Jk analaumiwa bure! Tatizo ni "watanzania wenyewe". | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jk analaumiwa bure! Tatizo ni "watanzania wenyewe".

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Analyst, Feb 26, 2011.

 1. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Lawama kemkem zimekuwa zinatolewa dhidi ya JK kuhusiana na utendaji-kazi wake na sifa kadhaa nzuri zinatolewa juu yake. Nikianza na SIFA MBAYA: JK kashindwa kuwadhibiti mafisadi (pengine hata anashirikiana nao), Hajui wapi awe mkali na wapi atabasamu, Hajui afanye nini kuimarisha uchumi (japo alisoma Uchumi pale Mlimani) ndo maana hali ipo hivi, hashauriki kirahisi hasa na watu wasio karibu yake, ana udhaifu katika judgement (Uteuzi wa Makamba kuwa katibu Mkuu ni mfano), alitaka urais lakini inawezekana hakujua akiwa rais atapaswa kufanya nini kuhusiana na matatizo ya walalahoi, ni mwoga katika kufanya maamuzi magumu n.k. SIFA NZURI: Ni mpole (Vinginevyo Mwanahalisi ingechomwa Moto na Hosea angekuwa Maswa analima), Anaheshimu pesa (la sivyo RA n YM wangekiona), anasema anachokiwaza hata kama kinamtia aibu yeye mwenyewe (Mfano aliwahi kusema hajui kwa nini nchi hii ni maskini, na juzi juzi kasema hawajui wamiliki wa Dowans, yaani hamjui Rostam, Karamagi wala Lowasa) U know I like this Guy! n.k. Makamba anazo sifa zaidi nzuri za huyu bosi wake.
  Hoja yangu ni kwamba wakati tunajaribu kumlaumu sana Kiongozi aliyechaguliwa na wananchi (au kuchakachuliwa ushindi na TISS) tunasahau kwamba hata wakati tunamshangilia mwaka 2005 hakuna aliyefuatilia nguvu ya umma aliyokuwa nayo ilitengenezwa na nani. Je kuna anayejua utendaji wake "kwa hakika" ulikuwaje kabla hajagombea urais? Je ni kweli kwamba hapakuwa na watu waliokuwa wameonesha uwezo tayari ndani ya chama chake kuliko yeye? Kama walikuwapo, nani alizuia chama kisiwafikirie? Unapotafakari kwa undani utagundua kwamba asilimia kubwa ya watanzania walifurahia mtu waliyeamini wanampenda na kusahau kwamba kwa umasikini wetu mchapakazi mzuri anatufaa zaidi (hata kama hana beautiful smile). Jamani tusidanganyane, huyu jamaa hatufai kabisa kwa hali iliyopo na tunaompa nafasi ni sisi wenyewe. Mnakumbuka baadhi ya viongozi wetu ki-imani waliwahi kumwita chaguo la Mungu? Basi leo hii hawataki hata kumsikia. Mwisho Mkwere akaona aseme nchi inaelekea kwenye udini ili walau kupunguza kasi ya Chadema. Miaka fulani CUF ndo walikuwa hapo, UDININI na leo ni rafiki zao (CCM) kule Zanzibar na Bungeni.
  Matukio yanayotokea nchini tangu awamu ya nne ianze kazi inaonesha sisi wananchi ndo vimeo. Kwanza hatufuatilii kwa karibu nchi yetu inaendeshwaje, na wale tunaofuatilia hatufanyi lolole kuwasaidia wenzetu wa vijijini kujua tunayoyajua ili kwa pamoja tuchukue hatua ikiwemo kuwanyima kura hawa wafanyakazi wa Rostam waliodai wanaomba ridhaa kututumikia walalahoi (ambao siku zote ndo wengi). Viongozi wengine wa kijamii nao vimeo tu! Angalia siasa za watu kama kina Cheyo, Mrema na jamaa wa CUF. Wao vyeo na mafao nd0 mafanikio ya upinzani. Hawajui adui yetu mkubwa ni hizi shida zinazochangiwa kwa kiasi kikubwa na ufisadi wa CCM ya RA. Viongozi wa Dini nao wanarumbania udini ambao kimsingi haupo ila umesemwa na wanasiasa walioona wanapoteza madaraka na si wananchi walio wengi ambao mpaka naandika post hii wanaishi vizuri pasipo kubaguana.
  Mnajua wakati mwingine nahisi RA na jamaa zake wana-control nini kifanyike hapa nchini kuliko Mihimili yote mitatu ya dola kwa pamoja. Inasemekana hata huyu spika mpya ameingia hapo kwa nguvu za RA ndo maana Sitta kapigwa teke. Kama hiyo ni kweli, itakuwa vipi endapo hawa wenyeviti wa kamati za Bunge kama J. Makamba ni zao la mambo ya RA?
  Ndo maana narudia kusema tatizo ni sisi watanzania wenyewe. Inawezekana JK yupo sahihi kabisa kwa anayoyafanya kwa kuwa ndivyo alivyoagizwa na waliompa nguvu ya kuingia Ikulu (sawa na Mama Makinda na Uspika wake) kama sisi wenye Ikulu tunaruhusu RA afanye yote hayo tatizo litaendelea kuwa sisi.
   
 2. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  :a s 13:
   
 3. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Jamaa umeöngea ukweli mtupu, tatizo ni sis wenyewe hasa vijana na ulimbuken wetu tulimshabikia sana 2005. Nashukuru Mungu kuwa tangu 2005 Jk sikumkubali kwan huwa naamin mara nyingi viongozi poa hawana tija ya uongozi nafikiri ndivyo ilivyo. Makinda kawekwa na RA nasikia imetumika mil. 600 kumng'oa Sitta. Kwa hiyo makinda yupo kwaajili ya kulinda maslahi ya mafisadi.
   
 4. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Nadhani ni muda mzuri kila anayeweza kukaa chini na kufikiria kusaidia nchi yetu akae chini afikirie na atoe ushauri wa nini kifanyike kwa kupeleka maoni sehemu husika kama kwa ndugu zetu CDM ili watuongoze kuelimisha jamaa japo ni ngumu sana lakini naimani tutafanikiwa.
   
 5. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Kwahiyo yuko pale ili kuwatumikia mafisadi?
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,607
  Likes Received: 3,909
  Trophy Points: 280
  Surely!!!

  I will never waste my time blaming Kikwete! never! you better challenge sensible people,can you challenge kichaa?? CDM this energise me to challenge you, ukifika hatua hamtaki challenge the forget it it over!

  Good post though
   
 7. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hata kama sio tatizo lake jk nani alaumiwe ina maana familia baba akishindwa kutoa malezi mema nani atalaumiwa? kama yeye alikubali wamuweke hao mafisadi basi akuabaliane na chochote kinachompata kiwe kizuri hata kibaya. Na uje huu ni urafi wa madaraka kama huwezi uliomba uongozi iliweje? wajinga ndio waliwao shauliyake na ukilazi wake.:A S 13:
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Kikwete ni Mtanzania au si Mtanzania?

  Kama tatizo ni "Watanzania wenyewe", na Kikwete ni Mtanzania, Kikwete naye ni tatizo au si tatizo?

  Be precise please.
   
 9. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa vimeo ni sisi wenyewe watanzania tunaoendelea kuruhusu kutawaliwa na Rostam Aziz, muajemi.
   
 10. S

  Shamu JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2011
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Good point. Unajua WTZ, na waandishi wa habari wengi wao hawajui sheria za nchi. Wao baada ya kulilaumu Bunge wao wanamlaumu Rais.
  Unajua TZ ni moja ya nchi yenye demokrasia, kwa hiyo Bunge lina nguvu sana. Kwanini Wanahabari hawaambii WTZ kuwapa pressure Wabunge wao? bali wao wanatumia kumlaumu Rais. Hii inaonensha ni jinsi gani WTZ hawajui sheria.

  Angalia hata hapa JF, wengi wao wanamlaumu Rais directly.
  Kwa kumalizia, tatizo la WTZ, ni kutokujua sheria za nchi.
   
 11. D

  Dopas JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2011
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huyo Makinda siku zake ni 'numbered', atakiona kile kiti moto na kuachia mwenyewe kama ataendesha Bunge kama lililopita, labda ajirekebishe na kujali maslahi ya watanzania kuliko ya kina EL na RA waliomtuma.
   
 12. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,195
  Likes Received: 1,914
  Trophy Points: 280
  Sasa utufahamishe wa kulaumiwa.
  Mwanangu akiwa mwizi watasema mtoto wa mgen ni mwizi.
  Ndivo ilivyo kwa rais yeye ndio mwenye mamlaka na anayeteua kina mwinyi na anaona anafaa tumlaumu nani? na yeye ni mtg hakutoka kenya.
  Nina uchungu hapa tulipo fikia hadi viongozi kutowajibika kwa kushindwa kutekeleza wajibu walioapa hadharani.

  Naona huko tunako elekea iko siku patachimbika.
   
 13. Jayfour

  Jayfour Senior Member

  #13
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Iwe ni udhaifu wa bunge, iwe mahakama, au baraza lake la mawaziri yote hiyo ni mihimili ya serikali yake...sisi wananchi tulio wengi hatuhitaji tuwe wanasheria (tuna fani zetu nyingine) tunachohitaji kujua ni: je mtu tuliyempa dhamana ya kutuongoza na kuunda serikali anatupeleka kule tunakotaka..!!??
  Mfano mzuri wa kuuzingatia ni rais wa Rwanda, Paul Kagame..ameitoa kwenye matatizo makubwa na sasa nchi ya mfano wa kuigwa barani Afrika.
  Kwa vile yeye ndiye mwenye serikali, lo lote linalokwenda kombo yeye ndiyo wa kubeba mzigo wa lawama kisha aweza kugawia mihimili yake na taasisi zake..!!! Wananchi hatutaacha kumlaumu kwani tunazililia kura zetu za mwaka 2005 ambazo ndizo zilzomuweka madarakani hadi leo.
   
 14. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Wa kulaumiwa ni watanzania wengine wote isipokuwa RA, EL, JK na timu yao ya watu kama Karamagi, Ngeleja nk. wale ambao kwa namna moja au nyingine wanaunga mkono ufisadi na wameamua kufanya hivyo kwa maslahi yao. JK na wenzie wanajua aliyewaajiri ni RA na ndo maana wapo tayari kupoteza mapenzi ya watanzani wengine wote kumlinda na kumtajirisha zaidi na zaidi.
  Watanzania tuliobaki tunapaswa kujilaumu kwa kuwa tumemsaidia RA ktk kila hatua ya mipango yake ya kuiteka serikali na Chama Chao. Watanzania tuliobaki ndo tunasaidia kuchakachua matokeo ya kura za uchaguzi na kuwashangilia waajiriwa wa RA tukijidanganya tumewachagua sisi. Watanzania tuliobaki (nje ya kundi hili ambalo kati yao hakuna mwenye shida) na baadhi ya vingozi wetu wa Imani ndo tunakimbilia kulaumu udini wakati kauli hizo zinaanzishwa na watu wanokusudia kukwepa lawama kama Makamba na JK ili kuwatisha wananchi dhidi ya kuunga mkono upinzani hasa Chadema. Tunachotakiwa kufanya ni kutafuta namna ya kurekebisha makosa yetu haraka iwezekanavyo. Vinginevyo matizo yaliyopo nchini yatatuua.
  Angalia historia yote ya ufisadi hapa nchini uone pointi yangu. JK yupo tayari kuonekana muongo, fisadi, msanii (ktk maana mbaya), tapeli, muoga nk. Yupo tayari kudharauliwa na kila mtu. Yupo tayari kusingizia udini na chochote kingine lakini hayupo tayari kumwabia RA "sasa basi"
  Utawala wa "RA" ndo sababu ya kila tatizo la utawala hapa nchi. Sasa hivi JK hawezi hata kusimama mbele ya raia na kuwakataza jambo lolote baya kwa hofu kuwa watamwuliza wewe mbona....! Angalia juzi juzi kauli ya Hosea kumponda imewekwa hadharani lakini JK yupo kimya! Atamwambia nini wakati Hosea anayajua madhambi yote ya wanamtandao na bosi wao RA?

  Ufisadi unaoendelea katika vyombo vya serikali ambao haufiki katika vyombo vya habari ni mkubwa sana sasa hivi kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi hii! Unajua sababu nini? Hakuna kiongozi yoyote anayethubutu kumkaripia mtu kwa kuwa kila mtu anaona haya. Haya; Rais (analinda mafisadi), Mawaziri wengi walaji tu wengine hata uteuzi wao RA ndo anajua kigezo, Makatibu wakuu mmh...! Wakurugenzi na Wakuu wa Idara zinazojitegemea hovyo. Kwa ufupi waadilifu ni wachache sana.

  Ngazi ya juu kabisa ya serikali wapo kumtumikia RA. Baadhi yetu tunalijua hilo. Mambo mengine yanakwenda ki-bahati bahati tu lakini hakuna ufuatiliaji wowote wa dhati.
   
Loading...