JK akitaka kujisafisha na Dowans atafute ujasiri na afanye hivi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK akitaka kujisafisha na Dowans atafute ujasiri na afanye hivi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Feb 7, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  WanaJF:

  Baada ya kutafakari hotuba ya JK aliyotoa akiwa katika magwanda ya kijani hasa katika sehemu ile aliyojaribu kujisafisha kutokana na sakata la kampuni ya Dowans – ni dhahiri ameshindwa kukidhi kiu ya Watanzani wengi kuhusu kuhusika/kutokuhusika kwake katika sakata hilo.

  Ameshindwa kukidhi kiu kwa sababu yeye tu ndiye alikuwa anazungumza – hakuna mtu wa kumuuliza -- maana kulikuwapo maeneo mengi alifunika funika tu au kupindisha ambapo kama kungekuwa na watu makini wa kumuuliza kutoa ufafanuzi, basi angenasa mtegoni bila ya wasiwasi wowote.

  Mimi naona ili kukata mzizi wa fitina kabisa kabisa atafute angalau ka-ujasiri kidogo aitishe mkutano na waandishi wa habari ili alielezee sakata hilo na aruhusu kuulizwa maswali. Asichuje waandishi watakaohudhuria – kila chombo cha habari (TV, Radio na magazeti makubwa) yatume wanahabari wawili.

  Akiweza kujieleza vizuri hapo ndipo tutajua kuwa hahusiki na sakata hilo (na si lazima awe hana hisa katika Dowans kama anavyong'ang'ania).

   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Akifanya hivyo hawezi kuwapumbaza Watz -- labda katika mkutano huo asiwemo Kubenea na wale wahariri wa Mwananchi na Raia Mwema.
   
 3. olele

  olele JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 814
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 80
  amesema yeye hawajui wamiliki wa dowans (rais huyo, au mwenye nchi hajui wageni wake) lakini waziri wake ngeleja anawafahamu ndo maana alisema ni lazima walipwe (isingewezekana kumlipa mtu usiyemjua) kwa hiyo rais anashindwa na waziri wake sasa yupi anafaa kuwa rais??
   
 4. l

  limited JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kwa hiyo labda yesu aje kwa mara ya pili, na si dhani kama kuna kiongozi wa kiafrika anadhubutu
   
 5. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Jk hata kama mkimfanyaje, nchi hii kashindwa. kila siku anaambiwa tu la kusema na anasema hilo hilo. hamshangai rais hajui wamiliki wa Dowans wakati serikali yake ndiyo inayodaiwa? ukifika wakati wa kulipwa anamlipa yeyote atakayejitokeza au atamlipa mmiliki yule mhusika? Mbona maelezo yake hata mtoto wa darasa tano atayatilia mashaka. Jk ni rais au mwenyekiti wa mtaa? anajua kusoma na kuandika?
   
 6. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Utakuwa uamuzi mgumu sana! Ni sawa na kuamua kuogea acid ambayo unajua itaunguza ngozi tu!
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Usimuamshe aliyelala mkuu.

  Wacha CCM imfie mikononi mwake.

  We are not fools anymore.
   
 8. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mmmmmmmmh mmh! koo limekaba
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,784
  Trophy Points: 280
  JK achochea moto  *Wasomi, wanasiasa wasema naye amegeuka kuwa mlalamikaji
  *Wadai angeeleza serikali itakavyokabili genge la wahuni

  Tumaini Makene na Grace Michael
  Majira

  HOTUBA ya Rais Jakaya Kikwete ya kuadhimisha miaka 34 tangu kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi imechochea moto na
  mijadala nchini, huku kauli kuwa hakuna uharaka wa kuilipa Kampuni ya Dowans sh. bilioni 94 ikiibua maswali zaidi kuliko majibu.

  Wasomi na wasiasa waliozungumza na Majira jana walisema Rais Kikwete ameungana na wananchi wa kawaida na kuwa mlalamikaji, badala ya kutoa mwongozo wa nini cha kufanya kuondokana na suala hilo na kueleza jinsi ya kulikabili 'genge la wahuni wanaotafubna rasilimali za nchi na kuteka mamlaka ya taifa'.

  Miongoni mwa waliozungumaia hotuba hiyo, ni Mhadhiri Msaidizi Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala, Chuo Kikuu Dar es Salaam, Bw. Bashiru Ally alisema kuwa hotuba ya rais ilipaswa kujikita katika kuzungumzia masuala yanayolikabili taifa kwa upana wake, kwani Dowans ni dalili tu ya tatizo kubwa nchini.

  Alisema mathalani badala ya kuzungumzia Dowans, kwani kama alivyokiri mwenyewe tayari ilishazungumziwa na wasaidizi wake, rais alipaswa kuliambia taifa kupitia sherehe hizo za CCM, kuwa serikali yake itakabiliana vipi na genge la watu wachache walioteka mamlaka za nchi.

  Alisema kuwa hotuba ya juzi ya kutimiza miaka 34 ya CCM ilipaswa kujikita katika kuangalia malengo makuu ya chama hicho kikongwe, masuala ya itikadi, sera na mwelekeo wa taifa, badala ya kuangalia maslahi ya muda mfupi kama vile kushinda uchaguzi, kila baada ya miaka mitano.

  "Kwangu mimi issue si kulipa au kuilipa Dowans, Dowans ni dalili ya ugonjwa mzito unaolikabili taifa...ugonjwa wa kutowajibika, kikundi cha watu wachache kujilimbikizia mali, mfumo wa sheria kutofanya kazi, tatizo la kuuza na kununua kura, watu wanachukua posho zinazozidi mishahara yao.

  "Hivyo hotuba ya jana (juzi) ilijikita zaidi katika kuangalia ushindi wa hali ya uchaguzi, msukosuko ambao CCM inapata kutoka kwa wapinzani kwenye uwanja wa CCM, kuwatia moyo wana-CCM na suala la kufanya mageuzi ndani ya chama...hivyo kulikuwa na imbalance (hakukuwa na uwiano sawa) na mambo mengine ya mtazamo mpana juu ya mweleko wa taifa.

  "Hata ukisema chama kinafanya mageuzi, unajiuliza mageuzi kutoka wapi, CCM imepita katika vipindi mbalimbali, malengo makuu ya CCM zamani haikuwa kushinda uchaguzi, ilikuwa ni kujenga taifa huru, lenye usawa na heshima kwa watu, uzalendo, maadili. Taifa ambalo lilikuwa linazungumzia juu majirani na Bara la Afrika zima kwa ujumla.

  "Kuna changamoto ya kuangalia masuala ya itikadi, sera na mwelekeo wa taifa, chama si mashine ya kutafutia kura, ni uongozi, na uongozi ni dira...masuala ya kushinda uchaguzi ni malengo ya muda mfupi sana, hakuna dira ya miaka mitano, la sivyo CCM nacho kitakuwa kimetumbukia katika mtazamo finyu," alisema Bw. Ally.

  "Kwa kweli badala ya kuzungumzia Dowans tu kwa sababu Pinda na Chiligati walishasema kama alivyosema, basi rais alipaswa kuzungumzia bigger picture (mtazamo mpana) si smaller picture, juu ya matatizo yetu, angetuhakikishia namna gani serikali yake imejipanga katika mapambano dhidi ya ufisadi.

  "Itapambanaje na genge la wahuni wanaotumia fursa zao za kiuchumi kuteka mamlaka ya nchi...ufisadi unaoangamiza sekta karibu zote, energy (nishati), ardhi, huduma za jamii, mfumo wa utawala, ufujaji wa rasrimali za umma," alisema Bw. Ally kwa kirefu.

  Aliongeza kuwa hotuba hiyo ingeweza kueleza mwelekeo wa taifa katika wakati huu ambapo makatibu wakuu au wakurugenzi wa idara, wanajitwalia fedha na marupurupu mengi, huku wakitembelea magari ya kifahari, wakati wanafunzi vyuoni na shuleni hawana uhakika wa chakula.

  Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA), Bw. John Mnyika alisema kuwa Rais Kikwete hawezi kuepuka mzigo wa tuhuma dhidi ya Dowans. Pia anapaswa kuwaeleza Watanzania jinsi serikali ilivyoweza kuingia mkataba na kampuni feki, ambayo hatimaye iliuhamishia kwa mtu mwingine.

  "Rais hapaswi kulalamika kama anavyolalamika mwananchi wa kawaida...Katika hotuba ya jana, Rais Kikwete kakiri mwenyewe kuwa Richmond ilikuwa kampuni feki, yeye mwenyewe anasema kuwa alikuwa ameishtukia, sasa ilikuwaje kampuni hiyo ikaendelea kufanya kazi na hata ikaweza kuhamisha mkataba wake kwenda Dowans.

  "Ilikuwaje serikali yenye vyombo vyenye mamlaka...vyombo vya dola vilivyokuwa na taarifa kuwa Richmond ni kampuni feki, ziliruhusu kampuni hiyo iingie mkataba na serikali, kisha vyombo hivyo vikaruhusu kampuni hiyo feki ikahamisha mkataba kwenda kampuni nyingine...atuambie iwapo uhamishaji wa mkataba huo ulipitia katika baraza la mawaziri, ambalo yeye ni mwenyekiti wake.

  "Lakini pia Rais Kikwete anapaswa kutuambia ni lini hasa mkataba ulihamishwa kwenda Dowans, tarehe ngapi na mwezi gani...na upande wa pili wa serikali (TANESCO) walipewa taarifa na kuridhia lini. Maana katika mkataba wa Richmond na TANESCO ilikubaliwa kuwa mkataba huo hauwezi kuhamishwa kwenda kampuni nyingine bila makubaliano ya pande hizo mbili.

  "Lakini kulingana na taarifa zilizopo kutoka vyanzo mbalimbali zinaonesha kuwa Richmond na Dowans walifikia makubaliano ya kuhamisha mkataba kabla hata upande wa pili wa serikali (TANESCO) haujaridhia suala hilo...sasa rais atuambie ni lini mkataba ulihamishiwa Dowans na lini TANESCO waliridhia kuhamishwa kwa mkataba huo.

  "Kwa sababu kuhamisha mkataba wa Richmond na TANESCO kwenda kwa mtu mwingine bila pande hizo mbili kukubaliana kama ilivyokubaliwa katika mkataba, kisheria ni batili...sasa ilikuwaje mamlaka zikaruhusu kuhamisha mkataba ambao tayari ulisema lazima kuwe na makubaliano ya pande mbili.

  Naye Mbunge wa Kigoma Kusini, Bw. David Kafurila amesema kuwa maelezo hayo yameongeza utata, hatua inayolazimu suala hilo kurejeshwa bungeni kujadiliwa upya.

  Akizungumza na Majira jana kwa njia ya simu, Bw. Kafurila alisema kuwa hotuba ya rais aliyoitoa akiwa mjini Dodoma katika sherehe za maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) imezidi kuongeza utata katika sakata la malipo yanayodaiwa na Dowans.

  "Maelezo ya Rais yamezidi kutuonesha kuwa kuna umuhimu sasa wa suala hilo kujadiliwa bungeni...hawezi akatuambia eti hawajui kabisa wamiliki wa Dowans huku akitaka wanasheria waangalie uwezekano wa kupunguza deni hilo au kulikwepa kabisa, wanapunguziana deni na nani huyo ambaye hajulikani? alihoji Bw. Kafurila.

  Alizidi kuhoji kuwa inakuwaje Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) asimjulishe rais wamiliki wa kampuni hiyo baada ya kupitia hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC) iliyoitaka TANESCO kulipa fedha hizo, mpaka ifikie hatua Rais anasimama mbele ya maelfu ya Watanzania na kusema kuwa hawajui wamiliki hao.

  "Mwanasheria Mkuu baada ya kupitia hukumu alishauri walipwe, na siku chache baadaye Waziri wa Nishati na Madini Bw. Willium Ngeleja alitaja wamiliki wa kampuni hiyo, hivyo tutaaminije kama hao waliotajwa ndio wamiliki halali na wakati Rais anasema hawajui?" alihoji.

  Bw. Kafurila alisema kuwa haiwezekani rais aeleze kutowafahamu wamiliki wa Dowans na wakati serikali ilikuwa ikiwalipa fedha wakati wakizalisha umeme hapa nchini.

  "Rais ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri na tangu Dowans ianze kuzalisha umeme hadi leo ni lazima suala hilo liwe limepitia kwenye Baraza la Mawaziri hivyo hakuona kweli umuhimu wa kuwafahamu wamiliki hao?" alisema.

  Kutokana na utata huo, Bw. Kafurila alisema kuwa malipo hayo yalipwe au yasilipwe lakini serikali haiwezi kukwepa kuwajibika katika suala hilo kwa kuwa Watanzania wamengia gharama kubwa ya kujadili jambo hilo huku serikali ikiwa kimya lakini pia kutumia gharama kuwalipa mawakili na kuendesha kesi hiyo.

  Alizidi kuihoji Serikali kuwa imeshindwaje katika kesi hiyo na kampuni ambayo hata wamiliki wake hawajulikani lakini mbali na kutojulikana kampuni hiyo ni feki na yenye mkataba batili.

  "Serikali katika hili haiwezi ikajitoa kwenye kitanzi hiki ni lazima iwajibike kwa namna yoyote kwani suala hili limechukua muda wetu mwingi katika kulijadili badala ya kushughulikia mambo mengine," alisema Bw. Kafurila.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,784
  Trophy Points: 280
  Ni bora tu tukubali kwamba nchi yetu sasa hivi haina Rais. Kuna mtu tu yuko pale ambaye hajui atendalo kwenye chochote kile. Hataki kabisa kuwajibika kama kiongozi. Siku zote yuko radhi kukaa kimya kabisa pale ambapo Watanzania walio wengi wangependa kusikia kutoka kwake kuhusu matatizo mbali mbali yanayoikabili nchi yetu ikiwemo malipo makubwa yanayotaka kufanywa kwa Dowans ya $69m na RITES $87m na pia hali ya maisha kwa ujumla ikiwemo mgao wa umeme ambao unaendelea kwa mwezi wa pili sasa na haijulikani ni lini adha hii itamalizika rasmi, ugumu wa jhai ya maisha uliongezeka zaidi kwa kupanda gharama za vitu mbali mbali ikiwemo vyakula, petroli n.k.

  Pia anaonyesha usanii mwingine katika hili la kuunda jopo la kuunda kukusanya maoni toka kwa Tanzania ili hatimaye iandikwe katiba mpya. Sioni kwanini hadi hii leo hajatangaza rasmi hilo jopo ili lianze rasmi kazi ya kukusanya maoni toka kwa Watanzania na kuyafanyia kazi ili tupate katiba mpya ambayo inaendanna na wakati na pia kumpunguzia Rais madaraka makubwa aliyokuwa nayo, maoni yangu ni kwamba anafanya hivi ili kuchelewesha makusudi zoezi hili na hatimaye uchaguzi wa 2015 ufanyike kwa katiba ambayo imeshapitwa na wakati pia inayokipendelea sana chama kilichopo madarakani.

  Miye nashangaa sana kwa mtu ambaye ana mapenzi ya kweli na nchi yake na wananchi wenziye wamemkabidhi wadhifa mkubwa sana wa kuiongoza nchi yao kwanini mtu kama huyu asijiuzulu wadhifa wake pale anapogundua kwamba wadhifa aliokabidhiwa na wananchi wenzie umemshinda? Nasema kagundua maana hii hotuba yake ya hivi karibuni ambayo alidai kwamba hata Baba wa Taifa alishindwa inaonyesha dhahiri kwamba amekubali kushindwa kama kiongozi wa nchi pamoja na kuwa ndiyo kwanza amekianza kipindi chake cha pili cha miaka mingine mitano. Sasa kwa nini aendelee kuwepo madarakani kwa kipindi chote hicho hadi 2015 wakati hana uwezo wa kuiongoza nchi?


  NB:

  Msisahau wale RITES ambao waliingia nchini bila hata senti tano na wakapewa 51% za TRC bila kutoa hata senti moja. Kisha inasemekana wakajipatia mkopo wa $400 million kwa kutumia Assets za TRC ambao haujulikani ulitumika vipi. Hawa RITES walikuwa wakiingiza nchini mabehea mitumba kutoka India ambayo labda gharama yake ilikuwa ndogo sana na kisha kuonyesa kwamba wameyanunua kwa bei kubwa sana. Kiasi cha shilingi bilioni 10 kilipotea katika bank accounts za TRC wakati ikiongozwa na watu wa RITES, Serikali ilipotaka wakaguzi huru wafuatilie upotevu wa pesa hizo kwa kuviangalia vitabu vya TRC wahindi hao wa RITES walikataa kata kata, si ajabu pesa zilizopotea zilikuwa ni nyingi zaidi kuliko hizo shilingi bilioni 10. Pamoja na kutowekeza hata senti moja kule TRL nao wanakaribia kuvuna mavuno makubwa kutoka shamba la bibi, Serikali imeshaamua kwamba wanastahili kulipwa $87 million. Huu ni WIZI mwingine wa mchana kweupe ambao Watanzania popote pale tulipo tunastahili kusimama kidete ili kuhakikisha hao RITES hawalipwi hata senti moja za walipa kodi wa Tanzania.


  Kikwete hafai kabisa kuendelea kuwa Rais ni bora tu ajiuzulu mapema ili tupate kiongozi ambaye atakuwa tayari kulinda maslahi ya Tanzania na Watanzania bila woga wowote au shinikizo toka kwa mafisadi.


  Alutta Continua.
   
 11. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Huyu Mkulu anashangaza kweli! bora hata angekaa kimya.ina maana hajui kwa nini PM wake alijiuzulu hadi baraza la mawaziri kuundwa upya? sasa pale magogoni anafanya nini? haingiii akilini hata chembe kusema hawafahamu Dowans wala wamiliki wake,ni hakika sasa amekosa muelekeo wa kuwaongoza watanzania.
  Kauli yake kama Raisi ni ipi? maana pale alizungumza kama mwananchi wa kawaida mwenye kilio lakini hana la kufanya,wakati tulitegemea aongee kama Rais mwenye mamlaka na pia nguvu ya kuamuru msukumo wa jambo fulani utendeke
  Namhurumia sana huyu mzee mwezangu..ukomo wake wa kufikiri na ushauri wa wapambe wake utamgharimu hakika huko mbeleni.
   
Loading...