Elections 2010 Jk amechaguliwa na wana ccm tu na je ni rais wa wanaccm tu au?

marijanda

Member
Oct 27, 2010
50
4
katika maisha yangu nimepiga kura hii mara ya nne lakini mara zote tumeshuhudia watanzania wakijitokeza kupiga kura na hasa huwa karibu wakuwepo watu wanapiga kura mpaka sa vituo vinafungwa.
lakini cha ajabu mara hii ilipo fika saa sita/saba wasimamizi wa vituo vingi walikuwa wamepumzika na hata wengine kusinzia kwa vile hakukuwa na mpiga kura aliyepiga hodi ktk vituo vya kupigia kura.

nakumbuka katika chaguzi kuu kama tatu zilizopita wapiga kura wote waliopiga kura kwa kulinganaisha na waliojiandikisha walikuwa kama asilimia kati ya 70-85% lakini mwaka 2010 ni maajabu kuona ni nusu ya asilimia hizo yaani 42.%ambao kati yao ni asilimia 27%<5mil> tu ndo walimpigia kura ili awaongoze watanzania karibu 43mil hii haiiniingii akilini na sijui yeye na wakuu wenzake katika chama wanalichukuaje lakini pia nauliza yeye inaelekea hajashtuka kabisa analina ni sawa na ndo maana haja lizungumzia kabisa katika hotuba yake yeye alichoona ni changamoto ya wapinzani.

lingine ni wanachama wa CCM wako milioni tano nchi nzima hivyo ukilinganisha na kura alizo pata ndo ni sawa zinalingana so inaonekana ni wanachama ndo wamempigia kura peke yao. Japo pia hatujui kama halali kura ni ngapi na ngapi zilichakachuliwa.

nafiiri huu ndo mwanzo wa anguko la ccm kwa vile hajiulizi kwanini watu hakujitokeza wengi wanasema kuwa hata wapige kura hakuna differnce maana ni waleewale watashinda kwa hiyo wameona hwana haja ya kupoteza mda kitu ambacho kinadhihirisha kuwa wananchi wengi tayari wanajua suala la uchakachuaji uliokithiri.

shime watanzania na wanamageuzi safari yatu haijafika ndo kwanza imeanza na imetupasa kuendelea mpaka mageuzi ya kweli yatokee na ni sisi watanzania tutakaoleta.Tujue fika hakuna mtu kuja atakayeleta mageuzi ni sisi wenyewe hata kama tumeshindwa lakini tujue kuwa ndo mwanzo wa kujipanga na kuendelea kueneza sera ya mageuzi ili tujinusura na umaskini na ufisadi huu wa kiuchumi na kisiasa pia.

NAwasilisha karibuni kwa kuchangia mawazo

Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom