JK akihojiwa CNN--" Dynamic leader, dynamic country "....Toa maoni yako

Kuhusu hao baadhi ya waafrika wenzetu kweli itabidi niombe ushahidi.
Hao wengine wajepu,wachainiz na hata waarabu hawaendi huko kwa minajili ya kutembeza bakuli...Huwezi kuwa omba omba halafu unayemuomba umsumbue kukutafutia watafsiri,tumekubali kuwa na viongozi wenye mwelekeo huo na hivyo hatuwezi kujifanya eti tuko huru...Mkuu hatuko huru,kuanzia kiongozi mkuu wa kaya ambaye yeye ni mtumwa wetu mkuu na unafuu wake mwenyewe ni benefits zaidi kama kusafiri na kukutana na mabwana wakubwa wanaotu own,ndo ukweli.

Miafrika Ndivyo Tulivyo
 
Waheshimiwa, mlitaka president azungumze kilatini?
Muuliza maswali mwenyewe kauliza maswali cheap.. what did you expect?
Nadhani ame-perform equivalent na uzito wa maswali yenyewe!
 
Nimeangalia na kusikiliza mahojiano hayo ya Mh Rais na huyo dada wa CNN na kusema kweli nimesikitishwa sana,sitopenda kuongea kwa kuponda,kulaani ama kubeza mahojiano hayo,lakini nimefikia conclusion kuwa JK hakutakiwa kuwa Rais.

Kweli ni mtu mzuri,anaonyesha ni mtu mzuri as a person na pengine dedicated,lakini hakutakiwa kuwa Rais,angepewa uwaziri wa mambo ya nje wa kudumu.

Binafsi nadhani mahojiano hayo ni mpango maalum wa hao wanaomtumia ndugu yetu huyu,pengine kina Sinclair....Nina imani kabisa kuwa JK amewekwa kwenye nafasi ya uraisi na watu flani,hilo liko wazi kabisa. Level of understanding ya Mh Rais kuhusiana na mambo hayo pia hajaniridhisha na ndio maana nikasema lazima kuna watu wenye nguvu kuliko yeye ambao wanaiendesha nchi,yani nimesikitishwa mpaka mwisho.

JK ni mwananchi mzuri sana na inaelekea kweli ni mtu wa watu,tatizo ni urais ambao kusema kweli hakutakiwa awe....No wonder kina Bush walimpenda sana na mabepari wa ndani na nje ya nchi wanampenda,nilishangazwa sana itakuwa vipi Bush ampende mwafrika smart mwenye akili na mapenzi ya kweli kwa mwafrika,kweli nilishangazwa,JK anaweza kuwa ana vision lakini utendaji hakuna na hivyo urais haumfai,lakini nimegunduwa kuwa Bush na wenzake waliutumia udhaifu wa uongozi wetu na ndio maana wa forge urafiki wa hali ya juu huku JK akilia kuwa anaomba Mungu Obama na yeye aipende Afrika kama Bush?

Sijapata nafasi ya kuangalia ama kusikiliza hotuna nyingi tu za Rais wetu,ila msimamo wangu umebadilika,simchukii JK,ila namwonea huruma,namwonea huruma sana. Aombewe Mungu amalize muhula wake huu kisha wazalendo wairudishe nchi kwenye msitari.....Kwasababu inawezekana Muungwana ana nia njema lakini sisi ni binadamu na tuna dhaifu zetu na mara nyingine binadamu wenzetu ndio wanatumia nafasi hiyo ya dhaifu zetu hizo kwa maslahi yao binafsi,wazalendo wakiona hili waondoe tofauti zao,tatizo tulilonalo ni kubwa mnoo!Cha muhimu ni JK mwenyewe aelewe hilo kama kweli anasikiliza maoni ya walio wengi ambao pia wanampenda kama binadamu bila kuangalia kama ni rais ama la.
Inasikitisha.
 
Yeleewiii,...........yaani Nkamangi umesahau kuwa JK alikuwa Foreign Minister for about 10 years.........where else could he improve whetever issues is talking about............mburah!
Ogah,
Sikujua unatoka Kirua (mburah!)
 
Nimeangalia na kusikiliza mahojiano hayo ya Mh Rais na huyo dada wa CNN na kusema kweli nimesikitishwa sana,sitopenda kuongea kwa kuponda,kulaani ama kubeza mahojiano hayo,lakini nimefikia conclusion kuwa JK hakutakiwa kuwa Rais.

Mkuu Mushi, tafadhali aisee,.........yaani siku zote hizo bado ulikuwa unampa benefit of doubt!.........

........Kweli ni mtu mzuri,anaonyesha ni mtu mzuri as a person na pengine dedicated,lakini hakutakiwa kuwa Rais,angepewa uwaziri wa mambo ya nje wa kudumu.................

aisee Arawa.....hata hiyo haiimfai.......it is unfortunate kwetu Watanzania.....haki ya mungu....
 
Mkuu Mushi, tafadhali aisee,.........yaani siku zote hizo bado ulikuwa unampa benefit of doubt!.........

aisee Arawa.....hata hiyo haiimfai.......it is unfortunate kwetu Watanzania.....haki ya mungu....

Kama nilivyosema hapo awali,sijapata nafasi ya kusikiliza hotuba za JK,ni habari tu za magazetini na mitandaoni na sometimes baadhi ya hotuba zake za mwisho wa mwezi ambazo ni za kusoma tu baada ya kuandikiwa.

Sijawahi kupata nafasi ya kumsikiliza akihojiwa ama akiwa kwenye debate,kama wabongo walimsikiliza kwenye debates inawezekana walifikia conclusion tu kama mimi kuwa the guy seems to be having some sort of a vision for our country,lakini ukweli utekelezaji ni zero.

Nimemsikiliza na umtizama kwa makini,anaonekana ni mtu mzuri labda pia msikivu na mtu wa watu,lakini nimegunduwa urais haumfai kama anazungukwa na watu wanaomzunguka hivi sasa na kama anaridhia haya yote yanayotokea nchini mwake.

Matatizo tuliyonayo nchini ni makubwa na so critical to the extent kwamba wala hatuhitaji mwandishi wa cnn kuja kuhoji,maswali tunayo sisi,hayo aliyoulizwa ni maswali yanayoweza kujibiwa na waziri wa mambo ya nje ama balozi,yeye anawajibika zaidi kwa wananchi primarily,lakini hilo ni tofauti na ndio maana nikasema mwenye kuongoza ni mwingine.

Benefit of doubt aliipata kwasababu ya aliyokuwa akiyasema kuwa ataafanya,maisha bora kwa kila mtanzania nk,na hilo halina dalili zozote za kuwezekana chini ya utawala wake huu,hata kama akipewa miaka mingine 20,kwa utaratibu huu tutazidi kutumbukia kwenye umasikini zaidi.Unaposema hastahili hata huo uwaziri wa mambo ya nje unakosea kwasababu cheo hicho ndicho kilipekea wengi kuamini kuwa ataiweza kazi ya Urais.

Kupata nafasi ya kumsikiliza mtu ni tofauti na kusoma habari zake tu ama chambuzi zenye kuhusiana na maamuzi yake.

Msimamo wangu uko pale pale,kwamba JK is a good man but not presidential material,huo ni ukweli,kwamba kama asingekuwa rais wangeweza kum groom for that position,hilo inategemea na mfumo wetu wa utawala,waliomweka hapo wana maslahi yao,wanautumia udhaifu wake na wanamsafirisha kila siku huku nchi wakiwa wameishikilia wao..It is realy unbelievable...Mambo kama hayo ya Afrika waliyoyaonyesha halafu unapoangalia kuona wawakilishi wetu,hata kama hupendi siasa unaweza kujikuta umejitolea kwa namna yoyte ile,hata kama si leo,binafsi nimeamua nitajitolea maana mambo haya si mambo,inasikitisha sana,no words realy lakini naililia Afrika kila mara nikisoma ama kuona mambo kama haya. Sasa mimi ni mwananchi wa kawaida tu ambaye nasoma ama kusikiliza mahojiano hayo,vipi hao viongozi anaokutana nao? Kama tunawakilishwa kihivyo,basi tutapata marafiki kama kina Bush wa kumwaga.
 
..naona amefanya vizuri zaidi kuliko ule mdahalo wa IMF/WB uliofanyika Benki Kuu.

..nadhani wanaomfunda JK wasisitize zaidi hizi one-on-one interviews kuliko midahalo inayohusisha maraisi wengine ambayo imekuwa ikimu-expose JK.
 
................Unaposema hastahili hata huo uwaziri wa mambo ya nje unakosea kwasababu cheo hicho ndicho kilipekea wengi kuamini kuwa ataiweza kazi ya Urais.....................

BIG NO........unakumbuka mchakato wa uchaguzi 1995.........baada ya hapo ilikuwa ni makusudi kabisa ya Mkapa kumpa huyu jamaa Foreign Affairs ili angalau jamaa ajifunze...........lakini wapi.......

.........Imagine JK sitting before Zacharia/Riz Khan......for an interview
 
Kwenye siasa za hapo bongo,kulikuwa na imani kuwa ni lazima kiongozi anayetarajiwa kuwa Rais wetu awe na foreign exposure,hata Mkapa inasemekana aliwekwa wizara ya mambo ya nje ili kumtayarisha kuwa rais....Kikwete nadhani amepewa nafasi za uwaziri toka enzi za Mwinyi,sijui kuhusu enzi za Nyerere,lakini habari ndiyo hiyo kuwa it was for grooming purposes.

Ni tatizo ambalo sasa tumejifunza,tumejifunza kwasababu tulitoa benefit of doubt,huwezi kutoa benefit of doubt halafu tena usijifunze kwasababu kujifunza ndio msingi unaoanzia kutoka kwenye to give benefit of doubt,and then if things happens to go in unexpected way,then tunajifunza na kurekebisha.

Hili la kumchagua JK ni sisi wenyewe na system yetu ndiyo vya kulaumiwa,kwasababu sisi ni omba omba na jamaa alikuwa anafanya kazi nzuri sana ya kuomba omba toka akiwa waziri,then tukahusisha hilo la kupata misaada chini ya uwaziri wake,labda na mapato ya utalii tukasema ana uwezo wa kidiplomasia amabo ni muhimu sana kuwa nao hususan kwa rais wa Afrika,asuming kwamba tunaowaomba hawana nia mbaya,hilo ni kosa,sisemi wana nia mbaya,lakini siwezi kusema wana nia nzuri kwasababu kama ni misaada ndio inatakiwa kutupatia maendeleo badala ya sisi wenyewe,then we deserve JK....Lakini kama tunataka kuchukua a different venue towards success,then we have to rethink. Na ndio maana nikasema sipendi kumchukulia JK kama adui,ningependa aone mwenyewe kuwa system yetu imemwangusha na atumie busara hiyo kutoa mchango wa kutupeleka kwenye direction ya tofauti la sivyo sioni amani.
Hayo ni maoni yangu tu.
 
Kuna anaejua kama kuna mtu katika safu ya JK ambayo anayapitia maswali yatakayo ulizwa na kuyapatia majibu toka kwa wahusika katika serekali? Maanake majibu aliyotoa JK kidogo yanaonyesha hayakutafutiwa majibu fasaha.

Kwa mfano alipoongelea zao la pamba... duu mbona kachemsha sana?

Na swali la binafsi aliloshitukiziwa juu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe barani Africa... jibu alilotoa makes me wonder if Africans are serious na matatizo yanayotukumba... kazi yetu sisi ni ku blame our problems on other people....

Shame on our leaders....
 
Skasuku,naomba nitofautiane na wewe kwenye hili.
Kuhusu jibu la zao la pamba kwa maoni yangu lilikuwa jibu sahihi ila hakuwa constructive na kutoa maelezo ya kina,alijibu swali hilo kirahisi,hata hivyo kwenye hilo nampa pongezi licha ya kwamba hakutoa maelezo enye uzito zaidi kama hadhi yake ya urais inavyotaka. Alichosema kuhusu mfano wa pamba ni pale aliposema kuwa wanunuzi wa pamba walikopa benki kulingana na bei ya mauzo ya wakati huo kabla ya hii credit crunch....Kwamba baada ya hapo,bei zilishuka,na kama bei ikishuka ina maana umeshaingia hasara kwani anticipation yako ilikuwa ni kuuza kwa bei ya juu zaidi,kwa hiyo waliokwisha nunua pamba waliingia hasara kwani hawawezi kuuza kwa bei ya juu ili kupata faida hence incurring loss while still liableto debt repayment....Same thing kwa wakulima kwani bei za vitu kama mbolea nk lazima zilikuwa based on the higher price on the product,kwa mantiki hiyo unakuwa unalipa deni la mkopo kwa hasara ama pengine hata kushindwa kulipa.

Kuhusu kwenye swali la vita ya wenyewe kwa wenyewe,nadhani ni kweli alishtukizwa,hata hivyo he did his best ukilinganisha na vile tunavyomchukulia.

Lilikuwa ni swali la kimtego,na lilikuwa la kumsaidia na ndio maana naamini interview hiyo iliandiwa kwa ajili yake na watu flani wenye manufaa kwa namna moja ama nyingine na yanayoendelea Tanzania...Kwasababu swali aliloulizwa ni kwamba kama mapigano hayo ya wenyewe kwa wenyewe huko Afrika yangekuwa ni ulaya je yangeruhusiwa? Yeye alichotakiwa kujibu kama alitaka kuwa sarcastic kama alivyo intend to be,angemwuliza huyo dada kuwa ni nani hasa huyo anayemaanisha kuwa "Angeruhusu mapigano Europe?" Je alimaanisha wananchi wenyewe wa ulaya ama international insititutions such as UN?

Ukweli ni kwamba ni majukumu ya wenye kupigana pamoja na jumuiya za kimataifa kusuluhisha mapigano ya wenywe kwa wenyewe,ni wazi dada huyo kama ilivyo kwa wengi wenye kutoa maoni yao kuhusu mapigano ya wenyewe kwa wenyewe wana maoni yao tofauti,wengine wanaamini ni udikteta,tamaa za madaraka,ukosekananji wa demokrasia,ufisadi nk. Hayo ndio mambo makuu yenye kuendeleza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe Afrika,na katika mapigano hayo kuna matabaka,kwa nchi nyingine ni ya kikabala na nyingine ya kidini nk. alamuradi tu sababu ni zile zile.

Tanzania ni Taifa lililojaribu kuepuka hayo,lakini ni mambo ambayo JK mwenyewe anayaona yakishamiri chini ya utawala wake na yeye kazi yake ni kwenda huko nje ya nchi na kujifanya mzalendo na kudai kuwa na serikali ya Afrika moja,kama huwezi kumake one Tanzania then dream yako ni sawa na day dreaming.....Nimemtizama Mh Rais na nimeshangazwa kweli kweli,yani kuna unafiki wa hali ya juu viongozi wetu wanapokuwa nje ya nchi na wanapokuwa nyumbani unasiktisha.

Kwa kifupi kuhusu hilo swali la mapigano ni kwamba labda angesema kuwa mpigano ya sehemu kama Europe yangeweza kupewa kipaumbele zaidi ya inavyofanyika kuhusu mapigano ya Afrika,mfano halisi ambao hata wazungu hawa wanalimana wenyewe kwa wenyewe ni jinsi walivyo ignore Rwanda genocide na pia Darfur.

Lakini sasa sijui ni kwamba hakulielewa swali ama aliamua kuwa mwoga wa kusema ukweli na kubakia na unafiki kama alivyoundeleza yeye na Bush.

Majibu mazuri kuhusu hayo ya vita ni mawili kwa maoni yangu,either jumuiya ya kimataifa ingeyashughulika mapigano hayo ya ulaya kwa haraka zaidi kuliko inavyofanya kuhusu mapigano ya Afrika,ama sisi kama Afrika tungejitahidi zaidi ya inavyofanywa kwa mataifa mengine duniani kujaribu kutatua tofauti za hao wazungu zenye kupelekea kuleta mapigano ya wenyewe kwa wenyewe,JK alitakiwa aelewe wazi kuwa ni sawa na kuambiwa kama umshindwa kusimamisha mapigano hayo,na bado kuna kuna lawama kuhusiana na hilo,je yeye angefanya nini kama ni ulaya wanapigana?...Na ukweli wa swali hilo ni kwamba dada yule ni kama alimwuliza JK swali kama Afrika ndo ingekuwa Europe na Europe Afrika,je sisi kama Waafrika ngozi nyeusi na utajiri tungewasaidia vipi masikini hao weupe wanaopigana wenyewe kwa wenyewe,yeye alimjibu yule dada kama ifuatavyo "What would you do?"

Hapo inaonyesha kuwa kila mtu ana namna ya kujibu,hata hivyo he should have done better kwasababu jibu lake hilo lime imply kuwa Mh Rais hana clue ya namna ya kuyamaliza matatizo ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe Afrika,ama hata wazo la namna ya kuweza kuepeukana nayo...Ama ata least vyanzo na namna ya kuepukana na such consequences...Ndio maana nadhani wazungu hawashangazwi kwani hakuna kutumia akili yako,ni kuomba tuu! N wao wana assume kama hao viongozi wetu ndio the best material basi sisi sijui ni nini?
Labda alitakiwa aseme ukweli tu,tungeomba na kundendelea kuomba,no solutions but bakuli.
 
Last edited:
Wanabodi,

Let us learn to give credit where it's due. Frankly speaking, JK has improved a lot in this interview. He has answered many questions eloquently and more importantly without hesitations. I think those people at the State House have listened to our criticisms and worked on them. I am going to give him B- .
 
Hata mimi nadhani aliperform vizuri tu, hususan kadri muda ulivyokuwa ukienda elequency iliongezeka. Kiufupi jamaa ngeli anaijua, grammar imetulia. nampa B+
 
Naaah..I say it was just a fluke. And who knows, maybe they had the questions in advance.

I want to see him more in impromptu settings to be able to tell whether there is an improvement or not. But frankly speaking, I don't think he can ever improve for he is naturally not an eloquent speaker let alone a policy wonk....
 
Hata mimi nadhani aliperform vizuri tu, hususan kadri muda ulivyokuwa ukienda elequency iliongezeka. Kiufupi jamaa ngeli anaijua, grammar imetulia. nampa B+

Haya mimi nayaita maajabu,na kweli inawezekana watanzania wanapata wanacho deserve and nothing more.

Kusema ukweli baadhi ya maswali aliyajibu kwa usahihi kwasababu yalikuwa rahisi sana na ni maswali yanayojirudia na ambayo yamekuwa yakiulizwa kwenye mijadala mbali mbali,sisi wabongo tunababaika sana tu na kiingereza na ndio maana watu wanafagilia eti eloquency,yani ingekuwa nimesimuliwa ningeamini uongo mwingi na sifa za uongo toka humu ndani kutoka kwa baadhi ya members,kweli tuko tofauti na ndio maana issue ni moja lakini uelewa ni tofauti,na maelezo pia ni tofauti.
Kwa kifupi kuna maswali ambayo ni kama hakujibu kile alichoulizwa ama sijui ni nini.

Alipoulizwa aelezee kuhusu humble upbringing yake na how possible did he get there as a president na ana nini cha kusema kuhusu hilo yeye alidai kuwa Babu yake ndiye alimpenda na akaamua kuishi naye,na pia kwamba babu yake sijui uncle alikuwa chief,then akaendelea kwa kusema kuwa alienda jeshini na akawa pia mwanachama wa ccm na ndio maana akawa rais....Ukweli ni kwamba hilo siyo jibu sahihi,kwasababu hakuelezea kama ali work hard to get there or what,na ni what kind of circumtances zilimwezesha kufikia hapo alipo,sasa kama ni kuwa mjukuu wa chief na kuwa mwana ccm pekee ndivyo vilivyompa uwezo wa kutokea kwenye umasikini hadi urais,then hakuna situation yoyote ambayo inaweza kumweka kwenye kundi la watu wa kawaida waliotokea kuwa viongozi wakuu wa nchi,tayari alikuwa na lots of priveledges na ndio maana alijibu alivyojibu.

Ni swali ambalo majibu yake yalitakiwa aonyeshe kuwa kama ni kweli alipata shida wakati anakuwa kama watanzania walio wengi then amweleze mwandishi kuwa he lives the life as an example or a role model to the people with similar backgrounds ambao ndio watanzania walio wengi.
Maisha anayoishi na matendo ya serikali yake,ukiondoa maneno matupu na matukio ya kisiasa ya kwenda kula gengeni nk,si vitu ambavyo vinaendana na sifa anayopewa ya humble beggining,na kusema eti kwenda kujenga huko kijijini kwake ndo namna ya kuonyesha uzalendo,hapo amechensha,Rais ni kiongozi wa nchi na maelezo yake ni lazima yawe conceptual,kwasababu kuna mambo mengi sana ya muhimu ambayo kama yangefanyika vijijini kote,basi tungekuwa mbali na shida na matatizo ya watanzania walio wengi ya umasikini vingepungua sana.

Kwa kifupi msimamo wangu upo pale pale,siwezi kumpa sifa kwenye maneno hata siku moja na kuendeleza upofu unaoendelezwa na watanzania wenzangu na tena wengi wetu tu humu ndani ya Forum.
 
Sema wewe nikisema mimi nitaambiwa ni "hate" bure....
 
Sema wewe nikisema mimi nitaambiwa ni "hate" bure....

Ndivyo ilivyo Nyani,generation hii hakuna kitu,bure,ndio maana tuko hapa...Hata watu tunaofikiri kutokana na umri wana busara,wote bure sana tuu,ndio wametufikisha hapa.
Kwa kifupi wazee walio wengi bila kujali chama ni kitu moja tu,the way of thinking and everything...Yani mtu akija na maneno hapa na pale,aah,utendaji pembeni,na huwezi kuwa na maneno mazuri na utendaji hovyo.
New generation regardless of party affiliation ndo cha muhimu kwani bongo za zamani hazina mpango.
Hata kijana kama Nape Nnauye ndio at least labda wataanzisha mabadiliko humo ndani ya chama,tusubiri tuone,lakini nimegunduwa kitu kimoja kuwa sisi kama watanzania bado sana. Kama JK bado anachota vichwa vinavyojiita wachambuzi hapa,shangazwa na mwananchi masikini ambaye hajui a wala be....Kaazi kweli kweli.
 
Kikwete amewahi kutoa one on one interview ndani ya Tanzania?

Amewahi kuulizwa swali hata moja na mwandishi mzalendo?

Wapi, lini, nani alimuuliza, na alijibu nini?
 
Back
Top Bottom