JK amevuja katiba na hati ya Muungano ktk mabadiliko ya baraza la mawaziri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK amevuja katiba na hati ya Muungano ktk mabadiliko ya baraza la mawaziri?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mikael P Aweda, May 18, 2012.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wanandugu wa JF,
  Nimekuwa nikitafakari kuwa tulipoungana mwaka 1964 tulikuwa na mambo 11 na leo tuna mambo 22.Sawa kabisa uhalali wa kuongezeka ni hoja nyingine. Lakini kuna mambo mengi yasiyo ya Muungano ikiwepo afya na mengine mengi. Mambo yasiyo ya Muungano kwa upande wa Zanzibar yako chini ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Baraza la wawakilishi. Mambo yasiyo ya Muungano ya bara yanashughulikiwa na Serikali ya Muungano kwa kuwa Serikali ya Tanganyika haipo, na Bunge la Tanganyika halipo. kwa mantiki hiyo, mambo yote yasiyo ya Muungano ( afya etc) ya bara yatashughulikiwa na Serikali ya Muungano.
  Mambo yasiyo ya Muungano kwa upande wa zanzibar yanasimamiwa na wanzanzibar kupitia serikali yao na yanatungiwa Sheria na baraza la wawakilishi la Zanzibar na yanasimamiwa na mawaziri wazanzibar.

  Sasa naomba tujiulize.
  Kwa kuwa afya haiko ktk mambo ya Muungano na kwa kuwa mambo yasiyo ya Muungano bara yanashughulikiwa na Serikali ya Muungano. Kwa maoni yangu Rais anapoteua Waziri wa Afya kutoka Zanzibar ni kinyume na katiba na hati ya Muungano. Hii ni kwa sababu mzanzibar hawezi kuwa waziri wa afya wa Tanganyika kama ilivyo ngumu kwa Mtanganyika kuwa waziri wa afya ktk serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Zbar wana waziri wa afya.

  Kwa kuwa tumeungana ktk mambo 22 na kuwa kuna mambo mengi sana yasiyo ya Muungano, hivyo basi Mzanzibar akiwa Rais wa Muungano ina maana kuwa atakuwa pia Rais wa Watanganyika ktk mambo ya muungano na yasiyo ya muungano. Kwa mantiki hiyo na kwa mujibu wa katiba na hati ya Muungano, ni kinyume na katiba na hati hiyo kwa Mzanzibar kuwa na maamuzi ktk mambo ya watanganyika ambayo hatujakubaliana na kuyaingiza ktk ya Muungano. Mfano Rais Mzanzibar kusaini miswada ya sheria ili kuwa sheria kamili ktk mambo yasiyo ya Muungano ni kosa. Kwa sababu hiyo, kabla ya mabadiliko ya Katiba Dr Bilal hana uhalali wa kuwa Rais wa Muungano.(Je,Ali H.Mwinyi ilikuwaje?)

  Kwa kuwa Bunge la Muungano linatunga sheria ya mambo ya Muungano na yasiyo ya Muungano, na kwa kuwa mambo yaisyo ya Muungano ya Zanzibar yanatungiwa sheria na Baraza la wawakilishi wazanzibar - wabara hawaruhusiwi kikatiba kushiriki huko. Na kwa kuwa hatuna Bunge la Tanganyika, mambo yasiyo ya Muungano ya watanganyika yanashughulikiwa na Bunge la Muungano. Hivyo basi, kwangu mimi si sawa na wala si haki kwa wabunge wa Zanzibar kujadili, kupitisha au kupigia kura ya maamuzi mambo yasiyo ya Muungano yanayohusu watanganyika ktk bunge la Muungano. Hii ni mantiki ya kawaida tu.

   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huku ni kuwadhalilisha wabunge wote wa CCM toka Tanganyika. Kwamba miongoni mwao hakuna anayefaa kuongoza wizara ya afya hivyo Rais amelazimika kuchukua mtu toka Zanzibar.
   
 3. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  vingapi vya muungano vimevunjwa mbona hampigi kelele? hilo la kupewa MWinyi uwaziri wa Afya limewauma sana! mbona mna maneno sana ?!
   
 4. R

  Rayase Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  I wish mtalaam na mwelevu wa mambo ya katiba anisaidie nami pia! Tunaposema hili jambo/haya mambo ya Muungano na /jambo mambo yasiyo ya muungano nini maana, dhana (logic ) yake. tusaidieni tafadhari jamani
   
 5. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,813
  Likes Received: 1,057
  Trophy Points: 280
  nilitegemea kabla hujatundika hapa ungekuwa umeshaiuliza katiba kutusaidia...... tusubiri majibu kwa werevu!
   
 6. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  FJM hiyo nalo neno. Halafu nashangaa wabunge wa ccm bara hawamhoji, wamekaa kimya.
   
 7. Naibili

  Naibili JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,681
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Tatizo nyie watu huwa ni wagumu kuelewa, hawa jamaa wametufanya kama watanganyika ni mambumbu, kuna mtu anaitwa makamu wa rais huyu ndo anamkaimu Rais, anaweza kufanya maamuzi yoyote hata ambayo hayamo kwenye muungano, Na tuombe isije tokea tena, tukiwa na rais anayetoka visiwani anaweza kutuuza watanganyika kama akiamua, lakini Rais anayetoka Tanganyika hawezi kuamua jambo lolote lisilo la muungano huko Zanzibar! kilichobaki ni kuidai tanganyika yetu.
   
 8. e

  evoddy JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 302
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kimsingi huyu rais wetu ana matatizo mengi sana kwenye sheria maana uteuzi wake mwingi unamashaka,aidha washauri wake wa kisheria ni mbumbumbu wa katiba.Angalia swala la uteuzi wa tume ya taifa kukusanya maoni juu ya katiba mpya,amewateua wabunge kushiriki wakati sheria yenyewe inakataza hii inaonyesha kuwa rais wa Tanzania anamatatizo ya kisheria.

  Kuhusu hili la wizara ya afya sielewi huyu mwinyi yuko wapi maana serikari ya awamu ya tatu alikuwa mbunge kutoka jimbo la Mkulanga awamu ya nne katokea Zanzibar sasa tujiulize huyu ni wa wapi hasa?
   
Loading...