JK akasirika

Msijali nitafikisha ujumbe. Be happy now eeh. Jamani tusipoangalia tutapata stress kwa kufikiria jinsi ya kurekebisha mambo ya hii nchi. I mean yanatia uchungu sana esp kwa sababu kila siku hakuna jema la kufurahisha nyoyo zetu kutoka serikalini.
 
Hivi Mkichagua Kiongozi akawa mbambaishaji/Msanii, wale waliomchagua wanaitwaje?

Je ni hatua gani zinachukuliwa kwa wale wanaoelewa hili hili jambo lisirudie tena angalau iwe badala ya 80% iwe 30% na zilizobaki zihalibike.


LOL!! KM...Waulize Wamarekani baada ya kumchagua Kichaka 2000 na bado wakamchagua tena mwaka 2004 na madudu aliyoyafanya ambayo sasa yanaathiri dunia nzima. Je wanastahili kuitwaje!?
 
Ukiachilia ufisadi unaotokea kwenye migodi na BOT bado kunaubadhilifu wa hali ya juu sana katika sector mbalimbali za kiuchumi ndani ya serikali.
Maliasili ni moja ya eneo ambalo kwa muda mrefu hata vyombo vya habari na serikali imekuwa kimya juu yake kwa kutokufahamu upungufu wa maadili wa watendaji wake. Maofisa maliasili ni mafisadi wakubwa zaidi hata ya wale tunaowafahamu. Tambua watu hawa ujitengenezea vipato haramu kupitia udhalilishaji mazingira. Licha ya kuaribu misitu yetu ambayo ni chachu ya mvua na uhoto wa asili pia wameshiriki kuaribu mazaria ya samaki kwa kuruhusu vifaa vya uvuvi ambavyo ni hatarishi kwa mazao ya samaki.
Mh Rais hapaswi kusema watachukuliwa hatua. Watumishi wa wizara ya maliasili wengi wao wamejilimbikizia mali isivyokuwa kawaida. Wanamajumba makubwa, magari ya nguvu na hata vitega uchumi vyenye mitaji mikubwa ambavyo kamwe haviendani kabisa na mishahara yao, madaraka yao na hata elimu yao. Katika wizara hii, walewaliokuwa wanaonekana hawana mpango basi walikuwa wanatupwa upcontry kama maafisa maliasili basi huko jamaa uishi na kufanya mavituz, anaangamiza msitu mmoja adi mwingine huku akijipatia mali kwa kasi bila serikali kumfuatilia wala kujua anafanya nini maana katupwa. Hawa jamaa ndo wanatufikisha kwenye majanga ya ukame. Ni jera na kutaifisha mali zao ndo njia sahii. Watumishi wote wa maliasili wanapaswa kuchunguzwa sawa tu na wale wa TRA
itabidi upangue wizara nyingi...siyo maliasili na utalii pekee ili kurudisha crebility yako kwa Watanzania.

JK akasirika

2007-11-19 17:18:18
Na Mwandishi Wetu, Jijini

Kuna habari kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Jakaya Kikwete amekasirishwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya maafisa wa ngazi za juu katika Wizara ya Maliasili na Utalii nchini na yuko mbioni kuwapangua wote wizarani hapo.

Kwa mujibu wa taarifa toka kwa chanzo chetu kimoja, ni kwamba hazitapita siku nyingi kabla Rais hajapitisha panga kali katika wizara hiyo ili kuweka mambo sawa.

``Rais ana taarifa za mambo mengi yanayofanywa kinyume na sheria wizarani hapo? kwakweli anakasirishwa na namna watu waliopewa dhamana kubwa ya kulitumikia taifa wanavyolihujumu taifa.

Wengi atawaopangua na wengine wanaweza kumwaga unga katika muda mfupi ujao,`` kikasema chanzo chetu.

Chanzo hicho kimeongeza kuwa baadhi ya maafisa wasio waaminifu wanaweza kuchukuliwa hatua kali zaidi za kisheria.

Inaelezwa zaidi kuwa miongoni mwa yale yaliyomkasirisha Rais na hata kuamua kutaka kuchukua hatua ya kupangua vigogo kibao wizarani hapo ni pamoja na kushamiri kwa biashara haramu ya magogo ambayo hufanywa kiujanjaujanja na baadhi ya maafisa wa juu wizarani hapo.

Katika hatua nyingine, Rais Jakaya Kikwete amekaririwa jana akisema kuwa maafisa wasio waaminifu katika Wizara ya Malisili na Utalii watachukuliwa hatua stahili katika muda usiokuwa mrefu kuanzia sasa.

``Ninazo taarifa kuwa kuna baadhi ya maofisa wasiokuwa waadilifu ndani ya wizara? hawa wamekuwa wakijihusisha na biashara haramu ya magogo, sasa wajiandae kwa kuwa watachukuliwa hatua zinazostahili siku si nyingi,`` amekaririwa akisema Rais jana wakati akiwa kwenye ziara yake mkoani Lindi.

Amesema maofisa hao wasiokuwa waadilifu wamesababisha kupakwa matope hata wale walio waaminifu.

JK akasema kuwa wilaya za Kilwa na Rufiji ndizo zilizoshamiri kwa biashara hiyo ya uvunaji magogo kinyume cha sheria.

Amesema kinachosikitisha zaidi ni kuwa watu hao wamekuwa wakivuna hata miti michanga na ile isiyokomaa.

SOURCE: Alasiri
 
LOL!! KM...Waulize Wamarekani baada ya kumchagua Kichaka 2000 na bado wakamchagua tena mwaka 2004 na madudu aliyoyafanya ambayo sasa yanaathiri dunia nzima. Je wanastahili kuitwaje!?

Huwezi kumlinganisha Bush na Kikwete bwana...Wamarekani maisha yao hayajabadilika sana...bado wanatanua na watu hawavai makatambuga au kutembea pekupeku na kushindia mlo mmoja kwa siku huku wakiambiwa maisha bora kwa kila mtu na kwamba ndege inapaa....
 
Mimi nafikiri mwandishi wa Arasiri angefikiria vizuri angebadili kichwa cha habari hii. Mimi nilitegemea aandike kuwa: either JK achekelea, au JK apata kigugumizi.

Na story yenyewe ndani ingelikuwa hivi pamoja na kuwajua wahujumu uchumi kwa mara nyingine JK ameamua kuwafumbia macho kama alivyofumbia MAFISADI, WAUZA UNGA nk.

Sasa pamoja na kupelekewa majina ya MAFISADI kutoka wizara ya mali-asili na raia wema amebakiwa kuongea tu jinsi atakavyo washughulikia na kujitapa kuwa uwezo na nia ya kuwashughulikia anayo ila tu waendelee na hakuna akayewasumbua...................
 
Huwezi kumlinganisha Bush na Kikwete bwana...Wamarekani maisha yao hayajabadilika sana...bado wanatanua na watu hawavai makatambuga au kutembea pekupeku na kushindia mlo mmoja kwa siku huku wakiambiwa maisha bora kwa kila mtu na kwamba ndege inapaa....

Si unaona bei ya petroli imeota mbawa! Dollar inaporomoka kama vile ilirushwa toka milima ya uluguru, uchumi pia unaifuata dollar nao unaporomoka NYSE nayo inaanguka kwa kasi ya ajabu. Wanaweza wakawa hawavai makatambuga, kutembea peku na kushindia mlo mmoja lakini wengi wanajutia kura zao zilizomweka jamaa WH
 
hivi kweli KIKWETE ni hardened soldier au alikuwa KADA tu...hasa wa kufundisha somo la UHAMASISHAJI na MAIGIZO...MIMI najua kuwa sifa ya kwanza ya askari ni watu wa VITENDO kuliko MANENO MATUPU..
NCHI NYINGI DUNIANI ZINAPENDA KUWA NA RAIS AMBAYE PAMOJA NA KUWA MSOMI AWE NA BACKGROUND YA JESHI..ILI AWEZE KUTEKELEZA MAJUKUMU VEMA...ie ISRAEL[ili uwe mtawala lazima pamoja na usomi uwe general au fields marshall mwenye distinction],AMERICA[bush mdogo alisumbuliwa sana na john carry..kwa kuwa alikacha kwenda VIETNAM..badala yake kwa kutumia umaarufu wa baba yake Akapelekwa kwenye jukumu rahisi la COAST GUARD]..hata watawala wa uingereza lazima wapite jeshimi.....
matendo na maamuzi ya muungwana hayaoneshi uhodari,sense of urgency,na ukakamavu unaotakiwa..kama RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA...
 
Jemedari wetu uwezo wake naona mdogo wa kututoa tulipo,hope agundue na awe na nia ya kupigana na rushwa na mifumo mibovu ya serikali mana ndio umaskini wote unaanzia hapo,hakuna mchawi mwingine zaidi ya sisi wenyewe
 
Si unaona bei ya petroli imeota mbawa! Dollar inaporomoka kama vile ilirushwa toka milima ya uluguru, uchumi pia unaifuata dollar nao unaporomoka NYSE nayo inaanguka kwa kasi ya ajabu. Wanaweza wakawa hawavai makatambuga, kutembea peku na kushindia mlo mmoja lakini wengi wanajutia kura zao zilizomweka jamaa WH

Sawa bei ya mafuta imepanda. Hata hivyo bado watu wanasukuma magari kama hawana akili nzuri. Juzi nimeenda kwa dealer wa Maseratti na nilipigwa na butwaa jinsi ma-salesman walivyokuwa busy. Wakati huo huo, bei ya mafuta imepanda karibu kila kona ya dunia hata bongo. Hayo ya dola kushuka ni kawaida ktk mambo ya fedha na masoko. Hata currency zingine hupanda na kushuka. Kwa hiyo dola inaweza ikashuka leo lakini miezi miwili ijayo ikapanda tena. Hizo recession unazosikia ni za muda tu. Kama zingekuwa prolonged na kufikia depression hapo ningesema uchumi wao uko ktk hali mbaya. Recessions ni vitu vya kawaida ktk uchumi. Huwezi ukawa na boom muda na wakati wote.

Na siamini kama Wamarekani wengi wanajutia kumpatia kura zao. Labda nitakubaliana na wewe ukisema nchi imegawanyika ktk mapande makuu mawili nitakubaliana na wewe. Tena hili la nchi kugawanyika lilidhihirika mwaka 2000 kwenye uchaguzi wao mkuu. Tazama asilimia alizopata Gore halafu zilinganishe na za Bush utaona the country is virtually split in the middle
 
Nchi imegawanyika hiyo ni kweli, lakini Kichaka wanajuta kumweka WH ndio maana unaona hata wagombea Urais wote wa Republicans katika kinyang'anyiro cha 2008 hawataki Kichaka awasogelee hata kidogo, maana kuonekana naye ni sawa na political suicide.
 
Mbona hata Gore hakumtumia Clinton....matokeo yake...akashindwa kwao Tennessee na Arkansas kule kwa bosi wake. Lakini sasa hivi in hindsight....watu wengi wanakubaliana kuwa angemtumia kwenye campaign...
 
Back
Top Bottom