JK acha kuwaendekeza hawa madaktari wanaogoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK acha kuwaendekeza hawa madaktari wanaogoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by wimbi la mbele, Jul 2, 2012.

 1. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hivi serikali gani itaendelea kuwakubalia kila kitu hawa wahuni? kama hawataki kazi kwa nini wasijiuzulu kisha wakatafute kazi zingine. wananchi wanakufa kwa sababu dakatari ambaye serikali imemsomesha kwa gharama kede kede anataka alipwe milioni 4 kwa mwezi pesa ambayo serikali haina.

  hawa jamaa ni wahuni na nadhani bora wakawa treated as such

  Nomba sana serikali iwafukuze kazi hawa jamaa ili tuendelee mbele.

  ndio sasa njooni mnitukane lakini nishatoa maoni yangu JF style...
   
 2. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hans Roger, kibanga, nipo hapa, malumbano, mushumbusi ni makada wazuri wa UDINI, CCM, UBAGUZI, sisiti kusema mmae mwabudu huko juu anawashangaa.

  Kwa kukwepa Ban na nyie kuja na ID tofauti kama wewe Hans Roger sitachangia mada yenye majina hayo njoo na majina yako halisi
   
 3. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,188
  Likes Received: 1,190
  Trophy Points: 280
  Ntafunguaje akauti uswis?
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,449
  Likes Received: 22,365
  Trophy Points: 280
  unapeleka kitambulisho chako cha kupigia kura na barua ya serikali ya mtaa unaoishi.
   
 5. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Ni kweli, mtu mzima tena msomi, hatakiwi kulialia au kudeka katika dunia hii. Lazima upime na uwezo wa kiuchumi wa Taifa lako, ila tu wanasiasa na wenyewe wanajipangia malipo makubwa mno!! mpaka wanashawishi hata migomo iendeshwe.
   
 6. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,954
  Likes Received: 2,096
  Trophy Points: 280
  Pesa ya serikali ni ya wafadhili na kodi ya wananchi. Serikali imewekwa na wananchi kwa ajili ya wananchi na ni ya wananchi. Wahuni ni wale wanao ona kuwa wamezaliwa kuendesha serikali na kufanya watakavyo bila kuheshimu katiba na haki za binadamu. Hivi vigogo walioweka pesa kule Uswiss wamezipata wapi hizo pesa? Sio za serikali hizo? Je sio wahuni hao? wanaowaacha sio wahuni?

  Masakata kama ya Radar, Richmond na Dowans, Kiwira, Meremeta, Mapanki sio ya kihuni hayo? Hivi ukimlipa daktari shillingi million 4, PAYE si itakuwa juu hivyo kuongeza mapato kwa serikali - ili hawalioni? Na asiye ona hili lazima atakuwa mhuni!

  Madaktari wamesoma kwa kodi yangu na nataka waboreshewe huduma kwa kodi yangu kwani kodi yangu si ya mtu mmoja kusafiri nje ya nchi kila kukicha, kwenda Bagamoyo kila weekend!!
   
 7. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mie Mkweche, Sijawahi, Sitajaribu hata Siku Moja kuunga mkono mgomo wa Watu wa sekta ya Afya wote!

  Kama kama tulivyowakabidhi wanajeshi kulinda Taifa na Wao Tumewakabidhi kazi ya Kulinda Afya zetu!Kama makundi haya yakigoma ni sawa na Taifa kuvamiwa na wavamizi!

  Kazi ya serikali ni kulinda uhai wa Watanzania kwa gharama yoyote.

  Nduli Iddi Amini Alivamia nchi yetu kule Kagera akaua watanzania Tukamchukulia Hatua za KUMPIGA!

  Je hawa madaktari sio wote(waliogoma) wamesababisha Wanzania wangapi Kufa! Je, wanatofauti gani na Nduli Idi Amini alieua watanzania Tukampiga!Mtu atumie Bunduki au Taaluma yake Kuua Mtanzania ni Lazima Aadhibiwe!

  MAISHA YA WATANZANIA YANATHAMANI KUBWA KULIKO MADAI YOTE!

  Narudia WAGOMAJI HAWAJAIGOMEA SERIKALI BALI WAMEGOMEA WATANZANIA MASIKINI AMBAO KIMBILIO LAO NI HASPITALI ZA SERIKALI!

  SHERIA ZA KAZI ZITUMIKE NA HAWA NI WATU WASIO NA UTU!NI HATARI SANA KWA USTAWI WA TAIFA! MAJINA YAO YAANDIKWE KWENYE KITABU CHA WAHALIFU! WAMEFUNGIWA DUNIANI NA MBINGUNI
   
 8. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,263
  Trophy Points: 280
  Hujakosa imani nayo kwa kuwahadaa wananchi, kwa kuwaambia wezi wa hela za EPA wazirudishe kishkaji, na change ya rada irudi bila hata kumjua muhusika. Uishangae kwa kutowaadhibu madaktari? Wanaopigania haki zao na zetu pia?

  Ar u sure u don't need to see a doctor buddy?
   
 9. M

  MASIKITIKO JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 842
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 60
  Nirudishie wallet yangu na simu yangu.
   
 10. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mbona wanajeshi hawalalamiki kwa mishahara viduchu wanavyopewa? Mshasikia wakigoma? sasa kwa nini hawa madaktari wanataka wapewe special treatment?

  Nashauri iwepo tracker ya kujua wagonjwa wangapi washakufa kutokana na huu mgomo
   
 11. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  mbona wabunge wanaosinzia bungeni wanalipwa 10,000,000 na walisomeshwa naserikali ?nenda ukanoe hiyo akil then urudi uongee na gt's
   
 12. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  ninakuambia nenda kajipange mkuu akili wanajeshi kila kitu wanachopurchase hakina kodi wana mesi zao ,supermarket zao vitu vyao ni vya bei ya chini bila kodi nani kakuambia wana mshahara mdogo wale wa drs la 7 nakubali ila sio wenye degree,wale hawalipii kodi vitu vingi hata gari wanaingiza bure na hawana faida sana wanasubiri vita itokee na fujo na kama wangekuwa hawaridhiki wangedai,wanalipiwa nyumba@an every thing sasa madactari wanaobebe roho za watu wanalipwa kama mishahara ya wahindi bana?
   
 13. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,188
  Likes Received: 1,190
  Trophy Points: 280
  na buzwagi itaniwekea pesa?
   
 14. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nchi za nje madaktari wanaangaliwa sana wakikohoa kidogo wanasikilizwa kwa sababu huduma za afya zikipungua lazima viongozi wa nchi wajiuzulu.
   
 15. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  yaani wewe ndo matapishi kabisa..sasa JK na madaktari nani mhuni?
   
 16. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #16
  Jul 2, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,842
  Trophy Points: 280
  Usitangulize uwoga mbele! Alaf una muiga nape kila kitu maana na yeye kila siku ana sema njooni mnitukane!

  Na kwa nini utukanwe au uliyo yaandika huna imani nayo?

  Kwa hiyo ni halali kwa wabunge kulipwa million kumi?

  Angalia usije ukawa unaongea tu.
   
 17. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #17
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Unajua kuna madaktari walienda kwenye hii fani kwa upendo waliokuwa nao kwa wananchi lakini wengine walienda kutafuta sifa miaka ile ukiwa PCB unaonekana kichwa sasa ndio matatizo yake haya. Mimi naona hata ule mgomo wa kwanza rais alikosea kuwakubalia zile nyongeza na kubadilisha safu wizarani ilitakiwa watimuliwe kipinde kile kile serikali imewalea sana matokeo yake ndio haya.
   
 18. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #18
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wabunge si mnawachagua wenyewe kwani mlilazimishwa kwenda kupanga mistari siku ya uchaguzi?
   
 19. t

  thatha JF-Expert Member

  #19
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ilikutana tarehe 28 Juni 2012 kujadili na kutathmini hali ya utendaji na utoaji wa huduma hivi sasa katika Hospitali. Imebainika kwamba utoaji huduma umeathirika kutokana na mgomo wa baadhi ya madaktari unaondelea kwa takriban wiki moja sasa tangu ulipoanza Jumamosi yatarehe 23 Juni 2012.


  Baada ya tathmini hiyo, Bodi ya Wadhamini imeagiza yafuatayo:


  (i) Madaktari waliopo kazini waendelee na kazi kama kawaida;
  (ii) Madaktari waliogoma warejee kazini kutii amri ya Mahakama Kuu Kitengo cha kazi, kwa mujibu wa Kifungu Na. 76 (1) na (2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004.
  (iii) Madaktari waliopo likizo warejee kazini mara moja. Utaratibu wa kufidia likizo na nauli zao umeandaliwa.
  (iv) Uongozi wa Hospitali uwachukulie hatua za kinidhamu wafanyakazi wote watakaoendelea kutokuhudhuria kazini na kufanya kazi bila sababu za msingi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu za kazi;
  (v) Uongozi wa Hospitali ufute mara moja ‘rotations' za Madaktari waliopo kwenye mafunzo kwa vitendo (interns); na
  (vi) Uongozi wa Hospitali uwapange (re-deploy) Madaktari na Madaktari Bingwa waliopo kwenye maeneo yaliyoathirika wakati huu wa mgomo.


  Aidha, Bodi ya Wadhamini inawashukuru sana madaktari na wafanyakazi wote ambao wameendelea kuwahudumia wagonjwa wetu na wananchi kwa ujumla. Vilevile, Bodi ya Wadhamini inawasihi madaktari na wafanyakazi wote wawe na subira na waheshimu sheria, kanuni na taratibu zilizopo pamoja na maadili ya taaluma zao.
  _________________
  Dkt. Gabriel Upunda
  KAIMU MWENYEKITI
  BODI YA WADHAMINI
   
 20. U

  Udaa JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 727
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  jk na kampani yake.
   
Loading...