JK adanganywa tena, azindua bwawa wakati kesi iko mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK adanganywa tena, azindua bwawa wakati kesi iko mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jul 3, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  RAIS Jakaya Kikwete amezindua mradi wa Bwawa la Manchira lililoko wilayani Serengeti wakati tayari wananchi wamekwishafungua kesi Mahakama Kuu ya Mwanza wakidai fidia. Kesi hiyo iliyofunguliwa ni matokeo ya viongozi wa serikali wilayani hapa kuhusika kuwalipa fidia watu wasiohusika na kuwaacha walengwa waliofanyiwa tathmini.

  Kesi hiyo ya madai namba 21/2009 ilifunguliwa katika Mahakama Kuu ya Mwanza kitengo cha ardhi chini ya Jaji Nyangarika inahusisha wananchi 77 ambao wanadai kiasi cha Sh2 bilioni.

  Mmoja wa wawakilishi wa wananchi hao, Jackson Mwita aliwaambia waandishi wa habari wakati wakimsubiri Rais Kikwete bwawani hapo kuwa kutokana na fedha walizotakiwa kuwalipa wahanga wa mradi huo zililipa watu wasiokuwa na maeneo huku uongozi wa serikali ukiwapuuza walalamikaji.

  Alisema kuwa wanashangaa mradi huo kuzinduliwa kwa mbwembwe wakati tayari Halmashauri imefikishwa mahakamani na wameitwa mara tatu bila kuhudhuria mahakamani.

  “Tulipanga kumfikishia Rais ujumbe kwa njia ya mabango, ajue kuwa kadanganywa maana eneo lina mgogoro, lakini tumetishwa maana leo anafungua kesho akasikia amri tofauti atabaki kujiuliza kwa kuwa wasaidizi wake si wa kweli,”alisema Mwita.

  Hata hivyo, wananchi hao baada ya kutishwa kupitia wenyeviti wa vitongoji ambao inadaiwa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Edward Ole Lenga alikutana nao usiku na kuwataka wahakikishe wananchi hawatoi mabango, walifikisha kilio chao kwa waandishi wa habari.

  Wananchi hao walidai kuwa wamechoshwa na kunyanyaswa na mkuu wa wilaya hiyo hasa wanapofuatilia haki zao kwa madai kuwa hawatapata chochote na watatembea hadi soli za viatu ziishe kwa lengo la kupata haki zao.

  Wakati huo huo katika hali isiyo ya kawaida na ambayo imezua maswali mengi ni kitendo cha mkuu wa wilaya hiyo kuamuru mwandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo mkoani hapa, Augustine Mgendi kukamatwa kwa madai kuwa alikuwa akiwachochea wananchi waandike mabango kuhusu malalamiko yao.

  Kitendo hicho kinadaiwa kililenga kuwanyamazisha wananchi na waandishi wasiibue uozo huo ambao umeishagharimu serikali karibu Sh 2 bilioni kwa ajili ya fidia, fedha ambazo zinaishia mikononi mwa wajanja na kuwaacha walengwa.

  Hata hivyo, mwandishi huyo aliachiwa baada ya kuhojiwa kwa saa zaidi ya nne na Jeshi la polisi na ikiwa ni pamoja na juhudi za waandishi kufuatilia kwa karibu. Hata hivyo, hakufunguliwa jalada.

  Kwa zaidi ya mara mbili serikali imeishatoa fedha kwa ajili ya kulipa fidia wananchi hao, malipo ambayo yanadaiwa kutawaliwa na ufisadi kwa baadhi ya viongozi kujiingiza ndani na kuwalipa wasiokuwa na maeneo na ambao wengi ni wafanyabiashara.

  Kwa mara zote hizo mbili msimamizi mkuu wa malipo hayo ni mkuu wa wilaya hiyo na timu yake.

  Akizindua mradi huo uliogharimu zaidi ya Sh10 bilioni, Rais Kikwete alisema kuwa ametimiza ahadi yake aliyoitoa wakati anagombea urais 2005 ya kukamilisha bwawa hilo.

  Alisisitiza utunzaji wa bwawa hilo utasaidia uhai wake kuendelea kwa muda mrefu, kwa kuwa likitunzwa vema huenda likadumu kwa zaidi ya miaka 50.

  “Kuoga, kunywesha mifugo humo ni marufuku kwa kuwa maji hayo yanatumika kwa ajili ya kunywa na serikali kwa sasa ina mpango wa kuhakikisha inajenga mtambo wa kutibu na kusafisha maji,”alisema Rais Kikwete.

  Alisisitiza uundaji wa kamati za maji huku akisisitiza kuwa wanawake wawe wengi, kwa kuwa miradi iliyosimamiwa na wanaume matokeo yake yamekuwa si mazuri.

  Mapema Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya akitoa taarifa fupi ya mradi huo alisema, mradi huo umejengwa kwa fedha za serikali na umegharimu Sh10.2 bilioni na lina lita za ujazo milioni 14.2

  Hii si mara ya kwanza kudanganywa kwani rais ameshadanganywa zaidi ya mara kumi mojawapo ikiwa ni ile ya kudanganywa kwamba, Daraja la Mkenda lililopo Ruvuma ambalo ni njia muhimu kuelekea Msumbiji, lilikuwa limekamilika.

  Kutokana na hali hiyo, Rais alilazimika kukatisha safari yake mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Monica Mbega, (wakati huo) ambaye alionekana pia kutofika katika daraja hilo kabla.

  Katika tukio jingine, Rais aliwahi kupewa taarifa zisizo sahihi kuhusu tuhuma za rushwa zilizokuwa zikimkababili Anatory Choya kisha akamteua kuwa Mkuu wa Wilaya, lakini siku siku chache baadaye akafunguliwa mashitaka na Takukuru.

  Mwaka jana, akiwa ziarani Mbeya Rais msafara wake ulishambuliwa kwa mawe na watu, lakini wasaidizi wake wakaja kutoa taarifa kwamba watu hao walikuwa ni wahuni na walikuwa walimsubiri Rais kwa muda mrefu bila mafinikio.

  Hata hivyo, baadaye uchunguzi huru ulibainisha kwamba tukio hilo lilikuwa na mafungamano ya kisiasa na makovu ya mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM kwa mwaka 2005.

  Mlolongo huo mrefu wa upotoshaji taarifa kwa Rais uliibuka tena katika utoaji wa magari ya misaada, ambako badala ya kupewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Longido alipewa wa Ngorongoro.

  Tukio hilo lilimfanya mkuu huyo wa nchi kufura na kumzodoa mkurugenzi huyo, lakini baadaye ikabainika mkurugenzi huyo alikwenda kutokana na makosa ya maafisa wa Ikulu.

  Katika mlolongo huo, tukio kubwa kabisa ni Rais kutia saini kwa mbwembwe Sheria ya Gharama za Fedha za Uchaguzi ambayo ilichomekwa vipengele nje ya Bunge kitu ambacho ni kinyume cha sheria.

  Tukio hilo ambalo ni la uvunjifu wa katiba, liliibuliwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa ambaye awali, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fedrerick Werema, alikanusha.

  Hata hivyo, baadaye sheria hiyo ilirudishwa bungeni na kukarabatiwa kwa mgongo wa mabadiliko ya sheria mbalimbali.

  Mei mwaka huu, Rais alipewa taarifa za upotoshaji kuhusu mazungumzo ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) na serikali, kwa kuelezwa shirikisho hilo halikuhudhuria mkutano wa saa 4:00 asubuhi kama ilivyopangwa.

  Hata hivyo, Tucta wakatoa ushahidi wa barua za mwaliko wa mkutano huo wa Aprili 22, ambazo zilikuwa mbili moja ikionyesha walitakiwa kufika katika mazungumzo Hazina saa 4:00 asubuhi na nyingine saa 8:00 mchana.

  Katika kuonyesha upotoshaji kwa Rais, wasaidizi hao walimpa barua iliyokuwa ikionyesha walipaswa kukutana saa 4:00 asubuhi huku ile ya saa 8:00 wakawa wameificha.

  Rais akizungumza na wazee wa mkoa wa Dares Salaam aliwashambulia viongozi wa Tucta hasa Naibu Katibu Mkuu Nicolas Mgaya, akimwita mnafiki, mzandiki, mchochezi na hiana.

  Wakati huo huo ahadi ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa aliyowahi kuitoa Rais Kikwete kuwa utajengwa Serengeti ameshindwa kusema utaanza lini.

  Rais Kikwete akiwa ziarani wilayani humo aliwahi kusema kuwa Serikali itajenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wilayani hapo kwa ajili ya kurahisisha usafiri kwa watalii na kukuza uchumi wa wilaya na taifa.

  Akihutubia wakazi wa mji wa Mugumu na viunga vyake wakati wa uzinduzi wa mradi wa bwawa la Manchira, Rais Kikwete alisema kuwa ahadi yake iko pale pale kuwa utajengwa.

  Alisema kuwa uwanja huo licha ya kukabiliwa na vikwazo vingi ikiwemo taarifa kutoka kwa nchi jirani kuwa kujengwa kwa uwanja huo kutasababisha nyumbu kutoa mimba kwa wingi.

  “Maneno ni mengi kuhusu uwanja huo, lakini nasema ahadi iko pale pale, tutajenga na huenda nyumbu wakaongezeka maana hayo si maneno ya kitaalam, maana wageni wanapata shida sana hapa, wanateremkia Kilimanjaro, wanakuja kwa magari, lazima tujenge,” alisema bila kufafanua ni lini.

  Kuhusu barabara ya lami kutoka Makutano hadi Tabora kupitia Hifadhi ya Serengeti alisema itajengwa kwa baadhi ya maeneo ambapo kilometa 50 ndani ya hifadhi hazitajengwa ili kuhifadhi mazingira.

  CHANZO: Gazeti la MWANANCHI
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  A stomach-blow to the head of state again!
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hivi muungwana huwa hana ka-unit kake kaupelelezi ka-kumchunguzia mambo kama haya kabla hajaj-icommit ku-officiate a function? Huyu mtu kuna siku atajikuta ana-officiate function iliyoandaliwa na majambazi!
   
 4. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  anapenda kudanganywa kutokana na jinsi alivyokuwa mkurupukaji wa kuongea kwa sifa bila utafiti binafsi.
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ka-unit kapo ila hawapo serious, wanafanya kazi kwa mazoea.
   
 6. b

  buckreef JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi hapa sioni rais kadanganywa vipi? Kama kesi iko mahakamani basi ni mahakama ndio ilikuwa na uwezo wa kusimamisha ujenzi wa bwawa hilo.

  Kama mahakama haijasimamisha ujenzi na bwawa limejengwa kwanini mnaona rais kadanganywa hapo?

  Sasa mlitaka bwawa lisifunguliwe mpaka kesi iishe hata kama hakuna amri ya mahakama kupinga kufunguliwa kwa hilo bwawa?

  Hata kama rais angejua kuna kesi mahakamani bado angeenda kuufungua tu huo mradi. Kesi ya madai haiwezi kusimamisha shughuli za serikali.
   
 7. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Huyo mkuu hapendi hii issue ya kuwa na spy Unit yakwake ili imfanyie kazi na ukisha ona ivyo ujue kuwa kuna tatizo la mawasiliano kati ya IKULU na Usalama hii ni lazima nawambieni au kuan makundi ndani ya usalama department. kwani nasema hivyo kutokana na matukio yote yaliyo tokea IKULU hatuja pata kujua ni akinanani waliwajibisha kwa makosa kama hayo yaliyotokea recently ilikuwa ni kuongeza vipengere kwenye Sheria ya uchaguzi, nyama yake ilikuwa ni magari ya hospital ati la loliyondo kumbe ni la kwingine, kauli za ajabu kuhusu wafanyakazi katika hotuba aliyo toa statistic lilikuwa wrong aliye mpa hizo nae alichemka mbaya sana.

  Hii yote ni kutokuwa makini na utendaji kazi, IKULU ni mahali ambapo wananchi hupenda kusikia kauli zikitoka huko na sasa kama zikija kwa wanachi zikiwa nazo zimechakachuliwa mmmhh hii ni mbaya sana , kama rais mpaka anafika Mgumu na huku Ikulu haijui kabisa kianchoenda fanyika ni nini inasikitisha sana,

  Ikulu inapaswa kujua kabisa mafali ya mahali rais anapo kwenda kwa ufanisi zaidi wasije chemka lakini hujiendeaga tuuu basi ndio hayo sasa yanawakuta

 8. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280

  Hao waliopeleka kesi mahakamani watapewa haki yao kweli iwapo Presida amashabariki mradi? Huoni kuna conflict kati ya mahakama , serikali na walalamikaji? Rais alikuwa na uwezo wa kuamuru kesi hii ifanyiwe fast track kama alikuwa na hamu saaaana ya kuzindua mradi wenye utata .
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Rais Jakaya Kikwete akifungua bomba la maji kushiria kuzinduliwa rasmi kwa mradi wa maji wa Mugumu- Serengeti, katika wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara jana, uzinduzi huo ulifanyika katika bwawa la Manchira. katikati ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof Mark Mwandosya

  Anthony Mayunga, Serengeti

  RAIS Jakaya Kikwete amezindua mradi wa Bwawa la Manchira lililoko wilayani Serengeti wakati tayari wananchi wamekwishafungua kesi Mahakama Kuu ya Mwanza wakidai fidia.Kesi hiyo iliyofunguliwa ni matokeo ya viongozi wa serikali wilayani hapa kuhusika kuwalipa fidia watu wasiohusika na kuwaacha walengwa waliofanyiwa tathmini.

  Kesi hiyo ya madai namba 21/2009 ilifunguliwa katika Mahakama Kuu ya Mwanza kitengo cha ardhi chini ya Jaji Nyangarika inahusisha wananchi 77 ambao wanadai kiasi cha Sh2 bilioni.

  Mmoja wa wawakilishi wa wananchi hao, Jackson Mwita aliwaambia waandishi wa habari wakati wakimsubiri Rais Kikwete bwawani hapo kuwa kutokana na fedha walizotakiwa kuwalipa wahanga wa mradi huo zililipa watu wasiokuwa na maeneo huku uongozi wa serikali ukiwapuuza walalamikaji.

  Alisema kuwa wanashangaa mradi huo kuzinduliwa kwa mbwembwe wakati tayari Halmashauri imefikishwa mahakamani na wameitwa mara tatu
  bila kuhudhuria mahakamani.

  “Tulipanga kumfikishia Rais ujumbe kwa njia ya mabango, ajue kuwa kadanganywa maana eneo lina mgogoro, lakini tumetishwa maana leo anafungua kesho akasikia amri tofauti atabaki kujiuliza kwa kuwa
  wasaidizi wake si wa kweli,”alisema Mwita.

  Hata hivyo, wananchi hao baada ya kutishwa kupitia wenyeviti wa vitongoji ambao inadaiwa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Edward Ole Lenga alikutana nao usiku na kuwataka wahakikishe wananchi hawatoi mabango, walifikisha kilio chao kwa waandishi wa habari.

  Wananchi hao walidai kuwa wamechoshwa na kunyanyaswa na mkuu wa wilaya
  hiyo hasa wanapofuatilia haki zao kwa madai kuwa hawatapata chochote na watatembea hadi soli za viatu ziishe kwa lengo la kupata haki zao.

  Wakati huo huo katika hali isiyo ya kawaida na ambayo imezua maswali mengi ni kitendo cha mkuu wa wilaya hiyo kuamuru mwandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo mkoani hapa, Augustine Mgendi kukamatwa kwa madai kuwa alikuwa akiwachochea wananchi waandike mabango kuhusu malalamiko yao.

  Kitendo hicho kinadaiwa kililenga kuwanyamazisha wananchi na waandishi wasiibue uozo huo ambao umeishagharimu serikali karibu Sh 2 bilioni kwa ajili ya fidia, fedha ambazo zinaishia mikononi mwa wajanja na kuwaacha walengwa.

  Hata hivyo, mwandishi huyo aliachiwa baada ya kuhojiwa kwa saa zaidi ya nne na Jeshi la polisi na ikiwa ni pamoja na juhudi za waandishi kufuatilia kwa karibu. Hata hivyo, hakufunguliwa jalada.

  Kwa zaidi ya mara mbili serikali imeishatoa fedha kwa ajili ya kulipa fidia wananchi hao, malipo ambayo yanadaiwa kutawaliwa na ufisadi kwa baadhi ya viongozi kujiingiza ndani na kuwalipa wasiokuwa na maeneo na ambao wengi ni wafanyabiashara.

  Kwa mara zote hizo mbili msimamizi mkuu wa malipo hayo ni mkuu wa wilaya hiyo na timu yake.

  Akizindua mradi huo uliogharimu zaidi ya Sh10 bilioni, Rais Kikwete alisema kuwa ametimiza ahadi yake aliyoitoa wakati anagombea urais 2005 ya kukamilisha bwawa hilo.

  Alisisitiza utunzaji wa bwawa hilo utasaidia uhai wake kuendelea kwa muda mrefu, kwa kuwa likitunzwa vema huenda likadumu kwa zaidi ya miaka 50.

  “Kuoga, kunywesha mifugo humo ni marufuku kwa kuwa maji hayo yanatumika kwa ajili ya kunywa na serikali kwa sasa ina mpango wa kuhakikisha inajenga mtambo wa kutibu na kusafisha maji,”alisema Rais Kikwete.

  Alisisitiza uundaji wa kamati za maji huku akisisitiza kuwa wanawake wawe wengi, kwa kuwa miradi iliyosimamiwa na wanaume matokeo yake
  yamekuwa si mazuri.

  Mapema Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya akitoa taarifa fupi ya mradi huo alisema, mradi huo umejengwa kwa fedha za serikali na umegharimu Sh10.2 bilioni na lina lita za ujazo milioni 14.2

  Hii si mara ya kwanza kudanganywa kwani rais ameshadanganywa zaidi ya mara kumi mojawapo ikiwa ni ile ya kudanganywa kwamba, Daraja la Mkenda lililopo Ruvuma ambalo ni njia muhimu kuelekea Msumbiji, lilikuwa limekamilika.

  Kutokana na hali hiyo, Rais alilazimika kukatisha safari yake mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Monica Mbega, (wakati huo) ambaye alionekana pia kutofika katika daraja hilo kabla.

  Katika tukio jingine, Rais aliwahi kupewa taarifa zisizo sahihi kuhusu tuhuma za rushwa zilizokuwa zikimkababili Anatory Choya kisha akamteua kuwa Mkuu wa Wilaya, lakini siku siku chache baadaye akafunguliwa mashitaka na Takukuru.

  Mwaka jana, akiwa ziarani Mbeya Rais msafara wake ulishambuliwa kwa mawe na watu, lakini wasaidizi wake wakaja kutoa taarifa kwamba watu hao walikuwa ni wahuni na walikuwa walimsubiri Rais kwa muda mrefu bila mafinikio.

  Hata hivyo, baadaye uchunguzi huru ulibainisha kwamba tukio hilo lilikuwa na mafungamano ya kisiasa na makovu ya mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM kwa mwaka 2005.

  Mlolongo huo mrefu wa upotoshaji taarifa kwa Rais uliibuka tena katika utoaji wa magari ya misaada, ambako badala ya kupewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Longido alipewa wa Ngorongoro.

  Tukio hilo lilimfanya mkuu huyo wa nchi kufura na kumzodoa mkurugenzi huyo, lakini baadaye ikabainika mkurugenzi huyo alikwenda kutokana na makosa ya maafisa wa Ikulu.

  Katika mlolongo huo, tukio kubwa kabisa ni Rais kutia saini kwa mbwembwe Sheria ya Gharama za Fedha za Uchaguzi ambayo ilichomekwa vipengele nje ya Bunge kitu ambacho ni kinyume cha sheria.

  Tukio hilo ambalo ni la uvunjifu wa katiba, liliibuliwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa ambaye awali, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fedrerick Werema, alikanusha.

  Hata hivyo, baadaye sheria hiyo ilirudishwa bungeni na kukarabatiwa kwa mgongo wa mabadiliko ya sheria mbalimbali.

  Mei mwaka huu, Rais alipewa taarifa za upotoshaji kuhusu mazungumzo ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) na serikali, kwa kuelezwa shirikisho hilo halikuhudhuria mkutano wa saa 4:00 asubuhi kama ilivyopangwa.

  Hata hivyo, Tucta wakatoa ushahidi wa barua za mwaliko wa mkutano huo wa Aprili 22, ambazo zilikuwa mbili moja ikionyesha walitakiwa kufika katika mazungumzo Hazina saa 4:00 asubuhi na nyingine saa 8:00 mchana.

  Katika kuonyesha upotoshaji kwa Rais, wasaidizi hao walimpa barua iliyokuwa ikionyesha walipaswa kukutana saa 4:00 asubuhi huku ile ya saa 8:00 wakawa wameificha.

  Rais akizungumza na wazee wa mkoa wa Dares Salaam aliwashambulia viongozi wa Tucta hasa Naibu Katibu Mkuu Nicolas Mgaya, akimwita mnafiki, mzandiki, mchochezi na hiana.

  Wakati huo huo ahadi ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa aliyowahi kuitoa Rais Kikwete kuwa utajengwa Serengeti ameshindwa kusema utaanza lini.

  Rais Kikwete akiwa ziarani wilayani humo aliwahi kusema kuwa Serikali itajenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wilayani hapo kwa ajili ya kurahisisha usafiri kwa watalii na kukuza uchumi wa wilaya na taifa.

  Akihutubia wakazi wa mji wa Mugumu na viunga vyake wakati wa uzinduzi wa mradi wa bwawa la Manchira, Rais Kikwete alisema kuwa ahadi yake
  iko pale pale kuwa utajengwa.

  Alisema kuwa uwanja huo licha ya kukabiliwa na vikwazo vingi ikiwemo taarifa kutoka kwa nchi jirani kuwa kujengwa kwa uwanja huo kutasababisha nyumbu kutoa mimba kwa wingi.“Maneno ni mengi kuhusu uwanja huo, lakini nasema ahadi iko pale pale, tutajenga na huenda nyumbu wakaongezeka maana hayo si maneno ya kitaalam, maana wageni wanapata shida sana hapa, wanateremkia Kilimanjaro, wanakuja kwa magari, lazima tujenge,” alisema bila kufafanua ni lini.

  Kuhusu barabara ya lami kutoka Makutano hadi Tabora kupitia Hifadhi ya Serengeti alisema itajengwa kwa baadhi ya maeneo ambapo kilometa 50 ndani ya hifadhi hazitajengwa ili kuhifadhi mazingira.

  JK adanganywa tena, AZINDUA BWAWA WAKATI KESI IKO MAHAKAMANI

  Hawa Washauri wa Mzee J.Kikwete Wanamfanya Mzee J.Kikwete kama Babu yao?
   
 10. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,427
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Na sijui hali hii itaendelea hadi lini. Rais kudanganywa imekuwa ni jambo la kawaida sana na chanzo cha tatizo kama lilivyoelezwa ni matokeo ya ufa wa uchaguzi 2005 na kingine kilichoongeza ufa huo ni majeruhi ya Richmonduli. Kumekuwa na kambi ya muungwa na kambi ya EL zaidi ktk nyadhifa za ukurugenzi,ukuu wa wilaya na baadhi ya sehemu ukuu wa mikoa. Tutegemee nini ndani ya miaka mingine mitano ikiwa hali kwa sasa iko hivi???
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mengine anajitakia
   
 12. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #12
  Jul 4, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,454
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Kawaida yake,hata First Lady lazima atakuwa anamdanganya sana tu
   
 13. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sometime we should not just criticise things. Oterwise we shouldtry tomake sound contructive cricitisims Otheriwse Miradi ya maji ni muhimu sanakwa wanachi . Sometime inabidi itekelezeke tu at some expense kwa wananchi wachache kuumia kwa kupata fidia kidogo.

  Hapa Rais hajadanganywa na lazima kaambiwa hili. At the worst case scenario sana sana serikali itaambiwa ilipe hiyo fidia kwa hao wadai kama kweli wana haki. Bwawa haliwezi kuvunjwa.

  Although wengine watasema kafanya hivi kwa kuwa ni mwaka wa uchaguzi my self nasema if i were in his shoes hata kama sio mwaka wa uchaguzi ningefungua bwawa hili.

  Pamoja nakuelezea upande wa matataizo mwandishi alitakiwa atoe analysis japo ya bwana hilo. litasaidi wanavijiji wangapi?, kabla ya mradi huo most closest acces ya maji ilikuwa km ngapi?wanachi wangapi wamekuwa relocated? na wangapi wamelipwa shilingi ngapi?

  Nadhani sometime waandishi wanatakiwa kuandika habari kwa syle ambayo waaache wasomojai waamue . sio kuwaaamulia wasomaji kwa

  Chukulia Scenario Hizi
  Rais kufungua Hospitali wakaiti kuna wakazi wanamefunga kesi ----- kwa nini asifungue
  Rais kufungua hoteli ya kitalii wakati kuna ---- Hiii sawa kabisa naweza kuwaunga mkono wanacriticise
  Rasi kufungua shule wakati kuna mwananchi kashutiki sule imechukua eneo lake ------- Kwa nini asifungue
  Rais kufungua eneo la wazi kwa jili ya michezo wakati kuna kesi ------- Kwa nini asifungue.

  Lets think critically but contsructively
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ohoooo, mmeshafika huko???!!!
   
 15. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Lakini wanamwonea sana muungwana..
   
 16. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu Buckreef,

  Tupo pamoja hapa. Sioni suala la Rais kudanganywa linakujaje hapa. Ukweli ni kwamba mradi wa ujenzi umekamilika, kisima kipo na maji yapo. Sasa Rais kadanganywa nini? Hiyo kesi iliyoko mahakamani ni ya madai na kwamba watu hawakulipwa walichostahili suala ambalo wadai watapashwa kuithibitishia mahakama madai yao na mahakama kutoa uamuzi, lakini bwawa lipo.

  Inwezekana nimekosea au nimeshindwa kuona ni wapi Rais amedanganywa kwenye suala hili. Kama yupo anaweza kunisaidia kunionyesha Rais amedanganywa vipi, tafadhali karibu!!!

  Tiba
   
 17. B

  Bull JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  JF Imeingiliwa nadhani kuna watu wenye chuki binafsi humu jf, aidher upeo wa wachangiaji wengi ni mdogo. Asante mkuu umewafahamisha vya kutosha!!

  Kupeleka kesi ya fidia mahakamani haina maana kuwa ujenzi ule ni haramu, bali ni process za kawaida, wakati mahakama watapo amuru kama wanastahiki fidia watalipwa lakin ujenzi na maendeleo hayawezi kusimama

  Je! mlitaka tusianzishe East afria community kwa sababu kuna watu hawajalipwa fidia zao!!!
   
 18. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Anako, ila anakatumia kuwapeleleza kina Magufuli, Mwandosya, na watu woote wanaopiga vita ufisadi....kwa ujumla ni wale woote wanaoonekana threat kwa wanamtandao ambao ni mafisadi!
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Jul 4, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Duh! hilo bwawa limegharimu Tsh billion 10?.... haya makubwa jamani duh.. haya tutafika. Haya maswala ya wananchi kunyang'nywa ardhi limekuwa swala la kawaida kabisa kwani sisi ukoo wa Mkama hapo Pasiansi, Mwanza tumechukuliwa (ardhi) shamba la toka mababu zetu ati wanajenga bwawa la maji machafu..Just less than 100 metre kutoka ufukoni mwa lake victoria..Tumekubali kuachia ardhi lakini nyie wenzangu nambieni haya maji machafu kando ya ziwa, mwisho wake yanaishia wapi?..Au malengo hasa ni kuuza ardhi hiyo kwa mwekezaji wa Beach Hotels!
   
 20. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #20
  Jul 4, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Jamani JK ameshasema kuwa kipindi hiki yeye alikuwa anapata uzoefu na kujifunza kwa hiyo bado anajifunza hadi awamu hii ikiisha ndio atakuwa anajua anachofanya(kwani uzoefu na kujifunza huchukua miaka mitano )
   
Loading...