JK amteua Dkt Chrisant Mzindakaya kuwa Mwenyekiti Bodi ya NDC

Kivumah

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,428
1,050
Dr.-Chrisant-Mzindakaya.jpg

Dkt Chrisant Mzindakaya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt Chrisant Mzindakaya kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa- NDC.

Taaifa iliyotolewa leo kwa Idara ya Habari na Wizara ya Viwanda na Biashara na kuwainiwa na Katibu wake Mkuu Bi Joyce Mapunjo, imesema kuwa uteuzi huo umeanza tangu Julai 8,2011.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami kwa upande wake amewateua wajumbe wengine tia wa Bodi hiyo.

Wajumbe walioteuliwa ni Prof Idris Kikula ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Makenya Maboko (Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) na Prof. Ntengua Mdoe (Mhadhiri Mwandamizi, chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine).

Wajumbe wengine walioteuliwa katika bodi hiyo ni Dkt Marcelina Chijoriga, mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bwana Gabriel Masenga (Mkemia wa kampuni ya Far Chemical and Traveling Agency), Prof Abdulkarim Mruma (Giorogical Survey of Tanzania) na Bi Sondo (Wakili wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania).

Wengine ni Bi Eline Sikazwe (Mkurugenzi wa MAendeleo ya Viwanda, Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Bwana Gideo Nassari ambaye ni Mkurugenzi wa NDC.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, utendi huo utadumu kwa mudA wa miaka mitatu.
 
hao wajumbe mawazo yao ni POSHO tuu,hawana mawazo mapya ya kuteta tija ktk taifa letu
 
Hivi hakuna watu wapya? Ni lazima wale wale tu wa 47? Tubadilike jamani mpaka vijana wazeeke?
 
Hii siyo bodi mpya maana kabla ya uteuzi huu Dr, Mzindakaya ndiye aliyekuwa mwenyekiti. Tunapozungumzia shirika la Taifa la maendeleo ningetegema kuona watu wenye mawazo ya ujasiriamali kama Mengi, Bakhresa nk. Kujaza watu wa "theory" kutaleta tija yeyote?
 
[h=1]Rais Jakata kikwete Amteua Dkt Chrisant Mzindakaya Kuwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa- NDC.[/h]

Dkt Chrisant Mzindakaya Wajumbe walioteuliwa ni Prof Idris Kikula ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Makenya Maboko (Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) na Prof. Ntengua Mdoe (Mhadhiri Mwandamizi, chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine).
Wajumbe wengine walioteuliwa katika bodi hiyo ni Dkt Marcelina Chijoriga, mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bwana Gabriel Masenga (Mkemia wa kampuni ya Far Chemical and Traveling Agency), Prof Abdulkarim Mruma (Giorogical Survey of Tanzania) na Bi Sondo (Wakili wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania).

Wengine ni Bi Eline Sikazwe (Mkurugenzi wa MAendeleo ya Viwanda, Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Bwana Gideo Nassari ambaye ni Mkurugenzi wa NDC.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, utendi huo utadumu kwa mudA wa miaka mitatu.

ina maana hakuna watanzania wanoweza kuweka mawazo yao kwenye hizo bodi mpaka hao tu wenye majukumu nyeti tayari?
kurundikia watumishi mavyeo ni tatizo na ndio maana bodi hazina mashiko maana wako busy sana hao watu kufanya hata utafiti mdogo zidi ya maamuzi au mijadala ya vikao
 
Hoja ya urafiki katika uteuzi

Mh. Maziri wa Viwanda na Biashare, Dr C.Chami, alikuwa mkufunzi pale UDSM, kwa hiyo alifanya kazina wafuatao

1. Prof Idris Kikula ,
2. Prof. Makenya Maboko (Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam)
3. Prof. Ntengua Mdoe (Mhadhiri Mwandamizi, chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine),
4. Dkt Marcelina Chijoriga, mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
5. Prof Abdulkarim Mruma (Giorogical Survey of Tanzania) -nadhani nae alikuwa mkufunzi pia kabla ya kwenda GST
 
nilijua tu kunakitu hapa hawa maprof wote kwenye bodi moja wanakwenda kufanya nini?
hali wanamajukumu kibao, kumbe ni kujuana ndiko kumetawala
hivi ni kwenye ma professa wana akili ya kiwala kitu kuliko watu wengine ambao sio ma prof au PHD HOLDER?
mimi siamini hivyo mbona nchi zilizoendelea watengaji wake wakuu sanaa wana degree moja lakini wakina hapa tanzania wanawaingiza hawa PHD holder wetu mjini
 
Hii siyo bodi mpya maana kabla ya uteuzi huu Dr, Mzindakaya ndiye aliyekuwa mwenyekiti. Tunapozungumzia shirika la Taifa la maendeleo ningetegema kuona watu wenye mawazo ya ujasiriamali kama Mengi, Bakhresa nk. Kujaza watu wa "theory" kutaleta tija yeyote?

mkuu umenena bora wangeweka hata shigongo mara mia ya hao nchi imekwisha , wenzetu wanafanya kama ulivyosema hakuna kuangalia elimu wanaangalia experience kwenye mambo kama haya, maana hao hata njia za kukwepa kodi wanazijua so wataleta mawazo jinsi ya kuboresha au kushauri serikali vizuri wako kwenye game
 
Jk kwa kuteua tu hajambo ila kuteua wachapakazi ndo kazi anavofuatilia kuteua angefuatilia na umeme hivyo hili tatizo lisingelikuwapo
 
Zile hela mabilioni alizokopa NDC karudisha huyu? Au ndiyo mambo ya kumchagua ngedere alinde mgomba wa ndizi? Mzee tokea tupo vidudu miaka ya 70 yeye bado yumo tu. Kudadeki! Rukwa kawakilisha ubunge miaka zaidi ya 30 hamna chochote alichofanya zaidi ya kujijengea ranchi kwa hela za kukopa NDC.
 
Loh, Hivi NDC ipo mpaka leo?
Je ina kazi gani siku hizi hususan wakti huu wa soko huria na utandawazi?
 
Back
Top Bottom