JK akiri serikali haiaminiki - AFICHUA KISA CHA KUACHWA MA-DC

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

• AFICHUA KISA CHA KUACHWA MA-DC

na Mwandishi wetu

RAIS Jakaya Kikwete amekiri kuwa Watanzania wengi wamekosa imani na serikali yake kwa kile alichodai kuwa kimechangiwa na utendaji mbovu wa baadhi ya watumishi.

Kikwete ametamka hayo jana, alipokuwa akifunga semina ya mafunzo kwa wakuu wa mikoa na wilaya iliyokuwa ikifanyika mjini hapa, na kudai kuwa utendaji mbovu wa baadhi ya watendaji wa serikali yake, umewafikisha wananchi wengi kuichukia serikali ya Chama cha Mapinduzi.

Alisema taifa limekosa maendeleo kutokana na tabia ya baadhi ya watendaji, kujihusisha na rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma na uonevu, mambo ambayo yamewakatisha tamaa wananchi.

Aidha aliongeza kuwa tabia ya viongozi kuchelewesha maamuzi katika kutatua kero za watu, zimekuwa zikiwakasirisha wananchi na kutoboa kuwa ndizo zilizomfanya kuwaacha baadhi ya waliokuwa wakuu wa wilaya.

Ameongeza kuwa baadhi ya wakuu hao wa wilaya, walikiuka maadili ya utumishi ikiwa ni pamoja na ulevi uliokithiri.

Kutokana na hali hiyo, Kikwete aliwaagiza viongozi hao kufanya kazi zao kwa uangalifu, kutotumia ubabe na kuheshimu mipaka na mgawanyiko wa majukumu yao ya kila siku.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amewataka viongozi na watendaji wa serikali kujiuzulu na kuwaachia vijana wasomi nafasi hizo ili waweze kutumia elimu yao kujenga taifa.

Alisema kuwa ni wakati muafaka kwa wazee kuwapisha vijana, watumie nguvu na elimu yao, na wao wabaki pembeni wakiwa washauri katika mambo mbalimbali, badala ya kung’ang’ania madaraka hata katika umri huo mkubwa.

Semina hiyo ilikuwa na lengo la kutoa mafunzo kwa wakuu wa mikoa na wilaya, kabla ya kuanza rasmi kazi zao, kufuatia kuteuliwa kwao na Rais Kikwete hivi karibuni.

Alitishia kuwafukuza kazi ikiwa watajiingiza katika udalali wa kuwatafuitia watu vyeo na na kuwa mashujaa wa kuwapiga vita wabunge wanaopigana dhidi ya ubadhirifu na kuacha kujiingiza katika kampeni za kuwalinda wagombea urais na ubunge katika maeneo yao.

Alisema kuwa tatizo la ajira hapa nchini ni ndoto kwa sababu ya kukosekana kwa viwanda vya kutosha. Aliwapiga marufuku wakuu hao kujihusisha na ugawaji wa ardhi, bali wasimamie mazingira bora ya uwekezaji, kuwa na mahusiano bora na wananchi.

Hii ya Wazee kuwapisha Vijana Haraka Haraka italisababishia Serikali ya CCM matatizo makubwa haswa; Ukiangalia Utendaji ya wajumbe wa CC Vijana na ni Wasomi ni hatari kama Vile Mchemba na Nape ni kama Vile hawajaenda Shule hawana Mwamko hawana Hekima, Muda wao Wote ni Ugomvi yoyote aliye upinzani ni Adui wao.
 
huyu mtu huwa siku zote haelewi..hata hayo aliyoyasema hayana ukweli.. uteuzi wake daima umekuwa ukiegemea ushikaji, undugu, urafiki n.k hana jipya kwa hilo labda awadanganye hao hao ma DC wake sioux wananchi, coz tunamjua vilivyo..swala la ajira ni kushindwa kwa serikali yake kusimamia sera za ubinafsishaji na uwekezaji hivyo kuuwa viwanda, na kuruhusu wageni kwa wingi kuja kufanya kazi nchini hivyo kuwajinya wazawa fursa ya kuajiriwa
 
Hii hali ya kusema wazee wawapishe vijana sijui wenzangu mnalionaje maana binafsi nikaangalia kwa mfumo wa elimu ya Tanzania yaani wengi wanaanza kupata mwangaza wa kufanya na kuijua kazi @30's sasa unakuta ndo anakurupuka na ukute elimu ndo kadegree kamoja kama Le Mutuz aje akurupuke kutafuta ya pili na umri ushaenda uwezo wa familia na kujisomesha bila boom kwetu bado sana ukichanganya na ma-extended families ndo maana wanaiba badala ya kazi
 
Hii ya Wazee kuwapisha Vijana Haraka Haraka italisababishia Serikali ya CCM matatizo makubwa haswa; Ukiangalia Utendaji ya wajumbe wa CC Vijana na ni Wasomi ni hatari kama Vile Mchemba na Nape ni kama Vile hawajaenda Shule hawana Mwamko hawana Hekima, Muda wao Wote ni Ugomvi yoyote aliye upinzani ni Adui wao.

Nngu007,
Mzee Kawawa aliwahi kusema ukifanya jambo Adui yako akakusifia ujue umekosea, lakini ukifanya adui yako akalalamika ujue uko sahihi! Toka Nape awe katibu mwenezi amekuwa akitukanwa kila aina ya matusi, kisa amekuwa mwiba kwa upinzani nchini!! Mbona kabla ya hapo alionekana shujaa?!!!! Mkimsifu kwa kila sifa, sasa anatukanwa mpaka matusi ya nguoni.... Siasa hizi za hovyo, siasa za kuamini ili mradi hakuungi mkono ni mshenzi hana maana, akigeuka leo kukuunga mkono anakuwa shujaa ghafla.... Huu ni upuuzi.
 
JK, preach what you do. Juzi tu hapa umetoka kumwapisha Mwandosya, umri umekwenda,anaumwa, leo unawaambia wazee waachie ngazi! Kwani Mwandosya asingeweza kuwa mshauri bila uwaziri?
 
huyu mtu huwa siku zote haelewi..hata hayo aliyoyasema hayana ukweli.. uteuzi wake daima umekuwa ukiegemea ushikaji, undugu, urafiki n.k hana jipya kwa hilo labda awadanganye hao hao ma DC wake sioux wananchi, coz tunamjua vilivyo..swala la ajira ni kushindwa kwa serikali yake kusimamia sera za ubinafsishaji na uwekezaji hivyo kuuwa viwanda, na kuruhusu wageni kwa wingi kuja kufanya kazi nchini hivyo kuwajinya wazawa fursa ya kuajiriwa

Toa mfano , wapi ameonesha undugu katika uteuzi wa Wakuu wa Wilaya na Mikoa. Ni vema tukanyamaza kama hatuna uhakika na tunayoayasema badala ya kulifanya jukwaa hili kuwa la majungu. Tuchangie mada iliyopo badala ya kuingiza hisia binafsi ,jambo amabalo linawakatisha tamaa wengine wenye nia njema ya kuchangia.
 
JK, preach what you do. Juzi tu hapa umetoka kumwapisha Mwandosya, umri umekwenda,anaumwa, leo unawaambia wazee waachie ngazi! Kwani Mwandosya asingeweza kuwa mshauri bila uwaziri?
Sidhani kama Mwandosya ni mzee kiasi cha kuwekwa kwenye kundi la kuwapisha vijana. Kuhusu ugonjwa, huo utakuwa ni unyanyapaaji, haifurahishi hata kutamka kuwa aachwe kwa sababu ya ugonjwa wake.
 
Nngu007,
Mzee Kawawa aliwahi kusema ukifanya jambo Adui yako akakusifia ujue umekosea, lakini ukifanya adui yako akalalamika ujue uko sahihi! Toka Nape awe katibu mwenezi amekuwa akitukanwa kila aina ya matusi, kisa amekuwa mwiba kwa upinzani nchini!! Mbona kabla ya hapo alionekana shujaa?!!!! Mkimsifu kwa kila sifa, sasa anatukanwa mpaka matusi ya nguoni.... Siasa hizi za hovyo, siasa za kuamini ili mradi hakuungi mkono ni mshenzi hana maana, akigeuka leo kukuunga mkono anakuwa shujaa ghafla.... Huu ni upuuzi.

haya maneno ungwaambia mzee makamba na lowasa yangekuwa na maana sana kwa kuwa maadi wa ko ccm.chadema hakuna uadui na ccm,angalia mahali kuna vikao vya ccm na chadema hata maji watu wanakunywa nenda kwenye mikutano ya ccm wenyewe ndo utajua uadui uko wapi?maji yote wanachukua wafagiaji wa ukumbi.
 
Wananchi wamekosa imani na serikali ya CCM kwa sababu ya utendaji mbovu wa Rais ambaye ndiye mwenyekiti wa CCM. huko kwingine kote ni kujaribu kuwatupia wengine lawama zako mwenyewe
 
Rais kikwete yuko sawa. Lakini nani wa kuhakikisha mawazo yake mazuri yanatekelezwa, au naye amekuwa mshauri. Kama anashauri, ushauri wake ni kwa nani? Hata hivyo tumekuwa na vijana kama ngeleja, maige, malima, masha n.k. Je utendaji wao wa kazi ni wa kuingwa na vijana au taifa? wanaomwandalia Rais hotuba wawe makini sana kumwepusha kutoa kauli zinazomrudia na kusababisha watu kuanza kuuliza nani ashikwe shati kwa serikali kutoaminiwa na wananchi. Kama Rais anaonyesha taswira ya kulalamika sasa akina 'pangu pakavu' tufanyeje, na kimbilio letu ni wapi?
 
Toa mfano , wapi ameonesha undugu katika uteuzi wa Wakuu wa Wilaya na Mikoa. Ni vema tukanyamaza kama hatuna uhakika na tunayoayasema badala ya kulifanya jukwaa hili kuwa la majungu. Tuchangie mada iliyopo badala ya kuingiza hisia binafsi ,jambo amabalo linawakatisha tamaa wengine wenye nia njema ya kuchangia.

Je hana uhusianao na maDC aliowateua wakina KIRIGINI,MAYENGA na mbunge wake wa zamani wa Chalinze Maneno aliyempa UDC Kigoma? Mifano hii michache inatosha!! Usitake tusema mengi kwani nani asiyejua ukware wa huyu mkweree na jinsi anavyohonga vyeo kwa washikaji zake!!
 
Sidhani kama Mwandosya ni mzee kiasi cha kuwekwa kwenye kundi la kuwapisha vijana. Kuhusu ugonjwa, huo utakuwa ni unyanyapaaji, haifurahishi hata kutamka kuwa aachwe kwa sababu ya ugonjwa wake.

It is high time Kikwete started walking his talk; anasema wazee wawapishe vijana ili wao wawe washauri lakini wakati huo huo anawateua wazee useless kabisa kuwa wakuu wa wilaya ; mfano ni Luteni mstaafu Yamungu huyu licha ya uzee pia ni mlevi na kitu anacholingia ni kwamba Kikwete ni rafiki yake!! Akumbuke pia kuwa ujana sio mara zote kuwa ishara ya kuweza kuwa mtendaji kuliko watu wa umri mkubwa; mifano ya kina Maige na Masha tunayo ingali hai!!
 
Wakubwa kigezo ili kuwa kiongozi si ujana wala uzee! Kama huo ujana ni Kigezo.! Basi na yeye ni mzee aachie vijana Bali kwa ufahamu nilionao, mojawapo ya kigezo mtu kuwa kiongozi ni HEKIMA!
 
Alisema kuwa ni wakati muafaka kwa wazee kuwapisha vijana, watumie nguvu na elimu yao, na wao wabaki pembeni wakiwa washauri katika mambo mbalimbali, badala ya kung'ang'ania madaraka hata katika umri huo mkubwa.
JK Gangwe, amejaza wazee kibao katika serikali yake na bado anawataka wawapishe vijana. Manake kama ni komedy wala haichekeshi.
 
Kifupi mkuu wa kaya haelewi afanye nini kwani inaonekana mambo yamemzidi kimo.Huwezi kusema ajira ni ndoto halafu wewe ndie mkuu wa nchi,nadhani kasahau kuwa ahadi ya ajira kwa vijana ndiyo iliyompa umaarufu 2005,hii ni sawa na baba mzazi kuungana na watoto wake kulia wakti watoto wakimdai mahitaji yao muhimu.kama Mkuu anatamka hivi basi.....no comment nisije pigwa ban bure!
 
Chagua watu wenye uchungu na nchi yao sio wachumia tumboni watakusumbua sana... Hata kama ni mtoto wa mfadhili achana nao tena hao ndio wabaya sana... Ushauri wa bure...
 
Back
Top Bottom