JK amcheza bintiye ngoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK amcheza bintiye ngoma

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Jafar, Jan 5, 2009.

 1. J

  Jafar JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Katika hali ambayo si ya kushangaza, Rais JK amemcheza ngoma bintiye (yaani kufundwa jinsi ya kuishi na mume). Ngoma hiyo ambayo ilihitimishwa mjini Bagamoyo (viwanja vya nyumbani kwao) siku ya Jumapili tarehe 4 Januari.

  Sherehe hizo ambazo zilichukua takribani si chini ya siku kumi, ambapo watu walikula na kunywa zilikuwa na mabinti wawili (waliochezwa), mmoja ni mtoto wa JK na wa pili ni mtoto wa shoga yake Salma kutoka kusini ambaye alipendelea wacheze ngoma pamoja. Kwa hiyo watu walishuhudia ngoma za kimakonde, kikwere na kizaramo kwa pamoja. Aidha, bendi ya muziki ya mjini hapo, Bwagamoyo Sound ya Mwinjuma Muumini ilitumbuiza siku zote hizo za sherehe (nje) bure. Huku Salma na kundi lake wakimwaga radhi mjini hapo, JK mwenyewe aliwasili tarehe 3 Januari Jumamosi jioni (saa 1 jioni) kwa ajili ya mkesha wa kuamkia Jumapili.

  Eneo la sherehe lilipambwa na majukwaa ya maturubai yaliyo nakshiwa kwa unadhifu. Maturubai hayo yapatayo kama 20 yalileta maandhari nzuri hasa usiku ambapo taa za kila rangi zilizungushwa kuunganisha maturubai hayo. Ulinzi mkali ulikuwepo watu wakishuhudia wingi wa FFU na magari maalum ya Ikulu yakiwa yamepaki pembeni.

  Sherehe ilifana.
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huu ni ufujaji wa hali ya juu.
  Hatukatai mtoto wake kuchezwa lakini tunahoji gharama hizo alizo tumia ni za nani?Kama ni za sisi walalahoi basi huu ni ufujaji.
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwa upande wangu nafurahi sana kama Rais anaendelea kuheshimu mila za kabila lake. Ni jambo la kujivunia.

  Hata hivyo nakuunga mkono kwamba inabidi tuelewe hiyo sherehe iligharimiwa na nani na hao watu wa usalama walilipwa na nani?? Nitaomba kuelimishwa iwapo Raisi anahudhuria au kushiriki mambo binafsi, suala la ulinzi linagharimiwa na Ikulu au yeye mwenyewe? Mimi nasikitika sana kwamba tumejenga utaratibu wa kishenzi hapa nchini wa kutumia pesa nyingi kwenye sherehe. Raisi alitakiwa kuwa mfano kwa kupinga suala hilo. Mambo ya kuwaiga Nigeria na nchi nyingine ni hatari kwa watu masikini kama sisi na hasa hasa kama viongozi wa juu wanashiriki na kuunga mkono kitu hicho.
   
 4. K

  KUNGUNI Member

  #4
  Jan 5, 2009
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nadhani tunakuwa wepesi kukimbilia kwenye kulaumu au kunung'unika kabla hatujapata ukweli wa jambo lenyewe. Hapa hatujaambiwa ni kiasi gani kimetumika katika sherehe hizi. Je ni kiasi ambacho JK mwenyewe kama JK hawezi kukimudu! Tupate details kwanza.
   
 5. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ninahakika kuwa lazima fedha yetu walipakodi kwa kiwango fulani l zilitumika katika unyago huu wa mwanae Jakaya; inawezekana gharama za pilau na malaji mengine alilipa mwenyewe na Subash Patel wake lakini gharama za magari na usalama they come with the office!! Kulinda utamaduni wetu ni jambo jema lakini tufanye kulingana na hali ya kipato cha nchi yetu kuiga style za wanigeria au lifestye ya mswati ni kujipoteza!! Please watawala fanyeni mambo mkijua kuna wananchi hata hapo Bagamoyo wanalala na njaa!!
   
 6. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2009
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Nampongeza Rais kwa kujali mila na desturi zetu hili ni jambo linalotakiwa kuigwa na viongozi wetu.
  Kuhusu ufujaji wa pesa, mimi naomba kutofautiana kidogo na fidel80 na Dark city. mimi nadhani cheo cha Rais ndicho kikubwa zaidi hapa Tanzania na siwezi kuamini kwamba Rais anaweza kukosa uwezo wa kufanya sherehe kama hiyo hasa ukizingatia kwamba utamaduni wa watanzania ndugu jamaa na marafiki tunachangiana ktk sherehe mbalimbali, lakini pia yeye kama raia mwingine anayo haki ya kufanya sherehe zinazohusu familia yake na suala la ulinzi ni la lazima na serikali lazima itoe ulinzi kuhakikisha kwamba kiongozi wa nchi anakuwa salama. Je tumwache bila ulinzi kwa sababu anafanya mambo yake binafsi ambayo pia ni haki yake? akipata madhara tutasemaje?
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo wewe huoni tatizo Rais wetu akifanya matanuzi ya kufuru wakati anashinda Ulaya akitembeza kopo la Matonya??

  Mimi naamini Rais anatakiwa kuwa mfano kwa raia wake kwa kila jambo analofanya. Kwa hiyo, sioni kama ni busara kwake kujihusisha na sherehe za kifahari wakati anaongoza nchi ambayo ni masikini wa kutupa; na kuna akina mama wajawazito wanakufa kwa kukosa 10,000/- ya kununulia gloves. Angeweza kufanya sherehe ndogo tu na ikapendeza sana ili wote tuige na tuache kupoteza pesa katika mambo ambayo si ya msingi. Nyerere angekuwa mtanuaji tungekuwa wapi? Kwani tungekuwa tofauti na Zaire ya Mobutu?
   
 8. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Mbali ya hizo garama, mimi naona ni upuuzi raisi wa nchi kuacha ikulu wazi anakwenda kucheza mdundiko ucku kucha! Kumbe ndo maana alimkata dry mkuu fulani aliye sema ngoma ya CHAGULAGA inachangia maambukizi ya virusi!. Sasa hizo ngoma za kizaramo ndo kabisaaaaa! make kumwaga razi ni kwa kwenda mbele na kujirusha kwenye mihogo huku kelele za mchiriku zikiwanyima jirani usingizi!

  Kibaya zaidi ni adha walio ipata askari wiki nzima iliyo pita kila siku kusimama barabarani kupigwa jua kali wakisubili msafara wa Salma upite akielekea bagamoyo kuanda shughuli asubuhi na kurejea jioni. Huo wa JK foleni ilikuwa mwisho watu tumeegeshwa pembeni mwa barabara nusu saa tukisubili msafara! ambao kwa vyovyote vile unatanua b aranabarani kwa gharama zetu!

  Vitu vingine bwana ukisha kuwa bosi inabidi uviangalie kwa jicho la tofauti hasa ukizingatia dhamana uliyo beba na kwamba mwenyewe ndo kioo cha jamii!
   
 9. J

  Jafar JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Japo kwa sasa ni vigumu kupata gharama halisi ya sherehe hiyo labda uwe ndani ya kamati ya ngoma lakini pia Paradise Hotel ya mjini hapo ilifaidika kwani pamoja ya kwamba JK na familia yake ndipo walipofikia pia hata ndugu wengi kutoka Msoga (Chalinze), Lindi na Mtwara, waliweza kuonja raha ya kulala hotelini hapo kwa siku hizo zote.
   
 10. k

  kananyayo Member

  #10
  Jan 5, 2009
  Joined: Dec 15, 2008
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hongera Rais kwa kujali na kudumisha utamaduni wako, hususan wakati huu ambao kuna malimbukeni wanaoshupalia tamaduni ngeni wakidhani kuwa ndio maendeleo ama kwenda na wakati. Mtoto kumfunda kabla ya kuolewa ni jambo la kiungwana, na stahiki tangu enzi za mababu. kuhusu gharama nasema no research no rights to comment.
   
 11. I

  Ipole JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Waswahili husema msahau kwao ni mtumwa kama wengi mlivyosema kuwa Rais anatakiwa awe mfanao wa kuigwa hiyo ni pamaja na kutosahau mila zake
   
 12. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huu ni upotofu wa kiimani......
   
 13. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Kwa hili JK nampa Nokia/.......5, aendelee kudumisha mila,
   
 14. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Gharama tupu....wakazi wamekula na kunywa week nzima..ok anyway ndio mila na desturi tuzidumishe ...ila gharama kubwa sana sana sana....mji mzima ulikuwa outing pale kwa week
   
 15. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #15
  Jan 5, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hongera sana Rais!
  Hiyo ni bora sana mara elfu kumi kuliko kitchen party zinazofanywa kwa wazi, mtu anawaza harusi yake na mnadhani kumfunda kwa masaa hayo manne inasaidia. Muhimu sana jamani kuwafundisha binti zenu, but I insist, indoors please! siyo na maspika juu, mchukua video mwanaume, wapita njia wanasikia.
  Hata hivyo natoa changamoto, na vijana wa kiume pia wafundwe kukaa na wake zao, wanayoyafanya wanawake kwao nao pia wanayahitaji hayohayo.
   
 16. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tatizo letu kubwani kusahau kuwa kuwa mtu anapochaguliwqa kiongozi basi mahitaji yake yote muhimu ya kibin adam yanakwisha bila kujali hayo ya kimila, sasa mtoto wake anatakiwa kuchezwa unyago, yeye rais afanyaje? angefanyia Ikulu je? classes zeteu za maisha zinatufanya tuishi kwa standard ya classes zetu not more! wengine toka tuzaliwe hatujawahi hata kufanyiwa birth day part na wazazi wetu kwa sababu ya maisha yao wengine birthday wanafanyiwa hata watumboni na kupoteza maana ya birth day so acheni JK afanye hayo that is his class
   
 17. S

  Stephano Member

  #17
  Jan 5, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa upande mmoja nampongeza rais kwa kulinda mila lakini upande wa pili nafikiria atawaambiaje jamii zenye asisli ya kucheza watoto wao kuacha kupoteza muda na fedha kwenye ngoma na badala yake wapeleke watoto shule?
   
 18. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2009
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hongera JK kwa kudumisha mila
  Bado najiuliza kwa muda wa hiyo wiki watu hawafanyi kazi za kujenga taifa wanakwenda kwenye ngoma na mziki wa bure haoni kuwa mandeleo yana didimia balaya kundelea?
  Sawa anawza akawa ametumia pesa zak kwa ajili ya sherehe ya bintie na za shostito wa wife, Je!hao wanausalama (FFU na wengineo) na magari ya ikulu yametumia garama za nani kama si za wananchi? nikimaanisha malipo yao ya siku wawapo nje ya kitua chao chakazi, usafiri hizi psa sio za walipa kodi?

  Maana ENZI ZA MWL MTU AKITAKA KUFANYA SHUGHULI YAKE ANAFANYA YEYE NA FAMILIA YAK NA JAMAA WAKARIBU TENA NYAKATI WATU WAMEPUNZIKA NA SIO WIKI NZIMA WATU WANASHEHRRKEA UBWABWA NA SODA,BIA ZA BURE HUU NI WIZI MTU...
   
 19. M

  Mkora JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kazi kweli kweli mbona husemi ufujaji aliofanya mwanasheria Shitandala
  Hata kujaza fomu hajui
  Na katupoteza kiti chetu Mbeya Vijijini
   
 20. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hee?? hivi wapinzani kugombea ubunge nao wanatumia pesa za walipa kodi?

  Mi nilidhani JK tunamsema kwa vile matanuzi ya unyago wa mwanae kwa wiki nzima lazima yametugharimu sana walala hoi!

  Hata hivo napatwa na kigugumizi huyu mkuu wetu atapate jeuri ya kuwambia watu wafanye kazi ili hali yeye mwenyewe anaalika kijiji kizima kipoteze wiki nzima kwa kucheza mdundiko na mdumange!
   
Loading...