JK Alikua akifurahia hoja za kuwawajibisha Mawaziri bungeni alipokua marekani..Ni kweli???

KML

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
861
133
Jamani ata nyie mnaamini kwamba JK alikua akifurahia swahiba zake mawaziri wakipondwa na kutakiwa wawajibishwe kipindi cha bunge eti wakati yeye yupo marekani, ivi ata Bunge alikua akilifatilia kweli..???​
 
Ni mnafiki mbona ikulu ilidai hana taarifa sasa hapo anamdanganya nani
 
Bonge la msanii! Kama anadai madudu haya mara ya kwanza aliyaona mwaka 2007, na haikumuuma kwa miaka yote mitano! Leo atatueleza nini tumwelewe? Mjusi ni mjusi tu hata ukimpaka rangi.
 
Jamani ata nyie mnaamini kwamba JK alikua akifurahia swahiba zake mawaziri wakipondwa na kutakiwa wawajibishwe kipindi cha bunge eti wakati yeye yupo marekani, ivi ata Bunge alikua akilifatilia kweli..???​

ata nyie = hata nyie
ivi ata = hivi hata
Japo maneno hayo yote yametumika kimakosa kwenye hizo sentensi, kwa kifupi sio kiswahili sanifu.

Mkuu nafikiri maneno hayo niliyoandika ndiyo yangefaa yatumike kwenye sentensi.

Kuhusu kauli ya Mh. Rais nafikiri ilikuwa ya kisiasa zaidi, sidhani kama anafurahishwa na haya mambo!
 
JK ni mjanja, anajua jamii inataka kusikia nini au ina mtazamo gani, hivyo akinena kinyume hataeleweka, all in all ndivyo mchezo wa siasa ulivyo. Ndiyo maana mara nyingi huchuna kimyaaaaa, anasikilizia kwanza jamii inasemaje kwa ujumla, ndipo anaibuka kusema neno, hapingi japo pia anaweza asifanyie kazi.
 
ata nyie = hata nyie
ivi ata = hivi hata
Japo maneno hayo yote yametumika kimakosa kwenye hizo sentensi, kwa kifupi sio kiswahili sanifu.

Mkuu nafikiri maneno hayo niliyoandika ndiyo yangefaa yatumike kwenye sentensi.

Kuhusu kauli ya Mh. Rais nafikiri ilikuwa ya kisiasa zaidi, sidhani kama anafurahishwa na haya mambo!
Aksante Mwalim
 
Back
Top Bottom