JK Aikana Sera ya Maisha Bora kwa Kila M-TZ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK Aikana Sera ya Maisha Bora kwa Kila M-TZ

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bill, Oct 5, 2009.

 1. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,163
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  ...Aikana sera ya maisha bora, Asema si yake, ilikuwapo tangu uhuru [​IMG] [​IMG] [​IMG] Source: Majira, Monday, 05 October 2009 08:16 Na Mwandishi Maalumu, Mwanza

  WAKATI kaulimbiu ya kampeni zilizomweka madarakani Rais Jakaya Kikwete 'Maisha bora kwa kila Mtanzania' ikizidi kuhojiwa na wananchi kama imesaidia kuboresha maisha yao, jana rais huyo ameikana akisema si yake bali ilikuwapo hata kabla ya uhuru.

  Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ilimkariri Rais Kikwete akiikana sera hiyo kuwa wanaosema ameileta yeye wanabeza, wakati sera hiyo ilikuwapo na itaendelea kuwapo hata baada yake.

  “Wapo watu wanaobeza kuwa hii sera ya maisha bora imeletwa na akina Kikwete. Sisi tumeendeleza sera ile ile ambayo taifa hili limekuwa linatekeleza tokea uhuru wetu… na wala kazi hii haitaishia kwangu mimi, hata wale viongozi watakaonifuata wataendeleza sera hii kwa sababu kazi ya kujenga maisha bora kwa wananchi haihishi, haina kikomo,” alisema.

  Rais Kikwete alisema kuwa hata kabla ya uhuru, Mwalimu Julius Nyerere alitambua ili uhuru na umoja viweze kudumishwa ni lazima wananchi wake wapate maisha bora na ndiyo maana akawatambua maadui wakuu watatu – ujinga, maradhi na umasikini- na njia za kukabiliana na maadui hao.

  Rais Kikwete ameyasema hayo mjini Mwanza juzi jioni alipozungumza na vijana wa CCM ambao walioondoka mjini Mwanza jana kwenda Butiama, Mkoani Mara, kwa Matembezi Maalum ya kumuezi Mwalimu kwenye kumbukumbu ya miaka 10 tangu kifo chake, Oktoba 14, 1999.

  Vijana 166 kutoka mikoa yote ya Tanzania wanashiriki katika Matembezi hayo ya siku 10 na yatakayopitia njia ambayo Mwalimu Nyerere alitembea mwaka 1967 katika kuunga mkono na kuhamasisha Azimio la Arusha.

  Kaulimbiu ya Matembezi hayo ni “Uhuru na Kazi” na miongoni mwa mambo ambayo vijana hao watafanya njiani ni kukarabati Shule ya Msingi ya Mwisenge ambako Mwalimu Nyerere alipata elimu yake ya msingi.

  Rais Kikwete aliwashangaa Watanzania ambao wanabeza uhuru wa Tanzania na kufurahia wakati jina la Tanzania linaposhambuliwa na wageni na kuwasihi Watanzania kuzidi kumuenzi mwalimu.

  “Wamarekani wale wanaye George Washington… sisi tunaye Mwalimu Julius Kambarage Nyerere… na kila nchi ina mwasisi wake ambaye anakumbukwa kwa aliyoyasimamia,” amesema Mwalimu na kuongeza:

  “La kwanza la kumkumbuka Mwalimu ni uhuru wa nchi yetu. Huyu alikuwa ni kiongozi aliyeambiwa achague kati ya siasa ama kazi ya ualimu… huyu mzee wetu akachagua siasa na utumishi wa umma bila hata kujua atakula nini.”

  “Akachagua kupigania uhuru wa nchi yetu. Kama mnavyojua nyote hii kazi ya siasa ni kamari..unakwenda kugombea ukijua kuna kupata ama kukosa..lakini yeye alifanya uamuzi sahihi wa kupigania uhuru,”

  Rais Kikwete alisema kuwa uhuru siyo mipaka bali ni heshima ya nchi na ndiyo maana Tanzania haitasita kumkabili yoyote ambaye atajaribu kuchezea uhuru huo.

  Kuhusu umoja wa taifa, Rais Kikwete amesema kuwa Mwalimu alihakikisha kuwa uhuru wa nchi unazaa umoja ili nchi iwe moja na isigawanyike vipande vipande kwa sababu yoyote ile.

  “Aliondoa viashiria vyote vya kuvunja umoja wa taifa tokea mwanzo kabisa. Aliondoa uchifu ili kuondoa nguvu za ukabila. Alitambua hatari ya dini na akataifisha shule zote za dini ili vijana wetu waelimishwe na kulelewa kama vijana wa taifa moja na siyo vijana wa dini tofauti.”
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Oct 5, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Whaaat?
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hajaikana bali anachosema ni kuwa hii sera ilikuwepo - na huenda ilikuwa dormant katika mazungumzo ....hivyo utawala wake uliamua kuifufua na kuiendeleza na watakaokuja wataendelea nayo.
  Asichosema ni kwanini toka enzi hizoooooo hatukuwahi kusikia kiongozi akiahidi waziwazi kumpa kila MTZ maisha bora?
  Maisha bora ni nini?
   
 4. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35

  hajaikana anachosema ni kwamba ilikuwepo toka enzi za nyerere, tatizo ni kuendelezwa kwake tu.. japo kiukweli hata yeye imemshinda kilichobaki maneno tu.
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  asituchezee hapa ..we are tired na ujinga ujinga huu..kama ilikuwa dormant nani alimuambia ai activate...halafu ndo kuna mtu anasema Jk ni miongoni mwa marais bora duniani....
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Oct 5, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakuu zangu, ukisoma maelezo yake ni kwamba JK ameikana ahadi yake..Swala halikuwa ahadi hiyo ilikuwepo toka lini kwa sababu hakuna sera duniani unayoweza kuivumbua wewe ikakubalika kwa wananchi ambao hawafahamu lini na wapi iliweza kutumika..Hata huyo Nyerere mwenyewe aliikuta sera ya Maisha bora ikitumiwa nchi nyinginezo..Muhimu ni ahadi yako ktk kupanga priority zako ktk uongozi na ndicho alichotuahidi wananchi..

  Majibu ya JK ni ya kihuni kabisa, huwezi kuwaahidi wananchi MAISHA BORA kama Kipaumbele cha sera zako kisha ukaikana kuwa sii sera yako hali umeitumia sera hiyo kama kipaumbele kujipatia kura za wananchi. Kila ahadi aloweka anaanza kuzikana kihuni kihuni sasa nambieni ni sera ipi aloitunga yeye maanake hizo ahadi zimekuwa sii zake, zake yeye ni zipi?
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  haya hayo maisha bora yako wapi jamani ???????????????????????????????????????????? kama ilikuwepo toka long time
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  :):)
   
 9. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Hivi ni kati ya vitu vinavyo nikera sana kuhusu RAISI wenu.
   
 10. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hii ni sera ya ngapi sasa Rais wetu anakana...JK imefika mahali ni rahisi mno kutabiri atafanya nini next..!!
   
 11. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  hizi ndo gia za JK kwa ajili ya uchaguzi mwakani.
   
 12. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alikana sera zote live kwenye TV ya Taifa, akisema ilani ya CCM hakuiandika yeye. Kwa hiyo mtu asije akajipa matumaini ya blah blah yoyote inayoimbwa na chama chake.

  Hivi hatuna pa kuuliza? Maana huu ni wizi.
   
 13. f

  fili New Member

  #13
  Oct 5, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  heee vichekesho saaana aiseee
  sisi wadanganyika tunaendelea kudanganyika tuuu
  thus why I hate politics
   
 14. f

  fili New Member

  #14
  Oct 5, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukisema hajafanya lolote anachekacheka tuu unaingia matatizoni mbona watanzania hatupendi kukosolewa jamani kwanini!!??
   
 15. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,407
  Likes Received: 3,738
  Trophy Points: 280
  Vipi ile ya ajira 1,000,000 nayo aliikana..???? Au bado kwamba tunasubiri akane moja hadi nyingine.... mweeeeeeee.......ama kweli imbombo ngafu...!!!!!!!!!
   
 16. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Labda wakati umefika tumwuulize mheshimiwa rais alikuwa na ilani gani, alikuwa na anaendelea kuwa na sera gani. Uchaguzi ni mwakani asije kutulisha mkenge. Kumbe ndio maana alikwepa zile debate!
   
 17. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mi -sijui
   
 18. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwikwikwikwikwiiiiii!
  You just made my evening!
  Tutaendelea kubaki kuwa makondoo mpaka lini??
  Tanzania tunasikitisha kwa kweli!
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Oct 5, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Haya hiyo siyo yake!
   
 20. y

  yeromin Member

  #20
  Oct 5, 2009
  Joined: Aug 8, 2008
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Na ataikana sana coz haikuwa na plan ila maneno ya politics yaliyokosa utekelezaji
   
Loading...