JK aliwadanganya waislamu? ni kigeu geu au ?

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,385
wote tunakumbuka kuwa kipindi cha kampeni JK na ccm waliiwaahidi waislamu mahakama ya kadhi..sasa hivi hata kabla mwaka haujaisha kawageuka ..sasa hii tuiite ni kitu gani? .ina maana hata zile ahadi zlizozitoa kipindi cha uchaguzi hatazitekeleza
huyu mwanasiasa si ni kigeu geu?
 
Si kigeu geu,sasa angesema ukweli si wangemtosa kura,kama wanataka kuanzisha waanzishe lakin wasitegemee kupata pesa kwa serikali,serikali ta tz haina dini,wananchi ndio wanadini,na hizo pesa sijui watazitoa wap za kuanzisha iyo mahakama,sababu misaada yenyewe toka arabun ni tende,siyo pesa
 
isnt it funny...
watu wale wale ambao wangekasirika kama jk angeruhusu klile
bakwata wanachotaka,leo wanamuita jk kigeugeu kwa kukataa?
 
Kikwete ni kigeugeu lkn pia waislamu wenyewe ndio vinyonga haswaa hata ningekuwa mimi ningeitumia mbinu hiyo hiyo aliyoitumia kikwete kuwahadaa waislamu coz hatuna msimamo. Waislamu tulisahau vitu vingi sana wakati wa uchaguz na kuweka dini yetu mbele huku tukisahau kuwa tunayemchagua hatok kwenye chama cha uislamu japo ni muislamu mwenzetu. Tulisahau mabomu ya mwembechai, Tulisahau umaskini wa maisha waliokuwa nao waislamu wenzetu ambao kwa kiwango kikubwa umesababishwa na CCM. Tuliwatukana sana CDM mpaka kukiita chama cha mapadri kumbe tulikuwa tunakimbilia jiwe na kuitupa dhahabu. Ona sasa wengine kama MS wanaanza kuomba mwongozo kutoka Slaa tuliemkashifu kwa kumuita Padri. SHAME ON US
 
wote tunakumbuka kuwa kipindi cha kampeni JK na ccm waliiwaahidi waislamu mahakama ya kadhi..sasa hivi hata kabla mwaka haujaisha kawageuka ..sasa hii tuiite ni kitu gani? .ina maana hata zile ahadi zlizozitoa kipindi cha uchaguzi hatazitekeleza
huyu mwanasiasa si ni kigeu geu?
Wanasiasa wote kigeugeu,wajinga ni wanaoamini maneno yao.
Kuna mbunge Kenya alichaguliwa baada yakutoa ahadi lukuki,baada ya miaka mitano ukaja uchaguzi mwingine akaulizwa ahadi ulizotoa mara ile hujatimiza hivi kweli unataka tukuchague tena ? akawajibu ndugu zangu mliponichagua mara ya kwanza nilikuwa sina hela na sikufahamiana na watu serikalini lakini sasa hivi mambo yangu safi na najua watu wengi.
Sasa badala ya kumchagua mtu mwenye njaa atakaye jiendeleza yeye kwanza nichagueni niliyoshiba niwasaidie,na kweli wakamchagua na akateuliwa naibu waziri.
Siasa ni mchezo mchafu na wakuwatumia watu,ukishatumiwa unatupwa mbali mpaka utakapohitajika tena.
 
CCM Wametukana wakunga uzazi ungalipo. Subirini kitakachotokea ndani ya miezi hii mitatu ! Watarudi kuwapigia magoti waislam[wapigania uhuru wa tz waliosahaulika]. Wasidhani waislam ni wajinga kiasi hicho. Nanyie wanafiki waislam wakianza harakati zao msilalamike.
 
Waislam walikuwa wakipigania uhuru wa tz au uhuru wa waislam?
 
Back
Top Bottom