BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,099
Kuna faida gani ya kukumbatia wazee ndani ya chama kama hawasikilizwi? Warioba, Kawawa, Butiku, Mwinyi na wengi wengineo wametoa ushauri wao kuhusu katiba mpya na kupambana na mafisadi ndani ya chama, lakini kauli zao zimedharauliwa. JK acha usanii wa kuwapaka wazee mafuta ya mgongo!!!
JK aeleza umuhimu wa wazee katika CCM
Mwandishi Wetu
Daily News; Tuesday,June 24, 2008 @00:03
Rais Jakaya Kikwete amesema wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wana nafasi ya kukitumikia chama hicho kwa kutoa ushauri na kukilea kisitoke nje ya mstari wa kanuni zake.
Rais Kikwete aliyasema hayo Ikulu Dar es Salaam, jana alipozungumza na waasisi wa CCM wa Mkoa wa Mara waliofika kumtembelea na kumshukuru kwa kufanikisha ziara yao ya kutembelea sehemu mbalimbali za kumbukumbu na historia Tanzania Bara na Visiwani.
Nyinyi mnakijua chama vizuri zaidi kuliko vijana, mchango wenu hauwi na maslahi yoyote bali ni mchango wa dhati na mapenzi kwa chama, nyie mnayo nafasi kubwa ya kukisaidia na kukiweka chama kwenye mstari na kurudisha maslahi ya wanachama wake, alisema.
Wazee hao 17 wakiongozwa na Ramadhan Mawazo, tayari wametembelea Arusha kuona kumbukumbu za Azimio la Arusha, Dar es Salaam ambako wamemtembelea Mzee Rashid Kawawa na Zanzibar ambako walitembelea kaburi la Hayati Abeid Amaan Karume, majengo ya kihistoria na Mji Mkongwe.
Kesho wanatarajiwa kutembelea Dodoma ambako watapata fursa ya kuona shughuli zinavyoendeshwa bungeni. Katika risala yao wazee hao wamemshukuru Rais Kikwete kwa kufanikisha ziara yao na baadaye katika mazungumzo yao wamemuomba awasaidie kuendeleza chama chao cha kuweka na kukopa ambacho kinakabiliwa na matatizo ya kukopesheka kwa sababu ya umri wao.