JK afanye haya, ili aweke Historia, na kuwamudu wanaomchakachua kwenye CCM


N

Nyumbu-

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Messages
978
Likes
125
Points
60
N

Nyumbu-

JF-Expert Member
Joined May 26, 2009
978 125 60
Ndugu wana JF,

Maadam sasa kampeni zimeisha, na ni wazi JK ndiye Raisi mteule, ni vyema sasa tuanze kutoa ushauri wa jinsi ya yeye kujijenga upya na kuweza kufuta yale yaliyotaka kumgharimu kisiasa
1. Aunde serikari ya kitaifa kama ya Zanzibar. Kwa kufanya hivyo atakuwa si tu ameivusha TZ kutoka siasa za chuki, bali pia itakuwa rahisi kwake kuwashughulikia marafiki zake ambao ndio has waliomzunguka na tuhuma zao zinamuathiri moja kwa moja
2. Aunde baraza dogo la mawaziri , kwa kuiga mifumo ya upinzani, lenye watu makini, na si marafiki ili wamwogope na kufanya kazi ipasavyo
3. Baraza la mawazri liteuliwe nje ya wabunge ili liweze kuwajibika kwa bunge moja kwa moja , kuliko hivi sasa ambapa wabunge ndiyo hutuliwa kuwa mawaziri. Bahati mbaya ni kwamba ukishamteua kuwa waziri mtu kama Magufuli , tayari unakuwa umemziba mdomo wa kusimamia serikali kama mbunge. Angalia jinsi Marmo alivyozimwa na kusahau kabisa uzalendo aliokuwa nao kipindi cha Ali Hassan Mwinyi
4.Asiendekeze visasi na wale anaohisi ni maadui wake. Atafute namna ya kuyaondoa makundi kwenye CCM, kwa kuwawajibisha bila kuwaangalia usoni wale wote wanao endeleza mitandao isiyo rasmi
5.Apunguze gharama za uendeshaji wa serikali kwa kuyauza mashangingi yote serukalimni na kurudi kwenye magari ya kawada, lakini salama.
6.Aondoe kabisa matumizi ya dola za kimarekani katika uuzaji wa bizzaa zetu hapa ndani. Alazimishe mahoteli yote kuchaji bei kwa Shillingi, na si kama ilivyo sasa ambapo bei zimeandikwa kwa $ halafu ndo mtu analipa equivalent Tzs. Hii inashusha sana value ya shilingi yetu.

Unaweza ongeza!
 

Forum statistics

Threads 1,236,774
Members 475,220
Posts 29,268,064