JK alimtengenezea njia JPM utumbuaji majipu

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,983
11,403
Kazi ya kutumbua majipu kwa JPM isingekuwa rahisi kama asingechongewa njia, JK alivyoingia madarakani alianza na mzee Edo kazi ambayo haikuwa rahisi. JK ndio alianza kupeleka report ya CAG bungeni na kuwaacha akina zitto lisu na kafulila kuwakomalia mawaziri.

JK aliwatimua mawaziri 68 kwa muda mfupi wa utawala wake hivyo hakuna kigogo aliyejiona hawezi guswa na waliogangamala kama akina mama koku na mzee wa vijisenti walitimuliwa mbali na hakuna chochote kilichotokea na maisha kusonga kama kawaida.

Kazi nyingine kubwa ilikuwa ukataji wa majina NEC, majina yenye nguvu na yaliyotishia uhai wa chama yalikatwa bila kupepesa macho, pamoja na akina nchimbi kimbisa na mama michepuko kutishia nyau JK hakuonyesha kutetereka.

Kwa kazi kubwa ya JK imemrahisishia JPM kutumbua majipu kiurahisi vinginevyo vigogo wangemtikisa kama sio nje ya chama basi ndani ya chama.
 
Ngoja waje maana kuna watu wakilisikia hilo jina la JK wanaingiwa na wazimu
 
Suala la majipu lilianza tangu awamu ya pili. Baada ya baba wa taifa kututoka wale wezi,majambazi ya kuhujumu uchumi yakajionyesha ikiwa ni awamu ya tatu tumeshudia tani za dhahabu zikisafirishwa na mchanga wake kama vile wanavuna mashamba yao.

Ile hali ikaondoa imani baina ya viongozi na wananchi pia. Roho ya Ubinafsi ikaingia mioyoni mwa watanzania hususani viongozi ambao kilamtu alikuwa anangalia atoke vp.

Baada ya kuingia awamu ya nne hali ikawa mbaya zaidi ambapo tayari hawa mafisadi walikuwa wamejenga mizizi na kupata nguvu kubwa ndani na nje ya serikali.

Awamu hii mimi ninaona serikali inahangaika tu kwasababu ni tatizo la mfumo.

Ndio maana hata shughuli nyingi za kiuchumi haziendi kwasababu hawa mafisadi waliishilia nchi wakikamua sawa sawa.

Ni madhara makubwa yalisababishwa na kukosa Uzalendo hivyo nchi ikakosa uwezo wake wenyewe wa ndani kusimama kama nchi.

Hakuna cha Jk wala Magu hapa hasa hasa wanafanya hv kwa hofu ya upinzani ili uchaguzi ujao wasife.
 
KJ YUPI WA MSOGA AU BUTIAMA,KAMA WA MSOGA BASI WE NI KILAZA ULIYETUKUKA,YULE ANASTAHILI KUWA SEGEREA SIO MSOGA,KAMA WA BUTIHAMA SAWA
 
Wacheni sifa za kibwege hizo huyo mtu wenu ndiyo alifanya watu wakichukie chama mpaka JPM alikuwa anapata ukakasi kutamka neno ccm wakati wa kampeni, mshukuruni Februaly na timu yake vingenevyo hata zile pushups zilidunda, wacheni hizo. JPM ni namba nyingine kabisa huyo anajitegemea na anajiamini siyo huyo mtu wenu wa kukenua kenua.
 
Back
Top Bottom