Ilulu
Senior Member
- Mar 22, 2008
- 161
- 31
*Atengua uteuzi wa DC Temeke
Na Elisante Kitulo
24 October 2009
RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko madogo ya vituo vya kazi kwa baadhi ya wakuu wa Wilaya nchini ikiwa ni pamoja na kufanya uteuzi mpya wa mkuu wa wilaya mmoja.
Wakati huohuo, Rais ametengua uteuzi wa Bw. Said Mkumbo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke na kumhamishia katika Idara nyingine ya Serikali.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na kusainiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)ilieleza kuwa Rais amemteua Bw. Anatory Choya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbulu ambapo uteuzi huo umeanza Oktoba 10 mwaka huu.
Rais pia amefanya mabadiliko madogo ya vituo vya wakuu wa wilaya ambapo Bw. Francis Isaack aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbulu sasa anahamia Wilaya ya Bunda na Bi. Chiku Gallawa amehamishiwa Wilaya ya Temeke akitokea Wilaya ya Bunda.
Bi. Gallawa amehamishiwa Wilaya ya Temeke kuziba nafasi inayoachwa wazi baada ya Rais kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Saidi Mkumbo.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa kutokana na utenguzi huo, Rais ameagiza Bw.Mkumbo ahamishiwe katika Ofisi ya Waziri Mkuu. Hata hivyo taarifa hiyo haikueleza sababu za utenguzi huo.