JK ana mapungufu lakini ana credit katika utawala bora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK ana mapungufu lakini ana credit katika utawala bora

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Mar 18, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ni kweli rais wetu Jakaya Kikwete ana mapungufu katika sekta nyingi ikiwemo ya uchumi ingawa IMF imesema uchumi wetu unazidi kuongezeka mimi sioni kama wako sahihi lakini hili la utawala bora anajitahidi kwa kiasi chake tumpe credit maana ni nadra sana kwa viongozi hasa wa Afrika kuwafikisha mahakamani viongozi wa serikali iliyotangulia kama anavyofanya yeye
  [​IMG]
  Mawaziri wa zamani katika Serikali ya awamu ya tatu, Daniel Yona (kulia) na Basili Mramba wakizungumza na mawakili wao mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana. Yona na Mramba wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh11.7 bilioni.
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Mar 18, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Luteni bwana na wewe umeingia kwenye JK-Mkandara style ya kurubuni watu

  Mramba ni bosi wa Tanroad kwao wakati huu ninaongea na kesi iko mahakamani! kapewa ubosi wakati kesi inaendelea!

  Mramba na Yona walitakiwa kurudisha mali, na kwenda jela achana na story za kufikishwa mahakamani.

  Mimi leo ukasema niutangazie umma kuwa mimi ni mwizi na nikishafanya hivyo unanipa bilioni 5 nitakubali ebo!! aibu wapi mbele ya fedha watoto wao wanakula na kunywa mpaka vizazi vya tatu na nne! ndio utawala bora!

  He fooled many sorry that he got you, uchafu wa CCM na serikali yake hauishii kwa Mramba na Yona, wako wengi yeye JK akiwa namba moja, sijapata mantiki ya mwizi kumpeleka mwizi mwenzake na still mwizi mwenzake akapewa heshima ya mtawaka bora!

  mwanachadema vipi tena mbona unaniangusha mkuu!

  rushwa ni kila kona, nchi hii na JK angesema aanze kupambana anayo angeweza tu, hakuna cha utawala bora hapo mkuu! unafikiri ile 70% alikuwa anatania??

  akina Karamagi, chenge, Lowassa, ...name it ni utawala bora? hawa wote next day walitakiwa wafikishwe mahakamani! kikubwa wafilisiwe na fedha zirudi, ni jambo la wazi kuwa kwenye richmond JK yumo! Mwakyembe analijua hili, yeye JK analjua hili! wananchi tunalijua hili !yet Luteni unasema utawala bora!


  JK amewalisha nini watanzania wenzetu?

  sorry sita argue na wewe katika swala hili.
   
 3. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ni sawa unayosema hata mimi nimesema at least amejaribu ukilinganisha na watawala wengine barani Afrika
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Mar 18, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Afadhali umesema unalinganisha na wengine Africa, at least una la kusema, japo haujasema specific ni watawala gani! wako watawala wazuri africa, chukulia mfano Botswana they are doing good.

  Ukitaka tujiweke katika hali nzuri ya kuheshimika, JK mpime na watawala wengine duniani siyo africa, sio vizuri kumpima dhaifa na dhaifu. Kama tunapanda magari ya wazungu, kunagalia TV za wazungu na kufurahia internet za wazungu and all other technilogical advantages, hata kula watu siku hizi wanakula kizungu, achili mbali kuongea! Kwa nini mambo ya uongozi tusiige wale wazungu wanaoafnya bora, mengine tunaiga mengine tunaacha.!why?

  Matatizo yetu ya uongozi yanaanzia ngazi ya chini kabisa, kuanzia ngazi ya familia, kata, shule za msingi, kijiji, tarafa , wilaya , maofisini n.k

  Tunahitaji kiongozi anayejua root cause ya problem na kuziondoa, bila hivyo, JK will always be the best among very bad leaders
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hajajaribu chochote. Ni changa la macho tu. Redio mbao zinasema Mramba kapelekwa kizimbani kwa sababu alimpunja Muungwana mshiko kwenye dili la Alex Stewart. Figures zilipotolewa Mwungana akagundua kuwa Mchaga amemwingiza mjini. Na yule ni mtu wa kisasi.
   
 6. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,987
  Likes Received: 3,735
  Trophy Points: 280
  Afande, umekurupuka usingizini nini?
   
 7. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sijakurupuka mzee kwa nini unasema hivyo
   
 8. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Jakaya ni msanii aliyekubuhu kwani hizi kesi zote za wakina Mramba na Yona na hizo za EPA ni dongo la macho ; hizi kesi wakina Mramba na Yona wataachiwa na kulipwa mahela mengi tu na serikali kwa usumbufu , wakati zile kesi za epa zitaahilishwa mpaka baada ya uchaguzi October jamaa akishinda Urais na kesi zote zitafutwa a' la GOLDENBERG ya Kenya!!

  Msumbiji wana uongozi wa mfano usiofanya mzaha na vita dhidi ya rushwa; juzi juzi tu waziri wa zamani wa mawasiliano/uchukuzi huko Msumbiji amefungwa jela miaka kamasikosei zaidi ya ishirini kwa kosa la ubadhrifu na rushwa!! Jakaya anaweza kazi kama hiyo? Kama anaweza mbona Rostam na Lowassa wako nje?
   
 9. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sawa huoni kule kupelekwa wahalifu kwenye vyombo vya sheria ni mwanzo mzuri
   
 10. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii kauli ni ya kishawishi ya kijumla jumla mno na potofu. Utawala bora maana yake nini? Hebu tuambie viashiria vinavyotumika kupima utawala bora, halafu mpime kwa kila kimoja uone kama maoni yako yatasimama. Kwa kuanzia mpime kwa kigezo cha rushwa, halafu uone alivyoshindwa kabisa. Watanzania wa sasa si wa kudanganywa. Rushwa imetapakaa na wala rushwa katika serikali na chama chake wanalindwa kama mboni ya jicho. Kwa hakika ameshindwa vyote, utawala bora na uchumi sawia.
   
 11. T

  TANURU Senior Member

  #11
  Mar 19, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku wakuu na wahusika halisi wa KAGODA wakifikishwa mahakamani angalau ndiyo tutaona kuwa amedhamiria kupambana na Rushwa.
   
 12. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160

  Luteni, mi sijaona kama amejaribu.
  Haya yote ni drama tu, wachache wanatolewa ili administration yake ipate credit kwa wakubwa. Huyu naye ni wale wale tu.

  I salute you Wareboya, you have nailed it well.
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu huwezi kusema maneno haya ikiwa kweli wewe ni Mtanzania na unaelewa maana haswa ya Utawala bora..

  PUNGUFU kubwa la KIkwete ni Utawala Bora!.na sidhani kama unaweza nambia hayo mapungufu yake nje ya Utawala bora...

  Muhimu tuzingatie kwamba kati ya mazuri kumi ukifanya mabaya Nane, na ukafanya mazuri wawili haina maana wewe utasifika kwa mazuri hayo mawili!..

  Hata yule mwanafunzi aliyeshindwa mtihani huwa anapatamajibu sawa ya baadhi ya maswali.. Ukapata 20/100, bila shaka ume fail mtihani, haihesabiki credit ya kupata hizo 20.
   
 14. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Luteni, mgonjwa ni mgonjwa tuu, akiwa wodi ya kawaida au ICU wote wanahitaji tiba. Hapa hakuna cha at least, Utawala bora umemshinda, full stop
   
 15. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Sawa, lakini umesoma hati zile za mashtaka zilivyoandaliwa na hao wanasheria wetu wa ofisi ya DPP? ukishazisoma utapata picha zile kesi ni za aina gani, na lengo la kuzipeleka mahakamani ni nini. Ni kuzuga tuu na kujipatia credit hizo unazozisema
   
 16. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #16
  Mar 19, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hawa watu kama akina Luteni ni cancer ya taifa letu.
  Kuna usanii unaendelea ,na Watnnzania wengi wako fooled so much!

  Mramba yuko Tanroads kila mtu anajua yeye na Anna Mkapa walivyotufanyia.
  Hawa ni wezi wakubwa,tungekuwa na mahakama huru,wangesota KEKO mara moja
   
 17. m

  mzee wa noti New Member

  #17
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  LUTENI hata mkapa aliwahi kumpeleka aliyewahi kuwa waziri wa ujenzi NALAILA kiula mahakamani, tusemeje? yeye ni malaika.kikwete kawapeleka kina mramba mahakamani kwa ajiri ya sababu za kisiasa na kukomoana. jiulize kwa nini mawaziri wote waliopolekwa mahakamani kwa kesi ya Rushwa wanatoka kaskazini?ndio kusema mawaziri kutoka maeneo mengini ni safi?au Luteni ulikuwa unatafuta public opinion .serikali ya Kikwete haina tofauti na ya Mkapa kwa ufisadi ngoja naye atoke madarakani usikie uchafu
   
 18. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2010
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nadhani Luteni anataka kulinganisha na viongozi waliotangulia.Ukweli ni kuwa katika uhuru wa kutoa maoni,kuandamana na kudai haki bila kupigwa na polisi hilo amewazidi watangulizi wake na pia voingozi wenzake wengi katika Africa.
   
 19. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #19
  Mar 19, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kuna mtu siku hizi anazuiwa kuandamana au mmesahau mabomu ya machozi miaka ya tisini na maji ya kuwasha kama mmesahau mwulizeni Mrema, mabadiliko hayo pia ni dalili nzuri za utawala bora
   
 20. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #20
  Mar 21, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimesikitika sana kusoma hii thread.
  Katika moja ya eneo la utawala bora ambalo serikali ya kikwete imeshindwa hata kupata asilimia 0 ni kwenye ajira za ushindani katika ngazi ya juu. Ajira kuanzia wakuu wa idara za serikali kuu na halmashauri za wilaya, wakurugenzi mbalimbali na mameneja. Utawala wa Kikwete umekuwa ukiteua watu badala ya kuwashindanisha kwa sifa kama inayobainishwa kwenye miongozo ya utumishi lakini mbaya zaidi hao wanaoteuliwa hawana sifa sitahili. Tumeona kuanzia ATCL, TANESCO, Wakurugenzi wa Halmashauri zote za wilaya n.k none delivered!!

  Kikwete ameshindwa kabisa kufuata misingi ya utawala bora. Ameshindwa na ataendelea kushindwa!!!
   
Loading...