Jk alakiwa olasiti arusha na swaga za m4c

Status
Not open for further replies.
Ni aibu ya kutoweza kuelewa baina ya mambo ya kitaifa na mambo ya kichama
Jaribu kuangalia ziara za rais au makamu wake, utaona zile rangi za satini, njano na kijani, kwenye ziara za serikali, kwahyo ni kawaida kiongozi.
 
Hata pale mnapoenda kufungua barabara ambazo ni kodi za wananchi huwa mnavaa nguo zenu za kijani na njano ila watu huwa hatusemi.

Kama hamsemi kuwakanya CCM ilhali mnajua kwamba si jambo sahihi haina maana kuwa hugeuka kuwa sahihi CHADEMA ikilifanya
 
Nkwingwa sijakuelewa hapo.

Ina maana unachosema ni sawa kwa CCM kuvaa magwanda yao kwenye shughuli za kitaifa kwa sababu wao ndiyo wanaunda serikali na si sawa kwa wafuasi wa CHADEMA kupeperusha vijibendera vyao na kuvaa magwanda yao mbele ya rais?

Pia unaona ni sawa kwa CCM kuendesha vikao vyake Ikulu?
Bebe ngosha,
Hapana nilikuwa najibu hii ya statement ya Josephine inayosema CHADEMA ni chama tawala Arusha na bandiko lake ni hili hapa,
Gaijin,
aibu ipi,kwani chama Tawala Arusha ni kipi.
Mbona huwa usemi aibu pale sare za CCM zinapovaliwa kwenye sherehe za kitaifa.

Hilo la CHADEMA kuvaa mavazi yao nimelijibu hapa,
Hakuna cha ajabu kwa wanaCHADEMA kuvaa nguo au kubeba bendera za CHADEMA kwenye mkutano wa Rais. Hii ni haki yao ya msingi kabisa katika katiba.

Ningependa tena kama wapenzi/wanachama wa vyama vyote vya siasa wawe wanakutana katika mikutano kama hiyo na kukaa pamoja na mibendera yao ili kuondoa ujinga uliojengeka katika vichwa vya wajinga wachache kuwa kutofautiana kiitikadi ni uadui.

Kosa na kukosa ustaarabu ni pale wanapoanza kuzomea badala ya kusikiliza.
 
Gaijin,
aibu ipi,kwani chama Tawala Arusha ni kipi.
Mbona huwa usemi aibu pale sare za CCM zinapovaliwa kwenye sherehe za kitaifa.

Chadema is taking advantage of this incident for political gains. now that elections for 3 wards are underway, it is perfect time for cdm to get those vital christian votes! good move eh? I wont be surprised if we come to find they are involved in this issue. It has not been reported yet that ccm members wait for Mbowe to shout "ccm daima" lets wait and see...
 
Hakuna cha ajabu kwa wanaCHADEMA kuvaa nguo au kubeba bendera za CHADEMA kwenye mkutano wa Rais. Hii ni haki yao ya msingi kabisa katika katiba.

Ningependa tena kama wapenzi/wanachama wa vyama vyote vya siasa wawe wanakutana katika mikutano kama hiyo na kukaa pamoja na mibendera yao ili kuondoa ujinga uliojengeka katika vichwa vya wajinga wachache kuwa kutofautiana kiitikadi ni uadui.

Kosa na kukosa ustaarabu ni pale wanapoanza kuzomea badala ya kusikiliza.

Ahaaa! Hapo sasa umenena kama mtoka Ng'wamapalala.
 
Kama hamsemi kuwakanya CCM ilhali mnajua kwamba si jambo sahihi haina maana kuwa hugeuka kuwa sahihi CHADEMA ikilifanya
Ushamba unasumbua tu, mbona haya mambo JK kaishayazoea!.

Kule Kimara alipokelewa na bendera za CDM, CCM na CUF wala hapakuwepo na shida.

Ispokuwa MaCCM walipotaka kumtoa madiwani wa CDM jukwaani ndiyo ikaonekana wanataka kuifanya shughuli ya chama (CCM) badala ya serikali.
 
Mama,

Sikutegemea kama upeo wako wa uelewa wa mambo ya siasa ya Tanzania uko kidogo kwa kiasi hiki!!

Hata kama una chuki za kiasi gani, hapo kwenye nyekundu umejidhalilisha; mimi binafsi nimekufuta kwenye orodha yangu ya watu niliokuwa nadhani wana hoja. HOJA ZA CHUKI KWANGU NO. Nakushauri grow up stairs by choosing the right word to address the one you hate.
 
Ni aibu ya kutoweza kuelewa baina ya mambo ya kitaifa na mambo ya kichama

Mambo ya Kitaifa????
Unataka tushiriki kwenye Dhambi iliyoasisiwa na CCM.
Yaaan Dwa ya CCM ni kutokuwapa Pumzi kabisa
 
hivi hili tukio linahusiana na siasa?

Ndio, limeasisiwa na CCM ambacho ni Chama cha Siasa.
Mnaasisi Mambo, yakienda Kombo mnataka kuja na Ngonjera za "Jambo la Kitaifa"
Elimu ya Lema imesaidia wengi sana Kuzidi kufunguka
 
Kama hamsemi kuwakanya CCM ilhali mnajua kwamba si jambo sahihi haina maana kuwa hugeuka kuwa sahihi CHADEMA ikilifanya
Tumejiaminisha kuwa sisi ni watanzania na wanachadema na tunaishi eneo lilipotokea tukia na ndio maisha yetu ya kila siku,nilikupa mfano tu ili uone kuwa ulichokisema nawe huwa unakifanya hivyo usipige kelele.Ukiishi nyumba ya vioo usianzishe ugomvi wa mawe
 
Hakuna cha ajabu kwa wanaCHADEMA kuvaa nguo au kubeba bendera za CHADEMA kwenye mkutano wa Rais. Hii ni haki yao ya msingi kabisa katika katiba.

Ningependa tena kama wapenzi/wanachama wa vyama vyote vya siasa wawe wanakutana katika mikutano kama hiyo na kukaa pamoja na mibendera yao ili kuondoa ujinga uliojengeka katika vichwa vya wajinga wachache kuwa kutofautiana kiitikadi ni uadui.

Kosa na kukosa ustaarabu ni pale wanapoanza kuzomea badala ya kusikiliza.

Mkuu,
Inategemea nani anazomewa, RC wa Arusha anastahili hii Kadhia
 
Ushamba unasumbua tu, mbona haya mambo JK kaishayazoea!.

Kule Kimara alipokelewa na bendera za CDM, CCM na CUF wala hapakuwepo na shida.

Ispokuwa MaCCM walipotaka kumtoa madiwani wa CDM jukwaani ndiyo ikaonekana wanataka kuifanya shughuli ya chama (CCM) badala ya serikali.

Jambo kuzoelewa na Kikwete haimaanishi kuwa ndio "umjini"

Kikwete kazowea kwenda kwa waganga na wapiga ramli, ndio kusema ni jambo bora?

Itakirihisha iwapo Kikwete ataenda kukutana na wahanga wa mafuriko Jangwani, yeye na msafara wake wakiwa kwenye sare za CCM
 
Hata kama una chuki za kiasi gani, hapo kwenye nyekundu umejidhalilisha; mimi binafsi nimekufuta kwenye orodha yangu ya watu niliokuwa nadhani wana hoja. HOJA ZA CHUKI KWANGU NO. Nakushauri grow up stairs by choosing the right word to address the one you hate.
Mkuu, nitamchukiaje mtu ambaye hata simfahamu zaidi ya kusoma komenti zake . kwa komenti zake za nyuma sikutegemea kama atakuwa anafikiria kitu kama hiki kisiasa katika Tanzania.

Mkuu, Samahani kama nimekukwaza kwa hilo na ninashukuru kwa kunikanya kama njia moja ya kueleweshana na kujenga.

Next time, nitachagua jinsi ya kutumia maneno lakini pia ukiniona sehemu nimeenda nje ya mstari, ninakuomba tena unikanye.

We're just human.
 
Tumejiaminisha kuwa sisi ni watanzania na wanachadema na tunaishi eneo lilipotokea tukia na ndio maisha yetu ya kila siku,nilikupa mfano tu ili uone kuwa ulichokisema nawe huwa unakifanya hivyo usipige kelele.Ukiishi nyumba ya vioo usianzishe ugomvi wa mawe

Mie siwezi kuwa nakifanya kwa sababu si mwanachama wa chama chochote kile.

Sijawahi kujinasabisha na chama na wala nia na madhumuni hayo hayapo

CCM ikifanya uovu na ikanyamaziwa, haimaanishi kwamba uovu huo huwa wema ukifanywa na upinzani.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom