JK alitambua Udhaifu Wake na Kumtimua Kazi ya Uspika Samwel Sita,La Sivyo Hasingemaliza Awamu ya II | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK alitambua Udhaifu Wake na Kumtimua Kazi ya Uspika Samwel Sita,La Sivyo Hasingemaliza Awamu ya II

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kanga, Jul 11, 2012.

 1. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Katika kutafakari utendaji na ufanisi wa uongozi wa Rais JK katika kipindi cha kwanza na pia kuelekea kpindi cha awamu ya pili ni wazi kuwa kasi ya utendaji wa Rais JK ilikuwa ya kiwango cha chini sana kisicho na mwelekeo wowote ule wenye matumaini huku akiendelea kuelea na kukumbatia uswahiba.Mhimili wa bunge ulikouwa chini ya uongozi wa spika Sita ulijibainisha wazi kuwa ni wa viwango na speed safi ambayo dhaihiri serikali chini ya kiongozi wake rais JK alishindwa kutembea sambamba na kasi ya viwango vya bunge.Ni katika wakati huo uswahiba wa JK na Lowasa uliingia nyongo na serikali kuvunjwa na kuunda upya baraza la mawaziri, huku tuhuma na maazimio mbalimbali ya bunge yakiwa mengi hayajatekelezwa.
  Katika awamu ya pili JK ambaye awali inaonekana ni dhaifu hakuweza kwenda sambamba na kasi ya bunge huku akijua kuwa kuna unafiki kati yake na viongozi wenzake alioota mapema kumuondoa Sita kwenye Uspika wa Bunge na kumfanya waziri wa kawaida ili kulinda nafasi yake ya Urais ambayo hakika ilikuwa rehani kama SITA angeendelea kuwa SPIKA WA BUNGE.Madudu ya taarifa ya mdhibiti na Mkaguzi wa Serikali iliyopita hakika KIKWETE ASINGEBAKI SALAMA pia udhaifu katika kushughulikia ISSUE YA JAIRO KATIBU MKUU AMBAYE TAARIFA NYINGI ZINADAI ANALINDWA NA IKULU NA KWAMBA ALIKUWA NDIYE AKIANDALIWA KURITHI MIKOBA YA LUHANJO KAMA KATIBU MKUU KIONGOZI MPAKA LEO LIMEBAKI SIRIKALI PAMOJA NA BUNGE KUTOA MAAZIMIO YAKE.
  Na kama Kikwete angeendelea kuendesha na kuongoza nchi hii kama chama cha wanaukoo na SITA akiwa bado SPIKA WA BUNGE ,naamini Bunge lingekuwa tayari limekwisha mrudisha kwake Msoga akaendelee na ujenzi na makazi yake ya kudumu baada ya kuacha uongozi wa nchi maana Bunge tayari lilikuwa limejijengea taswira kama taasisi yenye maamuzi na chombo cha kusimamia serikali na wananchi tayari walikuwa wameliona na kukubali utendaji wa bunge enzi ya SITA tofauti sasa chini ya mama Kiroboto ambye bunge limekosa mwelekeo kabisa.ASANTE SITA HISTORIA UMEANDIKA NCHINI KAMA KIONGOZI WA BUNGE, LAKINI VIONGOZI DHAIFU WAKABADILI VIGEZO YA KUTAKA SPIKA MWANAMKE AMBAVYO WWALIJUA UTASHINDWA KUKIDHI KUWA MWANAMKE GHAFLA.
   
 2. Wile GAMBA

  Wile GAMBA JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 1,809
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  NI bora b. kirobot akaisoma, huyu mama anasikitisha sana
   
 3. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,992
  Likes Received: 1,046
  Trophy Points: 280
  Duu, inamaana ingetangazwa wiki kadhaa kabla Mh Six, angekidhi vigezo?

   
Loading...