BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,117
itabidi upangue wizara nyingi...siyo maliasili na utalii pekee ili kurudisha crebility yako kwa Watanzania.
JK akasirika
2007-11-19 17:18:18
Na Mwandishi Wetu, Jijini
Kuna habari kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Jakaya Kikwete amekasirishwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya maafisa wa ngazi za juu katika Wizara ya Maliasili na Utalii nchini na yuko mbioni kuwapangua wote wizarani hapo.
Kwa mujibu wa taarifa toka kwa chanzo chetu kimoja, ni kwamba hazitapita siku nyingi kabla Rais hajapitisha panga kali katika wizara hiyo ili kuweka mambo sawa.
``Rais ana taarifa za mambo mengi yanayofanywa kinyume na sheria wizarani hapo? kwakweli anakasirishwa na namna watu waliopewa dhamana kubwa ya kulitumikia taifa wanavyolihujumu taifa.
Wengi atawaopangua na wengine wanaweza kumwaga unga katika muda mfupi ujao,`` kikasema chanzo chetu.
Chanzo hicho kimeongeza kuwa baadhi ya maafisa wasio waaminifu wanaweza kuchukuliwa hatua kali zaidi za kisheria.
Inaelezwa zaidi kuwa miongoni mwa yale yaliyomkasirisha Rais na hata kuamua kutaka kuchukua hatua ya kupangua vigogo kibao wizarani hapo ni pamoja na kushamiri kwa biashara haramu ya magogo ambayo hufanywa kiujanjaujanja na baadhi ya maafisa wa juu wizarani hapo.
Katika hatua nyingine, Rais Jakaya Kikwete amekaririwa jana akisema kuwa maafisa wasio waaminifu katika Wizara ya Malisili na Utalii watachukuliwa hatua stahili katika muda usiokuwa mrefu kuanzia sasa.
``Ninazo taarifa kuwa kuna baadhi ya maofisa wasiokuwa waadilifu ndani ya wizara? hawa wamekuwa wakijihusisha na biashara haramu ya magogo, sasa wajiandae kwa kuwa watachukuliwa hatua zinazostahili siku si nyingi,`` amekaririwa akisema Rais jana wakati akiwa kwenye ziara yake mkoani Lindi.
Amesema maofisa hao wasiokuwa waadilifu wamesababisha kupakwa matope hata wale walio waaminifu.
JK akasema kuwa wilaya za Kilwa na Rufiji ndizo zilizoshamiri kwa biashara hiyo ya uvunaji magogo kinyume cha sheria.
Amesema kinachosikitisha zaidi ni kuwa watu hao wamekuwa wakivuna hata miti michanga na ile isiyokomaa.
SOURCE: Alasiri