JK aelimishwe: Katiba Mpya siyo ya kwake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK aelimishwe: Katiba Mpya siyo ya kwake

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rutashubanyuma, Jan 1, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  JK yaelekea haelewi misingi ya kuandika katiba mpya kuwa yapaswa kuwa ni shirikishi kuanzia uteuzi wa wale watakayoyakusanya maoni ya wananchi........................uamuzi wa JK kuunda Tume yake mwenyewe ambayo haitokani na wadau na ambayo haina nguvu ya kisheria inamaanisha lengo lake ni kuiwekea viraka katiba iliyopo.....................kama wale waliomtangulia waliopachika viraka 15 kwa katiba iliyopo.......................Hii yamaanisha ya kuwa..........

  Maoni ya wananchi yatachakachuliwa kama yalivyochakachuliwa siku zilizopita...........


  Huko nyuma tume za Raisi ziliundwa na zikapeleka mapendekezo yake kwa vyombo vya kisheria kwa marekebisho lakini havikuweza kuandaa katiba mpya........Sababu kuu ni kuwa wananchi wenyewe kupitia Bunge lao hawakushirikishwa katika kusimamia mchakato mzima ila ni Ikulu au Ofisi moja tu ya Raisi ndiyo iliyosimamia na kuratibu mchakato mzima..........

  ..........na huu mchakato wa JK lengo lake ni kuhakikisha ya kuwa CCM tu ndiyo itakuwa na uamuzi wa mwisho juu ya sura ambayo marekebisho ya katiba yatakavyokuwa na kwa hili nchi hii siyo wageni.......................

  Tume ya Nyalali iliyoundwa na Raisi Mwinyi pamoja na kuwa ilisimamiwa na Jaji Mkuu iliishia kuona mapendekezo yake ya sheria 40 za kidhalimu kuishia kwenye makaratasi tu.......................

  Hii yote ilitokana na hapakuwepo sheria ambayo iliipa nguvu tume hiyo kuwa mapendekezo yake yatajadiliwa moja kwa moja na Bunge bila ya kukarabatiwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu....................

  Wakati wa Mkapa tuliona "WHITE PAPER"....hakuna raia hata mmoja leo anayeweza kusema hivi ni vigezo vipi ambavyo Ikulu ilivitumia katika kuhakikisha ya kuwa mapendekezo ya marekebisho ya 13 ya Katiba yaliamuliwa na kupelekwa Bungeni

  Tunachohitaji ni...............Bunge na wala ofisi ya Raisi kusimamia mchakato huo.......

  1) Bunge kupitisha sheria ya mchakato mzima wa uandaaji wa ukusanyaji wa maoni ya raia wote, utaratibu mzima utakavyofuatwa kuhakikisha hakuna ambaye ataweza kuchakachua maoni tajwa........................

  2) Wajumbe wa Tume wafanye maombi rasmi baada ya nafasi hizo kutangazwa na Ofisi ya Bunge kwenye vyombo vya habari...................

  3) Maoni ya Wananchi kupelekwa kwa Mwanasheria Mkuu na yeye anapaswa kuyaundia muswada bila marekebisho yoyote yale..................

  4) Bunge linaweza kuyarekebisha kama theluthi mbili ya Bunge lote linaafiki marekebisho hayo...................

  5) Sheria ya kura ya maoni iundwe ili kuruhusu raia kuwa na sauti ya mwisho juu ya katiba hiyo ambayo kweli itakuwa ni mpya........................

  Nje ya utaratibu huu katiba iliyopo itakuwa imewekwa viraka na JK kama maraisi waliomtanguliwa walivyofanya kwa kujiundia Tume ya Katiba ambayo waliibabatiza ni ya wadau wote bila ya kuwapa watanzania kushiriki katika kuichagua....................au kuiunda na Tume hiyo kutokuwa na ubavu wa kisheria.........

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Redet: JK soma alama za nyakati
  Friday, 31 December 2010 20:48 0diggsdiggSalim Said

  MWENYEKITI Mwenza wa Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (Redet), Dk Benson Bana, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kusoma alama za nyakati na kubeba ajenda ya katiba mpya ili kuweka vipaumbele vyake na kujijengea heshima baada ya kustaafu kwake.
  Akizungumza na Mwananchi kwa simu jijini Dar es Salaam jana, Dk Bana alimtaka Rais Kikwete kuwapa Watanzania salamu bora za mwaka mpya kwa kuwaahidi katiba mpya kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji mwaka 2014.

  "Kama napata fursa ya kukutana na rais leo (jana), kabla hajaanza kuwahutubia Watanzania, ningemshauri na kumuomba kabisa asome alama za nyakati, ni aibu ajenda ya katiba mpya kuongozwa na wapinzani, wanaharakati na watu wengine wakati serikali ipo," alisema Dk Bana na kuongeza:
  "Mifano ipo ya kutosha, wenzetu wa Kenya na Uganda wameachana kabisa na katiba hizi za watu waliojifungia vyumbani na kutunga katiba bila ya kushirikisha jamii husika."

  Dk Bana anaungana na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Jaji Omar Makungu, Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, mawaziri wakuu wa zamani, Joseph Warioba na Frederick Sumaye na Jaji Mkuu mstaafu Augostino Ramadhan kuunga mkono hoja ya kuundwa katiba mpya.

  Madai ya Katiba mpya, pia yamewahi kutolewa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, ambaye alisema bayana kuwa katiba mpya iandikwe mapema kabla ya mambo kuharibika.
  Dk Bana anapingana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, aliyetaka katiba iliyopo iwekewe viraka.

  "Suala la katiba mpya halitaki mjadala mrefu na wala sio la kuweka viraka, haya tumeweka viraka halafu iweje? Itasaidia nini? Hivyo viraka tumeweka mpaka tumechoka, lakini hakuna mabadiliko matatizo yanaendelea kuzidi," Dk Bana alipinga vikali kauli ya Jaji Werema.

  Alisema katiba mpya ni msingi kwa Tanzania ya sasa na kwamba, serikali haipaswi kupata kigugumizi katika kuchukua ajenda hiyo ya kuanzisha mchakato wa kuipata haraka.
  Dk Bana ambaye pia ni Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Siasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema katiba iliyopo haijibu maswali ya msingi ya Watanzania kuhusu mustakbali.

  "Katiba ndio msingi wa taifa kwa kila kitu, hivyo pamoja na mambo mengine, lazima ijibu maswali ya msingi ya Watanzania, mambo ya Tume huru ya uchaguzi, nguvu ya rais, viongozi wa umma wawajibike kwa nani, katiba lazima iweke wazi mambo haya mazito," alisema Dk Bana.

  Alifafanua kuwa, katiba mpya lazima iwe na fikra na mawazo shirikishi sio suala la mtu au kikundi cha watu kujifungia ofisini na kuandika katiba kwa niaba ya Watanzania.
  Madai ya katiba mpya yalizidi kupamba moto baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2010 ambapo Rais Kikwete alitangazwa mshindi kupitia CCM.

  Pia, Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, tayari amewasilisha hoja binafsi ofisi za Bunge ili iweze kujadiliwa katika kikao kijacho cha bunge na CUF wamewasilisha mapendekezo yao ya katiba mpya kwa Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Unapoona hata wapambe wa JK wanatoa tafsiri sahihi ya katiba mpya ujue basi JK kweli atakiwa kuelimishwa tunaposema tunadia katiba mpya tunamaanisha nini........................siyo mtu mmoja au kikundi cha watu kituchagulie wakusanya maoni ila watokane na ridhaa ya watanzania kwa kufuata utaratibu wa kisheria ambao hata majirani zetu wa Kenya waliufuata.............................
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Pole sana Dr. Bana Jk hakukutafuta kabla ya kuisoma hotuba yake vinginevyo angelisema amemwagiza Mwanasheria mKuu apeleke mapendekezo Bungeni ya kuandaa mchakato shirikishi wa kuiandika katiba mpya ambao utasimamiwa na kuratibiwa na Bunge tofauti na mikakati mingine ya awali ambapo no Ofisi ya Raisi ambayo amekuwa ikisimamia mchakato tajwa.............
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Jk anataka kuteua watu wake maswahiba wake na huu ni sawasawa kabisa na kuiandika katiba vyumbani maana siyo shirikishi..............kuna ugumu gani kwa nafasi za wajumbe wa Tume kutangazwa magazetini na ukawepo ushindani wa wazi na kamati ya Bunge ya sheria na katiba ikafanya mchujo>

  Pia zikaundwa sheria za mchakato mzima ili kuupa ubavu wa kisheria?
   
 6. W

  We can JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Katiba si ya Bunge, Katiba si ya Rais, Katiba si ya CHADEMA, Katiba si ya CCM, CUF, TLP..., Dini fulani, nk. Hivyo, wanaoteuliwa kuratibu suala zima la Katiba wanapaswa kuteuliwa na Wananchi wenyewe (au wawakilishi wao, yaani Wabunge).

  Katiba iko juu ya Rais, Iko juu ya mtu yeyote, ndiyo maana kila mtu aliyeajiriwa na wanachi, hupaswa kuapa kuilinda KATIBA.
   
 7. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #7
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  If that is the case mbona Mkuu keshateua watu wake? kamalizia kwa kusema inaongozwa na mwanasheria aliyebobea.
   
 8. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Nadhani tume ya raisi ni kama independent committee tu, kwa hivyo aiwezi pitisha sheria bila ya bunge na mara nyingi report huishia on the branch of the executive where the report is related with. Mara nyingi kazi yake huwa ni kutoa mapendekezo kutokana na mjadala waliopewa, hivyo ingawa mapendekezo yake yanaweza kuwa 100% what we need lakini hawana nguvu wala raisi hana nguvu ya kusema ndio iwe sheria bunge ndio lenye nguvu ya kuamua hivyo.

  Na chochote kinachoamuliwa na tume iliyo independently lazima kipitishwe wizara husika na tume yao na wao waichambue kabla ya serikali kuamua kufanya hiyo repoti hiwe 'white paper' na ndio majadiliano yaingie bungeni.

  Tume ya wizara aina maana ya kuwa na wafanyakazi wa wizara husika pekee, bali lazima hiwe na wabunge wa pande zote kwenye mchakato wa kutunga policy au sheria. na wabunge huchaguliwa kutokana na background zao (proffesions or understanding) kuwakilisha kila tume ya bunge. Baada ya hapo depending on topic tume inachagua baadhi ya wanajamii watakao waona wana faa kuwakilisha jamii nzima hili mchakato huwe fair na pande zote zisikilizwe.

  Ndio maana nchi za wengine unaona upinzani, mashirika ya biashara, religious institutes au chochote bunge inachojadili kinaweza kuwa kinapigiwa kelele kama kundi fulani ndani ya committee ikiona kuna mabavu fulani ambayo serikali inataka weka ndani ya white paper kinyume cha matakwa yao. Na mara nyingi haya makundi hupata habari kutoka kwa wahusika wao waliopo ndani ya parliamentary committee.

  well that is the political side of things kwenye kujaribu kuelezana tofauti kati ya hizo tume mbili.
   
 9. afroPianist

  afroPianist Member

  #9
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  The premises above are well argued and have some strong points..so what is the way forward for now? Should we just sit and hope that the President will "hand pick" the right people that will sincerely represent our voices
   
 10. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #10
  Jan 1, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  The president can select whomever he chooses, reading from other posts i think he mentioned something like an established lawyer on the matter for his part, to lead the committee.

  On our part before it goes to parliament the opposition should be sure they send the right people from the members of the parliament and make sure they select the right voices from the nation because that is where it really matters.
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Yeye JK amempataje?

  Kazi za serikalini ni kutangazwa kwenye magazeti na waombaji kujitokeza, kuchujwa na halafu washindi kupewa majukumu..................huu ndiyo utaratibu shirikishi................mingine yote ni ubabaishaji tu..............
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Upinzani watahakikisha vipi luwa waliochaguliwa ni "strong people" wakati hakuna ushindani.............uko dunia ipi?

  Unless there is competitive envisaged in our laws............hakuna suala la kuhakikisha wanazo sifa ni kuwa sifa ni zipi...................siyo makaratasi tu ila rekodi ya kupigania masilahi ya umma........................

  Tuna maprofesa kama Pama...............Kabudi ambao kazi yao ni kutetea serikali tu kwa minajili ya mkate wao binafsi................Kabudi ndiye aliyetumiwa na Mahakama ya Rufaa kubeza hoja nyeti ya mtikila ya Mgombea binafsi...............................

  The issue is not paper qualifications.............the issue is an unquestionable record in fighting for human rughts..................
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Wadau wote ni kujitokeza na kumwambia JK kuwa...............man your out of touch with Tanzanian constitutional aspirations.............................What we need is a bunge owned process that is fully legislated and devoid of executive machinations................as we are witnessing just now...............................

  Siyo kazi ya Raisi kuteua Tume ya kukusanya maoni ya Katiba Mpya.........labda ingelikuwa ni ya viraka hapao sawa.....................

  Kenya Bunge lilunda Tume na wajumbe wake walipatikana kwa utaratibu wa uwazi wa nafasi kutangazwa magazetini, wagombea kujitokeza, kamati husika ya Bunge kuwachuja na kuwafanyia zoezi la kuwasaili........................Raisi kazi yake ilikuwa kuwathibitisha tu mapendekezo yaliyopitishwa na Bunge..........................................

  katiba mpya maana yake ni Bunge kuthibiti utawala na hili haliwezi kuanza kama uteuzi nyeti kama huu Raisi anaufanya kiholela holela tu bila kuanzia kwenye hilo Bunge lenyewe............................It will be a faulty start....................to good governance..........
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Kikwete: Ni mwaka wa Katiba mpya Friday, 31 December 2010 20:58

  Neville Meena na Fedy Azzah
  Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuanza mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya. Katika salamu zake za mwaka mpya kwa Taifa jana, Rais Kikwete alisema "...nimeamua kuunda Tume maalum ya Katiba, yaani Constitutional Review Commission. Tume hiyo itakayoongozwa na mwanasheria aliyebobea, itakuwa na wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali katika jamii yetu kutoka pande zetu mbili za Muungano".

  Alisema jukumu la msingi la Tume hiyo litakuwa ni kuongoza na kuratibu mchakato utakaowashirikisha wananchi wote vikiwemo vyama vya siasa, wanasiasa, wafanyabiashara, asasi za kiraia, mashirika ya dini, wanataaluma na makundi mbalimbali ya watu wote, katika kutoa maoni "wayatakayo kuhusu Katiba ya nchi yao".

  Kwa mujibu wa Rais Kikwete, baada ya kukamilisha kukusanya maoni, Tume itatoa mapendekezo yake yatakayofikishwa kwenye vyombo stahiki vya Kikatiba kwa kufanyiwa maamuzi. "Baada ya makubaliano kufikiwa, taifa letu litapata Katiba mpya kwa siku itakayoamuliwa ianze kutumika,"alisema Rais Kikwete.

  Rais alisema lengo la kuandikwa kwa Katiba mpya ni kuiwezesha nchi kuwa na Katiba inayoendana na taifa lenye umri wa nusu karne na kwamba mchakato huo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara na kwamba Katiba inayokusudiwa ni ile itakayolipeleka taifa miaka 50 ijayo kwa salama, amani, umoja na kuwepo maendeleo makubwa zaidi.

  "La nne ambalo tulilokubaliana kufanya ni kuanzisha mchakato wa kuitazama upya Katiba ya Nchi yetu kwa lengo la kuihuisha ili hatimaye Katiba yetu ya sasa tuliyoachiwa na waasisi wa taifa letu, imeifanyia nchi yetu mambo mengi mazuri na kuifikisha Tanzania na Watanzania hapa tulipo," alisema KIkwete na kuongeza:

  ".....mwaka 2011, nchi yetu inatimiza miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, miaka 47 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar na miaka 47 ya Muungano wa nchi zetu mbili. Yapo mabadiliko mengi yaliyotokea katika nyanja mbalimbali za maisha ya nchi yetu na watu wake katika kipindi hiki. Kwa ajili hiyo ni vyema kuwa na Katiba inayoendana na mabadiliko na matakwa na hali ya sasa".

  Alisema ana matumaini kwamba mchakato huo utaendeshwa kwa amani na utulivu kama ilivyo sifa ya Tanzania na mazoea yetu ya kujadiliana bila kugombana.

  "Wananchi watapewa fursa ya kutosha ya kutoa maoni yao kwa uhuru na pawepo kuvumiliana kwa hali ya juu pale watu wanapotufautiana kwa mawazo,"alisema Rais Kikwete na kuonya kuwa pasiwepo kutukanana, kudharauliana, kushutumiana, kubezana, kuzomeana wala kushinikizana.

  "Naomba washiriki waongozwe kwa hoja badala ya jazba. Tukiwa na jazba, hasira na kushinikizana kamwe hatutaweza kutengeneza jambo jema. Na inapohusu Katiba ya Nchi itakuwa hasara tupu. Haitakuwa endelevu na kulazimika kufanyiwa marekebisho mengi mwanzoni tu baada ya kutungwa,"alisema.

  Alitoa wito kwa Watanzania wenye maoni yao kujiandaa kushiriki kwa ukamilifu katika mchakato huo na kutoa maoni ambayo yatawezesha nchi kuwa na Katiba itakayokidhi matakwa ya sasa na ya miaka 50 ijayo.

  Tangazo la Rais Kikwete kuhusu kuanza kwa mchakato wa kuandikwa kwa upya kwa Katiba, ni faraja kwa makundi mbalimbali ya kijamii ambayo tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu, Oktoba 31, 2010 yamekuwa yakitoa wito wa kaundikwa kwa Katiba mpya.

  Moto wa kudai katiba mpya, uliwashwa na Chadema Novemba mwaka jana, baada ya kutangaza kutotambua kura zilizomweka madarakani Rais Kikwete. Kutokana na hali hiyo, chama hicho kilianza mchakato wa kushikiza kuundwa kwa katiba mpya kwa kususia hotuba ya Rais Kikwete wakati wa akizindua Bunge la Kumi.

  Pia wabunge pamoja na viongozi wa chama hicho walisusia sherehe za kuapishwa kwa Rais. Katika kuendeleza madai hayo, hizi karibuni mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chadema John Mnyika aliwasilisha hoja binafsi kwenye Ofisi za Bunge, hoja iliyokuwa na lengo la kudai katiba mpya.

  Hivi karibuni pia, CUF walifanya maandamano ya kuwasilisha rasimu ya katiba mpya kwa waziri wa Katiba na Sheria. Pia viongozi mbalimbali wastaafu, walipo madarakani wamekuwa wakieleza umuhimu wa kuwa na Katiba mpya.

  Miongoni mwa waliojitokeza adharani na kuunga mkono uwepo wa katiba mpya ni pamoja na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, mawaziri wakuu wa zamani, Joseph Warioba na Frederick Sumaye , Jaji Mkuu Mstaafu na Agostino Ramadhani, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Jaji Omar Makungu pamoja na waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye aliahidi kumshauri Rais juu ya suala la kuundwa kwa Katiba mpya.

  Madai ya Katiba mpya pia yamewahi kutolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa ambaye alisema bayana kuwa katiba mpya iandikwe mapema kabla ya mambo kuwa mabaya, akitoa mfano wa mapungufu ya katiba ya sasa kuwa ni rais kupewa madaraka makubwa.

  Lakini akiwa Ikulu kwenye hafla ya kuapishwa Jaji Mkuu Mpya, Mohamed Othman Chande, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Frederick Werema, alisema kuwa haona haja ya kuandikwa katiba mpya badala yake katiba iliyopo, iwekewe viraka.

  "Kuandika Katiba mpya hapana, lakini kufanya marekebisho kwa kuondoa au kuongeza mambo fulani kwenye katiba, ruksa," alisema Jaji Werema.

  Wakati huohuo, Rais Kikwete ameutangaza mwaka 2011 kuwa mwaka wa maadhsimisho ya miaka 50 ya Uhuru ambayo kilele chake kitakuwa tarehe 9 Desemba, 2011 ambapo kutafanyika sherehe kubwa na za aina yake nchi nzima na wananchi kushirikishwa kikamilifu.

  "Kwa kutambua umuhimu wa aina yake wa maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Desemba, 2011, tumekubaliana na viongozi wenzangu serikalini kuwa tusherehekee siku hiyo kwa uzito unaostahili," alisema.

  Kadhalika Rais alisema jambo jingine ni kufanyika kwa tathmini ya kina ya mafanikio tuliyoyapata na tahmini hizo kuandikwa katika vitabu ili kuhifadhi kumbukumbu hizo muhimu kwa vizazi vijavyo.

  "Vitabu na nyaraka hizo vitakuwa kumbukumbu zenye manufaa makubwa kwa wenzetu watakaokuwepo mwaka 2061 wakati wa kusherehekea miaka 100 ya Uhuru wa Tanzania Bara" alisema na kuongeza kuwa pia yatafanyika maonyesho maalum katika Uwanja wa Maonyesho wa Julius Nyerere, Dar es Salaam na kote mikoani kwenye viwanja vya maonyesho, kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali katika miaka 50 tangu Uhuru wa Tanzania Bara.
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  JK aridhia Katiba Mpya

  Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 31st December 2010 @ 23:59 Imesomwa na watu: 538; Jumla ya maoni: 0


  [​IMG]  BAADA ya malumbano, mijadala, maandamano na kauli za hapa na pale kudai uundwaji wa Katiba Mpya, hatimaye Rais Jakaya Kikwete amesikia na ameunda Tume maalumu ya Katiba.

  Tume hiyo kwa mujibu wa Rais, itaongozwa na mwanasheria aliyebobea na kuwa na wajumbe kutoka makundi mbalimbali ya jamii za pande zote mbili za Muungano.

  Hayo yamo katika hotuba ya salamu za Rais Kikwete aliyoitoa jana kwa Taifa katika kuaga mwaka 2010 na kukaribisha mwaka mpya wa 2011.

  "Jukumu la msingi la Tume hiyo litakuwa ni kuongoza na kuratibu mchakato utakaoshirikisha wananchi wote bila kubagua, vyama vya siasa, wanasiasa, wafanyabiashara, asasi za kiraia, mashirika ya dini, wanataaluma na makundi mbalimbali ya watu wa nchi yetu kote nchini, katika kutoa maoni yao juu ya yatakayohusu Katiba ya nchi yao," alisema Rais katika hotuba yake.

  Alisema baada ya kukamilisha kukusanya maoni, Tume itatoa mapendekezo yake yatakayofikishwa kwenye vyombo stahiki vya kikatiba kwa kufanyiwa uamuzi.

  "Baada ya makubaliano kufikiwa, Taifa letu litapata Katiba mpya kwa siku itakayoamuliwa ianze kutumika," alisema Rais.

  Alieleza matumaini yake kwamba mchakato huo utaendeshwa vizuri, kwa amani na utulivu kama ilivyo sifa ya nchi na mazoea ya kujadiliana bila kugombana, ambapo wananchi watapewa fursa ya kutosha ya kutoa maoni yao kwa uhuru na kwa uvumilivu wa hali ya juu pale watu wanapotofautiana kwa mawazo.

  "Pasiwepo kutukanana, kudharauliana, kushutumiana, kubezana, kuzomeana wala kushinikizana.

  Naomba washiriki waongozwe kwa hoja badala ya jazba. Tukiwa na jazba, hasira na kushinikizana kamwe hatutaweza kutengeneza jambo jema.

  "Na inapohusu Katiba ya nchi, itakuwa hasara tupu. Haitakuwa endelevu na kulazimika kufanyiwa marekebisho mengi mwanzoni tu baada ya kutungwa.

  Nawaomba Watanzania wenzangu wenye maoni yao, wajiandae kushiriki kwa ukamilifu katika mchakato huu," alisema.

  Rais alisema uamuzi huo unatokana na makubaliano yaliyofikiwa kati yake na viongozi wenzake kufanywa, hili la Katiba likiwa ni moja miongoni mwa mambo manne yaliyokubaliwa.

  Aliyataja mengine kuwa ni kuutangaza mwaka 2011 kuwa wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, ambayo kilele chake kitakuwa Desemba 9, ambapo kutafanyika sherehe kubwa na za aina yake nchi nzima na wananchi kushirikishwa kwa ukamilifu.

  Pili, kufanyika tathmini ya kina ya mafanikio yaliyopatikana nchini, katika juhudi za wananchi kujiletea maendeleo katika miaka hiyo 50.

  "Kila wizara, idara na taasisi za Serikali na hata sekta binafsi, zifanye tathmini ya eneo lake. Tathmini hizo ziandikwe katika vitabu ili kuhifadhi kumbukumbu hizo muhimu kwetu na kwa vizazi vijavyo," aliagiza.

  Alisema vitabu na nyaraka hizo vitakuwa kumbukumbu zenye manufaa makubwa kwa watakaokuwapo mwaka 2061 wakati wa kusherehekea miaka 100 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

  Pia ilikubalika yafanyike maonesho maalumu katika Uwanja wa Maonesho wa Julius Nyerere, Dar es Salaam na mikoani, kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali katika miaka 50 tangu Uhuru wa Tanzania Bara.

  Na lingine ndilo la mchakato wa kuitazama upya Katiba ya nchi kwa lengo la kuihuisha ili hatimaye kuwa na Katiba inayoendana na Taifa lenye umri wa nusu karne.

  "Katiba yetu ya sasa tuliyoachiwa na waasisi wa Taifa letu, imeifanyia nchi yetu mambo mengi mazuri na kuifikisha Tanzania na Watanzania hapa tulipo.

  "Tuna nchi moja huru, ya kidemokrasia na inayoendesha mambo yake kwa kuzingatia utawala wa sheria, kuheshimu haki za binadamu na mgawanyo wa madaraka miongoni mwa mihimili mikuu ya Dola.

  Nchi yenye amani, utulivu na watu wake ni wamoja, wanaopendana na kushirikiana na maendeleo yanazidi kupatikana," alisema.

  Hata hivyo, aliwahadharisha Watanzania kuacha kupoteza muda muhimu wa kujiendeleza na badala yake kugeuzwa ‘mbuzi wa kafara' kwa ajili ya kuendeleza maslahi ya kisiasa ya watu fulani.

  "Najua wapo baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa ambavyo vimepanga mikakati ya kuendeleza malumbano ya uchaguzi na kutaka Watanzania waishi kama vile nchi ipo kwenye kampeni za uchaguzi.

  "Wamepanga wakati wote kutafuta jambo au hata kuzua jambo, ili kuwachochea wananchi waichukie Serikali.

  Wamepanga kuchochea migomo vyuoni na maandamano ya wananchi mara kwa mara. Kwao huo ndiyo mkakati wa kujijenga kisiasa, ili kujiandalia ushindi kwenye uchaguzi wa mwaka 2015," alisema.

  Alikumbusha kuwa uchaguzi ulishaisha Oktoba 31, na malumbano ya kampeni za uchaguzi yalimalizika wakati huo. Sasa ni wakati wa kuendelea kufanya shughuli za kawaida za kujiletea maendeleo.

  "Kuendeleza malumbano na kuendelea kuishi kama vile kampeni za uchaguzi bado zinaendelea si sahihi hata kidogo.

  Kwa jinsi watu hao walivyokuwa wabinafsi na wasivyokuwa na huruma na wenzao, wako tayari kuchochea ghasia bila kujali madhara yatakayowakuta watu watakaoshiriki," alisema.

  Alisema wanachotaka ni ghasia kutokea na vyombo vya Dola kuingilia kati ili waiambie Jumuiya ya Kimataifa jinsi Serikali ilivyo katili.

  "Nawasihi ndugu zangu msiwasikilize wala kuwafuata wanasiasa hawa. "Nawaomba, wakiwafuata wakumbusheni kuwa wao wana fursa nyingi za kusema wayatakayo bungeni na kwingineko, waache kuwatumia kama chambo au wahanga wa maslahi yao," alisisitiza.

  Akifafanua kuhusu uchaguzi, alisema ulikuwa na ushindani mkali na nguvu ya vyama vya upinzani iliongezeka na kwamba ni jambo jema kwa utawala bora na uwajibikaji nchini.

  "Bila shaka Bunge litachangamka kama tunavyotarajia sote. Nimewakumbusha mawaziri wajibu wao wa kuwa makini na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi bungeni.

  Kwa upande wa Chama tawala, hatuna budi kujipanga na kujijenga upya kwa kuzingatia mazingira mapya ya kisiasa nchini," alisema.

  Kuhusu umeme, alisema mwaka jana haukuwa na utulivu wa kutosha kwa upatikanaji wa umeme kwani mara kadhaa yalikuwapo matukio ya kukatika na mgawo wa umeme, kutokana na uharibifu wa mitambo ya kuzalisha umeme hasa katika kituo cha Songas na vituo vya Tanesco.

  Alisema kwa sasa Tanesco ina mipango kadhaa inayoendelea nayo ya kuongeza uzalishaji wa umeme nchini ambapo kwa msaada wa Serikali, ndani ya miezi 12 ijayo, Tanesco itaongeza uzalishaji wa umeme kwa megawati 160, (100 Ubungo kwa kutumia gesi asilia na 60 Mwanza kwa kutumia dizeli nzito).

  Alisema kwa kushirikiana na sekta binafsi pia, ndani ya miezi 36 ijayo Tanesco wanatarajia kukamilisha ujenzi wa vituo vya umeme Kinyerezi (megawati 240) Somanga Fungu (230) na Mtwara (300).

  Inatarajiwa pia kwamba katika kipindi hicho mradi wa kuzalisha megawati 200 Kiwira utakamilika. Kuhusu bei ya umeme, alisema anatambua kuwapo mazungumzo katika jamii kuhusu uamuzi wa Ewura wa kukubali ombi la Tanesco kuongeza bei ya umeme.

  "Wakati mwingine mazungumzo yamekuwa na hisia kali na hata jazba kutawala". Alisema Wizara, Tanesco na Ewura wameeleza kwa ufasaha misingi iliyotumika mpaka kufikia uamuzi huo. "Sina maelezo mazuri zaidi ya hayo.

  Ninachotaka kusema ni kuwaomba Watanzania wenzangu kutokubali suala hili la kibiashara na kiuchumi, kugeuzwa kuwa la kisiasa na kutafutiwa majawabu ya kisiasa".

  Aliwaomba Watanzania waamini na kukubali maelezo ya Tanesco na Ewura kwamba katika miaka minne hii gharama za uendeshaji, uzalishaji, usafirishaji na usambazaji umeme zimepanda kama zilivyopanda katika shughuli nyingine.

  "Hivyo basi, kutaka bei ya umeme ibaki kama ilivyokuwa miaka minne iliyopita hautakuwa uamuzi sahihi kiuchumi na kibiashara kwa Tanesco."

  Aliwatakia wananchi mafanikio mema katika shughuli za kujiletea maendeleo na kuendeleza hali zao za maisha na Heri ya Mwaka Mpya.
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Kikwete forms constitution team

  By DAILY NEWS Reporter, 31st December 2010 @ 16:00, Total Comments: 0, Hits: 244

  PRESIDENT Jakaya Kikwete on Friday broke his silence on constitutional reform saying that he has formed a Special Commission to oversee the required review following a heated national debate on the matter.

  In his New Year's message welcoming 2011, President Kikwete said that the commission would be headed by a competent lawyer and comprises representatives of all sections of the society from both sides of the Union.

  Recently political parties, academicians, religious organizations and a cross section of the public have been engaged in a hot debate of whether the current constitution should be overhauled, amended or remain untouched.

  The president's stance comes few days after Prime Minister Mizengo Pinda told editors that he would personally initiate the process by advising the president to form a panel to oversee the process of reviewing the constitution.

  "The primary function of the commission will be to oversee and co-ordinate the process that will involve all people without discriminating political parties, businessmen, community based organizations, religious organizations, academicians and other people within and outside the country," the president declared.

  According to him, upon completion of receiving recommendation, the commission will submit its report to relevant constitutional organs for further decisions.

  "After reaching an agreement, our nation will have a new constitution to be applicable on an agreed date," President Kikwete told the nation in his speech broadcast by TV and radio stations on Friday evening.

  "Our existing constitution, which was acquired from our founders, has done a lot of good things and has brought us and the nation here. We've got one independent country, with mature democracy, good governance and stable rule of law.

  Ours is a country with peace, harmony and political stability whose people live in peace and love," noted the president. He warned, however, that members of the public should not be used as sacrificial lambs by some politicians.

  The president was optimistic that the process would be conducted in an atmosphere of peace, harmony and sobriety to enable all people to air their views despite diversity of opinions.

  He cautioned that undue pressure, emotions and hatred should not prevail during the process as such approach may cost the country and render the whole process meaningless and costly.

  President Kikwete said that the decision to allow the process was one of four key decisions reached by him and other leaders. He mentioned other decisions as the 50th anniversary of of independence to be held this year.

  The decisions also include an indepth assessment of achievements made in the past 50 years and special trade fairs to be held at Mwalimu Nyerere Trade Fair grounds in Dar es Salaam and throughout the country to showcase achievements made in the past 50 years of the independence.

  On power tariffs, the president asked the public to accept new arrangements due to the prevailing commercial and economic situation. He called on them to ignore politicians who had politicized the tariff hike.

  Mr Kikwete told the nation that within the next 12 months, Tanesco will increase power output by 160MW and in the next 36 months the effort will see another 970MW from various power projects.

  The president finally wished all the 'wananchi' a happy and prosperous New Year.
   
 17. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #17
  Jan 1, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kaka

  Kama kuna matatizo ya naivity sasa hawa upinzani wanaoleta madai ya katiba mpya wanatumia mistari hipi ya kusema yote iliyopo haifai, hivyo mpya pekee ndio itakayo saidia? surely the're not that stupid.

  pili tume ya raisi si bunge, bunge ndio lenye kupitisha chochote kabla ya kuwa sheria. Na mara nyingi kwenye demokrasia mchakato wa sheria au policy au katiba bunge uteuwa baadhi ya wapinzani kupigizana kelele na wao hili kuhakikisha kunakuwa na usawa as much as possible.

  Ni wao wabunge waliopo kwenye tume ya serikali (au bunge), pamoja na wanajamii muhimu waliochaguliwa ndio wanaoweza kuona mapungufu mapema wakati bado report inaandaliwa au sheria inaundwa sasa kama hawajui wanachokifanya huko na kutujuza watanzania tusiikubali sijui niseme nini tena. Hila bunge ndio lenye kupitisha hivi vitu mathematically upinzani unashindwa by votes.

  Na wao kama hawakuikubali wanaweza anza upya kutuletea hasira ya kuwa jamaa amna walichobadilisha hivyo tusiikubali watu waanze fujo upya tena. Hila kama hawajui nini wanakitaka kutoka kwa serikali na chance wanapewa kwa namna ya kushirikishwa kabla ya serikali kutoa white paper then i dont know how i can contribute in this thread in terms of political democracy process.

  Asubuhi njema.
   
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  You have done well..........................hakuna uwazi na ushirikishwaji wakati process is already owned by the executive.........................it is morally wrong to call it an inclusive process when only one person claims he has included all stakeholders.............constitutional process must be seen and perceived to have been owned by the electorate through their representatives in the House.................
   
 19. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #19
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  JK acts on constitution
  By The guardian team  1st January 2011  [​IMG] Forms special Review Commission to oversee the process
  [​IMG] Asks public to understand need for new electricity tariffs  [​IMG]
  President Jakaya Kikwete


  p { margin-bottom: 0.08in; }
  President Jakaya Kikwete said yesterday Tanzania needed a new constitution to march with the country's 50 years of nationhood.
  In his end-of-the year address to the nation, Kikwete said: "We, in the government, have agreed to lead the process for the constitution review in order to come up with a document that accommodates the current dynamics and developments."
  He said in fast-tracking the process he had formed a special Constitutional Review Commission. He said the body, which is led by the Attorney General, comprises members from different groups from both sides of the union - Zanzibar and Mainland.
  According to the president, the commission has been tasked to oversee the constitutional review processes by collecting views of social groups, political parties, business people, civil societies, religious organizations and experts.
  After collecting stakeholders' inputs, he said, the commission will give its recommendations which will be forwarded to the relevant organs for decision-making.
  "After these processes, the nation will have a new constitution," he noted, adding: "We want to have constitution that matches with the 50-years-old nation (Tanzania)."
  This year, Tanzania will mark 50 years of Tanganyika's independence, 47 years of the Zanzibar Revolution and 47 years of the Union.
  Kikwete, however, defended the current constitution engineered by the founders of the nation saying it moved the country from the post-independence period to "where we are now."
  The existing constitution, he said, contributed to the country's social, political and economic development.
  "But there are many changes that have occurred between the post-independence days and today, which require a constitution that accommodates all current developments and changes," said the president.
  The President's stance on the constitution has come at a time when the country was engulfed in heated debate over whether it should have a new constitution or not.
  Attorney General Frederick Werema's recent remarks that the country did not need a new constitution have been received with mixed feelings with a section of the public accusing him of trying to strangle debate on the issue.
  At one time, Constitutional Affairs and Justice Minister, Celina Kombani, played down public demand for new constitution on the simple reasons that "the process is unnecessarily expensive.
  Kombani's provoked heated public debates, with some people calling for resignation of the constitutional affairs' minister, accusing her of undermining concerns of Tanzanians for constitutional reforms.
  Prime Minister, Mizengo Pinda recently in a meeting with editors, promised to advise the president on the need to have new constitution.
  Dwelling on the country's security, President Kikwete said the situation was stable with all borders safe and secure and that there was no threat from any place or people regarding the security of the country.
  On democracy, President Kikwete said it has grown tremendously, admitting that opposition parties were becoming stronger and therefore posing a challenge to the ruling party.
  "Last year's general election posed great challenge and the power of opposition parties has increased tremendously," admitted the president.
  On the management of public funds, Kikwete said he had directed concerned authorities to ensure they supervise revenue collection and expenditure of public funds more efficiently.
  "I am not satisfied with the use of public funds. The discipline in this is still wanting," he commented.
  On the economy he said the country expected the economy to grow by up to 7.2 per cent compared to 6 per cent of 2009.
  He said inflation has also gone down from 12.1 per cent in 2009 to 5.5 per cent 2010 and it was expected that it would continue to go down.
  On agriculture and food, the president said the food situation was good in 2010, but could not be sure it would stay the same this year. He noted that short rains which farmers use to supplement food crop production had failed in some areas, while they were late in the Southern Highland regions which are the country's food granary.
  On the hike of electricity tariff granted to the Tanzania Electric Supply Company by the Energy and Water Utility Regulatory Authority, the president said the decision had been carefully weighed to ensure that the public did not bear unnecessary burden while Tanesco was protected from running its business at a loss.
  He warned against turning the issue into a political one.  SOURCE: THE GUARDIAN
   
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Jan 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Kahama MP says new constitution long overdue
  By Lusekelo Philemon  1st January 2011
  [​IMG]
  Kahama lawmaker James Lembeli


  p { margin-bottom: 0.08in; }
  Kahama lawmaker James Lembeli yesterday has said that Tanzania needs a new constitution which will meet the current people's needs.
  Apart from constitutional needs, the outspoken MP asked the government and other relevant authorities to ensure that the suspects linked to grand corruption scandals be taken to court, irrespective of their status.
  He made the remarks here when talking to journalists from different media outlets.
  The parliamentarian expressed his fear, saying corrupt people, if they were not swiftly delt with by being taken to court, would mar the drafting of the country's constitution because of their influence in the government and the ruling party.
  In his view, the current constitution had a number of shortfalls, hence the need to be drafted afresh to suit the current people's demands.
  He said Tanzania was no longer a socialist country as it was before, hence there was an urgent need to draft a new constitution to reflect the current situation.
  Lembeli urged the government to open its eyes and listen to people's outcry, saying a constitution was for the people and not animals.
  "There is no need to be blind on this. It is high time Tanzania came up with a new constitution which will suit the interests of many people," he said, adding:
  "By remaining silent on this it means that the government is trying to instigate unnecessary chaos."
  He said top government leaders were there for public interest, hence they should be working in the people's interests and not in their own interests.
  "The issue of a new constitution needs no debate; the people have waited for too long for it. So, this time around is the chance to act and change the current constitution which gives room to corrupt people."
  He said corrupt people have been destroying the country in various ways as they have the money to anything they want. He however warned that the war on corruption would not cease until Tanzania was free from the vice.
  Lembeli is one of CCM parliamentarians crusading against corruption.  SOURCE: THE GUARDIAN
   
Loading...