge safari ya kampeni ambayo hapaswi kutoa maagizo bali kunadi sera zake). Kwa ilivyo sasa, ni vigumu sana kutofautisha (1) Aliyefika hapa na kutoa agizo ni Raisi wa nchi Jakaya Kikwete na (2) Aliyefika hapa ni Mgombea wa Uraisi Tanzania kupitia CCM, Jakaya Kikwete."

  Maswali haya yanatokana na Mgombea huyo wa urais Jakaya Kikwete kumuagiza Wakala wa Hifadhi ya Chakula (SGR) kuongeza kiwango cha ununuzi wa nafaka kutoka tani 150,000 hadi 400,000 ili kuwapa soko la uhakika wakulima huko Tunduma.


   
 2. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Siasa za nchi zetu hizi ni takataka kabisa! Unadhani katika hali hiyo kuna usawa wa kufanya kampeni? Nadhani kupunguza hali hii ni vizuri kungekuwa na sheria ya mgombea akiwa rais inabidi akaimu hiyo nafasi kwa spika wa bunge mpaka hapo atakapochaguliwa tena au mtu atakapoichukua nafasi hiyo. Sasa ni vurugu tu, jamaa anfanya hongo kwa wananchi wakati huu.
   
 3. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Kisheria yeye ni Rais hadi atakapo patikana Rais mwingine. Na kwa sababu hiyo ndiyo maana ananafasi kubwa sana ya kutoa ahadi na pengine kuzitimiza wakati huu wa kampeni ili kuwashawishi wananchi wampigie kura.

  Hii ndiyo Tanzania.
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Conflict of interests!
  Nadhani ni busara madaraka ya Uraisi yakome pale tuu anapoanza kampeni
   
 5. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  ITS CALLED THE INCUMBENCY FACTOR......and it is legitimate advantage even in the most developed democracies..Opposition should stop lamenting and learn how to deal with it
   
 6. D

  Dick JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ikiwa hivyo, nchi itabaki na umbwe(vacuum) la uongozi, kitu ambacho hakitakiwi.
   
Loading...