JK alimtaka Lema agombee ubunge kupitia CCM Lema akagoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK alimtaka Lema agombee ubunge kupitia CCM Lema akagoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kurunzi, Apr 11, 2012.

 1. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Nimesoma makala ya Paschally Mayega ameandika makala nzuri sana na zaidi ya yote anamnukuu Lema akisema Jk na makada wengine wa ccm walimuita katika kikao cha faragha kumtaka agombee ubunge kupitia ccm kwenye uchaguzi wa 2010.

  Ikiwa ndivyo hukumu hii inabaraka zote za ikulu na hata CDM ikikata rufaa kunauwalakini kumbuka kesi ya mgombea binafsi chini ya Jaji mkuu AR. sembuse Jaji Othuman Shost wake na JK yetu macho.

  Zamani tulisoma hivi, “Paulo una mikono michafu usije kucheza na sisi” Rais
  wangu hukumu ya Mahakama Kuu chini ya Jaji Gabriel Rwakibarila dhidi ya Godbless Lema wengine wanaweza kusema ndiyo mfano wa vijana wa Jaji Mkuu mstaafu aliotuachia.

  Inawezekana vipi mtu asomee uhakimu mpaka awe jaji asijue kuwa kesi za kashfa huwa
  hazirithiwi? Endapo anayedaiwa kukashfiwa akifariki basi na kesi hiyo huishia hapo. Wakili mmoja amesema, “Kama Lema alitamka
  maneno hayo na kudhihirika kweli kuwa yalikuwa ni ya kashfa basi shauri la kukashfiwa
  lingefunguliwa na Dk. Batilda Burian mwenyewe aliyekashfiwa na si mtu mwingine.” Ameongeza
  kuwa, “Hukumu ndiyo inayotamka adhabu.

  Huwezikuhukumiwa halafu uende kwenye vifungu vya sheria kuanza kuangalia nimetiwa hatiani adhabu yangu inakuwaje. Mahakama ndiyo yenye jukumu hilo la kutamka vifungu vya adhabu na si kutamka kutengua matokeo ya
  uchaguzi na kuacha kutamka vifungu vya kanuni ya adhabu”.
  Hukumu hii kwa hakika ndiyo inayozidisha wasiwasi wa Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani kubaki katika Tume ya Katiba. Rais wangu tunaheshimu utawala wa sheria
  kama tunavyoziheshimu mahakama zetu. Ni hukumu hii iliyopelekea Mwenyekiti wa
  CHADEMA kitaifa, Freeman Mbowe, aseme kuwa serikali na vyombo vingine vyenye mamlaka ni lazima wajue kuwa, enzi za kuwaburuza watu zimepitwa na wakati.
  Alisema, “Sitaki kuingilia uamuzi wa mahakama, lakini ni ukweli kuwa hukumu hii ilivuja hata kabla ya kusomwa, tulipewa taarifa za ubunge wa Lema kutenguliwa, sasa hili ni
  jambo la hatari kama tutaendelea kuvujisha uamuzi wa kisheria nchi inaweza kuingia
  kwenye machafuko pale watawala wanapoingilia vyombo vya kisheria”. Hukumu kuvuja ni
  kashfa, tena ni aibu! Jaji Gabriel Rwakibarila aliisoma hukumu yake akitumia lugha ileile waliyokuwa wanatumia wakoloni, Kiingereza utadhani alikuwa hataki wananchi wengi waelewe alichokuwa anasema.

  Alionekana kama mtu aliyekuwa anashindana na kitu ndani ya nafsi yake kilichokuwa kinataka
  kumtoka kupinga kile alichokuwa anakisema, hivyo kila baada ya maneno kadhaa alikunywa maji yakutosha kana kwamba alikuwa anakishindilia kirudi ndani.

  Yawezekana ni kweli kutumia lugha ya kigeni ilisaidia kupunguza maafa. Kama walioelewa kidogo tu walihuzunika mpaka wakazimia,
  angesema Kiswahili wakaelewa zaidi si wangekufa kabisa! Na waliokuwa wanalia tu bila
  kujua jaji anasema nini, wangejua nao wangezimia. Akiipokea hukumu yake, Godbless alisema, “Safari ya ukombozi ilianza zamani, wengine walikufa, wengine walipoteza viungo vyao lakini
  safari iliendelea. Msiogope nyinyi mlio wengi maana mkiogopa mimi nitaogopa zaidi, lakini nawatia moyo msiogope kuweni jasiri haki haiwezi kudhalilishwa.” Mwanamume huyu akaendelea, “Kabla ya uchaguzi rais aliniita
  kwenye kikao ambacho pia kilihudhuriwa na makada kadhaa wa CCM Arusha na kunitaka nikubali kugombea ubunge kupitia CCM lakini
  nilikataa kutokana na msimamo wangu katika ukombozi wa taifa hili.” Godbless Lema
  ameanguka lakini atabaki akionekana mbunge katika vifua vya Wana wa Arusha na katika
  mioyo ya wanyonge na maskini wa nchi hii ambao wametapakaa katika nchi. Godbless nenda kaimarishe chama chako kwakuwa wewe sasa ni mbegu iliyo bora, iliyorutubishwa ambayo kwayo utastawi mti
  utakaozaa matunda ambayo ni uhuru wa kweli! Waliokuwa wanalia na kuomboleza kwao
  ulikuwa kama nuru yao ndogo ya mshumaa iliyokuwa inawaka katika giza lao nene!
  Uliwajaza wanyonge wa nchi hii matumaini kwa harakati zako na kwa hilo wewe utabaki kuwa tumaini kwa wote waliodhihakiwa. Umepigana
  vita iliyo njema, nenda ukasubiri tuzo yako pamoja na wateule wake wengine!
  Wanachadema na wote wenye mapenzi mema
  kwa maskini wa nchi hii, huu si wakati wa kulia
  pamoja na Godbless Lema! Angalieni Lema
  ameangukia wapi. Inameni chini muokote silaha yake, tangulieni mbele kwenye mapambano.
  Mapambano ya Godbless si ya bunduki, ni yakuwafungua waliofungwa kifikra.

  Mapambano yake ni ya kuwapa wananchi elimu ya uraia.
  Mapambano ya kuwafanya wananchi kuelewa haki zao. Kuelewa wajibu wao kwa nchi yao na kwa viongozi wao waliowachagua.

  Mapambano hayo lazima yaendelee! Silaha yake ni ujasiri katika kuisimamia kweli na
  ujasiri katika kuitetea haki.
  Nawe Godbless usiwe na moyo uliopondeka. Kama Mwenyezi Mungu alikuandikia ubunge
  kwa ajili ya maskini wa nchi hii, basi uwakilishi wako utakurudia kwa maana imeandikwa,
  “Kama kweli haikushinda leo, basi itashinda kesho!”. Wafanya hila wajue kuwa wakifanyacho ni sawa na kulazimisha watu waokote maembe chini ya mnazi.
   
 2. A

  Afghan Member

  #2
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Imekaa vizuri mkuu. Hawa watawala wetu wanalazimisha wanachokitaka kiwe hata kama ni kinyume na haki. Lakini usihofu, Mungu yupo anayaona haya na atatenda yaliyo mapenzi yake.
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mengi yatasemwa sijui tuamini lipi jambo la msingi ni kukata rufaa haya mengine ni bla bla tu.
   
 4. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Chadema kwa uwongo hawajambo sasa Lema, ulikuwa wapi kusema haya maneno baada ya kushindwa kesi Arusha ndio umekuja na hiyo single huko ni kutapatapa.
   
 5. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Umeandika vizuri sana, sasa ni vizuri kwenda ndani zaidi, mfano kwanini walikuwa wanamtaka lema, si wana Lamwai pale lumumba?
   
 6. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2012
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wewe mwenyewe ni bla bla. Kama hayo mengine ni bla bla kwanini unachangia?
   
 7. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hivi kwa nini watanzania tusitumie kipimo cha kuitetea ccm kuwa ni mwanzo wa kuharibika kwa ubongo?

  mimi nashauri kuwa ukiona ndugu yako anaitetea ccm kwa wakati huu andaa mipango ya kuwasiliana na dokta wa kichwa pale mirembe.

  namba yake tutairusha hapa sasa hivi.
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Wamtake Lema ana nini kuna watu wana upeo mkubwa ndani ya Chadema mtu kama Zitto Kabwe, John Mnyika hawa wanakubali kila sehemu ya Tanzania ukisema wanatakiwa na JK watu wanaweza kukuelewa.
   
 9. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #9
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  JK aache watu wenye akili timamu akamuombe Lema? Lol
   
 10. B

  Bujigile JF-Expert Member

  #10
  Apr 11, 2012
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 247
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Inawezekana kweli walimtaka Lema agombee kupitia CCM maana tangu atamke hayo maneno si Nnauye wala msemaji wa Ikulu (JK kuhusishwa) kakanusha maneno hayo maana hao huwa wepesi sana kukanusha hata kama ni kweli.
   
 11. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #11
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hivi kwani JK naye ana upeo?!!
   
 12. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #12
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kwani yeye JK ana upeo gani?!! Labda upeo wa kufungua zipu.
   
 13. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #13
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  CCM ni chama cha wachumia tumbo. Mzalendo gani anakitaka?. Hongera Lema.
   
 14. s

  sangija Senior Member

  #14
  Apr 11, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ww mwenyewe mwongo,na cdhan kama zinakutosha! kama hujui nyamaza! watu kama nyie bas tu!!!!
   
 15. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #15
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ni ngumu sana kwa Lionel messi(GODBLESS JONATHAN LEMA) kuchezea simba/yanga(ccm)hakuna politician smart kama Lema hapa Tz,na bado hamjauona moto wake wakati huu na atakaporudi mjengoni
   
 16. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #16
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  NI vema kukata rufaa, lakini ni vema zaidi kujiandaa na mapambano maana hali ya kuoneana haiwezi kuisha bila kusimamia ukweli na haki.
   
 17. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #17
  Apr 11, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kunya anye kuku akinya bata kaharisha......muongo #1 ni magamba na makada wake
   
 18. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #18
  Apr 11, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  weka takwimu kwa hilo unalolisema.
   
 19. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #19
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ukitaka kujua maneno haya yamepikwa ili kuwapotosha wananchi, angali yanavyojirudia rudia kwa sababu bila kufanya hivyo yanakosa mvuto.
  Hukumu ilikuwa ni kati ya Mdai, mdaiwa na pengine mashahidi, kama mdaiwa alikuwa haelewi lugha angeomba isomwe kwa lugha anayojua. Lakini pia naomba nitofautiane kabisa na wewe kuwa LEMA ni Slaha ya ukombozi, mimi binafsi ukiniambia nikuambie mtu namaba moja ambaye hakustahili kuingia bungeni ni LEMA kutokana na historia yake ya alikotoka, na hapa naomba niwe serious kidogo kwa sababu sitemei kumuita mheshimiwa mtu kama Lema, hana sifa hizo, ni kudhalilisha taifa la Tanzania. Kubwa zaidi kwa taarifa yako ni kwamba hata huku CHADEMA viongozi sasa watapata kupumua japo wamebaki watu wawili ambao wakitoka hakika Chama kitakuwa kistaarabu ile Mbaya.
  PUMZIKA salama STEVEN CHARLES KANUMBA.
   
 20. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #20
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,799
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  kichwa chako kimejaa vumbi hakuna unalolijua wewe zaidi ya kuropoka hivi vi elfu 10 mnavorushiwa vinawapofusha macho!!
   
Loading...