JK anasoma nyakati? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK anasoma nyakati?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ebrah, Jun 26, 2011.

 1. e

  ebrah JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Salaam great thinkers!
  nina swli najiuliza kila kukicha nashindwa kupata jibu kamili, " HIVI RAIS JK " anajua kusoma majira na nyakati mbalimbali zinazojitokeza hapa nchini kila kukicha?
  Toka alipokuwa anakaribia kumaliza kipindi chake cha miaka mitano ikulu, aliona kabisa kuwa sehem kubwa ya UMA wa watanzania ulipoteza imani nae, na serikali yake kwa ujumla, haya yote ni kutokana na kutotimiza sehemu kubwa ya ahadi zake kwa watz.
  Vyama vya upinzani vilijitahidi sana kumkumbusha njia lakini hakuamka, kitu kilichomfanya kuanguka vibaya katika uchaguzi, hadi kuiba kura aweze kurudi tena ikulu.
  sasa nashindwa kuelewa alitumia nguvu zote hizo kurudi ikulu kwa sababu gani? kwani kwa madudu yaliyofanyika kama kweli alikuwa muadilifu alitakiwa kujiuzulu pamoja na kina Lowasa.
  watu wengi hutafuta "second chance" ili kusafisha mapungufu yao na kurekebisha pale walipokosea walipopata nafasi ya kwanza, lakini kwake yeye na serikali yake imekuwa sivyo, kwani madudu yanaongezeka kila kukicha.

  Sasa anataka kutuaminisha nini? kuwa aliiba kura zetu na kutumia nguvu zaidi kurudi awamu hii ali

  1. aibe zaidi na kujijengea maisha baada ya kustaafu?

  2. apoteze kabisa mwelekeo wa nchi yetu?

  3. kuficha aibu ya kuongoza kwa kipindi kimoja?

  4. ajaribu kujirekebisha lakini uwezo huo hana, na anadhihirisha kushindwa kwake?

  Jamani naomba nisaidieni kumdefine huyu mtu na serikali yake, kwani majira yanavyoonyesha ameshindwa na hana uwezo tena wa kujirekebisha, na badala yake anazidi kufanya madudu.

  Hivi karibuni tumeshuhudia hadi wana ccm wenzake wakimgeuka, kina sita, mwakyembe, nape, katika awamu ya kwanza kabla na baada ya uchaguzi, sasa hivi lowasa na kajidhihirisha wazi kabisa amemgeuka na anampinga, na mbaya zaidi wabunge sehemu kibwa wameonyesha kuwa wapo upande wa lowasa, hivyo wamemgeuka JK, na hata wakijifanya wako naye ni kwa sababu ya madaraka aliyonayo tu!

  JE! kwa haya yote huyu jamaa hajifunzi? au ndo sikio la kufa?
   
 2. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  aliye lala usimwamshe
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  ukimwamsha utalala mwenyewe, na utajuta ukizinduka kwani utakuwa mwenye bahati ukijikuta na angalau under.we.ar!!!!!!
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Kwani kunatatizo gani?, urais kwetu ni ufalme: ukishateuliwa na CCM ujue unakula nchi kwa miaka 10. Hata akiamua kujifungia ndani for the rest of the time- kutakucha tu.
   
Loading...