JK aliulizwa maswali haya na wazee wa Serengeti,na majibu yake kuhusu BILILA

SAGANKA

JF-Expert Member
Jun 9, 2012
313
202
Mwaka 2009 JK alifika Mugumu Serengeti,ilikuwa ufunguzi wa Hotel ya Bilila.Kituko cha kwanza kufanya ilikuwa kumfukuza mkuu wa mkoa ambae alihudhuria hafla hiyo as if ilikuwa dhifa ya kitaifa.Akatolewa balu,kwamba akaendelee na majukumu ya kitaifa.

Wangoreme ni kabila dogo mkoani Mara,ila ni kati ya makabila giant wilayani serengeti ukiacha wakurya.Waliposikia kuwa jk anakuja Mugumu wakateua wazee wanane wakaonane nae ili wamweleze matatizo ya mwangoreme.Baada ya kumweleza wakawa na maswali yafuatayo:

1.Katika uteuzi wako wa wakuu wa mikoa na wilaya na nafasi nyingine kitaifa,wangoreme umeamua kututupa(kwa maana ya kwamba hakuna mongoreme hata mmoja aliyeteuliwa),je ni kwasababu hatufai?

2.Tulikuwa na mtu mmoja kutoka Ngoreme aliyekuwa mkuu wa wilaya(ni Dr. Deogratius Mwita-alikuwa mkuu wa wilaya ya Kilombelo enzi za Mkapa),ndiye peke yake katika kabila letu aliyekuwa na wadhifa wa juu.Ulipoingia madarakani badala ya kumpandisha,ukamvua ukuu wa wilaya bila kutupatia mwingine,ni kwanini?

2.Tulikusikia ukikemea habari ya kuchanganya biashara na siasa,je Hotel ya Bilila sio biashara?

Majibu yake kufuatia mpagilo wa maswali ni kama ifuatavyo:

1.Hakuna kabila lisilofaa,isipokuwa nafasi ni chache.

2.Mnishukuru saana kwa kumwondoa mtu yule katika nafasi ya ukuu wa wilaya,ningemuacha wananchi wangemmaliza.Nilipokea malalamiko mengi sana ya kwamba anatembea na wanafunzi wa Sekondari,hivyo kumwondoa ilikuwa ni heshima kwake,kwa serikali na hata kwenu ninyi Wangoreme.

3.Nadhani mngenishukuru kwa kuwekeza Tanzania na hasa Serengeti,kwani vijana wetu watapata ajira.Hii ni bora sana kuliko wale wanaokwenda kuwekeza nje,maana wanajenga uchumi wa mataifa mengine.

Kwakua hoja yangu ilihusu Bilila,je hayo ni majibu sahihi ya swali aliloulizwa?
Na je anaekataa kuwa BILILA si ya JK anaona hayo majibu? na unasemaje?
 
Nakumbuka wakati huo pia alimpa aliyekuwa mbunge wa Serengeti unaibu waziri. Bwawa la maji Mugumu likakamilika. Kukaja na wazo la kujenga uwanja mkubwa na mzuri wa ndege. Barabara ya lami kupitia Butiama, Nyamuswa, ilianza kujengwa. Wangoreme kwa ukabila wenu mkamwangusha Mbunge yule kwenye kura za maoni mwaka 2010 kwa kuwa ni Mkurya! Mkapitisha huyu Dr Kebhwe, kwa kuwa ni wa kwenu!
 
Wangoreme ni 35% ya population ya Serengeti,huku wakurya wakiwa 46% na waisenye,waikoma,wanata na wangine wakiunda 19%,je una maana hiyo asilimia 35 ndo ilimwangusha Wanyancha?
 
Mkuu WildCard hapa mdau SAGANKA anazungumzia hoteli ya Bilila na wangoreme kushindwa kuchomoza kwenye nafasi za uongozi wa nchi hii.

Ni kweli kabisa Dr. Deogratias Maro Mwita alikuwa na tuhuma nyingi za "kuwowa" vibinti vya sekondari, na niseme wazi sio tuhuma ni habari za ukweli tangu akiwa mbunge wetu kuanzia mwaka 1990-2000. Lakini hiyo haiwezi kujustfy mungoreme mwingine kutoteuliwa kuwa DC au RC.

Na kimsingi mimi nisingependa kujikita kwanini wangoreme hawajapata uteuzi huo isipokuwa tupanue wigo kwamba ni kwanini uteuzi wa maDC na maDC wengi wanakuwa wa makabila fulani na kutoka mikoa fulani zaidi? usiniambie kwamba wao tu ndio wenye uwezo!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mwita Maranya hapo juu waeza dokeza ni makabila/mikoa gani ambayo huzawadiwa sana hivi vyeo visivyo na tija kwa maendeleo ya taifa? (DCs na RCs)
 
Nimekaa Mugumu kidogo. Ukiondoa Wakurya, "makabila" mengine haya pale wilayani ni wamoja sana wakiongozwa na Wangoreme. Wana haki ya kuwa hivo kwa sababu za kihistoria tu. Tukianza kugawa hivi vyeo vya KISIASA kwa kuangalia vikabila vingi hivi tulivyonavyo hatutaishia hapo. Mambo haya ni sawasawa na kula nyama ya mtu.
 
Mkuu Mwita Maranya naomba ni-admit kwamba to me,you are a special guy,unawahi kuelewa.Wazee wa kengoreme hapo ndo uwezo wao ulifikia,ni wajibu wetu kulijadili jambo hili kwa mapana,hasa katika topic ya "Distribution of National cake" Wazee hao walitoa mwanga wa kuangalia swala hili.Thanks man.Hat hivyo draft ya katiba tayari,cjui tutaonanaje ili tuweze kuijadli kabla ya registration.
 
Mkuu Mwita Maranya hapo juu waeza dokeza ni makabila/mikoa gani ambayo huzawadiwa sana hivi vyeo visivyo na tija kwa maendeleo ya taifa? (DCs na RCs)
Sifa mama za kuteuliwa uDC nchi hii ni hizi:
-Watoto wa vigogo na makada wa CCM kama akina Mongella, Mirumbe, Nchimbi,...
-Wabeba mikoba wa vigogo wa CCM kama akina Konisaga, Mashimba,....
-Waandishi wa habari wanaojua kuwapamba wakubwa kama akina Muhingo, Beti Mkwasa, Halima KIhemba, Selemani Mzee,...
-Rejects za Ubunge akina Ibra Marwa, Kolimba, Danh Makanga,....
-Vyakula vya wazee....
U-DC hauna ukabila.
 
Nimekaa Mugumu kidogo. Ukiondoa Wakurya, "makabila" mengine haya pale wilayani ni wamoja sana wakiongozwa na Wangoreme. Wana haki ya kuwa hivo kwa sababu za kihistoria tu. Tukianza kugawa hivi vyeo vya KISIASA kwa kuangalia vikabila vingi hivi tulivyonavyo hatutaishia hapo. Mambo haya ni sawasawa na kula nyama ya mtu.
Kwani Kebwe alikuwa hafai?na je umoja wa wangoreme ulikuwa wapi wakati Wanyancha alipogombea na kuwa mbunge?,au mongoreme hakugombea wakati huo?
 
Mungeendelea na Dr Wanyancha saa hii jimbo la Serengeti lingekuwa na waziri kamili. JK alishamkubali huyu jamaa. Sasa huyu Kebhwee....Ah, sijui. Wangoreme punguzeni ukabila, fitna na visasi. Mkoa ule una makabila matatu tu, Wakurya, Wajita na Wajaluo. Dr Wanyancha alipita wakati ule kwa sababu ya kupambana Mongoreme dhaifu sana wakati ule.
 
wewe mosena nyambabe sio mtu dhaifu
 
Mungeendelea na Dr Wanyancha saa hii jimbo la Serengeti lingekuwa na waziri kamili. JK alishamkubali huyu jamaa. Sasa huyu Kebhwee....Ah, sijui. Wangoreme punguzeni ukabila, fitna na visasi. Mkoa ule una makabila matatu tu, Wakurya, Wajita na Wajaluo. Dr Wanyancha alipita wakati ule kwa sababu ya kupambana Mongoreme dhaifu sana wakati ule.
Inaonekana huwafahamu vizuri watu wa Serengeti.Dr Mwita aliteuliwa kuwa Naibu waziri wa TAMISEMI,alikuwa mongoreme,lakini Ngoreme ni moja ya maeneo aliyopata kula chache uchaguzi uliofuata.Na ilikuwa miaka 3 tu baada ya kuteuliwa kuwa naibu waziri.Wangoreme wakaamua kumpa Dr.Wanyancha hadi pale alipowaita kakabila kadogo ndipo wangoreme wakaamua kuachana na mtu wa madharau huyu.Unasema alipambana na mtu dhaifu wakati Mwita alikuwa naibu waziri.Kwa taarifa yako sasa watu wa Serengeti hawatabiliki.Watakupiga chini na uwaziri wako.Na ni haki yao,haiwezekani wakuchague eti kwasababu tu wewe ni waziri,never on earth.
 
angekutana na hoja za mtu kama Mzee MATOGORO JK asingetamani kurudi serengeti, yule mzee ni noma kwa hoja sema wajinga hawamkubali
Umekonga moyo wangu,nampenda mzee huyu.Nashangaa sana kwa yeye kuniita professor kila akiniona.Lakini pia nashangaa kwanini ameng'ang'ania kwa wazee wa Hakiiiii!
 
Back
Top Bottom