JK aahidi kutuma wataalamu wa kilimo na wakulima wa zao la nanasi Ghana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK aahidi kutuma wataalamu wa kilimo na wakulima wa zao la nanasi Ghana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 13, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]JUMATATU, AGOSTI 13, 2012 06:26 NA MWANDISHI WETU, ACCRA

  Rais Jakaya Kikwete, amesema Tanzania itatuma wataalamu wa kilimo na wakulima wa zao la nanasi nchini, kwenda Ghana kujifunza ukulima wa kilimo cha kisasa cha aina mpya ya nanasi ambayo ndiyo yenye soko duniani.

  Rais Kikwete aliyasema juzi, wakati alipotembelea mashamba mawili makubwa ya kilimo cha kisasa cha mananasi aina ya MD-2, ambayo ndiyo inauzwa zaidi duniani, katika siku yake ya tatu ya ziara ya siku nne nchini Ghana.

  Rais Kikwete, aliamua kutembelea mashamba hayo ya Koranco Farms katika Kijiji cha Obotweri na lile la Bomart Farms, lililoko Kijiji cha Dobro, eneo la Nsawan, yote mawili yakiwa kiasi cha kilomita 150 kutoka mjini Accra, ili kujionea mwenyewe kilimo cha aina mpya ya mananasi iitwayo MD-2, ambayo iliingizwa Ghana kutoka nchi ya Costa Rica, kiasi cha miaka 30 iliyopita.

  Mananasi aina ya MD-2 , ndiyo yanayouzwa duniani na mbegu aina hiyo ya mananasi haipo Tanzania, ambayo wakulima wake, wanaendelea kulima na kupanda aina ya asili ya mananasi ambayo hayana soko duniani.

  Ziara hiyo, Rais Kikwete ambaye alisindikizwa na Waziri wa Chakula na Kilimo wa Ghana, Kwesi Ahwoi ilianzia shamba la Koranco Farms ambalo lilikuwa shamba la kwanza Ghana kulima mananasi aina ya MD-2.

  Kwenye shamba hilo, Rais Kikwete ameambiwa kuwa yeye ni Rais wa pili wa Tanzania kutembelea shamba hilo, kufuatia ziara ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, wakati wa ziara yake Ghana miaka ya 1980.

  Kwenye shamba hilo, lililoanzishwa miaka 30 iliyopita na lenye ukumbwa wa ekari 800, Rais alitembelea shamba lenyewe na kiwanda ambacho vyote vinakadiriwa kuwa na thamani ya dola za Kimarekani milioni 20.

  Mkurugenzi Mtendaji wa shamba hilo, Emmanuel Koranteng amemweleza Rais Kikwete kuwa, shamba hilo linaajiri wafanyakazi 50, inapandwa kiasi cha miche 60,000 katika eka moja na mananasi yake yanauzwa katika nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU).

  Kwenye shamba la Bomarts, Rais Kikwete ameelezwa na Mtendaji Mkuu wa shamba hilo, Anthony Botchway kuwa, shamba hili lilianzishwa miaka 27 iliyopita na kuwa mananasi aina ya MD-2 yamekuwa maarufu zaidi kuliko aina nyingine duniani.

  Amesema kuwa nchi ya Costa Rica inajipatia pato la kiasi cha dola za Marekani milioni 600, kwa kusafirisha na kuuza mananasi aina hiyo nje ya nchi hiyo.

  Rais Kikwete ambaye alikuwa katika ziara ya siku nne nchini Ghana, ambako pia ameshiriki mazishi ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Hayati John Evans Atta Mills, anaondoka huko kesho kurejea nyumbani.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Ghana walijifunzia wapi? Kwanini tusiwapeleke huko GHANA walipojifunzia? kama ni kwenye SOKO la DUNIA? kwanini

  Sisi tunakwenda au tunapenda second-hand? kila kitu cheap; na hakidumu... MBONA VIATU VYAKE na SUIT sio SECOND

  HAND? Sababu toka GHANA walipofundisha kitu kipya kimegundulika sasa tukiwapelewa watu wetu huko watapata utaalamu mpya...
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Tuna madini, Gas na mengineyo mengi yeye anashughulika na vitu ambavyo tunaweza kununua kwa kutumia pesa ya madini na Gas kama waarabu asituletee udhaifu wake hapa
   
 4. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee atakuwa hajapona Kifafa. Bado anatoa ahadi tu.
   
 5. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Mfamaji haishi kutapatapa...Wahenga hawakuwa wajinga kututengenezea msemo huu! Tafakari!
   
 6. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Modes tumovuzishie hii thread kwenye ujasiriamali kule huku itachafuliwa sasa hivi na vijana wa Nape
   
 7. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,563
  Likes Received: 16,531
  Trophy Points: 280
  Nadhani rais wetu hajui kwamba kuna mananasi mazuri sana yapo Tanzania.Labda hajawahi kufika Mkuranga kuna mananasi yanaitwa mpingo.Tunachohitaji watanzania ni namna ya kuzalisha kisasa na kupata mikopo ya muda mrefu ya kuwekeza.
  Labda ningemuomba siku moja badala ya kwenda nchi za watu afanye utalii maeneo ya Mkuranga ajionee mwenyewe.Tuna mananasi mzuri na ni matamu sana lakini hatuna soko.Hatuhitaji ya kutoka Ghana.
   
 8. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  My dear President JK,

  You can do your country a favour by funding your excellent researchers to produce even better varieties from the local sources rather than "copy & paste" technologies. In the long term, it will be sustainable. Wasomi wa nchi hii wanakuona kituko kwa ulimbukeni wako. Please, spare us the embarrassment.

  Bahati mbaya sana kila ikija bajeti sehemu ya kubana matumizi ni kupunguza pesa za utafiti. Na hata pale zinapopangwa, mgawo hautoki treasury.
   
 9. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  anahaidi mpaka lini? toka 2005 anahaidi...Yesu atarudi kabla hizo ahadi zake hazijatekelezwa...tushachoka na ahadi...
   
 10. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #10
  Aug 13, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Mnafiki sana huyu mzee. Hapa Dar es Salaamu tunakula mananasi kutoka Bagamoyo, Badala ya kufanya research namna ya kuboresha kilimo cha mananasi bagamoyo yeye anakwenda kuangalizia ghana, basi aende na kwenye machimbo ya dhahabu sasa. Yaani yeye mwenyewe haamini kama kinachofanyika nyumbani kwake ni sahihi anatuongoza vipi sasa? hivi ni lazima kila kinachofanyika hapa kiwe blended na namna ingine kutoka nje?
   
 11. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #11
  Aug 13, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mananasi yetu matamu sana yanaishia kuoza mashambani kwa vile hayana soko la huakika. Badala ya kuanza kuangaika na MD2, serikali ingewasaidia wakulima na kuekeza zaidi kwa njia za kisasa na kutafuta soko la nje.

  Maembe yetu pia matamu sana, sema hatuko serious serikali imefocus zaidi kwenye kuomba omba.

  Tuna vitu vingi sana sema jembe la mkono linatuangusha na serikali haijali wakulima.

  Wakulima wanaitaji msaada mkubwa kutoka serikalini
   
 12. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ninavyofahamu mimi SUA wapo wataaamu wazuri sana wa mambo ya Vipando. Na wanauwezo wa kuzalisha mbegu nyingi na kwaharaka huku ikidhibitiwa viwango. Tatizo si kwamba wakulima wetu hawapendi kulima kilimo cha kisasa, tatizo ni soko. Kama watalima ukulima huu wa kisasa kwa kutegemea soko la ndani, basi gharama ya uzalishaji itakuwa kubwa kulingana na bei za soko letu la ndani. Hapa Tanzania kuna mizengwe mikubwa ya kupata kibali cha kwenda kuuzia huko, sasa kwa mazao kama mananasi ambayo shelf life yake si kubwa. Ukianza kuhangaikia kibali zaidi ya miezi sita na maranyingine usipate hicho kibali, basi ujue imekula kwako. Ila cha kushangaza zaidi, ni vigumu kwa wakulima wetu kupata hivi vibali, ila wafanyabiashara wa vitu mbalimbali wanavipata faster. Hivyo kama mpango huu utaletwa, bado unaweza usimnufaishe mkulima zaidi ya mfanyabiashara. Rejea hekaheka za KILIMO KWANZA uone nani mfaidika.
   
 13. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Serikali yetu inashangaza sana.

  Yeye anasafiri kila siku baada kutafuta soko la bidhaa zetu anaangaika kuomba misaada na kuuza nchi.
   
 14. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Tatizo ndio linakuja hapo.

  Wafanyabiashara wengi wakubwa ndio hawa viongozi wetu. Kwahio kila kitu kikitokea wanatumia njia ya kumnyonya mtu wa chini. Mwisho wa siku wote tunakosa wao wanakimbilia kwenye ufisadi.

  Serikali ikiamua ku-invest kwenye kilimo na kutafuta soko la nje sio mbaya pia kwani italetea taifa mapato na kutoa ajira na wakati huo huo wakawa wananunua kwa wakulima wengine pia kwa bei inayofaa.
   
 15. M

  MTK JF-Expert Member

  #15
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  The last time I checked JK alikuwa pia ameahidi kuleta wacuba wa kutokomeza malaria since his infamous trip ya "kubembea" to that Salsa Island; hatujaona follow up?
  when a leader falls into the trap of being excited at each and everything that crosses ones sights ujue kuna shida hapo; nothing gets done! mtawasubiri sana hao wataalamu wa mananasi na by the time JK leaves office sijui ataulizwa nani maana uongozi wa Tanzania hauna policy continuity ni wa kupokezana vijiti tu then mtu mpya naanza mambo yake kwa slogan zake na mbwembwe zake na kamati za ufundi za kwake pia; distinct and exclusive of the last!
   
 16. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Jakaya mwenyewe ni mkulima wa mananasi pale Kiwangwa sasa hayo anayosema kayaona huko Ghana yanayouzika nchi za nje ni mananasi ya aina gani? Tatizo tulilokuwa nalo katika kuuza matunda yetu nchi za nje sio aina ya matunda bali ni utaalam wa preservation na packaging. Nina uhakika kabisa kuwa mananasi ya Kiwangwa yakiwapackaged vizuri yatapata soko nchi za nje. Asitupotezee kodi zetu za kuwalipa waalimu mishahara mizuri kwa kuwapeleka ndugu zake huko Ghana kwenda kutalii kwenye mashamba ya mananasi!!
   
 17. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #17
  Aug 13, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Anasema ni aina ya MD-2 ndio ya kisasa na yana soko nje.

  Angeonja na kutuambia kwamba ni matamu kuliko ya hapa nyumbani.

  Zile safari zake zote tumeingia hasara kubwa sana.
   
 18. Wachovu

  Wachovu JF-Expert Member

  #18
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 1,197
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  Huyu mzee hana akili kweli kweli anashinda anarandaranda hajuihata kinachotokea kwenye nchi yake. Mananasi nayo ni ya kupeleka watu Ghana kujifunza ?
  Tunayo mengi mpaka yanaoza kwa kukosa soko , hawa wazee sijui vipi ? hamnazo kabisa
  Kwanikunakitu gani anashangaashangaaa !!!!!!!!!!!!!!!!

  Njoo Mkuranga ukajionee vipu wewe bwana dhaifu , kutwa kiguu barabarani usituletee za kuleta
   
 19. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #19
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,109
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  Nimesoma o level shule ya kilimo tulikuwa tunafundishwa kilimo cha aina nyingi kuanzia mboga mboga,matunda hadi Nafaka.Tuna vyuo vingi vya kilimo kutaja vichache ni Uyole,Tengeru pia tuna chuo kikuu cha kilimo.
  Sidhani kama kilimo cha mananasi cha Ghana kitatofautiana na cha huko tofauti iliyoko ni mbegu tu ila taratibu kwa kiasi kikubwa zitakuwa zile zile labda kujua aina ya udongo na hali ya hewa inayohitajika kwa aina hiyo ya mananasi.
  Bado hatujaweza kuvitumia vizuri vyuo vyetu upande wa utafiti ndio maana kila rais anapotoka nje ya nchi anabaki kushangaa naamini iwapo tutawekeza kwenye utafiti tunaweza kufanya vizuri zaidi.
  Hatujajua kama hayo mananasi ni ya asili au gmo maana tunaweza kuyakimbilia kumbe tunakaribisha tatizo jingine.
  Tuna mananasi mazuri sana hapa nchini na bahati nzuri sehemu alikotoka rais(bagamoyo) ndiko wanalima manansi kwa wingi lakini bado hajajua kuwa wakulima wanahitaji soko la uhakika na ili wawe na soko la uhakika inabidi tuwe na viwanda vya kutengeneza juice kwa wingi.Hivyo badala ya kuuza mananasi nje tunatakiwe tuuze juice kwani tukiuza fresh wao wanakuja tena kutuuzia juice kwa bei mbaya.
  Tukiwa na viwanda tutaongeza ajira na pato kwa taifa na yote yanawezekana.
  Mwisho Rais aelewe msiba umeisha anatakiwa kufanya kazi aliyoomba asikimbie matatizo yaliyoko huku wenzake wote walioenda kwenye msiba wamesharudi
   
 20. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #20
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280


  Video kwa hisani ya Tangibovu wa youtube

  Nadhani mawazo ya wana-Jamiiforums kuwawezesha wakulima wetu kupata taarifa ya namna ya kufungasha mazao yetu kwa viwango vya soko la nje ya nchi (kimataifa) basi wizara za mambo ya nje , biashara, serikali za mitaa, kilimo na maofisa ugani wataifanyia kazi kwa kasi zaidi ya kasi za Mh. Mwakyembe na Mh. John Magufuli.

  Huu si wakati wa kujifunza ni wakati wa kutenda.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...