JK aliulizwa maswali haya na wazee wa Serengeti,na majibu yake kuhusu BILILA

Humjui Mosena Nyambabe wewe, utakuwa umesimuliwa. Muulize hata James Mbatia wa NCCR Mageuzi waliyekuwa naye UDSM na kufukuzwa chuo miaka ile ya early 90s wakati wa vuguvugu la mageuzi nchini.
Baada ya hapo utafute japo speech zake akiwa kwenye majukwaa utaipata vizuri habari yake.

mosena ni strong political figure sema alikuwa akigombea kipindi kukiwa na mwamko mdogo wa wananchi pia kulikuwa hakuna support kubwa kutoka kwa vyama alivyokuwa akigombea yaan nccr na cuf kwani walikuwa na support ndogo katika kuweka mawakala kiasi kwamba alikuwa anapigana peke yake
 
Sana,hata mimi alitaka kunipa elfu 80,nikakataa kwa sababu zifuatazo, kwanza sihongeki mimi,maana najua nani anafaa.Pili hata kama ningekuwa nahongeka, I could not be cheap as such. Nikamkatalia,mtu mmoja anaitwa Shaweshi,ni mtendaji kata ya Mbalibali akaniambia niondoke maeneo yale kwakuwa jamaa ni mtu wa visasi anaweza kuni-ulimboka.
Kuna Mkoa wakipewa hongo wanapokea na kura wanapiga inavyotakiwa au wanvyoona inafaa.
Mama mmoja alipata shinikizo la damu baada ya kupigwa chini
 
Naomba nikusahihishe kidogo, mkoa wa Mara ndo mkoa unaoongoza kwa kuwa na makabila mengi sana kuliko mkoa wowote wa Tanzania, mkoa una makabila yafuatayo ambayo ninayakumbuka, kuna Wakurya, Wangoreme, Waikizu, Wanatta, Waisenye, Waikoma, Wajita, Wajaluo. Mbali na hilo kusema ukweli mpaka sasa mimi sijui kitu gani kiliwaroga mpaka wakampa ubunge Dr Kebwe yaani huyu jamaaaa anyway ya Mungu ni mengi sana na riziki hupangwa na Mungu sie wanadamu tutapambana we but at the end of the day Mungu ndo mtoaji wa yote
Hivi Nyerere alikuwa kabila gani kati ya hizi ulizotaja?
 
Hivi Nyerere alikuwa kabila gani kati ya hizi ulizotaja?

nyerere ni mkurya, ndani ya wakurya utakuta wazanaki, wasimbiti, wangoreme, waisenye, wanata, waikoma. wakabwa list ni ndefu.

ndani ya wajita utakuta wajita safi, wakwaya wazee wa gongo, wakerewe na waruri,

wajaruo wao hawana vipande vipande ni kabila moja tu.

wajita na wajaluo wote asili yao ni uganda na sudan kusini
 
Sifa mama za kuteuliwa uDC nchi hii ni hizi:
-Watoto wa vigogo na makada wa CCM kama akina Mongella, Mirumbe, Nchimbi,...
-Wabeba mikoba wa vigogo wa CCM kama akina Konisaga, Mashimba,....
-Waandishi wa habari wanaojua kuwapamba wakubwa kama akina Muhingo, Beti Mkwasa, Halima KIhemba, Selemani Mzee,...
-Rejects za Ubunge akina Ibra Marwa, Kolimba, Danh Makanga,....
-Vyakula vya wazee....
U-DC hauna ukabila.

Nawale ambao wanatoka sehemu au Mkoa mmoja na wazee wa kaya .....kama akina Ludovik Mwananzila ..
 
Mkuu WildCard hapa mdau SAGANKA anazungumzia hoteli ya Bilila na wangoreme kushindwa kuchomoza kwenye nafasi za uongozi wa nchi hii.

Ni kweli kabisa Dr. Deogratias Maro Mwita alikuwa na tuhuma nyingi za "kuwowa" vibinti vya sekondari, na niseme wazi sio tuhuma ni habari za ukweli tangu akiwa mbunge wetu kuanzia mwaka 1990-2000. Lakini hiyo haiwezi kujustfy mungoreme mwingine kutoteuliwa kuwa DC au RC.

Na kimsingi mimi nisingependa kujikita kwanini wangoreme hawajapata uteuzi huo isipokuwa tupanue wigo kwamba ni kwanini uteuzi wa maDC na maDC wengi wanakuwa wa makabila fulani na kutoka mikoa fulani zaidi? usiniambie kwamba wao tu ndio wenye uwezo!!

Mikoa gani? itaje
 
Mwaka 2009 JK alifika Mugumu Serengeti,ilikuwa ufunguzi wa Hotel ya Bilila.Kituko cha kwanza kufanya ilikuwa kumfukuza mkuu wa mkoa ambae alihudhuria hafla hiyo as if ilikuwa dhifa ya kitaifa.Akatolewa balu,kwamba akaendelee na majukumu ya kitaifa.

Wangoreme ni kabila dogo mkoani Mara,ila ni kati ya makabila giant wilayani serengeti ukiacha wakurya.Waliposikia kuwa jk anakuja Mugumu wakateua wazee wanane wakaonane nae ili wamweleze matatizo ya mwangoreme.Baada ya kumweleza wakawa na maswali yafuatayo:

1.Katika uteuzi wako wa wakuu wa mikoa na wilaya na nafasi nyingine kitaifa,wangoreme umeamua kututupa(kwa maana ya kwamba hakuna mongoreme hata mmoja aliyeteuliwa),je ni kwasababu hatufai?

2.Tulikuwa na mtu mmoja kutoka Ngoreme aliyekuwa mkuu wa wilaya(ni Dr. Deogratius Mwita-alikuwa mkuu wa wilaya ya Kilombelo enzi za Mkapa),ndiye peke yake katika kabila letu aliyekuwa na wadhifa wa juu.Ulipoingia madarakani badala ya kumpandisha,ukamvua ukuu wa wilaya bila kutupatia mwingine,ni kwanini?

2.Tulikusikia ukikemea habari ya kuchanganya biashara na siasa,je Hotel ya Bilila sio biashara?

Majibu yake kufuatia mpagilo wa maswali ni kama ifuatavyo:

1.Hakuna kabila lisilofaa,isipokuwa nafasi ni chache.

2.Mnishukuru saana kwa kumwondoa mtu yule katika nafasi ya ukuu wa wilaya,ningemuacha wananchi wangemmaliza.Nilipokea malalamiko mengi sana ya kwamba anatembea na wanafunzi wa Sekondari,hivyo kumwondoa ilikuwa ni heshima kwake,kwa serikali na hata kwenu ninyi Wangoreme.

3.Nadhani mngenishukuru kwa kuwekeza Tanzania na hasa Serengeti,kwani vijana wetu watapata ajira.Hii ni bora sana kuliko wale wanaokwenda kuwekeza nje,maana wanajenga uchumi wa mataifa mengine.

Kwakua hoja yangu ilihusu Bilila,je hayo ni majibu sahihi ya swali aliloulizwa?
Na je anaekataa kuwa BILILA si ya JK anaona hayo majibu? na unasemaje?

Lakini, kuna ukweli kwamba mikoa mingine ndo ina ma DC au RC wengi?
 
nyerere ni mkurya, ndani ya wakurya utakuta wazanaki, wasimbiti, wangoreme, waisenye, wanata, waikoma. wakabwa list ni ndefu.

ndani ya wajita utakuta wajita safi, wakwaya wazee wa gongo, wakerewe na waruri,

wajaruo wao hawana vipande vipande ni kabila moja tu.

wajita na wajaluo wote asili yao ni uganda na sudan kusini

dahh,wewe ninoma
 
Serengeti kwa sasa ina makatibu wakuu wa wizara wawili, Maswe wa Nishati na Madini na Selestine Gesimba wa Elimu( bado anakaimu lakini atapewa). Tena Gesimba ni Mongoreme kabisaaa! Hii kufikiria kugawana vyeo kwa viukoo vya mkoa wa Mara ni ujinga! Nchi kubwa sana hii na vikabila hivi ni vingi mno.
 
Hivi Nyerere alikuwa kabila gani kati ya hizi ulizotaja?

Rejea kwenye mchango wangu nimesema kuwa "mkoa una makabila yafuatayo ambayo ninayakumbuka. Sasa kwa kuwa umelikumbuka la Wazanaki wewe ongezea humo humo maana mimi sikulikumbuka na mbali na hayo yapo mengi tu nimeyasahau mfano Wanyichoka, Waancholi,Wachira so in short Mara ndo mkoa unaoongoza kwa kuwa na makabila mengi sana kwa hapa Tanzania
 
nyerere ni mkurya, ndani ya wakurya utakuta wazanaki, wasimbiti, wangoreme, waisenye, wanata, waikoma. wakabwa list ni ndefu.

ndani ya wajita utakuta wajita safi, wakwaya wazee wa gongo, wakerewe na waruri,

wajaruo wao hawana vipande vipande ni kabila moja tu.

wajita na wajaluo wote asili yao ni uganda na sudan kusini
Mkuu SoNotorious
Nadhani hujayatendea haki haya makabila, ingawa sipendi sana mijadala inayohusu ukabila lakini nimeona nichangie hapa manake hujaitendea haki histioria ya makabila haya.
Kusema WaIkoma Wangoreme Wanata na hata Wazanaki kuwa ni Wakurya huu ni upotoshaji wa hali ya juu sana. Wazanaki au WajaNaki kama wanavyojulikana ni kundi lililoingia Mara kwa njia ya Ziwa victoria kutokea Rwanda na hawana mahusiano na Wakurya. WaIkoma, WaIsenye na Wangoreme hili ni kundo toka kusimi mwa mkoa wa Mara liliongia Mugumu kama miaka 400 iliyopita kundi hili hufanya matambiko yao Bangwesi at the same time hufanya matambiko Mbulu (Mboolo) kama wenyewe wanavyopaita ni katika mazingira haya Machaba huaminika kuwa hawawezivuka gurument kwenda kaskazini ingawa anaweza safirishwa Arusha kwa urahisi bila shida. Ukifanya utafiti wa kina utagundua kuwa makabila haya hutofautiana ibada na mila inagawa rafudhi ya maneno hukaribiana sana. Anyway niishie hapa. Suala la Ubunge wa Serengeti ni la awamu pamoja na ubovu wa Mwita alivumiliwa amalize miaka yake 10 Wanyancha baada ya miaka yake kumi alitakiwa atoke aje mwingine yeye akawa king'ang'anizi wakati hata uwezo wa kujieleza kwa uma ulikuwa mdogo sana

Mpende Tz.yaani hadi sasa hujui Nyerere alikuwa kabila gani?Alikuwa mdengereko yule. Uongo?
Mkuu unaweza usiamini, mimi huwa sitilii maanani sana maswala ya makabila. Ndiyo maana hata sikuwa najua huko mara kuna makabila mengi namna ile. Ndiyo napata somo la jioni hapa JF. Loh!
Wazanaki nao??
 
Mkuu SoNotorious
Nadhani hujayatendea haki haya makabila, ingawa sipendi sana mijadala inayohusu ukabila lakini nimeona nichangie hapa manake hujaitendea haki histioria ya makabila haya.
Kusema WaIkoma Wangoreme Wanata na hata Wazanaki kuwa ni Wakurya huu ni upotoshaji wa hali ya juu sana. Wazanaki au WajaNaki kama wanavyojulikana ni kundi lililoingia Mara kwa njia ya Ziwa victoria kutokea Rwanda na hawana mahusiano na Wakurya. WaIkoma, WaIsenye na Wangoreme hili ni kundo toka kusimi mwa mkoa wa Mara liliongia Mugumu kama miaka 400 iliyopita kundi hili hufanya matambiko yao Bangwesi at the same time hufanya matambiko Mbulu (Mboolo) kama wenyewe wanavyopaita ni katika mazingira haya Machaba huaminika kuwa hawawezivuka gurument kwenda kaskazini ingawa anaweza safirishwa Arusha kwa urahisi bila shida. Ukifanya utafiti wa kina utagundua kuwa makabila haya hutofautiana ibada na mila inagawa rafudhi ya maneno hukaribiana sana. Anyway niishie hapa. Suala la Ubunge wa Serengeti ni la awamu pamoja na ubovu wa Mwita alivumiliwa amalize miaka yake 10 Wanyancha baada ya miaka yake kumi alitakiwa atoke aje mwingine yeye akawa king'ang'anizi wakati hata uwezo wa kujieleza kwa uma ulikuwa mdogo sana

sioni ulipothibitisha kuwa si wakurya zaidi ya kulalama, kuwa na lafudhi zinazokaribiana na maneno yanayofanana ni dhahiri kuwa haya makabila mengine ni simple extrapolation of one tribe which is kurya.
 
Back
Top Bottom