JK anamuenzi vipi Mwalimu?

AlamaZA NYAKATI

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
274
28
Karibu viongozi wote walitoa maoni kwa jinsi viongozi na watz wanavyomuenzi Mwalimu, lakini sijasikia kauli yeyote kwa mkuu wa nchi kuhusu Mwalimu......kunani?
 
Karibu viongozi wote walitoa maoni kwa jinsi viongozi na watz wanavyomuenzi Mwalimu, lakini sijasikia kauli yeyote kwa mkuu wa nchi kuhusu Mwalimu......kunani?
sina uhakika kama siku ya kumbukumbu ya kifo cha baba wa taifa alikuwa nchini...mgeni rasmi kule Mara alikuwa makamu wa rais...
atamuenzi vipi wakati hata kumuita baba wa taifa anaona anampa sifa..
 
Jamani wanajamvi,
huyu vasco da gama, ni rais wa kipekee katika dunia hii. Hajawahi kumuongelea hata kidogo baba wa taifa letu.
Rais wa visasi, visa, starehe, rushwa, mikataba feki, muongo, mdini,hasira,ndoa nyingi, nguvu za giza,safari, etc atakua na muda gani wa kumkumbuka nyerere.

Vile anavyovifanya ni kinyume na maagizo na maadili ya baba wa taifa. hawezi kamwe kumuenzi kama tufanyavyo sisi.

kwa kifupi JK ana bifu na marehemu
 
kila mwaka tuna nyerere day, karume day ina maana katika kipindi cha miaka yote kumi ya utawala wa kikwete atakuwa anahudhuria na kusema peke yake wakati tuna viongozi wengi wa kitaifa?
 
kawawa day? kambona day? mkwawa day? nakadharika tumuache Rais afanye na mambo mengine kadri itakavyoonekana inafaa kwa maslahi ya taifa. Kama kila Rais aliopo madarakani na watakachaguliwa ina maana hata kwa miaka 100 ijayo marais kila mwaka kwa miaka 100 wanatakiwa kusema au kuhudhuria nyerere day pasipo kuzingatia agenda nyingine za kitaifa? tujaribu kufikiri kwa kina kwa maslahi ya wote lakini bado nyerere ni nembo ya taifa letu na mtu muhimu kwa historia yetu sote.
 
kikwete alipomfukuzilia mbali yule jamaa aliyepora viwanja vya nyerere pale msasani ni moja ya ishara ya heshima yake kwa familia ya mwalimu kwani yule jamaa alishindikana kutoka tangu serikali ya awamu ya tatu na akakimbilia mahakamani lakini Kikwete aliamuru kuvunjwa kwa mali zote za mshenzi yule na hadi leo ameogopa kwenda mahakamani labda anasubiri kikwete atoke madarakani
 
tumekuwa tunalalamika Rais kuhudhuria kila tamasha na kila kongamano na asipoonekana tunamlaumu
 
maadhimisho ya mwaka huu yamefanyika kwa ngazi ya kila wizara kwa miaka 50 ya uhuru na nyerere day na kila wizara iko chini ya Rais mimi naona kwa mantiki hii Rais kashiriki na ndiye amesimamia mipango hii ili kumuenzi mwalimu kwamba kaleta uhuru na kila wizara itoe kipaumbele kumuenzi.
 
kuna tukuo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kituo cha chuo kikuu cha mlimani ambapo vyombo vya habari vimesema mgeni rasmi atakuwa Rais kikwete. tumeambiwa tukio hilo ni la kumuenzi Nyerere na kama sijakosea litakuwa la kutimiza mika 50 au 47 ya chuo kikuu.
 
Kila mwaka rais na mama kikwete hutembelea butiama na kama nakumbuka hivi majuzi mama kikwete alikwenda butiama ambapo pamoja na mambo mengine alimtunukia mama nyerere nishani ya mwanzilishi wa umoja wa wanawake tanzania uwt. Ndio maana naona hii post imekaa kichuki binafsi zaidi
 
katika kumuenzi mwalimu Rais ameandikwa na vyombo vya habari kwamba amekwenda mikoani kuhamasisha maendeleo kwa wananchi bila shaka ni jambo jema kuliko kusimama jukwaani na kusema maneno mengi wakati hivi sasa watanzania wanataka vitendo
 
Mleta thread inaonekana ana chuki binafsi na kikwete. Hili swali halipaswi kuulizwa na mtu mwenye akili timamu,unajidhalilisha mbaya kabisa....kwanza wewe umefanya nini kuadhimisha nyerere day zaid kulaum watu...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom