JK amedidimiza Uchumi: World Bank | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK amedidimiza Uchumi: World Bank

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malafyale, Jun 30, 2009.

 1. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,209
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  BENKI ya Dunia (WB) imeeleza kuwa, pamoja na viongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete, kuelekeza juhudi zao za kuzifanyia mabadiliko ajenda mbalimbali za uchumi wa nchi, takwimu za mashirika mbalimbali ya kimataifa zimebainisha kuwa, kwa miaka ya hivi karibuni, Tanzania inaendelea kudidimia mwaka hadi mwaka.

  Taasisi hiyo kubwa ya kifedha duniani ikiyanukuu mashirika ya Public Expenditure and Financial Accountability, Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uwazi katika matumizi ya fedha za umma pamoja na Transparency International, imebainisha kuwa vigezo vya gharama za kufanya biashara na ushindani wa biashara ya kimataifa viko chini.

  Mkurugenzi wa WB Kanda ya Afrika katika nchi za Tanzania, Uganda na Burundi, John Murray Mclintire, alibainisha hayo jana, jijini Dar es Salaam wakati akitangaza miradi ambayo serikali itasaidia kupitia sera ya kuisaidia bajeti.

  Miradi ambayo itasaidiwa na benki hiyo ni pamoja na dola milioni 190 kwa ajili ya kupunguza umaskini, dola milioni 220 kwa ajili ya kuisaidia Programu ya Usalama wa Chakula (AFSP), dola milioni 90, kwa ajili ya programu ya kuinua kilimo pamoja na dola nyingine milioni 151 kwa ajili ya upanuzi wa mradi wa huduma za mawasiliano kwa nchi za Malawi, Tanzania na Msumbiji.

  Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, sera ya mabadiliko ya kisheria na serikali za mitaa katika sekta za maendeleo za serikali na binafsi zimeonyesha ufanisi mdogo.

  ‘‘Ufanisi katika kiashirio cha kifedha umeshuka kutoka dola za Marekani milioni 200 hadi 190, hiki ni kielelezo kuwa hakuna mafanikio ya kisera zaidi yakiwa ni mazingira ya kufanya biashara kwa wazawa na wawekezaji kutoka nje na sera ya mabadiliko katika usimamizi wa fedha za umma,” alisema mkurugenzi huyo.

  Iliendelea kuelezwa kuwa, pamoja na ripoti ya mwaka 2008 ya upitiaji wa sera za nchi pamoja na ule wa kitaasisi kuonyesha kuwa Tanzania ilikuwa juu kwa asilimia 3.8, mwaka huu imeonyesha kushuka kwa asilimia 0.9.

  ‘‘Japokuwa uongozi wa nchi umeonyesha juhudi zake katika kuzifanyia ajenda mbalimabali marekebisho kwa ajili ya kujenga uchumi wa kisasa, utekelezaji wa marekebisho hayo kimfumo umekuwa ukidhoofika kwa miaka kadhaa sasa na kwa baadhi ya maeneo imeonekana kushindwa kufanya kazi kabisa,” aliongeza.

  Bila kuitaja awamu ya tatu iliyoongozwa na Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, Mkuu huyo wa WB alieleza kuwa, Tanzania imetekeleza marekebisho kadhaa na yameonyesha ufanisi mkubwa, hasa katika sera ya uchumi mkubwa (Macro economy) hali iliyothibitishwa na ukuaji wa kuridhisha wa uchumi na kupunguza kabisa mfumuko wa bei.

  Aliendelea kueleza kuwa, ukuaji wa uchumi umeendelea kukua kwa kiasi cha asilimia saba kwa miaka mitatu sasa, hali inayoonyesha kuwa kuna ufanisi katika hifadhi ya fedha za kigeni.

  Mkurugenzi huyo alisema kuwa, utafiti wa bajeti ya kaya, ndoto ya kufikia Malengo ya Milenia (MDGs), hapo 2025 imeonyesha hayatafikiwa hata katika maeneo ambayo awali yalionekana yangefikiwa na hata kuondoa umasikini na kupata huduma za afya na majisafi, na kushauri msisitizo katika maeneo hayo unatakiwa.
   
 2. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Maneo kama haya yangetoka kwenye Mdomo wa Lipumba, Zitto Kabwe watu wangesema kuwa ni siasa tu, Lakini kwa sasa hali ni mbaya sana kuliko hata kipindi cha Mkapa, Sasa wakati mwingine watawala wetu wanajua kuwa kuwa na pesa ndio kitu pekee bila ya kufanya au kutengeneza mazingira mazuri ya kuwezesha Watanzania, Mikakati kama Pesa au Mabilioni ya Jk ni Mfu na haiwezi kuinua maisha ya Watanzania, But ni kuanzisha viwanda na uwekezaji wa Wazawa, Ukweli ni kwamba Mzee wa Kaya ameshindwa kabisa
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Feedback muhimu yenye kuhitaji kuangaliwa kwa umakini
   
 4. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  basi na hili liwe hukumu katika uchaguzi ujao..tuachane na propaganda za kwenye majukwaa kwamba uchumi umekua
   
 5. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuna mambo mengi sana katika uchaguzi ujao waseme wanafanya nini hawa Jamaa na Taifa letu pia
   
 6. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,209
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Billion 34 kwa safari za waheshimiwa nje ya TZ,billion 19 za sambusa na chai wizarani,million 180 kumlipia bure mama Mongela pesa alizotumia kwa shughuli zake binafsi bunge la Afrika na nyingine nyiiiiiiingi zinazochotwa kila siku na watendaji wa baraza la mawaziri lililo kubwa sana kwa muundo tofauti na kipato chetu!Sasa WB walitegemea kuna maendeleo hapo?
   
 7. F

  Froida JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hali imeonyesha kabisa hali ya wananchi imekuwa maskini zaidi na maisha ya kawaida ni gharama sana,Kwa kweli Mkuu wetu angeweka mguu chini aache kwenda kupokea zawadi za jezi za Mpira wa kikapu
   
 8. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hakuna asiyelijua hilo kuwa huyu mtu wa bagamoyo hana lolote. Kusema ukweli, kama Mungu angesaidia mwakani akawepo mtu mwingine mwenye akili kuliko yeye, tungefika mbali. huyu anapendezesha sura tu, hana lolote, watu wanampenda ndo nyota yake, kupendwa kwake hakutusaidii lolote, kiufupi hana lolote kabisaaa.

  anachosubiri tu ni mwakani kuwakamata waislam wampe kura ili awaahidi kuwapa mahakama ya kadhi baadaye, ameikanya sasahivi kwasababu anaogopa wakristo wanamkacha kura mwakani. akpita tu kadhi anawapa, ndo anachosubiri. ref. kikao cha kondoa na mashehe.
   
 9. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tazama Hata Hizo Programme nyingi sana ni sawa na sio za uzalishaji kabisa nyingi kwa ajili kuendeleza na kufanye watu waishi tu, hakuna jipya hapa na Sisi kama watanzania tunataka programme za Viwanda na uwekezaji lakini sio hizi, ni kazi ya Serikali kufanya mambo hata
   
 10. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Mbona tuliyajua hayo siku nyingi?

  Uchumi tunao lakini tunaukalia.

  Wataalamu tunao lakini lazima wale na mafisadi ili wapewe kazi.

  Viongozi, HATUNA
   
 11. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,357
  Likes Received: 3,116
  Trophy Points: 280
  Habari ndo hiyo ndugu zangu,jk muua sura tu marekani sijaona chochote muuda wote aliokaa madarakani zaidi ya tabasamu lake tamu.Kwa kifupi amefulia! Ingekuwa nchi za wenzetu asingepata tena Urais kwa awamu ya pili lakini ka kuwa yal mambo ya ''UTARATIBU TULIOJIWEKEA CCM'' Rais anakaa mihula miwili
   
 12. s

  samvande2002 JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2009
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  na bado...
  hii nchi itaendelea kulost mpaka ikome yenyewe,
  theres too much unneccessary expenditures of public resources and too much of politics with few implimantations;
  ni ujinga mtupu unaoendelea katika serikali ya hii nchi...
  i dont give it a credit at all.
   
 13. Ngorunde

  Ngorunde JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2009
  Joined: Nov 17, 2006
  Messages: 1,124
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Labda wakisema hao wazungu watawala wetu wanaweza wakaelewa. Maana wakisema wanauchumi wetu wanaitwa ni wapinzani ambao hawathamini JUHUDI KUBWA ILIYOKWISHAFANYWA NA CCM AWAMU YA NNE KATIKA KUBORESHA MAISHA YA MTANZANIA.
   
 14. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Na ndio wao wanakwenda kuomba kwao na sasa wanasema, Hata hivyo huyu jamaa wa benki ya Dunia aliogopa naye kusema kwa Lugha ya Upinzani maana yeye ni mwakilishi tu
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Tatizo hapa JK ameshindwa kuunda team work ambayo inaweza kusisimua uchumi wa nchi lakini akiambiwa ndo kwanza anaziba pamba maskio kinacho baki oooh ni siasa sasa sijui siasa inatoka wapi hata pale kwenye ukweli. Kwa kweli JK ameshindwa kabisa lazima tuwe wazi na akipewa na 5yrs basi tutakuwa tumedidimia sana na kurudi kule kule tuliko toka. Angalieni nchi ya Rwanda wanavyo tuacha.
   
 16. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sasa yeye mwenyewe ni Mchumi, sisi tulitegemea akifikiri kama Economist lakini inakuwa kinyume chake na sisi huwa hatujui kama kweli kuna washauri wa uchumi wa Rais, naombeni jina lake kama kuna mtu anajulikana
   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ataanza kufanya kazi baada ya 2010 mkimchagua tena...maana sasa analinda ulaji wa mwakani msije mkamtosa ndo maana washikaji kibao kawachagua wengine hata sifa hawana ndo wanao muharibia.
   
 18. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #18
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sasa anazunguka kama Vasco Dagama tu, maana hata akisema kuwa alifanya nini miaka yote hiyo mitano 5 siwezi kusema na kutafuta au kufungua chuo cha Dodoma tu au kuna jingine
   
 19. T

  TrueVoter JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 868
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 80

  Mtu yeyote anayesema maneno ya jinsi hii, is more likely akili yake ina hitilafu kubwa, kama kiongozi hawezi kusumamia walio chini yake vzr, ni wapi anaweza aminiwa tena kufanya kazi aliyotumwa na watu kufanya???
   
 20. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #20
  Jun 30, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  avator yako iko bomba, lakini location yako nadhani ingekuwa best kama ingekuwa graveyard na sio UVUNGUNI
   
Loading...