JK amtembelea aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya VP wa TFF John Nchimbi MOI. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK amtembelea aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya VP wa TFF John Nchimbi MOI.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tusker Bariiiidi, Apr 14, 2010.

 1. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Wengi wetu tulionunua Magazeti ya jana tar.13/04/10,tulishtushwa na picha ya Rais wetu JK akiwa MOI akimwangalia majeruhi ambaye anaonyesha amejeruhiwa vibaya,tena baadhi ya magazeti yalikuwa wameweka picha hiyo katika kurasa ya mbele,caption nyingi zilieleza kuwa John Nchimbi (Majeruhi) ni mdogo wake Naibu waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa,Emmanuel Nchimbi... Mimi ni mmoja wa watu hao walioshtushwa na suala la Rais kuacha majukumu mengi yanayomkabili na kwenda kumuangalia mdogo wa naibu waziri... Kumbe John Nchimbi aliwahi kugombea nafasi ya makamu wa Rais wa TFF ambapo alishindwa na aliyekuwa akitetea nafasi hiyo Ramadhan Nassib,sasa Swali langu kwa Presidaa... Huko MOI alienda kumtembelea kama Mdogo wa Naibu waziri au kama aliyekuwa Mgombea wa u-VP TFF... Swali langu kwa Magazeti yaliyotoa picha ile Front page walikuwa na maana gani???
   
 2. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha mkuu,
  Umesahau Rais wetu ni mtu wa jamii?? Ha ha I am kidding!!! Kwani hujui Mh. Emamnuel Nchimbi ana inter-connection kubwa sana na Mkuu wa Nchi? Hivi mpiga debe mkubwa wa uchanguzi wa 2005 unamfahamu vilivyo? Ni Mh. Emmanuel Nchimbi? Kwanza huyu John Nchimbi anafanya kazi gani? Kila ofisi akiajiriwa haimaliziki mwaka au just a year na ka ushee anaacha kazi, na ukikaa kwa muda unasikia yuko tena sehemu fulani kaajiriwa!!!!!! Hivi huko Same alikuwa na shughuli gani hasa?!!!!! Ukitaka kumchunguza kuku au bata hutamlaaaaaaaaa. Yatakuumiza lakini meza kama kaa la moto!!! Hii ndiyo Tanganyika ati!!

   
 3. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kwani kuwa mgombea TFF au mdogo wa waziri kuna tatizo gani kujuliwa hali na Rais. mbona akitembelea watu wengine husemi
   
 4. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Alimtembelea nani??? Pili kwanini iwekwe Front page??? Mimi iliniogofya sana... ukizingatia kuwa niliiona hiyo picha kwenye uchambuzi wa Magazeti katika TV
   
 5. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  alimtembelea rafiki yake wa siku nyingi john Nchimbi. hata kubenea na wale wa mwananyamala aliowatembelea waliwekwa front page. pili mgombea makamu wa TFF ni mtu mzito kidogo
   
 6. U

  Ulisaja Kitojo New Member

  #6
  Apr 14, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mie natazama jambo hili pande zote mbili: Kwanza, kama Mkuu wa nchi huenda alitembelea Muhimbili kuangalia Wagonjwa, na bahati akamkuta huyu Nchimbi. Sasa magazeti kwa kuwa yanataka kuuza, wakaiweka kama habari muhimu. Pili, kwa kuwa Mhe. Rais ana urafiki na Mhe. Naibu Waziri, alimtembelea mgonjwa kama RAFIKI. Yote yawezekana. Ila swali kubwa linabaki: Je, KWANINI Mhe. RAIS hatembelei Hospitali NYINGINE hapa nchini? Hii natumai, ingetoa fursa sawa kwa wote. Ni mawazo yangu na mtazamo wangu!
   
 7. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2010
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Duh! the Presida is just Human at the end of the day! if you have feelings your human!!!!
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Anajali labda na mie atakuja kunitembelea .teteteteeh
   
 9. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Sielewi.. Kwa nini asimtembelee?
   
 10. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Wakati huo huo Gazeti lililomweka mdogo mtu Front page (MWANANCHI) limeweka picha ya Naibu Waziri Nchimbi katika ukurasa wa 10 akikabidhiwa 230,000/- na muasisi wa UWT-CCM... Kazi kweli kweli...
   
 11. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2010
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Thread kama hizi ndio zinazowafanya Clouds FM hususan kipindi cha Jahazi kuiponda jammi Forum.jamani ni lazima ujue Rais ni BinAdam na hakuzaliwa na haiba za Uraisi bali alikuwa ni mtu wa kawaida sana katika makuzi na hata kusoma na kuanza kwake kazi,
  Kipindi chote hicho ambacho ni zaidi ya miaka 50 alikuwa na maswahiba, maadui, ndugu jamaa n.k.

  Sasa lazima tuelewe kipindi chake cha miaka 10 ya uraisi wake hakiwezi kumtenganisha na jamii aliyoishi nayo kwa zaidi ya nusu karne.Tujadili mambo yenye tija jamani tuachane na mabo ya kipuuzi
   
 12. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hivi jamani kuna ubaya gani kwa kiongozi wa nchi kumtembelea mpiga kura wake aliyepatwa na matatizo kama yaliyompata bwana nchimbi?????
   
 13. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Ndio aende mpaka na wapiga picha wa Maelezo??? Front page karibu magazeti yote... Sishangai kwa Presidaa kwenda kuangalia wagonjwa ... Umenipata...
   
 14. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Ndio aende mpaka na wapiga picha wa Maelezo??? Front page karibu magazeti yote... Sishangai kwa Presidaa kwenda kuangalia wagonjwa ... Umenipata...
   
 15. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nina wasiwasi na uelewa wa mfikisha mada
   
 16. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #16
  Apr 14, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  mara utakapojifungua atakuja kukutembelea!!
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Apr 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kuna mambo mengine Rais anatakiwa kufanya katika private capacity. Siyo mtu kaenda kumsalimia bibi (picha), mara kaenda kumpeleka mtoto shuleni (picha), katoka msalani (picha)..! Ndio maana hata juzi hapa Obama aliwakimbia waandishi alipoenda kuwaangalia watoto wake mpirani. Rais kama alivyosema Barubaru ni binadamu na ana ndugu, marafiki na jamaa.. lakini ni muhimu kuyatengenanisha hayo na mambo na ya kitaifa.

  Kwa mfano, hivi wagonjwa wengine walipata nafasi ya kiasi gani kutembelewa na Rais? Kwa kitendo cha kuweka habari hiyo mbele wamempa upendeleo wa pekee mgonjwa huyo mmoja kwani tuna uhakika wa kutosha tu kuwa "mahitaji" yake yote yatatimizwa.. lakini vipi wale ambao hawajapata nafasi ya kutokea kwenye picha? Rais angeweza kutafuta muda muafaka wa kumtembelea bila ya kusababisha kuoneakana upendeleo fulani.

  Rais Marekani huwa anatembelea pale Walter Reeds Army Hospital.. kuwaona wapiganaji wa US wanaougulia pale.. ni mara chache sana utaona picha zake au hata taarifa kwani anafanya hayo kwa sababu ya moyo wake binafsi. Kikwete hawezi kufanya hivyo..
   
 18. T

  Tall JF-Expert Member

  #18
  Apr 14, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Kama kiongozi wa nchi na kama raia wa Tanzania,hakuna cha ajabu kumtembelea mgonjwa Muhimbili.Ndivyo nionavyo.
   
 19. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #19
  Apr 14, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Mzee Mwanakijiji... Umewa-Elimisha kina Baru*2 na P e n g o ... Sina shaka wamejua kwanini nilistushwa mno na picha ile... Ok ili kutimiza kusalimia wagonjwa namuomba Mh.Rais aende kumsalimia yule mlemavu wa ngozi pale Morogoro... Natumaini ata-shine tena mpaka FRONT PAGE za magazeti ya nje... Namshukuru sana MM
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Apr 14, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hilo siyo tatizo kabisa @ tall.. tutakuwa wajinga tukisema Rais asitembelee wagonjwa.. lakini.. think.. Mwananyamala wagonjwa walifikia kungojea kitanda watu sita; Temeke kina mama walikuwa wanalundikwa tu kwenye chumba cha "kupumzikia".. Rais hajafunga safari kwenda kujionea ili apigwe picha katika mazingira hayo.. kisa?
   
Loading...