JK ammwagia sifa Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK ammwagia sifa Lowassa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Sep 19, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa, kwa wapiga kura wa jimbo hilo wakati wa mkutano wa kampeni jimboni humo jana.  Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amemsifu Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kuwa ni mtu mwaminifu na mchapakazi.
  Akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika kiwanja cha Bomani, mjini Monduli jana. alisema wananchi wa Monduli wanapaswa kumchagua Lowassa ili awe Mbunge wao. Rais Kikwete aliwataka wananchi wa Monduli mkoani Arusha, kusahau matukio yaliyopita dhidi Lowassa.
  Lowassa aliwahi kuwa Waziri Mkuu baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani mwaka 2005, lakini alijiuzulu kutokana na kashfa ya zabuni ya mkataba wa kufufua umeme wa dharura uliyoihusisha kampuni ya Richmond Development Corporation.
  “Nawaomba wakazi wa Monduli, kura zenu zote mpeni mgombea huyu (Lowassa), kwani ni mchapa kazi na ndiye aliyewaletea ukombozi na anayeendelea kufanya hivyo,” alisema.
  Alisema kazi aliyoifanya Lowassa inafahamika kwa wakazi wa jimbo hilo, hivyo hawahitaji kuambiwa kwamba ndiye pekee anayefaa kuwa Mbunge.
  “Lowassa amewasaidia mambo mengi, na pia ni kiongozi mzuri ambaye nina uhakika hamtakaa kupata kiongozi kama huyu, ambaye atawaongoza vyema,” alisema.
  Alisema japo kuwa kuna vyama vingi vimejitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, lakini kati ya vyama hivyo hakuna kinachofanana na CCM kwa ubora. Rais Kikwete alisema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, CCM imefanya mambo makubwa, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule za sekondari za kata, ambazo ni moja ya ahadi zake alizotoa.
  Aliahidi kuwa kila shule ya kata itapewa walimu watano na kuongeza vyuo vikuu.
  Alisema anataka Wamasai waende shule badala ya kuchunga ng'ombe tu na ifikie mahali hata rubani wa ndege na viongozi wakubwa na kampuni mbalimbali wawe Wamasai.
  Akizungumzia watu wanaopitapita kuwadanganya Wamasai, Kikwete alisema wamekuwa wakijitokeza watu wanaojidai kutaka kuwasaidia Wamasai ili kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
  “Unajua mimi nasema serikali inawapenda na tumeandaa mpango mzuri kwa ajili ya watoto wa Kimasai, hivyo msidanganyike na watu hawa wenye vituo vya misaada ambao wanakuja na kujidai kuwa wanataka kuwasaidia … ni waongo,” alisema.
  Alisema watu wa aina hiyo wanafika jimboni humo na katika maeneo mengine kuwapiga picha na kuzipeleka nje kwa ajili ya kuomba misaada kwa lengo la kujinufaisha binafsi.
  Alisema watu hao wamekuwa wakidanganya kuwa serikali ya Tanzania haiwajali wala haiwasaidii watu wa pembezoni wakiwemo Wamasai.
  Rais Kikwete alisema serikali ya CCM imetenga zaidi ya Sh. milioni 800 kwa ajili ya kurekebisha barabara za Monduli ziwe katika kiwango cha lami.
  Aliahidi kuwa serikali imejipanga kuvuta maji katika sehemu nyingi zisizokuwa na maji ili yapatikane kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo.
  Alisema serikali itawafidia wafugaji waliopata madhara katika mwaka ulioisha kutokana na njaa iliyowakumba na kusababisha mifugo mingi kufa.
  Naye Lowassa aliwataka wananchi wa jimbo hilo kumpa kura za ndiyo Rais Kikwete, kwa vile amechangia kwa kiasi kikubwa kuleta maendeleo jimboni humo.
  Rais Kikwete alifanya mikutano katika maeneo ya Ngaramtoni, Longido, Namanga na Monduli.
  Alisema lengo la serikali yake kuanzisha shule za sekondari za kata ni kuhakikisha kuwa jamii nzima inapata elimu bila ubaguzi.
  Kuhusu soko la mifugo, alisema katika kipindi cha miaka mitano ikiwa CCM itaingia madarakani, itahakikisha inajenga minada.
  Alisema watalaamu wameishatumwa kufanya utafiti ili kuanza kutekeleza kazi hiyo.
  Habari hii imeandikwa na Woinde Shizza, Monduli na Hellen Mwango, Longido Arusha.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,309
  Trophy Points: 280
  Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni!.
  Ukiondoa tuhuma za richmonduli,
  Lowassa kweli ni :-
  Mchapa kazi kuliko JK!
  Mtendaji kuliko JK!,
  Mfuatiliaji kuliko JK!
  Ila hata yale mengine, pia ni kuliko JK! (JK alikuwa anajionyesha wazi wazi, EL, kimya kimya!)
  Hivyo hawa wote ni wale wale!.
   
 3. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  :mad2: EL
   
 4. nyengo

  nyengo JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2015
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 433
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kikwete na wana CCM mmesahau kuwa Kikwete alisema “Nawaomba wakazi wa Monduli, kura zenu zote mpeni mgombea huyu (Lowassa), kwani ni mchapa kazi na ndiye aliyewaletea ukombozi na anayeendelea kufanya hivyo"
   
 5. HHHK

  HHHK JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2015
  Joined: Aug 20, 2013
  Messages: 745
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Ndio maana watu wanaambiwa waweke akiba ya maneno
   
 6. m

  maskio popo Senior Member

  #6
  Oct 2, 2015
  Joined: Sep 3, 2015
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli akiba yamaneno inahitajika alipokuwa kigoma alisema kuwa mwenye richmond ni yule anaetembea na lisu amesahau kuwa mwaka 2010 yeye alikua nae. jambo jema nikuwa maamuzi ya walio wengi wanamtaka awe rais nami nataka awe rais wangu na nimeandaa sherehe fupi ya kujipongeza kwa ushindi wa kishindo nimalize kwa kusema peopleeeeeeees!!
   
 7. youngsharo

  youngsharo JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2015
  Joined: Jan 8, 2015
  Messages: 2,483
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  ahahahahaaa! oyooo!
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2015
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. SIPRITE

  SIPRITE JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2015
  Joined: Jul 15, 2015
  Messages: 487
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Dah uliye 2fufulia huu uzi
   
 10. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #10
  Oct 2, 2015
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,739
  Likes Received: 8,005
  Trophy Points: 280
  Asante sana kwa huu MVINYO wa kale. Hakika umekwiva!

  Nafarijika sana kujua kuwa hata Rais Kikwete ana imani kubwa sana na Lowassa
   
 11. Fisadidagaa

  Fisadidagaa JF-Expert Member

  #11
  Oct 2, 2015
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 901
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Hapa mazombi ya Lumumba huyaoni kutia makalio yao.
   
 12. Majigo

  Majigo JF-Expert Member

  #12
  Oct 2, 2015
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 5,418
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  ndo kusema old is gold?
   
 13. screpa

  screpa JF-Expert Member

  #13
  Oct 3, 2015
  Joined: Sep 10, 2015
  Messages: 5,651
  Likes Received: 7,261
  Trophy Points: 280
Loading...