JK aapa kuwatoa kafara wala rushwa: ASEMA WAMEMCHOSHA, ATAKAYEKAMATWA ATAKUWA MFANO

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

Monday, 05 September 2011 20:44
kikweteafyaaa.jpg


Rais Jakaya Kikwete

ASEMA WAMEMCHOSHA, ATAKAYEKAMATWA ATAKUWA MFANO, MAGUFULI ATEMA CHECHE

Patricia Kimelemeta

RAIS Jakaya Kikwete amesema ataanza kuchukua hatua kwa watendaji wakuu wa Serikali na wadau wa sekta ya ujenzi wenye tabia ya kuomba na kupokea rushwa wakati wa mchakato wa zabuni ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.Rais amesema hayo kipindi ambacho nchi inatikiswa na tuhuma nzito za ufisadi zinazohusisha vigogo mbalimbali serikalini wakiwamo baadhi kutoka Ikulu.

Katika kuthibitisha ukubwa wa tatizo hilo la rushwa na ufisadi nchini, Rais Kikwete akifungua mkutano wa wadau wa sekta ya ujenzi Dar es Salaam jana alisema sekta hiyo nayo inanuka rushwa kutokana na baadhi yao kutoa fedha ili kupata kandarasi.

"Sasa hivi kila kona rushwa, ukienda barabarani polisi wanaomba rushwa, watendaji wakuu wa Serikali wanachukua rushwa na makandarasi nao wanatoa rushwa ili waweze kupata zabuni, ni tatizo, lazima tuikemee, itatufikisha kubaya," alisema Rais Kikwete.Mkuu huyo wa nchi katika kuonyesha ukubwa wa tatizo la rushwa alisema: "Ukifika barabarani, trafiki anakusimamisha na kukulazimisha kuwasha ‘wipers' hata kama hakuna mvua, kumbe ana malengo yake ya kutaka kukuomba rushwa, kuna tatizo."

"Katika sekta ya ununuzi wa mali za umma ndiyo kabisa, wanaagiza mali za Serikali kwa kuongeza gharama, kuweka cha juu ili wakifanikiwa waweze kugawana huku wakifahamu kwamba fedha zinazotumika ni za Serikali. Lazima watendaji kama hao waangaliwe kwa umakini sana kwa sababu wanaweza kurudisha nyuma maendeleo ya nchi."

Alisema kutokana na hali hiyo, kila mmoja analo jukumu la kuhakikisha anabadilika na kuacha tabia ya kuomba au kuchukua rushwa kwa sababu tabia hiyo inachangia kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi.

Rais Kikwete alisema kiongozi bora ni yule anayechukia rushwa na kufanya kazi zake kwa uadilifu na weledi na siyo kuendekeza tamaa na kuwaomba rushwa anaowatumikia.

Dk Magufuli atema cheche
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli alimwagiza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads) kuvunja Bodi ya Ununuzi ya Mali za Umma kwa sababu imejaa rushwa.Mbali na agizo hilo, Dk Magufuli pia aliziagiza bodi ya wahandisi, makandarasi na wasanifu majengo, kukagua miradi ya maendeleo inayofanywa katika halmashauri ili kuona kama imekidhi viwango vya ubora kulingana na gharama ya fedha zilizotumika.

"Ninaziagiza bodi hizi zote kukagua miradi ya maendeleo katika halmashauri kuangalia kama zinaendana na gharama halisi ili tuweze kuwachukulia hatua wakurugenzi na watendaji waliosimamia miradi hiyo," alisema Magufuli.

Dk Magufuli alisema wakati umefika wa kuwachukulia hatua watendaji wanaoshindwa kuwajibika kwa mujibu wa sheria na kufanya wanavyojua wao.

"Naomba kwa ridhaa yako Mheshimiwa Rais, niache nifanye kazi yangu, hata kama watakuja ofisini kwako kuleta malalamiko wasikilize lakini waache, mimi nachapa kazi kama ulivyonikabidhi," alisema Dk Magufuli.

Dk Magufuli alisema kutokana na hali hiyo, wadau wa sekta ya ujenzi wanapaswa kutimiza majukumu yao ili kuondoa adhabu zinazoweza kujitokeza.

 
"Mtu achukie rushwa mpaka tumuone anachukia rushwa. Siyo mwingine ana sema anachukia rushwa unamwangalia unasema ah huyu?!"-JKN
 
Kwa maana hiyo ni kwamba MAFISADI nchini ni 'akina waale' na kwamba yeye mwenyewe ni mweupe kama sufu wala hayumo sio?????? My foot!!!! Utekelezaji mwema hivo hivo.
 
Hivi hizi ahadi zote hizi anazotoa kila ck anazikumbuka? Kila kukicha anatishia nyau 2. Na jamaa washamgundua wanaendelea tu kukamua manake kelele za vyura hazimzuii Ng'ombe kunywa maji!
 
Leo nimeelewa kumbe traffic wanatakiwa wakague waipa wakati wa msimu wa mvua tu. Watanikoma sasa. Kazi tunayo.
 
Kwa kweli nime-admaya sana hilo shati lake; huenda ikawa ni uzao wa 'Mark & Spencer' au 'Arrow' nisaaidieni kidogo jaama????????
 
Kwa kweli nime-admaya sana hilo shati lake; huenda ikawa ni uzao wa 'Mark & Spencer' au 'Arrow' nisaaidieni kidogo jaama????????

Leo bibi yangu kule kantalamba akisikia haya anaweza kusema kweli kiongozi wetu ameamua, lakini kama angekuwa na internet na anaweza kuona wikileaks angejua kuwa rais wetu mwenyewe alipokea rushwa ya hela na nguo. Kweli bongoi wajinga ndio waliwao.
 
hii si mara ya kwanza kwa yeye kusema maswala ya rushwa. Kesho atatuambia ana list ya wala rushwa. Huu ndo upuuzi tusioupenda. Kama raisi

kila siku unalia na wala rushwa sisi wengine tuseme nini? Ubabaishaji tuu
 
JK ana matatizo,eti wala rushwa anawafahamu eti aliwapa muda wajirekebishe.Hivi kuna tofauti gani kati ya rais wa manzese au wa tff na jk
 
Anza na POLICE wanaochukua rushwa ya mahindi yanayosafrishwa kupitia boda ya rombo tarakea kwani imekua ni kero ni bora serikali ingeruhusu na kukusanya kodi kuliko hii inayowaaidisha wachache
 
Leo nimeelewa kumbe traffic wanatakiwa wakague waipa wakati wa msimu wa mvua tu. Watanikoma sasa. Kazi tunayo.
mtu kama hjui kiswahili bwana! inakuwa shida kwelikweli, yaani unatafsiri mambo kama yalivyo, huna upeo mkubwa wa kufikiri kuwa mkuu wa nchi alikuwa na maana gani wakati anasema hayo!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kwani
  • wametunga sheria mpya ya kuwakatama ?
  • au kuna wataaalam wametoka masomoni juzi juzi wamekuja na mbnu mpya?
Anyway tunamtakie heri na mafanikio katika hiyo vita maana.........
 
mtu kama hjui kiswahili bwana! inakuwa shida kwelikweli, yaani unatafsiri mambo kama yalivyo, huna upeo mkubwa wa kufikiri kuwa mkuu wa nchi alikuwa na maana gani wakati anasema hayo!!!!!!!!!!!!!!!!

Hii hailingani na mkuu wa nchi hata kidogo, endelea kupaka wanja anyway.
 
hizi porojo dhidi ya rushwa tumechoka kusikia. kwanini wasinyamaze tu.....jamani. aarghh!!
miaka michache ilopita alisema nawafahamu wala rushwa` kwa hiyo waache hizyo tabia,
punde kadai na wauza dawa za kulevya pia nawafahamu....
sasa leo tena porojo eti nitawatoa kafara.....
kesho utasikia
---na majambazi nawafahamu, waache wizi mara moja
---na maharamia nawafahamu.........waache mara moja kuteka meli
---na wana jf nawafahamu....

chukua hatua dhidi ya rushwa mai friend, vita dhidi ya rushwa ni matendo bro.
 
Sasa hivi kila kona rushwa, ukienda barabarani polisi wanaomba rushwa, watendaji wakuu wa Serikali wanachukua rushwa na makandarasi nao wanatoa rushwa ili waweze kupata zabuni, ni tatizo, lazima tuikemee, itatufikisha kubaya," alisema Rais Kikwete.Mkuu huyo wa nchi katika kuonyesha ukubwa wa tatizo la rushwa alisema: "Ukifika barabarani, trafiki anakusimamisha na kukulazimisha kuwasha ‘wipers' hata kama hakuna mvua, kumbe ana malengo yake ya kutaka kukuomba rushwa, kuna tatizo."

aisee
sasa ana mlalamikia/analalamika kwa nani?
kwani Raisi ni Maguruli?
kwenye hotuba ya magufuli yeye kachukua hatau kwa yale yaliyo chini ya uwezo wake
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli alimwagiza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads) kuvunja Bodi ya Ununuzi ya Mali za Umma kwa sababu imejaa rushwa.Mbali na agizo hilo, Dk Magufuli pia aliziagiza bodi ya wahandisi, makandarasi na wasanifu majengo, kukagua miradi ya maendeleo inayofanywa katika halmashauri ili kuona kama imekidhi viwango vya ubora kulingana na gharama ya fedha zilizotumika

sasa kikwete ana shindwa nini kuwa kama magufuli kazi kulia lia tu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom