JK ahimiza ujenzi, ukarabati wa reli za Afrika Mashariki

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,320
33,121








Mwapachu%2810%29.jpg

Katibu Mkuu wa EAC, Balozi Juma Mwapachu.



Rais Jakaya Kikwete, amesema reli za nchi za Jumuiya Mashariki (EAC) zimechakaa sana na zimepitwa na wakati kwa kuwa tangu wakoloni wazijenge zimebaki vile vile.
Amesema umuhimu wa kuziunganisha nchi hizo kwa usafiri wa kisasa wa reli halina mjadala kwani hata viongozi wa nchi hizo wamekuwa wakielezea umuhimu wake kwa muda mrefu.
Aliyasema hayo jana wakati akifungua mkutano wa kujadili namna ya kuziunganisha nchi hizo kwa usafiri wa reli ili hatimaye usafirishaji wa bidhaa uwe rahisi na ziwafikie walaji kwa bei ya chini.
Alisema reli ya kwanza kujengwa na Wajerumani ya kutoka Tanga-Moshi katikati ya mwaka 1880 hadi 1911 na kwamba Waingereza walipokuja waliiendeleza hadi Arusha na ilifika huko mwaka 1929.
Alisema Waingereza walijenga reli ya Mombasa-Kampala kati ya mwaka 1896 na 1931 wakati ile ya Dar es Salaam- Kigoma kupitia Tabora ilijengwa na Wajerumani kati ya mwaka 1905-1914 na kutoka Tabora-Mwanza ilimaliziwa na Waingereza mwaka 1926.
Alisema mtandao wa reli Afrika Mashariki isipokuwa wa Tanzania na Zambia uliojengwa mwaka 1970s, ulijengwa kwa msaada wa China na ni nyembamba kiasi kwamba haiwezi kubeba mzigo mzito.
"Reli za sasa EAC kwa kweli ni za kizamani na zimechoka sana, lazima ujenzi na ukarabati ufanyike haraka sana maana tangu zijengwe na wakoloni enzi hizo hadi leo ziko vile vile," alisema.
"Lakini tusing'ang'anie kuunganisha kwa nchi za EAC tu, kuna masoko yako Comesa na Sadc ambayo nayo lazima tuyafikie, hatuwezi kuyafikia iwapo hatutawaunganisha na mtandao wetu wa reli...Tukifanya hivyo tutafaidi masoko ya nchi hizo na tumechelewa tunapaswa kulifanya kwa haraka suala hili," alisema.
Alisema nchi za EAC zinapaswa kuangalia namna ya kuitumia reli ya Tazara kwa kujiunganisha nayo kwani inakwenda hadi Afrika Kusini ambako kuna soko kubwa hali ambayo itafungua milango ya maendeleo si tu kwa nchi za Afrika Mashariki bali kwa nchi zote za ukanda wa maziwa makuu.
"Tazara kwa sasa tayari inatoa fursa hiyo kwa nchi za kusini mwa Afrika na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo," alisema.
Katibu Mkuu wa EAC, Balozi Juma Mwapachu, alisema zinahitajika Dola bilioni 20 ili kukarabati na kurekebisha miundombinu ya reli kwa nchi hizo.



CHANZO: NIPASHE
 
hiyo reli yake tu ya kati imemshinda! ije kuwa za east afrika? hizo ni blaa blaa tu, tulishazizoea!
 
Back
Top Bottom