JK akiri pesa za maendeleo zinategemea misaada, Posho na mambo machache kutoka makusanyo ya ndani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK akiri pesa za maendeleo zinategemea misaada, Posho na mambo machache kutoka makusanyo ya ndani

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Lyimo, Jun 20, 2011.

 1. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kutokana na Mh. Raisi kulalamika kuwa ukosefu wa fedha kutoka kwa wahisani ndiyo kunakamisha maendeleo Africa, hii inadhiirisha kuwa viongozi wetu wa Afrika sasa hawana mbinu ya kutegemea makusanyo ya ndani kwaajili ya kuendesha miradi ya maendeleo. Raisi Kikwete aliyasema hayo kwenye siku ya kwanza ya mkutano wa kimataifa wa taasisi ya Smart Partnership Dialoque.

  Sasa kwanini serikali isikubali kuondoa ama kupunguza posho zisizo za msingi ili kugharamia miradi ya maendeleo?
  Hivi kweli bilioni 987 kila mwaka ni ndogo kwa kuendesha shughuli za kimaendeleo? Eti zinatosha kwa kujitafutia umaarufu tu.
  Kwanini tunatoa misamaha ya kodi kwa wawekezaji wakubwa wakati hatujitosheleli kujiendesha?

  Nawaomba Viongozi wetu wa serikali na wabunge, waweke kipaumbele kwenye shughuli za maendeleo na swala la posho liwe kipaumbele cha mwisho kabisa ama liondolewe. Au hivyo vifungu vya sheria vinasisitiza posho za ajabuajabu ziwe kipaumbele namba moja?


  HABARI KAMILI YA MH. RAIS KUTOKA GAZETINI

  JK: Ukosefu wa fedha unakwamisha maendeleo
  RAIS Jakaya Kikwete amesema ukuaji wa kasi wa uchumi na maendeleo katika Bara la Afrika unakwamishwa na ukosefu wa fedha za kutosha za kugharimia miradi ya maendeleo.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu jana, Rais Kikwete alikuwa akizungumza kwenye siku ya kwanza ya mkutano wa Kimataifa wa mwaka huu wa Taasisi ya Smart Partnership Dialogue ambao pia unajulikana Langkawi International Dialogue 2011, ulioanzishwa rasmi mwaka 1995.

  Rais Kikwete alisema kwamba njia za jadi za kupata fedha za kutosha ili kuharakisha ukuaji kasi wa uchumi, hazina uwezo wa kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo.

  Rais Kikwete alisema kutokana hali hiyo ni lazima nchi za Afrika zitafute namna nyingine mpya ya kugharimia maendeleo ya bara hilo na watu wake.

  “Tatizo ni ukosefu wa fedha za kutosha kugharimia miradi inaweza kuzitoa nchi za Afrika na watu wake katika umasikini kwa haraka zaidi,” Rais Kikwete, mjini Kuala Lumpur, Malaysia.

  Shabaha kuu ya Smart Partnership ama Langkawi International Dialogue ni kufanya majadiliano ya kimataifa ya jinsi ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi duniani. Mada kuu katika mkutano wa mwaka huu ni ‘Enhancing Smart Partnership for Socio-Economic Transformation’.

  Akishiriki katika mjadala huo, Rais Kikwete aliwaambia mamia ya washiriki tatizo kubwa linalokwamisha ukuaji kasi wa uchumi na maendeleo katika Afrika ni ukosefu wa fedha za maendeleo kwenye sekta binafsi, sekta ya umma na kwa Serikali.

  Rais alisema chanzo kikuu cha fedha za maendeleo kwa nchi masikini za Afrika ni misaada ya maendeleo (ODA), lakini sasa fedha za ODA zimekuwa zikipungua na wakati mwingine hazipatikani.

  “Hata ukitofautiana na kampuni yenye asili ya nchi inayotoa misaada, basi utanyimwa misaada hata kama kampuni yenyewe ndiyo yenye makosa,” alisema Rais Kikwete.

  Rais alisema wakati mwingine inakuwa vigumu kuvutia fedha za maendeleo kutoka nje.

  “Hakuna fedha za kutosha kwenye masoko ya fedha ya ndani na msingi mzima wa kifedha ni dhaifu sana. Msingi wa fedha wa ndani ni dhaifu na hata msingi wa fedha za kigeni wa nchi zetu ni masikini,”alisema Rais Kikwete.

  Rais alisema hali hiyo imezifanya nchi za Afrika kujikuta katika wakati mgumu wa kutimiza wajibu na majukumu yake katika kuwaletea wananchi maendeleo.

  “Hivyo, sisi katika Afrika tunahitaji kutafuta na kuangalia njia nyingine za ubunifu zaidi za jinsi ya kupata fedha za maendeleo,” alisema Rais Kikwete.

  Mapema mkutano huo ulifunguliwa na Waziri Mkuu wa Malaysia, Dato’ Sri Mohammed Najib Tun Abdul Razak ambaye hotuba yake ilizungumza masuala mengi na matatizo mengi yanayoikabili dunia kwa sasa pamoja na umuhimu wa ushirikiano baina ya nchi zinazoendelea.

  Source: Mwananchi
  Sunday, 19 June 2011 20:57
   
Loading...